Zoezi la kuwaondoa Wamachinga kwenye njia za Watembea kwa miguu Dar es Salaam, sijaona dalili yoyote ya wao kuondoka

Kunywa uji ukalale achana na habari za machinga hatuondokiiiiii

Kwa Mujibu wa Maelekezo ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla kuanzia leo Septemba 13 wamachinga wote wanaofanya biashara zao kwenye njia za watembea kwa miguu wanatakiwa kuwa wameondoka wao wenyewe pamoja na mabanda yao.

Nimepita Mbagala sijaona dalili yoyote ya wamachinga kuondoka, na sasa naelekea Kariakoo kujionea hali halisi.

Popote ulipo ndani ya Dar es Salaam tuletee taarifa ya wamachinga kuhusiana na zoezi hili muhimu
Alalale achana na habari za machinga wewe
 
TRA na maofisa biashara wa Halmashauri wapitie upya aina za biashara zisizo za kimachinga alafu watoze kodi /leseni kama ambavyo wafanyavyo kwenye viduka vidogo mijini.

Tarura katika miji mikubwa wanayo mamlaka ya kukataza kufanya biashara kwenye kingo za barabara /waweke tozo kama wafanyavyo kwenye parking za magari. mfano wanaweza kutoa leseni za parking /uwazi wa eneo kwa wenye maduka /ofisi ili kuzuia machinga kupanga/kuweka huduma /bidhaa zao.

Maofisa afya/TFDA wanayo mamlaka ya kuzuia biashara holela za vyakula katika maeneo yasiyo rasmi, ubora na viwango.

Wakurugenzi wa halmashauri katika miji mikubwa kwa kushirikiana na watendaji walio chini yao hasa mipango miji wana wajibu wa kutenga maeneo au kubuni njia mbadala za Machinga kufanya shughuli zao. mfano maduka /vibanda vinavyo tembea au kuteua mtaa mmoja kwa ajili ya machinga.

Wakuu wa mikoa /wilaya wana wajibu wa kuratibu maeneo na aina ya biashara ili kuondoa mwingiliano wa bidhaa na huduma kurundikana sehemu moja.

Jeshi la zimamoto linao wajibu wa kutoa elimu juu ya majanga ya moto ambayo yanweza sababishwa na ujenzi holela wa vibanda vya machinga au kuzagaa kwa machinga karibu na maeneo yenye vituo vya mafuta mijini.

Tume ya Ushindani na wakala wa vipimo na TBS nao wana wajibu wa kusimamia /kutoa elimu ya namna ya kuboresha biashara ndogo ndogo ili zikuwe na kuondoa dhana ya Umachinga wa wajasiriamali wadogo wadogo.
 
Wamachinga wamebuni kuweka picha ya mama kwenye vibanda vyao ili visibomilewe...if unataka kuona pita hapa Shekilango upande wa kushoto kama unatokea town utaona kibanda kimechorwa picha ya Magu na Mama Samia
 
Machinga ni zao la kushindwa kwa sera za ccm kuhusu uchumi na ajira.Wawezacho kwa bidii ni kumbambika Mbowe kesi.
Kama wakoloni waliweza kumaliza tatizo la ajira kwa raslimali hizi hizi wao wanashindwa vipi sasa.
 
Kwa Mujibu wa Maelekezo ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla kuanzia leo Septemba 13 wamachinga wote wanaofanya biashara zao kwenye njia za watembea kwa miguu wanatakiwa kuwa wameondoka wao wenyewe pamoja na mabanda yao.

Nimepita Mbagala sijaona dalili yoyote ya wamachinga kuondoka, na sasa naelekea Kariakoo kujionea hali halisi.

Popote ulipo ndani ya Dar es Salaam tuletee taarifa ya wamachinga kuhusiana na zoezi hili muhimu
Mkuu halafu unarepoti wapi?
 
Wamachinga Wasibugudhiwe Waacheni wafanye Biashara popote
Agizo la Mwendazake liheshimiwe

Sent from my SM-J600F using JamiiForums mobile app
 
😁😁😁

AMK5Se.png
 
Makalla tulipomsifia amelewa sifa na sasa amesahau majukumu yake ya msingi

Nilimwambia Makalla legacy yake kwa Dar ni usafi na kuipanga Dar hasa kwenye maeneo ya kibiashara ila naona alivyosifiwa tu kidogo amelewa sifa na kujisahau kama viongozi wengine wa huko nyuma

Anatakiwa kujitafakari
 
Kwa Mujibu wa Maelekezo ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla kuanzia leo Septemba 13 wamachinga wote wanaofanya biashara zao kwenye njia za watembea kwa miguu wanatakiwa kuwa wameondoka wao wenyewe pamoja na mabanda yao.

Nimepita Mbagala sijaona dalili yoyote ya wamachinga kuondoka, na sasa naelekea Kariakoo kujionea hali halisi.

Popote ulipo ndani ya Dar es Salaam tuletee taarifa ya wamachinga kuhusiana na zoezi hili muhimu
Sawa Mheshimiwa lakini pamoja na Wamachinga kuwataka wasizibe njia za waendao kwa miguu natamani angetoa amri pia kuwa waendesha magari, waendesha pikipiki, bajaji pia wahindi wapika kuku na chips usiku watuachie njia za waenda kwa miguu. Ukienda nchi za wenzetu, huruhusiwi hata kusimama kupiga soga na rafiki njiani! Polisi watakuja kuwaambia ondokeni ili msizuie msafara wa waendao kwa miguu. Sababu ya kufanya hivyo ni kuheshimu waendao kwa miguu kwa sababu ndiyo wengi, pia wengine wameacha magari yao kupunguza traffic, wengine wanafanya mazoezi, ni haki yao pia ni kuokoa muda wa waendao kwa miguu ili wafike waendako haraka. Inaongeza tija kwenye uchumi na kuongeza furaha kwa wananchi wako! Hivi viongozi wetu hamsafiri nje ya nchi. Tazameni hata hapo Dubai!
 
Back
Top Bottom