Zoezi la Benki Kuu kutaka mabenki ya Update taarifa za wateja halihojiwi?

Huwa nahisi wanatafuta acc ambazo zinahela hata laki mbili na hazijawa updated kwa muda mrefu, afu wao waka-assume pengine wamiliki wa acc hizo walishakufa kwa maajali ya tz, ili wajinufaishe.

Kwa kawaida watu wengi wana-acc nyingi na pengine familia zao hawazifahamu kabisa.
Kwa hii serikali ya Jk iliyojaa uswahiba bila uadilifu ,hili uliloandika linawezekana kabisa
 
Hili zoezi limejaa walakini, na tayari wameanza kuongeza muda maana watu hawaja-respond vizuri. Walipa kodi Tanzania (TIN) ni around laki 8 -9 tu! Na asilimia kubwa kati ya hawa ni wafanyakazi wa mashirika ya umma na makampuni ya kati. Makampuni makubwa yamegundua njia nzuri mbili za kukwepa kodi,
1. Wanatoa misaada sana kupitia CSR, hivyo kodi inakuwa kidogo, mfano Vodacom
2. TIC. Hiki ni kichaka cha wakwepa kodi. Na kumbuka ukipata cheti cha TIC una miaka 5 bure bila kulipa kodi. It will be interesting kama ingetokea majina ya makampuni yote yaliyoorodheshwa TIC yakawekwa hadharani. Watu wangezimia!
 
Wakuu, mimi binafsi sijaona tofauti kati ya zoezi hili la BoT na lile la National Housing Cooperation la kukusanya details za clients wake. Kimsingi, lile zoezi la NHC lilikuwa linahitaji details nyingi zaidi - very personal- zaidi ya hizi tunazotakiwa kutoa kwa BoT. Ninachoshangaa ni kwamba watu wengi hapa jamvini tulilishadadia lile zoezi la NHC-kwa maelezo kwamba walichokuwa wanakifanya NHC hakikuwa kitu cha ajabu, na hata kwenye nchi nyingine wanafanya hivyo hivyo. kwa mtazamo wangu, watu wengi hapa waliunga mkono lile zoezi la NHC kwa kufikiri kwamba waliokuwa walengwa ni wahindi. Sasa kibao kemegeuka na hakuna cha mhindi, ****** wala mangi, watu mnaanza kulalama kwamba privacy zenu zimeingiliwa!!. Tuwe wakweli bwana. Kama ni sahihi kumwaga data zako zote kwa NHC, kwanini iwe taabu kumwaga the same data kwa BoT??? Mkuki kwa nguruwe???
 
Kila jambo linaloanziashwa na taasisi ya kiserikali hapa TZ ni halali haliulizwi!! Nchi hii ni kisiwa twafanya mambo pasipo kutoa sababu ya zoezi na faida kwa mteja husika atoae taarifa za ziada
 
Watu wenye vipato vya chini wataumia sana na utaratibu huu na hii itapelekea watu kuwa wezi wa kupindukia maana wata tafuta means nyingize za kuendesha maisha yao. Siku zote serikali yetu inafanya vitu kwa kukurupuka na hili ndio janga kubwa kwa nchi hii. Hebu tuone kipi kitakachojiri.
 
Wakuu, mimi binafsi sijaona tofauti kati ya zoezi hili la BoT na lile la National Housing Cooperation la kukusanya details za clients wake. Kimsingi, lile zoezi la NHC lilikuwa linahitaji details nyingi zaidi - very personal- zaidi ya hizi tunazotakiwa kutoa kwa BoT. Ninachoshangaa ni kwamba watu wengi hapa jamvini tulilishadadia lile zoezi la NHC-kwa maelezo kwamba walichokuwa wanakifanya NHC hakikuwa kitu cha ajabu, na hata kwenye nchi nyingine wanafanya hivyo hivyo. kwa mtazamo wangu, watu wengi hapa waliunga mkono lile zoezi la NHC kwa kufikiri kwamba waliokuwa walengwa ni wahindi. Sasa kibao kemegeuka na hakuna cha mhindi, ****** wala mangi, watu mnaanza kulalama kwamba privacy zenu zimeingiliwa!!. Tuwe wakweli bwana. Kama ni sahihi kumwaga data zako zote kwa NHC, kwanini iwe taabu kumwaga the same data kwa BoT??? Mkuki kwa nguruwe???

Naona umetumwa na BOT.
 
Naona umetumwa na BOT.

Mkuu,

Suala sio kutumwa au kujituma. Ni swala la kuzingatia haki na utaratibu kuliko ushabiki zaidi. Usinielewe vibaya kwamba ninatetea zoezi hili la BoT. Mimi ni mmoja wa waathirika kwenye lile zoezi la NHC. Sikujisikia vizuri ki hiivyo kutoa data zangu personal kiasi hicho, ila cha ajabu, baadhi ya watu hapa mkasema ni sahihi kabisa. Sasa iweje tena leo mnaona sio sahihi kutekeleza jambo kama hilo kwa BoT? Au tofauti ni ipi??
 
