Zitto: Watu wanaishi maisha ya uwongo na Fitna, Sina tatizo na Dr. Slaa

Zitto Kabwe unazidi kuwachanganya wafuasi wako, ni Bora ukanyamaza..
 
Wakuu mimi naona tufanye tufanyavyo slaa ameingia kwenye mtego wa kumchokoza zitto hawezi kukwepa kumkabili lakini kibaya zaidi dr slaa siyo saizi ya zitto zitto ni mwanasiasa wa ngazi ya juu sana kama akiamua kumjibu slaa hata wiki haiwezi kuisha slaa atakuwa hayupo kwenye siasa.

Umeandika habari ya kusadikika
 
Tatizo la zitto haeleweki, je kama hayo aliyosema ni sahihi, kwa nini hakuyasema kwenye mikutano yake ya hadhara? Je kwa nini asingepinga yale mabango yanayotukuza mtu(yeye) badala ya chama? Binafsi simuelewi zitto hata!
MMMh Mbona hamkuishauri KK kuwa kuna watu ni muhimu ndani ya CHAMA? Yaani KK ifanye maamuzi, watu waamue kujitenga nayo, alafu tumwambie Zitto awalazimishe watu wabebe mabango ya kuisifia KK kwa maamuzi ambayo hawakubaliani nayo?? Uliza CHASO, Ulizia KK ya Mkoa ya Mbeya mbona kwenye matamko yao ya kuunga mkono maamuzi ya KK (Taifa) hawakusema kuwa wanatambua Mchango wa Zitto? Kwanini hawakushauri KK pamoja na mashtaka na tuhuma 11 walizomwandalia Zitto basi wangesema na Positive contribution ya Zitto?? Kimsingi hoja ya Kusema Zitto angewakataza sijui angewashauri ni hoja inayoendekeza udikiteta kwamba watu na wanachama hawana uwezo wa kufikiria na kuamua kufanya lile wanaloona ni jema kwao mpaka waambiwe na Zitto.
 
Ungetuonyesha Zitto kafanya kitu gani kikazaa matunda ndani ya CDM na nje ya Chama (Serikali) tungeelewa ni mwanasiasa wa ngazi ya juu.
Ukiwauliza vijana wote walioko ndani ya CHADEMA watakuambia walianza kupenda siasa kutokana a Zitto (Muulize Joshua Nassari), Mtandao wa CHADEMA vyuo vikuu ni juhudi za Zitto, Maandamano ya kwanza ya CHADEMA yenye ajenda ya Kitaifa yaliitishwa na wananchi kussuport ajenda ya Zitto (Buzwagi Saga) na baada ya hapo CHADEMA iliadopt strategy ya Maandamano.
 
Usipotoshe sababu za Zitto kuvuliwa madaraka. Hakuvuliwa madaraka kwa kuwa na mawazo tofauti na Mbowe bali kwa usaliti dhidi ya chama ambao ameufanya kwa kipindi kirefu na ushahidi wa kutosha upo. Usifikiri kamati kuu ya CHADEMA ilikurupuka bali ilifanya maamuzi baada ya kuupitia ushahidi dhidi ya Zitto kwa kituo. Hilo la kudai alitofautiana na Mbowe na propaganda chafu za MACCM.
Uko wapi Huo Ushahidi? Katika Tuhuma 11 alizopewa hakuna tuhuma ya USALITI, hii umeitoa wapi mkuu??
 
Ukiwauliza vijana wote walioko ndani ya CHADEMA watakuambia walianza kupenda siasa kutokana a Zitto (Muulize Joshua Nassari), Mtandao wa CHADEMA vyuo vikuu ni juhudi za Zitto, Maandamano ya kwanza ya CHADEMA yenye ajenda ya Kitaifa yaliitishwa na wananchi kussuport ajenda ya Zitto (Buzwagi Saga) na baada ya hapo CHADEMA iliadopt strategy ya Maandamano.
bila Chadema madhubuti . ....buku saba zingetoka wapi pale Lumumba
 
Hana lolote mnafiki huyo aende zake ccm hawezi kutuambia et anajenga chama kwa mabango ya kujitukuza km zitto ni zaidi ya chama! Ina maana yeye ni zaidi ss wanachama? Make chama ni wanachama,wapuuzi ndo maana unaweza kushangilia upuuzi km huu wa zitto na ccm yake
 
Wewe ndo umechanikiwa, Zitto yuko smart na anajua analolifanya kwa ajili ya maslai ya taifa si ya Chama. Taifa kwanza chama baadaye.
 
tatizo ni kukosa nguvu ndani ya chama katika maamuzi lazima achanganyikiwe ndomaana yuko hivyo lazima atapetape
 
siasa za haka kajamaa bwana..... zinaleta mpaka kinyaa....

sijawahi one mtu wa ajabu ajabu kama haka kapuuuzi.
 
siasa za haka kajamaa bwana..... zinaleta mpaka kinyaa....

sijawahi ona mtu wa ajabu ajabu kama haka kapuuuzi.
 
Yale majina ya mafisadi walioficha fedha Uswis alishayatajaa.....na vp kuhusu ripoti ya North Mara alishawasilisha Bungeni manake yeye ilikua ya zamani kuliko hii ya Mh. Lembeli..
 
Zito Umeiandikia Kamati Kujibu Tuhuma ama mashtaka

Subiri maamuzi na sio kujitabiria hukumu
 
Back
Top Bottom