Zoezi la kuhakiki mali za vigogo kuanza Februari 20 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zoezi la kuhakiki mali za vigogo kuanza Februari 20

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MziziMkavu, Feb 20, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Feb 20, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  [TABLE="width: 491"]
  [TR="bgcolor: #E1E1E1"]
  [TD]VIGOGO wapatao 60 wataanza kukaguliwa mali zao ili kuweza kuhakiki mali hizo walivyozipata ikiwa ni mchakato ulioundwa na serikali kukagua viongozi wote wa watumishi wa Umma wa nchini[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="colspan: 3"]Mchakato huo utaanza Februari 20 mwaka huu na kumalizika mapema Machi, ambapo Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma wataendesha zoezi hilo kwa vigogo hao

  Hiyo imekuja baada ya kurejeshwa kwa fomu za utalaji kwa viongozi wote wa watumishi wa Umma wa Serikali kukamilika

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana ,Kamishna wa Tume ya Maadili, Jaji Mstaafu Salome Kaganda alisema kuwa, uhakiki huo ni nguzo bora ya kuijenga jamii ya Watanzania, hasa viongozi wa umma katika kuishi kwa kufuata misingi ya uadilifu, iliyowekwa na Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma.

  Amewataja baadhi ya viongozi watakaoanza kukaguliwa ni akiwemo Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta , Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano) Hawa Suluhu Mbunge John Mnyika na wengine wengi wakiwemo na wakuu wa mikoa, wilaya, MaMeya wa majiji, madiwani, wabunge na wakurugenzi wa taasisi mbalimbali za Serikali nchini.

  Kaganda aliwaambia wanahabari kuwa, si kwamba viongozi watakaonzwa kuhakikiwa wana kashfa wala tuhuma zozote si kweli bali ni sheria kwa viongozi kama hao kuhakikiwa mali zao na kuwaondoa hofu viogozi hao na kuwaomba ushirikiano katika zoezi hilo

  Amesema kuwa lengo lingine la kukagua viongozi hao ni kuboresha utumishi wa umma kwa kuwa sasa uadilifu umeonekana kushuka ikiwa na serikali kufanya utafiti wa kisheria zaidi kutaka kutenganisha biashara na uongozi

  “Sisi tunachokiomba kutoka kwao ni kutoa ushirikiano wa kutosha kwa maofisa wetu wakati wa zoezi zima la uhakiki wa mali zao,” alisema Kaganda

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  Chanzo.. Zoezi la kuhakiki mali za vigogo kuanza Februari 20
   
 2. J

  JACADUOGO2. JF-Expert Member

  #2
  Feb 20, 2012
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 930
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Uhakiki wa mali za vigogo! Hamna jipya.
   
 3. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #3
  Feb 20, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Wanafuja tu hela zetu hiyo tume ya maadili na utumishi wa umma.
   
 4. IKHOIKHOI

  IKHOIKHOI JF-Expert Member

  #4
  Feb 20, 2012
  Joined: Jan 30, 2012
  Messages: 366
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Serikali yote kwa ujumla imeoza, kwa kuwa tu uadilifu ni suala ambalo limefumbiwa macho. SHERIA ZIPO NYINGI SANA TATIZO HAKUNA ANAYEZISIMAMIA NA KUZITEKELEZA. Kwa hiyo anayefanya kosa ni sawa tu na asiyefanya kosa kwa kuwa hakuna adhabu yoyote. Hatuwezi kwenda mbele.
   
 5. t

  tenende JF-Expert Member

  #5
  Feb 20, 2012
  Joined: Jan 10, 2012
  Messages: 6,560
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Tume ya maadili ni JANGA la taifa haifai kitu. Wanalipwa kwa kitu wasichokifanyia kazi. Hivi sasa viongozi wengi wamejitajirisha kifisadi, na wengine wanamiliki mali nyingi kwa majina ya watu wengine. Haya tume inayajua lakini hawamgusi mtu!. Tume hii ife wapewe vijana wenye uchungu na nchi.
   
 6. t

  tenende JF-Expert Member

  #6
  Feb 20, 2012
  Joined: Jan 10, 2012
  Messages: 6,560
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Wazee wa siku 100 mko wapi? au ilikuwa geresha?
   
 7. Bubu Msemaovyo

  Bubu Msemaovyo JF-Expert Member

  #7
  Feb 20, 2012
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 3,436
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Mhasibu wa Mkoa wa Morogoro asipohakikiwa tujue mahoteli yote haya hela anatoa wapi nitadharau zoezi zima.
   
 8. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #8
  Feb 20, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Hapa hakuna kitu changa la macho tu wanatupiga
   
 9. satellite

  satellite JF-Expert Member

  #9
  Feb 20, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 603
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  huyo kaganda mbona kafreeze hata kabla ya zoezi?baada ya kuanza na kina chenge,lowasa,Jairo,manumba wanaanza na kina mnyika,sugu hivi huu si umbumbumbu?
   
 10. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #10
  Feb 20, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Hivi hili zoezi halina shinikizo la wafadhili? Nadhani kuonyesha kama zoezi hili ni serious, basi tume ingeanza na wale watumishi wenye tuhuma kwanza (wananchi wanawajua na wameshasemwa sana). Baada ya kujiridhisha wachukuliwe hatua. Zaidi ya hapo, zoezi hili litakuwa ni suala kuhamisha akili zetu kwenye mambo mengine
   
Loading...