mitale na midimu
JF-Expert Member
- Aug 26, 2015
- 10,420
- 17,722
Kwanza hatua tuliyofikia, upinzani hauwezi kuwa na uhalali wa kuisimamia Tanzania tangu walipokumbatia wale tuliowalalamikia na kuwasafisha kwa brashi ya chuma. Kauli iliyowahi kunitisha ni ile aliyoitoa EL kuwa anataka Tanzania iwe na matajiri wengi, miongoni mwa aliowataja ni mtu ambaye wapinzani haohao walimlalamikia kusign mikataba hotelini(sina hakika kama kweli alifanya hivyo).
Upande wa pili ni upande wa chama tawala ambao Unalalamikiwa kuwa zao la hao Matajiri Haramu(Sasa kinaendesha zoezi la Usafi na Nidhamu).Zoezi la kuwaadabisha wale waliojitajirisha kwa mali za umma, kwa mianya waliojitengenezea wenyewe ili wapite kwa maoni yangu linaendelea vizuri licha ya kukumbwa na changamoto makaburi.
Ila ninachokiona zoezi hili jema la kupongezwa lilipaswa liendane na kufufua matajiri wengi halali kila kona nchini kuziba mianya iliyoachwa wazi.
Upungufu wa pesa mifukoni mwa mtanzania kutokana na kuziba mianya ya wizi, pesa chafu za madawa, kujilimbikizia mali, udalalidalali na ujanjaujanja ulipaswa uambatane na urudishwaji mifukoni mwetu wa pesa halali kupitia wafanyabiashara halali walipa kodi, Wakulima wakubwa, Vibarua halali, ajira nzuri, Viwanda vinavyofuata sheria na mitelemko mingi ya upatikanaji fedha halali nchini n.k
Hili gap katika hili zoezi jema linaacha watu katika dilema, Je litaendelea kudumu au litaisha lini?
Wanaoona ng'ambo mtusaidie...
Wenu mkulima mzalendo njiani kuelekea shambani...
Mitale na Midimu