Zoezi la kukamata magari ya serikali yanayotumia namba binafsi kufanyika nchi nzima karibuni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zoezi la kukamata magari ya serikali yanayotumia namba binafsi kufanyika nchi nzima karibuni

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by R.B, Oct 20, 2012.

 1. R.B

  R.B JF-Expert Member

  #1
  Oct 20, 2012
  Joined: May 10, 2012
  Messages: 6,163
  Likes Received: 1,098
  Trophy Points: 280
  Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kusisitiza utaratibu wa usajili wa magari
  ya Umma unafuatwa na kutafanyika zoezi rasmi la kurejesha usajili wa magari yote.Serikali imetoa muda hadi kufikia Novemba 15,2012 magari ya Umma yaliyo na namba za kiraia, yarejeshwe namba stahiki za magari ya Umma . Baada ya hapo Operesheni hiyo iitakamata magari, pikipiki, bajaj na mitambo ya umma,Vilevle kutakuwa na aina ya namba za usajili zitakazotumika kama ST, PT, MT,JW, DFP, CW, SM na ,SU.Hadi sasa serikali imesajili vyombo vya moto,123,431 yakiwemo magari,,pikipiki,bajaj na mitambo ya umma (pichani anaefuatia mwenye sare za polisi) ni Mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani katika jeshi la Polisi nchini Kamanda Mohamed Mpinga
   
 2. Viol

  Viol JF-Expert Member

  #2
  Oct 20, 2012
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 18,982
  Likes Received: 1,087
  Trophy Points: 280
  bongo movie
   
 3. Van persie

  Van persie JF-Expert Member

  #3
  Oct 20, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 916
  Likes Received: 152
  Trophy Points: 60
  Safi, ila mi naona atoe muda wamgari ya serikal kuwepo mitaan. Maana utakuta gari ya serikal ipo baa saa tano usiku. Au jmapil gari ya serikal imepaki kanisan. Huku ni kuchezea kodi za watu.
   
 4. Nazjaz

  Nazjaz JF-Expert Member

  #4
  Oct 20, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 5,345
  Likes Received: 1,131
  Trophy Points: 280
  WAZIRI wa Ujenzi, Dk John Magufuli, ameanzisha operesheni maalumu ya kukamata magari ya umma yanayotumia namba za kiraia, baada ya kubaini kuwa yanatumika kufisidi fedha za Serikali.Waziri huyo pia ameahidi kuwachukulia hatua kali waliouziwa magari ya Serikali na bado wanatumia namba zile zinazoonyesha kuwa yanamilikiwa na Serikali.

  Alitoa onyo hilo jana jijini Dar es Salaam, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari huku akiahidi kuendesha operesheni kali ya kuhakikisha wote waliokiuka taratibu wanawatiwa mbaroni. "Operesheni hii itahusisha magari yote ya Serikali Kuu, Serikali za Mitaa, Wakala wa Serikali, Mashirika ya Umma na taasisi nyingine za umma," alisema Magufuli.

  Alisema hivi karibuni Serikali ilibaini kuwapo kwa magari ya umma yaliyosajiliwa kwa namba za kiraia na yanatumia namba hizo kwa manufaa binafsi na hivyo kuisababishia Serikali hasara. Dk Magufuli alisema kwa kuzingatia hali hiyo, atahakikisha kuwa utaratibu wa usajili wa magari ya umma unafuatwa. "Serikali itafanya operesheni maluum ya kurejesha usajili wa magari yote ya umma kwenye utaratibu," alisisitiza waziri huyo maarufu katika kusimamia sheria zinazohusu wizara yake.

  Alisema Serikali inatoa muda wa hadi kufikia Novemba 15 mwaka huu magari ya umma yenye namba za kiraia, yarejeshwe kwenye namba stahiki za magari hayo. "Baada ya hapo, tutatumia vyombo vya ulinzi na usalama katika kukamata magari, pikipiki, bajaj na mitambo ya umma na tunawaomba wananchi watusaidie kwa kutoa taarifa,"alisema Dk Magufuli. Dk Magufuli alisema Serikali iliweka utaratibu unaozuia matumizi ya namba za kiraia kwenye magari, pikipiki, bajaj na mitambo yake na kwamba hata hivyo utaratibu huo
  sasa umekiukwa. Alisema Sheria ya Usalama Barabarani ya mwaka 1973, inaipa mamlaka, Wizara ya Ujenzi kusajili na kutunza kumbukumbu za magari yote ya Serikali ambayo yatapewa namba zitakazotanguliwa na JW, PT,ST, MT,CW na DFP.

