Ziwa Victoria, Nyasa na Tanganyika yafanyiwe Hydrographic Survey na kutengenezewa ramani (Navigation Charts)

Offshore Seamen

JF-Expert Member
Mar 9, 2018
4,930
12,474
Kwanza nitoe pongezi kwa serikali kwa ujenzi wa meli katika Ziwa Nyasa na Ziwa Victoria na marekebisho ya meli zilizokuwepo.

Kwa kipindi kirefu ramani (Navigation Chart) ambazo zimekuwa zikitumika Ziwa Nyasa ni za zamani sana, hivyo inapaswa hydrophic survey ifanyike na zitengenezwe ramani mpya.

Ziwa Victoria napo ramani ni ya muda; inabidi itolewe mpya. Ziwa Tanganyika vyombo vingi hawatumii hizi chati, vyombo huongozwa kwa alama na uzoefu wa watu ziwani au baadhi hutumia GPS.

FAIDA YA KUFANYA HYDROGRAPHIC SURVEY
1. Hii itasaidia kuonesha maeneo hatari wakati wa uongozaji vyombo majini.
2. Kuonesha sehemu zenye makatazo ya kupita vyombo au kufanya shughuli za kibinadamu mfano uvuvi au kuogelea.
3. Kurahisisha uongozaji wa meli sababu ya kuwa na ramani ambayo ni sahihi.
4. Pia huonesha maeneo yaliyotengwa kimazingira au kazi maalumu.
5. Kuonesha sehemu sahihi za vyombo kuweka nanga.
6. Kuainisha sehemu za michezo ya majini, mfano Ziwa Victoria sehemu nyingi zina miamba ikitengenezwa ramani itaonyesha sehemu zilizo salama.
7. Kuonesha maeneo yenye upepo, mawimbi na mikondo ya maji.

Ramani itabaki kuwa na umuhimu ingawa sasa kuna matumizi ya GPS ila katika sekta ya majini ramani ya kuchapishwa ni lazima iwepo melini na kutokuwa nayo ni kosa kisheria.

Hivyo mamlaka husika (TPA) itumie wataalamu kufanya survey na kutengeneza hizo ramani.

Haya maziwa yakifanyiwa Survey huu uwekezaji utakuwa na tija zaidi sababu usalama utakuwa mkubwa sana maana meli zitakuwa zinatumia ramani ya sasa yenye taarifa sahihi.

USALAMA KWANZA
 
Back
Top Bottom