Zoezi la uandikishaji vitambulisho Msasani Mikoroshoni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zoezi la uandikishaji vitambulisho Msasani Mikoroshoni

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Luushu, Jul 25, 2012.

 1. L

  Luushu JF-Expert Member

  #1
  Jul 25, 2012
  Joined: Apr 8, 2012
  Messages: 595
  Likes Received: 233
  Trophy Points: 60
  Utaratibu mbovu watu walalamika waandishi wako taratibu watu wameaamka saa kumi usiku kuwahi namba mpaka sasa bado wapo mimi nilipata namba 158 nimenda kazini nimerudi nasikiliza namba bado sijaitwa namashaka na hili zoezi watu wengi hawataandikishwa
   
 2. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #2
  Jul 25, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,333
  Likes Received: 22,181
  Trophy Points: 280
  Kipaombele ni kuwaandikisha wageni, maana wao wanatoa hela ili wapate vitambulisho vya utaifa
   
 3. L

  Luushu JF-Expert Member

  #3
  Jul 25, 2012
  Joined: Apr 8, 2012
  Messages: 595
  Likes Received: 233
  Trophy Points: 60
  Uko sawa kabisa Bujibuji kwani kaja muarabu wamemtetemekea kama mpira wakati hana nyaraka zozote kuna wanaojiita wanyasa kumbe wamalawi uzushi mtupu mwanawane
   
 4. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #4
  Jul 25, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,673
  Trophy Points: 280
  Zoezi la uandikishaji ni bovu kuna uwezekano watu wengi wasipate vitambulisho.
   
 5. zacha

  zacha JF-Expert Member

  #5
  Jul 25, 2012
  Joined: Feb 28, 2009
  Messages: 489
  Likes Received: 200
  Trophy Points: 60
  cha ajabu ambacho mi sijaelewa mbona hakuna passpot(Picha) zinazopigwa au watakuja tena kudai hizo picha baadae maana naona wanataka taarifa tu halafu hakuna mambo ya kupigwa hizo picha..... hofu yangu isije watu wakasafiri nd' mkarudi tena muanze kuwaambia watu sasa tunahitaji sura zenu. kwa kifupi sijaelewa!
   
 6. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #6
  Jul 25, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  serikali yetu inafanya kila kitu ovyo ovyo sasa mbona hakuna hata taarifa za kutosha kama uandikishaji wa vitambulisho umeanza wao wanafanya kimya kimya/ ingekua wakati wa kampeni za uchaguzi kila kona kungekua na yale mabango ya kumtambulisha mgombea lakini mambo ya msingi kama haya hawayapi kipaumbele..... siasa.... siasa... siasa tu
   
 7. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #7
  Jul 25, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Sidhani kama kuna haja ya kuweka ultimatum ya muda kwa zoezi hili. Kwasababu tunajua kuwa litakuwa endelevu, wao wangetangaza tu kuwa usajili umkeanza na kila mtru aende kwa wakati wake, siku yoyote,akaandikishwe ili kupata kitambulisho chake. Hii ya kuweka ultimatum wakati zoezi litakuwa ni la kudumu ni janja ya kukaribisha rushwa
   
 8. mito

  mito JF-Expert Member

  #8
  Jul 25, 2012
  Joined: Jun 20, 2011
  Messages: 7,634
  Likes Received: 2,020
  Trophy Points: 280
  Mkuu umesahau cost implications za kulifanya liwe endelevu?
   
 9. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #9
  Jul 25, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Walioplan walishalifikiria hilo. Hili zoezi litakuwa ni la kudumukwa sababu kila wakati watanaaniz wapya wanaofikisha miaka 18 itabidi wapewe vitambulisho... ni kama zoezi la kuandikisha wapiga kura kwenye daftari la kudumu
   
 10. Chechetuka

  Chechetuka JF-Expert Member

  #10
  Jul 25, 2012
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 549
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hili ni zoezi la Kitaifa, kama una ushahidi kuwa kuna mtu amejaza fomu ya kuomba kitambulisho cha Uraia, wakati yeye ni mgeni, tafadhari toa taarifa kwa afisa wa NIDA
   
 11. Chechetuka

  Chechetuka JF-Expert Member

  #11
  Jul 25, 2012
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 549
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kinachofanyika sasa hivi ni Pilot Project. Kitambulisho cha Taifa ni HAKI ya kila Mtanzania anayestahili kupata.
   
