Zoezi la Kupokea Taarifa za walimu shule binafsi

Charles Ignatio

Senior Member
Oct 9, 2010
133
52
*ZOEZI LA KUPOKEA TAARIFA ZA WALIMU WOTE NCHINI WA SHULE ZA BINAFSI AMBAO WAMEKUMBWA NA TATIZO LA MISHAHARA YAO KUTOLIPWA KUTOKANA NA JANGA LA UGONJWA WA CORONA LINAENDELEA VIZURI*


Zoezi hili linaratibiwa na chama cha walimu wa shule za binafsi Tanzania- *TPTU* mpaka muda huu linaendelea vizuri na mwitikio wa walimu nvhini wanaotoa taarifa zao kwetu ni mkubwa, inatia moyo sana na inatupa ari kutafuta majawabu ya tatizo hili kwa busara na hekima kubwa, hii ni inashiria kuwa tatizo hili ni kubwa kuliko tunavyoweza kufikiria.

Tunalazimika kusimama katika hili kwa walimu wote wa shule za binafsi nchini ambao wapo katika tatizo hili bila kujali ni wanachama waliosajiliwa au sio wanachama waliosajiliwa tunasimama nao wote kama ilivyo wajibu wa chama hiki kisheria.

Tunakiri wazi kabisa kuwa tatizo hili limeathiri *walimu,wazazi,waajiri na wanafunzi* lakini katika hawa wote, mwalimu wa shule binafsi ambaye hajapata mshahara wake ndiyo anaeumia zaidi,chama kinawatoa hofu walimu wote nchini kuwa busara kubwa itatawala katika kutafuta suluhisho la hili tatizo baina ya *chama,waajiri na serikali* ili kupata mwarobaini wa walimu hawa kwani kila mtu katika janga hili hana hatia ila ni muhimu tukashirikiana bega kwa bega wakati huu wa shida kama ilivyokuwa wakati wa amani.

Tarehe *19/4/2020* siku ya jumapili ni mwsho wa kupokea taarifa za walimu wenye changamoto hii ili tuende kwenye hatua zingine ambazo chama kimejipanga kuzipitia kuhakikisha ufumbuzi wa tatizo hili kwa walimu unapatikana haraka.

Wasiliana nasi kwa simu namba *0767664494* tupate taarifa zako kama unapitia changamoto hii, share ujumbe huu kadiri uwezavyo uwafikie walengwa wengi zaidi wa tatizo hili hapa nchini.

*UMOJA NA MSHIKAMANO DAIMA*

Na Mwl JULIUS MABULA.
KATIBU MKUU.
CHAMA CHA WALIMU WA SHULE ZA BINAFSI TANZANIA-TPTU.
MAKAO MAKUU-MWANZA.
 
Poleni sana Waalimu wa watoto zetu.

Kuna zile pesa zilizochangwa na wadau kwaajili ya kusaidia waathirika wa Corona, zimefika 8Bil jana Waziri Mkuu alikabidhiwa na aliainisha zilipaswa ziwasaidie ninyi mnaofundisha watoto wetu.

Bado kuna pesa katika bajeti ya dharura na majanga

Ila Wallah Wabillah kwa awamu hii msitegemee sana kusaidika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Walimu mtaonekana kama hamjaathirika na hili tatizo...Na zitachangwa hela hamtalamba hata Mia.
 
Walimu hawana hatia
Shule haina hatia
Wazazi hawana hatia
Serikali haina hatia

Nani awajibike?

Kama unavyoshindwa kulipwa mshahara ndivyo hao wazazi wa wanafunzi ambavyo hawajalipwa kwenye kazi za sekta binafsi kama hotel, utalii na ukosefu wa kipato kutoka kwa wajasiriamali na wazazi they can no more afford paying school fees.

Issue ya corona imevuruga uchumi wa Dunia huko Ulaya ndio usiseme ona club kama Tottenham na nyingi za premier zimeshindwa kulipa wafanyakazi wote wasio wachezaji na badala yake wanalipwa na govt stimulus package.

Serikali ilipaswa kubeba dhamana ya kunusuru ajira binafsi watu wasifukuzwe kazi kwa kutumia stimulus , kwa maana ukimdai huyo mwajiri wako mshahara huo wa mwezi 3 na 4 atakupa kisha akikuambia na terminate mkataba kwa sababu sina uwezo wa kukulipa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom