Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,742
- 40,872
Na. M. M. Mwanakijiji
Baada ya Donald Trump kuchaguliwa kama Rais wa 45 wa Marekani siyo watu wote ndani ya serikali yake na kwenye chama chake walikubaliana naye. Kuna ambao walimpinga kuanzia alipotaka kugombea na wengine walimpinga baada ya kuchaguliwa. Ndani ya serikali yake kuna watu ambao waliikataa misimamo mbalimbali ya kiutendaji na kisera ya Trump kiasi kwamba hawakuwa tayari kufanya naye kazi.
Misimamo ya Trump ambayo imewakwaza wengi ni pamoja na ile inayohusiana na sera zake za uhamiaji, mazingira, ulinzi na usalama na hata mambo yanayohusiana na tabia yake ambayo baadhi ya watu wanaiona ni ya kibabe na yenye kutukuza mfumo dume. Tangu aingie madarakani wapo wafanyakazi na watendaji mbalimbali ambao waliamua kuachia kazi zao – wengine wakiwa wametumikia muda mrefu tu – ili kupinga kufanya kazi chini ya mtu ambaye hawamkubali kisera na kitabia. Nitatoa mifano michache tu.
Edward Price – Msemaji wa Baraza la Usalama la Taifa na Afisa wa CIA. Yeye alijiuzulu kupinga jinsi Trump alivyotoa nafasi kwa mshauri wake wa mikakati kuingia katika Baraza la Usalama na kuwaondoa baadhi ya majenerali. Akiandika kwenye gazeti la Washington Post, Price anasema hakudhania kuwa angefikia uamuzi wa kutoka CIA lakini sababu ya Trump aliamua kuachia ngazi. Hakuwa tayari kufanya kazi chini ya Rais ambaye anapuuzia taarifa za kiinteligensia.
Mustafa Ali – Afisa katika Idara ya Mazingira ya Marekani (EPA) ambaye alitumikia idara hiyo kwa miaka ishirini aliamua kujiuzulu wiki iliyopita kupinga mpango wa Trump kukata bajeti ya idara hiyo. Chini ya Trump bajeti yake ya mwaka huu kwa idara hiyo itakatwa kwa karibu asilimia 25 jambo ambali Ali hakuwa tayari nalo na aliona amepingana mno kimtazamo na Rais wake na hivyo aliamua kujiuzulu.
Mifano hiyo miwili ni ya watu wa serikalini; wapo wengine wengi pia. Ndani ya chama chake vile vile wapo watu ambao walimkosoa Trump na hawakuwa tayari kuendelea naye ndani ya chama. Mifano miwili hapa inatosha kuitoa.
Beth Fukumoto – Mnadhimu wa Kambi ya Upinzani kwenye jimbo la Hawaii aliamua kujiondoa ndani ya chama cha Republican kufuatia shinikizo la viongozi wa chama chake baada ya yeye mara kadhaa kumkosoa Rais Donald Trump. Kwenye maandamano ya wanawake yaliyofanyika Januari 21 (siku moja tu tangu Trump aapishwe) Fukumoto alizungumza kwenye maandamano hayo na kumuita Trump mbabe. Chama chake kilijaribu kumuasa lakini hakuwa tayari kunyamaza na hivyo kuamua kuhama meli.
George Willis – Mmoja wa sauti za wahafidhina wa Marekani ambaye alikuwa maarufu sana na kwa muda mrefu akiandika makala mbalimbali za kisiasa. Mshindi wa tuzo ya Pulitzer na mwandishi wa muda mrefu aliamua kuachana na Republican. Trump mwenyewe aliandika kwenye mtandao wa Twitter kupuuzia kujiondoa kwa George Willis.
Mifano hii ya aina mbili inanirudisha kwenye kichwa cha habari. Kuna watumishi na watendaji ndani ya Serikali ya Rais Magufuli ambao hawakubaliani naye – ama kifalsafa au kiutendaji au hata kiitikadi lakini bado wanataka kuendelea kuwa watumishi. Vile vile ndani ya Chama cha Mapinduzi.
Wengi tunakumbuka jinsi gani katika Mkutano Mkuu wa CCM uliompitisha mgombea wake wa Urais mwaka 2015 jinsi mbele ya Mwenyekiti Kikwete na uongozi wa juu wa chama hicho kundi la wajumbe liliposimama kuimba ‘Tuna imani na Lowassa’ wakionesha kukasirishwa na kitendo cha Kamati Kuu kuengua jina la Lowassa na hivyo kutengeneza njia nyeupe kwa John Magufuli. Ni wazi kuwa wajumbe wale hawakuwa na imani na Magufuli na walijionesha hivyo wazi. Siyo Magufuli tu kwa kuimba kwao walikuwa hawana imani na Kamati Kuu.
Tunakumbuka jinsi baada ya taarifa ya aliyekuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi ya CCM Nape Nnauye kutangaza majina yaliyopitishwa kwenda kwa Mkutano Mkuu jinsi Dkt. Emmanuel Nchimbi akiwa na Sofia Simba na Adam Kimbisa walivyosimama kupinga jinsi ukataji wa jina ulivyofanyika. Wote walikuwa wanajulikana ni mashabiki wa Lowassa. Wengi tunakumbuka jinsi Sofia Simba katika kumpamba Lowassa alisema mwaka 2009 wakati akimtetea Lowassa bungeni; maneno ambayo aliyekuwa mjumbe wa Kamati ya Richmond Lucas Selelii aliyaita yanafaa kwenye “kitchen party”.
