Zoezi la kuwasachi majumbani mwao wabunge wa ukawa DSM linaendelea, polisi pen za camera ziko kwangu

Crashwise

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
22,227
8,739
Zoezi la pekua pekua majumbani kwao linaendelea kwa wabunge wa ukawa wakianza na Halima James Mdee na sasa wanaelekea kwa Waitara.

Naomba kulirahisishia jeshi la polisi kuwa zile Pen zenye Camera tulizo zitumia kwenye chaguzi za meya wa Kinondoni na Ilala ninazo Mimi.

Ila kabla hamjaja kunisachi mkamateni aliyefoji barua ya zuio ya uchaguzi wa meya wa jiji la DSM na kupelekea kifinyo kwa kaimu mkurugenzi....

Updates
Habari za uhakika ni kuwa kesho ccm wanakutana na Mkurugenzi wa Jiji kupanga tarehe ya uchaguzi wa Mayor wa Jiji.

Hiyo ni baada ya kuwa na uhakika wa kukamatwa na kuwekwa ndani kwa madiwani Tisa pamoja na wabunge watano ambao ni Mh. Waitara, Mh. Anatropia, Mh. Lijuakali, Mh. Kubenea na Mh. Halima
 
Kwenye nchi nyingi za Afrika democracy ni zero kabisa nikifikiri Dr.Kizza Besigye alivyodhalilishwa juzi akavunjiwa vioo vya gari yake nakumwagiwa maji ya kuwasha, Waanga wengi wa vyama vya upinzani kutoka hapa nchini wengine hadi wakapoteza uhai,Prof;Lipumba alivyopigwa na kurushiwa kwenye PT kama kibaka, Leo hii viongozi wa ukawa kusachiwa bila sababu yeyote ile na usishangae wakabambikiwa na kesi...
 
Inakera na kuumiza sana inakupa nafasi ya kuwaza mbadala...
 
Mkuu angekuwa Chadema amefoji ile barua unadhani nini kingetokea? sasa anzia hapo kuwa wanafanya hayo kwa amri ya nani hivi unqjua wizara hiyo iko chini ya nani...

Niaibu .... nisawa Na mzazi anayekula chakula cha mwane....! Hajali km ni sawa au siyo sawa
 
Du! hii ni zaidi ya aibu? Kwani ukawa ndio walifoji barua useme wanatafuta coppy? Haaa kweli nchi imepata pigo kubwa kutawaliwa na ccm hii ni zaidi ya ajabu, haya wale viherehere wa kusema tunataka amani ya nchi mbona sasa wako kimya? kina Maria Nyerere mbona hawatoki front wakemee huu unyanyasaji unaofanyika? Au ccm ikifanya fujo ndio kujenga amani? Aibu yenu manyag'au nyie.
 
Back
Top Bottom