  Alisema magari, pikipiki, bajaj na mitambo ya umma itakayokamatwa, itapelekwa katika maeneo ya vituo vya polisi ama karakana za Tamesa mikoani na maeneo ya idara za ujenzi wilayani. Alisema wanaohusika kusimamia na kufanikisha zoezi hilo ni makatibu wakuu wa wizara zote, makatibu tawala wa mikoa yote, wakurugenzi watendaji wa halmashauri zote, watendaji wakuu wote wa taasisi na idara za serikali na watanzania wote.
   
 5. q

  querauk Member

  #5
  Oct 20, 2012
  Joined: Oct 13, 2012
  Messages: 54
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Dr Magufuli ni mnafiki na mwongo mkubwa yeye mwenyewe anatumia gari ya serikali yenye namba za kiraia. vilevile msisahau yeye ndiyo aliyeuza nyumba za serikali na akamwuuzia hata hawara yake . hivyo ashauriwe aache unafiki watanzania na hasa waandishi wa habari waache kutumika kumtangaza kibaka huyo wa mali ya umma
   
 6. Joel

  Joel JF-Expert Member

  #6
  Oct 20, 2012
  Joined: Sep 1, 2007
  Messages: 908
  Likes Received: 259
  Trophy Points: 80
  Hivi wanajamvi hamjui kuwa huyu jamaa ndiye aliyefanya ufisadi wa kutisha katika nchi hii kwa kuuza nyumba za serikali kiholela na sasa watanzania waingia gharama kubwa sana kulipia ufisadi wake wa tirioni kadhaa alioufanya?huyu jamaa anatafuta umaarufu tu kwani na yeye alikuwa anatumia gari ya serikali yenye private #,bahati nzuri kwake ameacha kuitumia kama wiki moja kabla ya kutoa tangazo hilo.
  Shame on him!
   
 7. M

  Morinyo JF-Expert Member

  #7
  Oct 20, 2012
  Joined: Aug 26, 2011
  Messages: 2,471
  Likes Received: 460
  Trophy Points: 180
  Hili zoezi litakuathili nini maana naona unalilaani sana.
   
 8. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #8
  Oct 20, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,893
  Likes Received: 5,346
  Trophy Points: 280
  yani huyu mwizi wa nyumba za serikali anawapiga mkwara wezi wenzake?
   
 9. K

  KIBE JF-Expert Member

  #9
  Oct 20, 2012
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 943
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Dunia kote kuna taasisi za ulinzi na usalama huwa hazitumi na haziwezi kutumia namba za serikali kwenye magari yake nenda cia,fba etc... Kwa tanzania taasisi kama takukuru,tiss na kikosi cha upeleleze cha polisi,, mi ya jeshi pia magari yao hayatumia namba za serikali kama stk,stj ,su etc.. Kutokana na kazi zake. Wanatumia namba za binafsi lakini ukiangalia kwenye vio vya magari hayo utakuta namba ya serikali mf.stk 1000,stj 2000 etc.
  Sasa nashindwa jua kama mh: Magufuli hilo analijua au la na sina uhakiki kama ameamua yeye pekee yake bila kuvishirikisha vyombo hivyo suala la magari yote ya serikali yanayotumia namba binafsi yawekwe kwenye namba za serikali.
   
 10. F

  FJM JF-Expert Member

  #10
  Oct 20, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Kwanini usiache Magufuli akafanya kazi yake ndiyo uje na malalamiko? Au na wewe umesajili gari ya serikali kwa number binafsi?
   
 11. chitambikwa

  chitambikwa JF-Expert Member

  #11
  Oct 20, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 3,940
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Alfu eti wabadilishe haraka, je mafuta waliyotumia na Km zote walizotembea si kuifirisi serikali?
   
 12. M

  MAGUNJA JF-Expert Member

  #12
  Oct 20, 2012
  Joined: Jul 3, 2012
  Messages: 974
  Likes Received: 442
  Trophy Points: 80
  Nakubaliana na aliyesema "bongo Movie". Hili jambo lilishaibuka miaka kadhaa iliyopita juu ya magari ya serikali kuwa na namba za kiraia. Ukatolewa utetezi kuwa magari mengine ya serikali hayakununuliwa na serikali moja kwa moja (kama magari ya miradi ya serikali). Ikafanyika kampeini ya kubadili namba mpaka ikapelekea magari yasiyopewa STK basi yapewe DFP ili yajulikane. Leo kwa usahaulifu wetu anakuja na story ile ile nasi tunampigia makofi!! Alafu wakosaji hawa wanapewa wiki tatu kurekebisha makosa yao!!! badala ya kukamata kuanzia leo. "BONGO MOVIES".
   
 13. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #13
  Oct 20, 2012
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  Hayo unayosema magufuli anayajua kuliko wewe, gari za tiss na pccb zinajulikana, tatizo kuna gari nyingi sana za serikali katika awamu hii ya nne tena zikiwamo vx v8 ambazo zipo mikononi mwa watu tena nyingine zikitumiwa na nyumba ndogo za wakubwa kwa mgongo kuwa ni za tiss, nyingi mno na tunazifahamu so acha kazi fanyike
   
 14. M

  MKALIKENYA JF-Expert Member

  #14
  Oct 20, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 1,198
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 133
  Ok kwangu mimi mwenye shamba NGEDERE alikula mazao yangu uko nyuma kuwageuka wenzie na kuanza kulinda shamba langu ni faida...wacha NGEDERE na PANYA wamalizane wenyewe kwanza.
   
 15. Kennedy

  Kennedy JF-Expert Member

  #15
  Oct 20, 2012
  Joined: Dec 28, 2011
  Messages: 11,233
  Likes Received: 2,915
  Trophy Points: 280
  Zoezi oyeee! Nangoja matokeo sijui mazuri au mabaya ni suala la muda tu.
   
 16. Dotworld

  Dotworld JF-Expert Member

  #16
  Oct 20, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 3,929
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  [​IMG]
   
 17. M

  MAMC Senior Member

  #17
  Oct 20, 2012
  Joined: Jan 3, 2012
  Messages: 140
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Nilisha andika humu mwezi wa 1- Magufuri pia atoe mwongozo kuhusu ufujaji unao- endela wa magari ya viongozi wa serikali!

  Haiingii akilini - dereva anaishi kimara na bosi anaishi tegeta, dereva analala na gari? Hayo mafuta na mileage nani analipa?

  Kwa nini gari isulale kwa boss na dereva akala dara dara au staff bus?

  Hatujiulizi? Private sector drivers wana fanyaje na gari za ma boss wao? Au na hii hadi ifanyiwe study tour?
   
 18. Mahebe

  Mahebe JF-Expert Member

  #18
  Oct 20, 2012
  Joined: Feb 7, 2009
  Messages: 320
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Zoezi hili nimelipanda!
   
 19. Nyalotsi

  Nyalotsi JF-Expert Member

  #19
  Oct 20, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 5,104
  Likes Received: 551
  Trophy Points: 280
  Ukiingia mtaani unakutana na vx, v8 kibao wanaendesha watoto wataamu kama zao. Kumbe kodi zetu ndo wanafuja na hawara zao? Wanaogopa stk kuonekana hotelini au mabibo na ifm. Mi naona hili zoezi wamekosea kulitangaza kwani hawatafanikiwa. Ilitakiwa lifanyike kimya kimya.
   
 20. Twilumba

  Twilumba JF-Expert Member

  #20
  Oct 20, 2012
  Joined: Dec 5, 2010
  Messages: 6,141
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Huu ni unafiki na uzandiki mkubwa!
  Kuna miaka fulani (nadhani early 2000) kuna zoezi la ku-establish Technology fulani ambayo inge-monitor magari yote ya serikali, ilikwenda vyema sana na nakumbuka kampuni ya Imperial ya south Africa ndio ilipata hiyo deal lakini katika hatua za mwisho kabisa zoezi likapotea juu juu!

  Kama yuko serious na kutaka kuokoa Rasilimali za nchi hii, swala si kusajiri hayo magari kwa namba za STJ, Suluhu ya kweli hapo ni gari zote kuwa monitored kwa teknolojia ya kisasa ambayo waliikana awali kwamba ni gharama wakati ukweli ni kwamba matumizi yao mabaya ya magari ya serikali yangebainika.

  Kampuni na taaisisi Binafsi zimeweza ku-establish system ya ku-monitor magari yao, na wamefanikiwa kuokoa ma-milioni, serikali inashindwa nini kutumia ma-milioni ku-establish system hiyo ili kunusuru na kuokoa ma-bilioni?

  Magufulia aache unafiki kwa hili hana nia thabiti ya kulikomboa taifa hili isipokuwa anataka umarufu usio na tija kwa watanzania!
  Mia.
   
Loading...