barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,739
- 32,866
Hii ni video inasambaa mtandaoni ikiwaonyesha walimu wakihakikiwa na wanaitwa majina mmoja mmoja kama Wanafunzi.
Muhusika anaita majina na kuwauuliza Wanafunzi "Huyu Mwalimu mnamfahamu!?"...Watoto wanajibu "Ndiyooo".Mwalimu mmoja mmoja anatoka mbele baada ya kuitwa jina lake na kupanga foleni kama anasubiri uji wa buruga!!
Hii ni udhalilishaji,hata kama ni "HAPA KAZI TU" basi itafutwe njia sahihi za kuhakiki walimu "hewa" ili kutunza utu,heshima na staha ya Mwalimu.
Wenye mamlaka husika tunaomba wawaelekeze watendaji wengine wanaofanikisha zoezi hili la kuhakiki wafanyakazi hewa wakiwamo walimu,kutumia njia rafiki ili kufanikisha zoezi hilo