Zitto Zuberi Kabwe ndiye mpinzani wa kweli Tanzania na aliye imara

Ushauri wangu waungane mgombea abakie lissu kwa sababu anauzika kirahisi( alinusurika na kifo ) wakishinda PM awe zitto.

Hapo kwa membe akili inakataa.

Kimsingi hata ikitokea wakaungana, bado Zito ndio sahihi hata kama Lissu ana mvuto zaidi. Tatizo ni kuwa Lissu ana kesi nyingi hivyo ni lazima watazitumia kumuweka ndani mpaka uchaguzi upite.
 
Kimsingi hata ikitokea wakaungana, bado Zito ndio sahihi hata kama Lissu ana mvuto zaidi. Tatizo ni kuwa Lissu ana kesi nyingi hivyo ni lazima watazitumia kumuweka ndani mpaka uchaguzi upite.
Ukweli ni kwamba Zitto asingeondoka CHADEMA angekuwa mwanasiasa tishio sana kwa ccm kuliko mwanasiasa mwingine yeyote aliyewahi kutokea katika taifa hili.

Pamoja na nguvu ya hoja aliyonayo Zitto toka ameondoka Chadema umma unamtazama kama busy body tu ambaye hana focus na mwelekeo wowote zaidi ya mtafuta ugali.

Tatizo jingine itikadi ya ACT wazalendo haimbebi sana Zito hasa ukizingatia kuwa ACT ni pro ujamaa wakati CHADEMA ni centrilist wenye mlengo wa social democracy hoja nyingi anazojenga Zitto huwa zinamlengo wa Social Democracy kuliko ujamaa ambao umechukua nafasi kubwa sana katika itikadi ya ACT.

kama wataungana watakuwa kwenye mtanziko mkubwa sana wa nani asimame kama mgombea wa upinzani hasa ukizingatia ACT wanataka kujitanua na CHADEMA wanataka kumaintain status quo yao, ACT hawana ushawishi sana huku bara kiasi cha kupewa nafasi ya kusimamisha mgombea ubunge itakuwa changamoto wapewe jimbo lipi ukiondoa jimbo la Zito peke yake.

Kiushawishi wa hoja Lissu na Zitto hawatofautiani sana japo mmoja ni Romanticist na mwingine ni Realist, Lissu ni mwanaharakati wakati Zitto ni mwanasiasa halisi.

Yapo maeneo mengi ya kuwapima hawa watu lakini madam Zitto hayuko CHADEMA itakuwa ngumu sana kupewa nafasi ya kugombea urais kupitia CHADEMA.
 
Hakuna mtu mnafiki km zito Tanzania bora hata Mbowe
Chadema wameshasahau
FB_IMG_15917229921781608.jpg
 
Ye mwenyewe anamzimia mbowe afu ww unasema yeye ndo bora
Toka nimfahamu zitto zuberi kabwe hajawahi kabisa kuniangusha

Amekuwa mwanasiasa makini sana mwenye kujenga hoja zinazoeleweka na zenye tija kwa taifa letu la Tanzania.

Sote tunafahamu zitto zuberi kabwe alifukuzwa CHADEMA na kujiunga na ACT wazalendo.

Pamoja na kufukuzwa uanachama hakuwahi kutoa kejeli Wala matusi kwa chama kilichomfukuza kama tunavyoona kwa akina Silinde na Lijualikali ambao wamefukuzwa uanachama wa CHADEMA.

Mh Kabwe Alikuwa na uwezo wa kuhamia chama tawala lakini hakuwahi kufanya hivyo ingawa profile yake ilikuwa kubwa Sana kisiasa.

Alijiunga na ACT Wazalendo ili kuimarisha upinzani kwani upinzani imara ndio nguvu ya taifa.

Mh Kabwe ameonesha kuwa ni mwanasiasa wa upinzani mwenye ukomavu wa hali ya juu kwani ameendelea kukiunga mkono chama Cha upinzani kilichomfukuza na ameonekana kuwa bega kwa bega katika kila tatizo ambalo chama chake Mama kinapitia pamoja na kuwa kilimfukuza.

Hakuna ubishi kuwa kwa Sasa mpinzani anaeweza kujenga hoja na kuitetea kwa masilahi ya taifa letu Ni mh Zitto Zuberi Kabwe.

Sote tunalifahamu sakata la mkopo wa elimu kutoka world bank lilivyokuwa na mpaka lilipoishia.

Nahitimisha kwa kusema mh Zitto Zuberi Kabwe ndiye mpinzani wa kweli na aliye imara kuliko yeyote mwingine hapa nchini.
 
Back
Top Bottom