 12. Chechetuka

  Chechetuka JF-Expert Member

  #12
  Jul 25, 2012
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 549
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Inaonekana ni kiasoi gani upo nyuma na taarifa. Taarifa zimetolewa magazetini, ktk Radio, Television na ktk matangazo ya magari yanayopita mitaani, wewe upo wapi?
   
 13. Chechetuka

  Chechetuka JF-Expert Member

  #13
  Jul 25, 2012
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 549
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Umeto angalizo zuri sana ktk mchakato huu, kwamba kama picha na alama za vidole hazitachukuliwa sasa hivi, kuna uwezekano wakati wa kuzichukua watu wengine wakawa safarini. Naishauri NIDA kuangalia na kuutumia vizuri ushauri huu kwani una mantiki kubwa na ya maana sana.
   
 14. Chechetuka

  Chechetuka JF-Expert Member

  #14
  Jul 25, 2012
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 549
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni kweli kuna mapungufu ktk baadhi ya maeneo, lakini sio kweli kuwa kuna watu watakosa Vitambulisho. Mapungufu yote yanafanyiwa marekebisho
   
 15. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #15
  Jul 25, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,333
  Likes Received: 22,181
  Trophy Points: 280
  Unataka kuniambia kuwa maafisa wa NIDA ni waadilifu kushinda nguvu ya pesa?
   
 16. kupelwa

  kupelwa JF-Expert Member

  #16
  Jul 25, 2012
  Joined: Aug 24, 2011
  Messages: 874
  Likes Received: 139
  Trophy Points: 60
  Mi pia ni mkaazi wa masasani bonde la mpunga ambayo ndo ina mikoroshoni pia, Zoezi hili serikali na wakala wa vitambulisho hawakujipanga kiuhalisia;Zoezi hili limegubikwa na mapungufu makubwa, kama watendaji wasiona ujuzi, hawakuandaliwa ipasavyo, ni kama ni zoezi la bora liende bila ufanisi, hawazingatii muda.Kuna mapungufu mengi mno kwenye zoezi hili, kama namna ya kupata jina, muda unaotumia ni mkubwa, unaweza kupoteza siku nzima, na pia kwa hao watendaji wa NIDA na waandikishaji ,hakuna anayeweza kutoa majibu ya namna ya kuliona jina .Pia hata ukilipata bado unatumia muda mwingi sana kuweza kuandikishwa.Mfano mimi kuna tatizo moja limetokea, wakati wanaandikisha majumbani , mwandikishaji alikosea akandika jina ambalo halipo kwenye vitambulisho.Nilipohoji, akasema atarekebisha bila tatizo.Leo nimekwenda na vitambulisho hivyo , imekuwa taabu kwelikweli , sababu hayo niliyowaelekeza mwanzo ndo limekuwa jibu, kwamba majumbani walitakiwa kuandikisha watu kwa vitambulisho ili iwe rahisi kuwatambua wakija kujaza fomu.Lo hii hata kupata majibu ni lipi lifanyike kutatua tatizo hilo , wasimamizi wote walikuwa hawajui ,iliane na boss wao awape jibu,mpka naondoka saa kumi hakuna jibu mpka kesho tena.je ina maana napoteza haki ya uraia?kimsingi hakuna watendaji wazuri , wenye weledi makini, wenye kujenga ufanisi na kupunguza muda, kutatua kero na usumbufu unaojitokeza, na pia maswali , je serikali haikutenga fedha ili NIDA ijipange? zoezi likumbwa na ubabaishaji mtupu.Na hofu yangu je huko vijijini , zoezi hili , je litakuwa la ufanisi?
   
 17. kupelwa

  kupelwa JF-Expert Member

  #17
  Jul 25, 2012
  Joined: Aug 24, 2011
  Messages: 874
  Likes Received: 139
  Trophy Points: 60
  unachozungumza ni mauzauza,unaweza kumshitaki sajeti wa polisi kwa pc?jibu utapoteza muda , hao hao mimi binafisi niwashauri mwanzo waandike kwenye daftari lao jina lililo kwenye vitambulisho , lakini wakapuuza, leo kumekuwa utata, wakati nataka kujaza fomu.mpaka naondoka pale hakukuwa na majibu
   
Loading...