Hili ni very interesting concept... au wanajua kuna watu hawatojaza hizo forms au kuprovide hizo taarifa zote? Hivi mtu akikataa kujaza au kuwapatia hizo taarifa what happens to his moneys?

Your money will be safe,but you will be blocked to access till you provide such informations.And this runs to the deadlines after that the assumption will be these money belongs to criminals.will be seized and other investigations will follow
 
Kwa mtazamo wangu mimi BOT wana target ya watu wao wanaowajua. Watu hawa wameshikilia zaidi ya 30% ya amana na sasa wanatishia kuzihamishia nje ya nchi. Hili limewashitua na kukurupuka kuona jinsi ya kuwabana. Kwa kuwa serikali inawaogopa sana watu hawa imeona njia pekee ya ama kupata huruma yao ama kuwashawishi wasihamishe amana nje ya nchi ni kuonesha kuwa wao si target na kulifanya zoezi kuwa la kitaifa.

Zoezi hili haliwatarget wafanyakazi wa serikali na kampuni kubwa zinazofuata sheria ambazo ndiyo base kuu ya kodi kwani mishahara yote hulipiwa bank. Zoezi hili linawahusu wale walioingiza watu madarakani na kisha kufaidika na mikataba ya serikali na sasa wanatishia kuhamishia hela zao nje kitu ambacho kitaiacha nchi katika mgogoro mkubwa wa kiuchumi na hivyo kusababisha hata instability kama serikali ikishindwa ku-meet its maturing obligations (dafaulting govt).

Tatizo kubwa ambalo serikali inalipata leo hii na Bank kuu ni kushindwa kusimamia uchumi. Tanzania kuna makampuni madogomadogo mengi ambayo yanaweza kufanya kazi na kama watalipwa wataendelea kutumia pesa nchini kuliko kuwapatia vultures and sharks ambao wanachumia Tanzania na kulia offshore. Hela inamilikiwa na watu wachache ambao hawana matumizi nayo na kuihifadhi tu, hili ndilo kosa la BOT. BOT wakiacha politics na kufanya kazi zao hakutakuwa na haja ya kukusanya taarifa za wauza nyanya wanaohifadhi mitaji yao bank.

Tatizo linaloikabili Tanzania leo hii ni kwamba kila kitu kinaangaliwa kisiasa, nani mfadhili wa CCM, huyo anakuwa safe hata kama nchi inafilisika. Huu ni ukoloni mamboleo ambao nchi imeingia bila kujijua, watu wanaachiwa kufanya madili ya kifisadi kwa kuwa tu some of the money will go back to assist the ruling party retain its power. Hapa kuna issue kubwa zaidi ya kujua nani anafanya nini na ana kipato gani. Nafikiri na suala la kumpata gavana wa bank kuu nalo liwekwe wazi kwenye katiba mpya ili kumuondolea rais ukiritimba wa kuweka wazi kimasilahi ya siasa zaidi ya masilahi ya nchi.
 
Hili ni very interesting concept... au wanajua kuna watu hawatojaza hizo forms au kuprovide hizo taarifa zote? Hivi mtu akikataa kujaza au kuwapatia hizo taarifa what happens to his moneys?

MM, Kwanza hii thread siyo ya jukwaa hili, ila kwa heshima yako nitaendelea...
Its simple, kama hufanyi hicho wanachotaka ... utaenda tu kwao, maana wataiblock acc yako then hautakuwa na jinsi zaidi ya kufanya wanachotaka..
Pia hawa jamaa, kama mchangiaji m1 alivyochangia hapa, wanayo syetem yao moja ambayo ina-link na mabenki ya kawaida (private) ambayo kwa mteja akiwa hajafanya any tranzaction kwa kipindi kinachozidi miezi sita ile acc inakuwa in-active mpaka tu... muhusika au jamaa yake aingize au kutoa pesa ndo inakuwa activated
SASA kwa kesi hii...kwa kuwa nchi hii inaongozwa na wezi, nahisi ZIPO ACC ambazo hata baada ya kuwa domant, kwa muda mrefu bado zinashikilia hela nje ya mzunguko....sasa wanawatega watu waje kuleta taarifa, incase kama taarifa hazitafika juu ya baadhi ya acc , tena zile ambazo ni domant, hawa JAMAA WATAFANYA EPA ingine.
Tusubili... na ninahisi hii ndo target yao
 
Your money will be safe,but you will be blocked to access till you provide such informations.And this runs to the deadlines after that the assumption will be these money belongs to criminals.will be seized and other investigations will follow

Jambo hili halitawagusa kabisa WAKINGA na WAPEMBA, maana wao suala bank halina mashiko....hela kaa nayo mwenyewe maana uliitafuta mwenyewe
 
Back
Top Bottom