Lakini pia tukumbuke kuna wengi waliojitokeza kwa maelfu kumuunga mkono Lowassa katika safari yake ya “matumaini” kuelekea Ikulu. Wengi walijiunga naye na wakaja hata na msemo wa “ulipo tupo” na Lowassa alipokatwa jina lake wengi walitarajia maelfu waliofuatana naye kwenye safari ya kutafuta wadhamini wangeamua kuungana naye huko kwa jirani. Na inawezekana hili lilitokea kwenye sanduku la kura kwani kupata kura milioni 6 si jambo dogo na halijawahi kufikiwa na mgombea yeyote wa upinzani. Hata hivyo, hawakumfuata kwa kuamua kuachana na CCM na kwenda CHADEMA kama yeye.
Hapa ndipo hoja yangu inapokuja. Wengi waliomuunga mkono Lowassa na ambao hawajawa mashabiki wa Magufuli walipaswa kuonesha kwa vitendo imani yao kwa Lowassa. Hili ni kweli kwa wabunge ambao wanaonekana wazi kumpinga Magufuli na sera yake; mfano mzuri ni watu kama Hussein Bashe. Bashe ni mwanasiasa kijana na machachari na labda ni miongoni mwa wachache ambao wameweza kuikosoa serikali ya Magufuli Bungeni. Ni wazi baada ya kashkash aliyopewa juzi kuelekea Mkutano Mkuu wa CCM umempa somo muhimu. Siyo yeye tu hata mpambe wa kampeni ya Magufuli na Mbunge wa Geita Mjini Bw. Msukuma naye amepata somo.
Kama hawa wote na wengine – wabunge na wajumbe wa ngazi mbalimbali za CCM – wanaamini kabisa kuwa nchi inaelekea kubaya chini ya Magufuli, kama kweli wanaamini Magufuli anaongoza vibaya nchi kwa kusigina Katiba au kuwa na ubabe fulani, hawapaswi kusema na kubakia; wanapaswa kusema na kujiuzulu.
Kujiuzulu huko siyo woga wala hofu; kujiuzulu huku ni misimamo kutofautiana. Nimewahi kuandika mara nyingi sana huko nyuma hasa kwenye masuala ya CHADEMA kuwa endapo viongozi wajuu wanatofautiana ama na chama chao au na uongozi wa juu wa chama chao hawawezi kusema “wanapinga” halafu wakataka kubakia kwenye vyeo vyao. Ni kanuni ya kawaida tu kuwa unapopingana na bosi wako kwenye jambo la msingi tena hadharani ni muhimu wakati huo huo ukajitangaza kujiuzulu nafasi yako.
Ni matumaini yangu kuwa viongozi wote wa CCM wa ngazi zote na hata walioko Bungeni au serikalini ambao hawakubaliani na Magufuli kama Rais au na uongozi na sera zake kama kiongozi mkuu wa chama wanapaswa kujiuzulu nafasi hizo mara moja. Hawawezi kuendelea kukalia nafasi wakati hawaamini katika ajenda, sera au mwelekeo unaotolewa na kiongozi wao.
Kutokujiuzulu ni kuwa kinyonga wa kisiasa. Viongozi hawa hawawezi kutaka kubadilika badilika rangi kila kiongozi mwingine anapoingia ndani ya chama. Walitaka kuwa hivi wakati wa Mkapa, wakawa vile wakati wa Kikwete na sasa wanataka kuwa na rangi nyingine wakati wa Magufuli. Kama wanaamini katika misimamo yao na katika tofauti ya msingi baina yao na Rais/mwenyekiti wao. Ni jukumu lao kujiuzulu nafasi zao.
Nje ya hapo, ni jukumu la Rais na Mwenyekiti wa chama chao kuhakikisha kuwa wanaondolewa ndani ya chama na serikali. Hii ni matunda ya demokrasia, ni zao la utawala wa pamoja na wa msimamo mmoja. Kama huamini ambayo chama kinaamini na kinataka kutekeleza ni jukumu lako kujiondoa. Ukweli huu siyo kwa CCM tu bali hata kwa vyama vingine vya kisiasa au vya kijamii. Kama hukubaliani na viongozi wako wakuu au kiongozi wako mkuu, ni jukumu lako kusema kuwa hukubaliani naye, na ukishasema hadharani hukubaliani naye basi jambo moja tu limebakia kufanya.
Kujiuzulu.
Niandikie: mwanakijiji@jamiiforums.com
Katika toleo letu la pili la majaribio la gazeti la Zama Mpya kuna mengi - habari na makala. Makala yangu mimi inahoji kama wana CCM hasa viongozi na watendaji wa ngazi mbalimbali wanaopingana au wasiokubaliana na Rais/Mwenyekiti John Magufuli wanapaswa kuachia ngazi zao badala ya kusubiri kufukuzwa uanachama au kupewa adhabu kama watoto wa shule! Jipatie nakala ya gazeti lako hili jipya bure kabisa (wakati huu wa majaribio - tunaendelea kuliboresha kabla ya kuanza kutokea mitaani):
Ukurasa wa Mbele:
Ukurasa wa Nyuma