Zoezi la kutafuta miili ya waliofariki kwenye ajali ya Ndege Ngorongoro lakamilika

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,557
21,505
oko.png
Kamanda wa Jeshi la polisi mkoani Arusha Bw Charles Mkumbo amesema kazi ya kuopoa miili ya watu 11 waliokuwa kwenye ajali ya ndege iliyotokea Jana Ngorongoro imekamilika na inatajiwa kusafirishwa leo mchana hadi jijini Arusha.

Bw mkumbo amesema miili hiyo inatarajiwa kuwasili katika uwanja Mdogo wa ndege wa Arusha saa Tisa kamili mchana.

Aidha kamanda mkumbo amesema Taratibu nyingine zitatolewa baada ya miili hiyo kuwasili ambapo itapokelewa na viongozi wa Ngazi mbalimbali Mkoani hapo.

Ndege hiyo Mdogo ya abiria Mali ya Kampuni ya ndege ya Coastal Air ilianguka Jana katika eneo la embakai wilayani Ngorongoro na kuja watu wote 11 waliokuwemo ambao walikuwa wanatokea Arusha kwenda Serengeti.

Chanzo cha ajali hiyo bado hakijajulikana

ITV
 
Unatakiwa ujue kuwa ajali za ndege zipo za aina tofauti. Kwa ajali hii ilikuwa ni vigumu hatua za kujiokoa kufuatwa kwa sababu ni tukio la ghafla la ndege kugonga mlima
kwahyo mkuu ivi inatokeje ndege inagonga mlima si naskia inanjia zake huko angani

au ni uzembe wa pilot??
 
kwahyo mkuu ivi inatokeje ndege inagonga mlima si naskia inanjia zake huko angani

au ni uzembe wa pilot??
Ina njia zake lakini pia kuna wakatininabidi kutoka nje ya njia kidogo kama kushuka chini au kwenda juu zaidi kutokana na hali ya hewa. Kilichotokea hapa ni kuwa rubani aliishusha chini kidogo na kutokana na ukungu hakuweza kuona mlima mbele yake
 
kwahyo mkuu ivi inatokeje ndege inagonga mlima si naskia inanjia zake huko angani

au ni uzembe wa pilot??
Ndege ndogo kwa route fupi,huwa hazinyanyuki sana.so kama ruba hana uzoefu na eneo husika na hali ya hewa ikiwa ya sio rafiki.hili hutokea.
 
Ina njia zake lakini pia kuna wakatininabidi kutoka nje ya njia kidogo kama kushuka chini au kwenda juu zaidi kutokana na hali ya hewa. Kilichotokea hapa ni kuwa rubani aliishusha chini kidogo na kutokana na ukungu hakuweza kuona mlima mbele yake
Kwani rubani Wa ndege hutegemea kuona mbele kama dereva Wa bodaboda! Au kuna vifaa vinavomuongoza kujua aendako!?
 
Kwani rubani Wa ndege hutegemea kuona mbele kama dereva Wa bodaboda! Au kuna vifaa vinavomuongoza kujua aendako!?
Anatakiwa aone mbele pia mkuu. Mara nyingi wakati wa kutua na kupaa lazima atumie macho
 
Anatakiwa aone mbele pia mkuu. Mara nyingi wakati wa kutua na kupaa lazima atumie macho
Nilisikia walisema kuwa ndege ilipoteza "mawasiliano" bila kufafanua! sasa ndo nikawa najiuliza, ilipoteza mawasiliano ndo chanzo cha kuannguka au ilivoanguka ndo ikapoteza mawasiliano!
Pamoja sana mkuu"
 
Ina njia zake lakini pia kuna wakatininabidi kutoka nje ya njia kidogo kama kushuka chini au kwenda juu zaidi kutokana na hali ya hewa. Kilichotokea hapa ni kuwa rubani aliishusha chini kidogo na kutokana na ukungu hakuweza kuona mlima mbele yake
Lazima kuna ka element ka uzembe,au kwakuwa yeye anaitwa Pilot na wengine madereva..
 
Kuna ndugu wawili wamekufa wakuzaliwa tumbo moja,mwenye kampuni ya utalii ya Maasai wondering na mdogo wake sijui kakake,afu mmoja sijui mtot wa baba mdogo.Mungu wapokeee waja wako na uwape kauli thabit,uwaepushe na adhabu za kaburi.
 
Back
Top Bottom