Zitto: Watu wanaishi maisha ya uwongo na Fitna, Sina tatizo na Dr. Slaa

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,566
2,000
Zitto Kabwe

Tatizo la baadhi yetu ni kuishi maisha ya uongo na fitna. Sina tatizo na Dr Slaa. Ni Katibu Mkuu wa chama na amefanya mengi mazuri kufikisha chama hapa.

Sasa hivi watu wanajitahidi sana kuchochea kwa kugeuza maneno ionekane kwamba nina tatizo na Katibu Mkuu wangu. Ziara yangu Kigoma haikuwa 'kumjibu Dr Slaa' kama inavyosemwa. Sina cha kumjibu Katibu Mkuu wangu.

Ninalo jukumu kama mwanachadema kutoa maelezo kuhusu tuhuma dhidi yangu na pia kuongea na wananchi kuhusu matatizo ya nchi yetu. Hayo sio majibu kwa Dr Slaa kwa sababu ni uonevu kusema Dr Slaa ni Kamati Kuu.

Mimi nitaendelea kutumikia wananchi wa Kigoma na watanzania wote kama mwanachadema na Mbunge. Anayesema naidhoofisha Chadema ni muongo na apuuzwe.
 

mjepo

JF-Expert Member
Aug 8, 2013
4,917
1,225
Wakuu mimi naona tufanye tufanyavyo slaa ameingia kwenye mtego wa kumchokoza zitto hawezi kukwepa kumkabili lakini kibaya zaidi dr slaa siyo saizi ya zitto zitto ni mwanasiasa wa ngazi ya juu sana kama akiamua kumjibu slaa hata wiki haiwezi kuisha slaa atakuwa hayupo kwenye siasa.
 

ungonella wa ukweli

JF-Expert Member
Mar 27, 2012
4,213
0
Tatizo la Zitto haeleweki, je kama hayo aliyosema ni sahihi, kwa nini hakuyasema kwenye mikutano yake ya hadhara? Je kwa nini asingepinga yale mabango yanayotukuza mtu(yeye) badala ya chama? Binafsi simuelewi zitto hata!
 

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
105,176
2,000
Hana nguvu yoyote ile amechanganyikiwa tu anabwabwaja bila mpango.

Kwa sasa zito ndiyo kapata nguvu mara dufu madereva wa zitto ni wale waliomchagua pamoja na wote wapenda demokrasia angalia picha kwenye mikutano yake yankigoma ndipo utajua kuwa zitto ni nani ndani ya chadema na katika siasa za nchi hii.
 

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,566
2,000
Wakuu mimi naona tufanye tufanyavyo slaa ameingia kwenye mtego wa kumchokoza zitto hawezi kukwepa kumkabili lakini kibaya zaidi dr slaa siyo saizi ya zitto zitto ni mwanasiasa wa ngazi ya juu sana kama akiamua kumjibu slaa hata wiki haiwezi kuisha slaa atakuwa hayupo kwenye siasa.

Wacha mambo yako Dr. Slaa kweli umlinganishe na Zitto?? Kama Zitto ni bora atoke akaanzishe chama chake na awe mgombea wakutane kwenye Sanduku.

Zittp ni ndinakuwili kama Jk anataka kupendwa kote kote CCM na CDM
 

KirilOriginal

JF-Expert Member
Feb 13, 2012
2,148
2,000
Swali je kwa nini kwenye majimbo ya wabunge wa ccm waliowajibishwa hatujaona maandamano na bendera kuchomwa? ccm manafiki mapandikizi Iacheni Chadema ifanye kazi yake
 

AlP0L0

JF-Expert Member
Apr 23, 2011
5,073
2,000
Tatizo la baadhi ya CDM wanamapenzi ya upofu, hii insue inampandisha sana ZZK na imesha mporomosha sana Dk Slaa.Majibu anayotoa ZZK yanaeleweka kuliko porojo za Dk Slaa.

NALIONA WAZI ANGUKO LA DK SLAA
, Dk Slaa hana ubavu wa kupambana na ZZK hii kila mwenye mawazo huru analiona.
 

Abdillahjr

JF-Expert Member
Oct 3, 2011
694
0
Anachoongea Zitto sicho anachokitenda na ikumbukwe alama za mnafiki ni tatu na Zitto ni zaidi ya mnafiki na msaliti bali ni ndumi la kuwili wa hovyo saana!!
 

Daudi Safari

Verified Member
Oct 5, 2012
327
250
Je, Zitto ana tatizo na kamati kuu? Maana yale matusi aliyoyaporomosha pale ujiji kwa kamati kuu ni dhahiri ana tatizo either na Mbowe ama Kamati kuu, ama Dr
 

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
105,176
2,000
Inampandisha kwa MACCM na si kwa CHADEMA anaonekana ni mnafiki tu anayebwabwaja bila mpango. Kama inampandisha kwanini MACCM msimchukue!? Mbona hamumkaribishi kwenye chama chenu na wakati mnamuona ni maarufu kuliko CHADEMA!? Mbona rafiki yake Kafulila kule NCCR hamkaribishi ili akaongeze nguvu ya chama!? Acheni kukurupuka bila kutafakari kwa kina.

Tatizo la baadhi ya CDM wanamapenzi ya upofu, hii insue inampandisha sana ZZK na imesha mporomosha sana Dk Slaa.Majibu anayotoa ZZK yanaeleweka kuliko porojo za Dk Slaa.NALIONA WAZI ANGUKO LA DK SLAA , Dk Slaa hana ubavu wa kupambana na ZZK hii kila mwenye mawazo huru analiona.
 

Adharusi

JF-Expert Member
Jan 22, 2012
13,928
2,000
Tatizo la zitto haeleweki, je kama hayo aliyosema ni sahihi, kwa nini hakuyasema kwenye mikutano yake ya hadhara? Je kwa nini asingepinga yale mabango yanayotukuza mtu(yeye) badala ya chama? Binafsi simuelewi zitto hata!
Ungeenda Kutengeneza wewe ilo bango la Chama
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom