Zitto: Watanidharau, watanicheka, watapambana lakini nitashinda!

Mtu yeyote makini ambaye kapitia makala ya Zitto lazima atajifunza kitu muhimu zaidi ya hapo itakuwa ni chuki, nadhana hata Mwambo kakusoma...pambana Zitto ndoto zako zitafanikiwa.

i concur with u
 
Wanajamii,

ZZK ametoa maelezo yake ya utetezi. Nadhani ni utetezi mzuri. Busara
ingetutuma tujadili utetezi huo badala ya kumjadili yeye binafsi. hapa
tunatoka nje ya mjadala. Nashauri turejee huko. Vinginevyo tusiendelee
kulalama kwamba taifa halipati chochote kutokana na raslimali zake
nyingi. Hii ndiyo hoja ya ZZK pamoja na mfano wa kampuni ya kirusi
inayotka kuvuna urani yetu bila kulipa kodi inayostahili na hali watoto
wa shule za msing wanakaa chini, sekondari hawana maabara, hospitali
hazitoshi na zilizopo nyingi hazina vifaa vya kupimia, watabibu nk.
Aidha bajeti ya serikali imeendelea kuwa tegemezi wakati taifa halina
viwanda vya kulisaidia kuingia katika ushindani wa karne ya 21.

Wakati makampuniya kigeni hayalipi kodi zinazotakiwa, wenyeji wakamuliwa
kwa kodi zakila aina pamoja na VAT. Tunalalamika sana kwamba viwango
vya kodi ni vikubwa lakini hatutaki kukuna vichwa kupanua wigo kwa
kutoza haya makampuni yanayovuna raslimali zetu bure. Changamoto ni
nyingi, na madini yetu yangetuwezesha angalao kufanya zaidi na kwa kasi
kubwa. Hii ndiyo hoja ya ZZK. Kwa nini tunasita kuijadili?

Mkuu umenena, wana bodi tujikite kwenye kujadili hoja na sio mleta hoja.
 
Nimewahi kusoma na vijana wengi kutoka Kigoma wakati nikiwa sekondari, na pia Chuoni. Nilichokuja kugundua wachache wanatabia ya usaliti wakiweka mbele masilahi binafsi. Wako ladhi kumsaliti yeyote na kuvujisha siri za ndani kabisa ili mradi tu waweze kufikia malengo yao.

Kulikuwa na katibu mkuu wa Chadema - Dr Walid Amani Kaborou, huyu usaliti wake kwa upinzani kila mmoja anauelewa. Amekuwepo pia Daniel Nsanzugwanko wa NCCR. Huyu pia anajulikana kwa usaliti wake. Kafulila amejaribu Chadema, akashindwa, NCCR pia ameshindwa. Hawa ni wachache, lakini pia kule chuoni alikuwepo rafiki yangu kutoka Kigoma ambaye kwa hakika alikuwa ni msaliti wa aina ile ile kama akina Walid Kaborou, siwezi kusimulia sana juu yake

Zito Kabwe ni msaliti na anajli zaidi maslahi binafsi. Baada ya kujipatia umaarufu, akiwa kijana kati ya Vijana wachache ndani ya bunge, akaweza kukaa karibu na rais na kukutana na viongozi mbalimbali duniani akaona anaweza kufanya lolote bila kujali amewezaje kufika hapo alipo.

Zito ni msaliti. Mtakaumbuka 2010 wakati wa kampeni, badala ya kumkampenia mgombea urais wa Chadema yeye alikuwa akitangaza kuwa 2015 atagombea urais. Kwa mwenye akili anaelewa huyu kijana namna gani vipi!

Zito huyu huyu, wakati wa vuguvugu la kutangaza matokeo ya urais, yeye yuko bize na Jack Zoka, afisa usalama anayeshughulika na siasa. Na walikuwa wakiwasiliana mara kwa mara. Hapa shaka kuu ipo kwa huyu bwana mdogo.

Zito, wakati wenzake wanaimarisha chama, yeye anajitangazia kugombea urais na hata siku moja hajawahi kushughulika na harakati za M4C. Kuna jambo hapa. Ikiwa anataka urais kupitia chadema ataupataje akiwa chama kitabaki kuwa cha msimu.

Zito Kabwela, anafahamu fika kuwa, enzi hizo alikuwa na nafasi kubwa ya kuweza kushika madaraka ya juu ndani ya chama na hata ya nchi ikiwa chama kingeweza kufanya vizuri katika uchaguzi mkuu siku zijazo. Lakini sasa matumaini hayo yanafutika taratibu baada ya kuona kuna Vijana wengi, wenye maono na uwezo mkubwa pengine kushinda hata yeye wameibuka chadema. Mfano Tundu Lissu, John Mnyika, Godbless Lema, Benson Kigaila na wengine. Sasa kwa kuelewa hili na kwa sababu za ubinafsi na usaliti anajaribu kutafuta namna ya kukivuruga chama, akiondoe kwenye lengo la msingi la kuimarisha uhai wa chama.

Zito Kabwe, atakuwa ndumila kuwili. Anatumwa na kutumiwa na pia ana tabia ya kujipendeza kwa wenye madaraka.

Conclusion: Zito anajiona anaweza, lakini namhakikishia hataweza. Kaborou alikuwa maarufu kumshinda yeye, Mrema (Augustino) alikuwa maarufu kumshinda yeye, lakini leo yupo wapi.

Kama ilivyo kwa wakristo, Yesu Kristo aliwaambia mitume wake "Sikuwachagua mitume 12 na mmoja wenu ni shetani?"

Wito wangu kwa WanaChadema, mjue kuna Viongozi wengi lakini miongoni mwao kuna wasaliti na mmoja wao ni Zito Zuberi Kabwe. Kwa mataendo yake kwa ustawi wa chama anajidhihirisha wazi.

Chadema, nawasihi muishi na huyu mtu kama mlivyoweza kuishi hata na Shibuda, mwisho wa siku ataamua kujinyonga mwenyewe kwani anguko lake litakuwa kubwa na la aibu.
Umetumia busara nyingi sana mkuu, mifano uliyotoa Ni hai. Mie napenda siasa za zitto lakini naona anakurupuka sana kutoa kauli. Mbona wenzake hawasemi kuhusu urais?
Ukiacha urais, zitto kaongea point kubwa sana kuhusu mdini na mafuta. Kijana Ni jembe
 
mpango wa Mungu haimaanishi kuwa ni mpango wa dini, Mungu sio muislamu wala mkristo kwa hiyo mpango wa mungu ni mpango wake kwa watu wake aliowaumba.
 
Mushi narudia nilichosema, tujadili sera sio watu. Zitto kazungumzia sera tupu kuhusu wizara, waziri, mikataba, leseni na mengineyo.
Alipotaja majina ya watu ni kwa kuwa alikuwa anachallenge fikra zao na athari zake katika sera. Na alichokisema Zitto kiko wazi kabisa. Hakuna persona attacks, na kazungumzia mwenendo wa mambo toka kitambo

Unaongeaongea ukirudiarudia na kumuattack Zitto, which is absolute ridiculous, and is what is unnecessary. Nitakuelewa ukizungumzia na kuchallenge mtazamo, utendaji wake kisera kama uko sahihi au la at the interest of we the citizents. Zitto hana habari na mtu, siku zote anachallenge sera na mifumo ya serikali na siasa ili iwe na maslahi kwa mwananchi wa kawaida, na sisi wote tufanye hivyo. Sio kuanza kujafilijadili watu, chuki binafsi tu, kama unaona na wewe una uwezo kuwa rais tangaza nia hagombwi mtu, titapima sera.
Zitto amezungumzia sera hapo juu?Hakuna kinachojadiliwa na members kwenye mjadala huu ambacho ni nje ya mada husika.

Amezungumzia kuhusu urais,na pia kujibu issue zilizoelekezwa kwake yeye binafsi,zingatia bold...unasema watu wasizingatie personal issue na wakati yeye kaziweka kwenye hiyo mada hapo juu?Amezungumzia "makala tatu zote dhidi ya Zitto",na hapo hakuna ubinafsi? ni upofu wako wewe mwenyewe na kuwazuia wana jamvi wasijadili mada iliyoko mbele yao ndiyo unakusumbua.


Hata wakati mkwaruzano wake na Muhongo ulipoanza,na pale Muhongo alipotoa shutuma za rushwa dhidi yake, na ambazo ziko kwenye uchunguzi baada ya kuundiwa tume ya Ngwilizi,yeye alihusisha tuhuma hizo na mbiyo zake za urais.Hakuna pahala ambapo alishaweka wazi ni kivipi tuhuma hizo ni mbinu za kumkwamisha kwenye mbiyo zake za urais.Na ndiyo maana sijashangazwa na hatua yake ya kuzijumuisha makala za urais pamoja na ile ya mkwaruzano wake yeye na Muhongo,zote mimi naona ni siasa zake tu licha ya kwamba yeye ndiye
Zitto amezungumzia sera hapo juu?Hakuna kinachojadiliwa na members kwenye mjadala huu ambacho ni nje ya mada husika.

Amezungumzia kuhusu urais,na pia kujibu issue zilizoelekezwa kwake yeye binafsi,zingatia bold...unasema watu wasizingatie personal issue na wakati yeye kaziweka kwenye hiyo mada hapo juu?Amezungumzia "makala tatu zote dhidi ya Zitto",na hapo hakuna ubinafsi? ni upofu wako wewe mwenyewe na kuwazuia wana jamvi wasijadili mada iliyoko mbele yao ndiyo unakusumbua.


Hata wakati mkwaruzano wake na Muhongo ulipoanza,na pale Muhongo alipotoa shutuma za rushwa dhidi yake, na ambazo ziko kwenye uchunguzi baada ya kuundiwa tume ya Ngwilizi,yeye alihusisha tuhuma hizo na mbiyo zake za urais.Hakuna pahala ambapo alishaweka wazi ni kivipi tuhuma hizo ni mbinu za kumkwamisha kwenye mbiyo zake za urais.Na ndiyo maana sijashangazwa na hatua yake ya kuzijumuisha makala za urais pamoja na ile ya mkwaruzano wake yeye na Muhongo,zote mimi naona ni siasa zake tu licha ya kwamba yeye ndiye aliyemtuhumu Muhongo kuwa ni "siasa za urais"

Angekuwa anataka kuzungumiza sera peke yake,basi angejibu makala iliyozungumzia hayo na si kujumuisha makala za sera na zile zinazohushu yeye kuutaka urais pamoja na vurugu zake ndani ya chama chake....Hilo liko wazi hapo chini,sasa hayo nayo ni sera za maendeleo ya nchi kama unavyotaka kutuaminisha wewe?ama ni ushabiki unakupofua?

Na kabla sijajikita kwenye kujibu hicho unachokiita sera za maendeleo ya nchi yetu,unaweza kuniambia uwazi anaouzungumzia Zitto ni wa aina gani?Ina maana anataka mikataba hiyo iwe wazi na kila mwananchi awe na uwezo wa kuipitia?Hilo swali hajawahi kulijibu na kama unaweza kumsaidia kulijibu,basi fanya hivyo ili tuweze kuona utofauti utakaokuwepo baina ya either mikataba hiyo kuwa wazi ama kupitiwa na TPDC.

Nakumbuka pia kama alivyosema Bulesi,Zitto alishawahi kusema kuwa kuipitia mikataba hiyo, hilo litawafukuza wawekezaji.Hilo linanifanya nitake kujuwa tofauti kati ya kuipitia mikataba vs kuiweka wazi.Maana kuiweka wazi bila ya kutakiwa kuwepo na marekebisho kwa kuipitia upya,sioni kama ndiyo solution dhidi ya mikataba mibovu,na pia sioni kwamba ni kivipi hatua zipi zitachukuliwa.


Yeye anasema Muhongo anataka umaarufu tu kwa kusema hayo maneno,yeye anachokitaka siyo umaarufu?ama pia siyo siasa?Swali langu la msingi linajirudia almost everywhere,yeye anasema eti "mapitio bora" ni uwazi wa mikataba yote tuliyoingia,hivi unaweza kuniambia ana maana gani hapo?Inaonyesha yeye hakatai mapitio,bali anataka kile anachokiita "mapitio bora",na hayo mapitio bora,kwa mujibu wake yeye,yanapatikana kwa uwazi(mikataba kuwa wazi),sasa swali ni lile lile,anaweza kutuambia huo uwazi ni wa aina gani?mapitio bora ni kitu gani?ama ni siasa tu?

Anasema kuwa Muhongo anataka kufurahisha watu na kutafuta umaarufu,sasa swali bado ni lile lile,je hayo mapitio bora yatakayopatikana kwa kuiweka mikataba wazi,yatasaidia vipi hatua kuchukuliwa?pengine akiweka wazi kuwa anamaanisha kitu gani kusema mikataba iwekwe wazi,basi na sisi tutajuwa kwamba ni kivipi mikataba hiyo ikiwekwa wazi, basi hatua zitachukuliwa,(endapo hatua hazitaweza kuchukuliwa baada ya mapitio),so aseme kama mikataba kuwekwa wazi ina maana na sisi wananchi wa kawaida tutaweza kuipitia?(maana tutaishinikiza serikali ifanye hivyo).Na kama sivyo,huo uwazi anaouzungumzia ndiyo upi na ni wa aina gani ili tuweze kuamini kuwa kuna hatua zitachukuliwa?(ama ni uwazi wa kuipitia bungeni kwenye wabunge wengi wa ccm?)

Hapo kwenye bold,tulishamwambia kabisa humu ndani,ila ni yeye anaonekana ni mbinafsi na asiyekuwa msikivu hata kidogo,umimi ukikutawala na ubinafsi,ni wazi unapofuka.Tulisema humu,na mimi nilishasema kwenye mjadala mmoja,kwamba inawezekana kabisa mikataba kuwekwa wazi siyo vibaya,lakini kuipitia napo si suala la kulipinga,sasa hapo juu ametafuna maneno mwenyewe(kama vile hakuona tulichomshauri),amesema "tunapaswa kufanya zaidi ya mapitio ya mikataba",amejikita zaidi kwenye sifa binafsi na kujisahau hata yale anayoyaongea na kujicontradict yeye mwenyewe,kwamba hatukupinga mapitio bali tulisema ni hatua nzuri.

Anasema mikataba isipitiwe,bali iwekwe wazi,then anasema kuiweka wazi ndiyo "mapitio bora",halafu tena anasema kuipitia ni sawa ila tufanye zaidi ya hapo.Very contradicting,na hapo ndiyo utajuwa ni siasa tu.Hilo linawafanya wengi wajiulize kuwa ni nani kamtuma?

Hapo kwenye bold,ndiyo maana halisi ya ubinafsi inapokuja,kusema unafanya makusudi inamsaidia ama kumwumiza mwananchi?Makusudi hayo yana manufaa gani kwa Taifa?

Ameshasema ni makosa kujadili issue ambayo iko mahakamani,sasa hapo ina maanisha kitu gani?Kwamba waziri alijadili jambo lilokuwa mahakani?Kwahiyo alitaka afanye kinyume na hilo ama alimaanisha kitu gani?

Viongozi wana taaluma za tofauti,na kama ameamuwa kufanya kazi na serikali ya ccm,basi mwenzake ana ujuzi wa tofauti na yeye anao wa tofauti,kwahiyo cha muhimu hapo kama hakuna ubinafsi wala visasi,alichotakiwa ni kusaidiana naye kwenye hilo la capital gain taxes badala ya kupingana na kususiana na kuonyeshana nani ndiyo mjuzi zaidi ama nani ni zaidi na huku maslahi yaliyoko mezani ni ya Taifa.

Kwasababu kelele hizo ndugu Zitto ni kama vile tu amechukizwa kwa kutokushirikishwa kwake kwenye hizo dili.Kama unafanya kazi kwa manufaa ya taifa,basi huwezi ku act kwa namna ambayo hasara ni kwa Taifa just because unataka kuondoa credibility ya kiongozi fulani ama kumkomoa.

Kwakifupi tu hapa,ni kwamba makala hiyo hapo juu ni ya kibinafsi tu na ndiyo maana michango ya watu humu imengukia pande zote za kuhusu yeye kugombea urais,kuhusu yeye kujuwa zaidi ya Muhongo,na kwamba yeye amekijenga chama chake kuliko wanavyompa credits.Kama angekuwa amesimamia issue za sera kwa maslahi ya Taifa,angezijibu tuhuma hizo kwenye makala za tofauti ili tujadili yote kwa namna za tofauti kadri inavyofaa.

Kabla ya kuedelea kujadili mambo binafsi ya viongozi,basi ninasubiri aweke wazi maana halisi ya "mikataba kuwa wazi",na jinsi ambavyo hilo litasaidia mikataba hiyo kutusaidia ama hatua kuchukuliwa.
 
Mushi narudia nilichosema, tujadili sera sio watu. Zitto kazungumzia sera tupu kuhusu wizara, waziri, mikataba, leseni na mengineyo.
Alipotaja majina ya watu ni kwa kuwa alikuwa anachallenge fikra zao na athari zake katika sera. Na alichokisema Zitto kiko wazi kabisa. Hakuna persona attacks, na kazungumzia mwenendo wa mambo toka kitambo

Unaongeaongea ukirudiarudia na kumuattack Zitto, which is absolute ridiculous, and is what is unnecessary. Nitakuelewa ukizungumzia na kuchallenge mtazamo, utendaji wake kisera kama uko sahihi au la at the interest of we the citizents. Zitto hana habari na mtu, siku zote anachallenge sera na mifumo ya serikali na siasa ili iwe na maslahi kwa mwananchi wa kawaida, na sisi wote tufanye hivyo. Sio kuanza kujafilijadili watu, chuki binafsi tu, kama unaona na wewe una uwezo kuwa rais tangaza nia hagombwi mtu, titapima sera.
Zitto amezungumzia sera hapo juu?Hakuna kinachojadiliwa na members kwenye mjadala huu ambacho ni nje ya mada husika.

Amezungumzia kuhusu urais,na pia kujibu issue zilizoelekezwa kwake yeye binafsi,zingatia bold...unasema watu wasizingatie personal issue na wakati yeye kaziweka kwenye hiyo mada hapo juu?Amezungumzia "makala tatu zote dhidi ya Zitto",na hapo hakuna ubinafsi? ni upofu wako wewe mwenyewe na kuwazuia wana jamvi wasijadili mada iliyoko mbele yao ndiyo unakusumbua.


Hata wakati mkwaruzano wake na Muhongo ulipoanza,na pale Muhongo alipotoa shutuma za rushwa dhidi yake, na ambazo ziko kwenye uchunguzi baada ya kuundiwa tume ya Ngwilizi,yeye alihusisha tuhuma hizo na mbiyo zake za urais.Hakuna pahala ambapo alishaweka wazi ni kivipi tuhuma hizo ni mbinu za kumkwamisha kwenye mbiyo zake za urais.Na ndiyo maana sijashangazwa na hatua yake ya kuzijumuisha makala za urais pamoja na ile ya mkwaruzano wake yeye na Muhongo,zote mimi naona ni siasa zake tu licha ya kwamba yeye ndiye
Acha kugeneralize,jibu hoja kama nilivyofanya.Nimejibu msitari kwa msitari kuhusiana na bandiko lake,na wewe kama unamjibia,jibu nlichobandika.Hicho unachokiita personal attack ni ku reveal ubinafsi wake kwa kuchambua hiyo hoja yake hapo juu iliyojaa ubinafsi.
 
pumba hujui kitu
Wewe unayejuwa kitu,jibu kama Tanzania inafuata uliberali!Ama wewe ndiyo mwandishi wa huo utumbo?If so,jibu swali na uache kuandika ujinga.Hapa tunajadiliana kwa hoja.Kama hiyo makala ndo umeandika wewe,basi hujui unachokizungumza.
 
Kundi hili hapa chini CHADEMA muwe nao makini sana kwani ni makamanda wa kichina.

Juliana shonza, Zitoo kabwe, John shibuda, Mtela mwampamba, Benard Saanane, Dr.kitila mkumbo, adam chagulani, Henry matata, Nyakurungu, Rose kamili,erasto tumbo, mbunge wa viti maalum kigoma yule binamu wa Zitto, Habib Mchange etc........

Muwe makini na hawa watu.
Hutaki unaacha.
 
JOHNSON Mbwambo ameandika katika Gazeti la Raia Mwema la Oktoba 3, mwaka huu, kuhusu dhihaka za Zitto kwa Prof. Muhongo (Waziri wa Nishati na Madini).

Nimesoma na nimemuelewa.

Kwanza naomba radhi iwapo tafsiri ya taarifa yangu niliyoitoa kwa vyombo vya habari na kuwekwa kwenye blogu yangu (zittokabwe.com) ilikuwa ina dhihaka.

Nimefundishwa kutodhihaki watu na hasa watu wanaonizidi umri na siasa zangu sio za dhihaka bali za masuala (issues). Kupitia kwa ndugu Mbwambo naomba radhi kwa wote walioona kuna dhihaka katika andiko langu. Sikuwa na nia ya kumdhihaki Waziri Muhongo. Nia yangu ni kuonyesha kuwa Waziri Muhongo alichokifanya ni kuwacheza shere Watanzania, kwa kuwaambia maneno ambayo yeye mwenyewe alikuwa anaamini kuwa hayawezekani.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Wizara yake, Eliakim Maswi, ilithibitisha kauli yangu siku chache tu baada ya kuitoa. Mbwambo kaandika makala yake kana kwamba hapakuwa na kauli ya kufuta maneno ya Waziri. Ninaamini Mbwambo aliiona kauli ile lakini aliamua kupuuza ili kujifurahisha na imani yake kwa Prof. Muhongo na mawaziri aliowataja kwenye makala yake kwamba ni mawakala wa mabadiliko. Mbwambo anaamini kabisa kwamba ndani ya utawala wa CCM, kuna mawaziri wenye nia ya dhati ya kuleta mabadiliko.

Nieleze wazi kwamba nilishtuka sana kuona toleo moja la Gazeti la Raia Mwema likiwa na makala tatu, zote dhidi ya Zitto Kabwe. Wakati makala ya ndugu Mbwambo ilikuwa inahusu suala nyeti sana la rasilimali za taifa na ni makala nzuri yenye mafundisho, makala mbili nyingine zilikuwa ni za siasa dhidi ya Zitto. Mwandishi Mayage Mayage aliandika makala yenye kichwa cha habari “Zitto, Urais 2015 kwa chama gani?” na Mwanasafu wa gazeti hili la Raia Mwema, Evarist Chahali aliandika makala yenye kichwa cha habari “Rais Kikwete anapofikiri kama Kabwe Zitto.”

Namwambia Mayage akasome vizuri historia ya ujenzi wa CHADEMA. Yeye anadhani CHADEMA imeanza mwaka 2010. CHADEMA kimejengwa na watu, si mtu mmoja. Wanaoamua mgombea wa chama si watu wachache anaowadhani yeye Mayage bali ni wanachama wa CHADEMA kutoka sehemu mbalimbali za Tanzania, ikiwamo Munanila, mkoani Kigoma anapotoka Mayage.

Huyu Chahali anasema ananijua sana. Inawezekana ananijua kuliko mimi ninavyojijua. Lakini mimi simjui na wala sijawahi kumwona ana kwa ana, nimekuwa nikimwona tu kwenye mitandao ya kijamii akinizushia, kunitukana na kunisema. Sikushangaa kusoma makala yake ya wiki iliyopita. Wote wawili nawakumbusha msemo wa Mahatma Gandhi aliposema; “Kwanza wanakudharau, kisha wanakucheka, kisha wanapambana na wewe, kisha unashinda".

Sasa nirejee kwenye makala ya ndugu Mbwambo. Prof. Muhongo simjui, licha ya kwamba nimekuwa mmoja wa wabunge walioko mstari wa mbele kuhakikisha utajiri wa nchi unatumika kwa manufaa ya nchi, sikuwahi kumsikia Prof. Muhongo mpaka alipoteuliwa kuwa Waziri wa Nishati na Madini.

Sikuwahi kusikia akipaza sauti yake dhidi ya mikataba mibovu ya madini licha ya kwamba yeye ni msomi aliyebobea katika masuala ya miamba. Wakati Bunge la tisa, chini ya Spika Samuel Sitta, likiwa limecharuka kutaka mikataba mibovu ipitiwe na kubadilishwa tulitarajia sana kupata ushauri wa wataalamu wetu lakini hawakuonekana, "walikwina"?

Walikuwa waoga kusema maana wangeharibu uhusiano kati yao na watawala. Tulihangaika wenyewe bila maarifa yoyote kuhusu sekta ya madini. Wengine ilibidi kuacha kazi za ubunge na kwenda masomoni ili kuongeza ujuzi wa masuala ya kisheria na kiuchumi kuhusu sekta ya rasilimali (madini na mafuta).

Wasomi wetu hawakuwa nasi. Walichague kuendelea kufanya kazi za ushauri kwa kampuni za utafutaji madini nchini. Leo Mbwambo anawaona hawa ndiyo mawakala wa mabadiliko. Labda anasema kweli. Ila mimi nimekata tamaa na mabadiliko kuletwa na watu waliomo serikalini, kwa sababu kadhaa.

Moja, kama alivyosema ndugu Mbwambo, nilipigia kelele sana mkataba wa Buzwagi na mikataba mingine ya madini. Niliendelea kupiga kelele mpaka sheria mpya ya madini ilipopitishwa na Bunge. Nimuulize Mbwambo kwamba, licha ya sheria mpya kuandikwa imechukua miaka mingapi kampuni za madini kufanya kazi zao kwa kutumia sheria hiyo mpya? Je, mikataba mingapi iliyopitiwa imerekebishwa au hata kuvunjwa? Pengine niwasaidie kuwakumbusha taarifa kwamba, hakuna kilichofanyika kwa mujibu wa sheria mpya, licha ya kufuatilia kwa kina bungeni kupitia michango na hata maswali bungeni sambamba na makala mbalimbali.

Tangu Waziri Prof. Muhongo na timu yake waingie ofisini ni maneno tu tunayosikia bila matendo. Hata suala la mgawo wa umeme ambalo ndugu Mbwambo analisema kama mfano, yeye anajua namna ambavyo wananchi wanalalamikia umeme kukatika hovyo, tena bila taarifa wala maelezo. Muhongo alifanikiwa sana kuaminisha watu wenye mawazo huru kama Mbwambo wakamwona yupo sahihi kiasi hata cha kufumbia macho mgawo wa umeme usio na maelezo, unaoendelea nchini.

Siwaamini mawaziri kwa sababu wanasema lolote linalowajia midomoni mwao hata kama wanaamini kuwa wanalosema haliwezekani kutekelezwa. Waziri wa Nishati na Madini alisema kuhusu mikataba ya mafuta na gesi ili kufurahisha watu. Huo ni msingi wa kwanza wa kauli yangu ambayo ndugu yangu Mbwambo ameitafsiri kuwa ni dhihaka. Nilikuwa nasema ukweli mchungu kwamba, serikali haiwezi kufanya lolote kuhusu mikataba. Nilitoa changamoto kuwa kama serikali kweli imedhamiria, iweke mikataba hii wazi. Je, wameiweka wazi?

Pili, Waziri wa Nishati na Madini anataka umma umwone kwamba anajua sana masuala ya sekta kuliko Mtanzania mwingine yeyote. Nitatoa mfano mmoja unaonihusu moja kwa moja. Katika mkutano wa Bunge uliopita, Tanzania ilitembelewa na Waziri Mkuu mstaafu wa Urusi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Kirusi iliyonunua leseni ya kutafuta uranium kule Selous. Kampuni ya UraniumOne iliyonunua leseni hii ya Mkuju River Project kutoka Kampuni ya Mantra ya Australia, kwa dola za Marekani milioni 980.

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ilitaka ilipwe kodi ya ongezeko la mtaji (capital gains tax) kampuni hii ilikataa. TRA wakaenda mahakamani kudai malipo ya kodi yenye thamani ya dola za Marekani milioni 116 ambazo ni sawa na asilimia 20 ya thamani ya mauzo na kesi inaendelea. Kwa mujibu wa sheria zetu kampuni zinapouziana leseni, lazima Waziri wa Nishati na Madini atoe idhini ya mauzo hayo. Mgeni huyo kutoka Urusi alikuja nchini kupigia debe idhini hii, ili itolewe leseni maalumu ya uchimbaji (special mining licence).

Nikasimama kutoa taarifa bungeni kwamba mawaziri wanakutana na huyu Waziri Mkuu mstaafu wa Urusi kuhusu leseni ya Mkuju River Project na kuweka wazi kwamba Kampuni ya UraniumOne hawajalipa kodi ya capital gains. Nilisimama kutoa taarifa baada ya majibu ya Waziri Muhongo kwamba, kilichouzwa si kampuni ya Tanzania bali Australia na hivyo hakuna kodi.

Kwa makusudi kabisa niliacha habari ya kesi ya TRA dhidi ya kampuni hii ili kuona umakini wa mawaziri wetu wapya kabla ya kukutana na lobbyists (washawishi) wa kampuni hizi za madini. Waziri Muhongo aliposimamishwa na Naibu Spika, Job Ndugai, akasema “Sisi tunajua zaidi kuliko Zitto" Kwanza Waziri hakuwa anajua.

Ni makosa kabisa kujadili suala ambalo mamlaka mojawapo ya nchi wamelipeleka mahakamani na linasubiri uamuzi. Lakini suala la Waziri kutokuwa na taarifa lilidhibitishwa na ujio wa Naibu Waziri George Simbachawene, aliponifuata na kuomba "details" kuhusu taarifa niliyotoa. Kulikuwa na haja gani kwa Waziri kusema bungeni yeye anajua zaidi na baadaye kumtuma Naibu wake kutafuta taarifa?

Huu ni udhaifu mkubwa sana wa uongozi. Kutojua si makosa, inawezekana kuwa wengine hatukusomea miamba lakini tumesomea masuala ya kodi kwenye madini na mafuta. Waziri makini anayejali nchi yake anawezaje kukutana na mwekezaji anayekataa kukulipa kodi yako bila wewe hata kuulizia utalipwa lini?

Unaulizwa bungeni unasema "ninajua zaidi" na Mwandishi mahiri kama Mbwambo anasema "mpeni nafasi atende"!

Nilipomsikia Waziri anasema ameagiza TPDC (Shirika la Maendeleo la Mafuta) kupitia mikataba nikajua na hili nalo hajui. Amesema tu ili watu wafurahi kwamba mikataba inapitiwa. Kupitia mikataba bila kuchukua hatua dhidi ya mikataba mibovu ni nini kama sio kutafuta umaarufu tu? Unapitia mikataba ili iwe nini kama huwezi kuchukua hatua?

Kuna mikataba ambayo imeingiwa kwa rushwa, sheria zetu zinasema kuwa mikataba iliyoingiwa kwa rushwa ni sawa na haipo. Hata sheria za kimataifa za mikataba zinatambua hivyo. Waziri anaposema kuwa tunapitia mikataba ili kuhakikisha kuwa mikataba ijayo inakuwa mizuri ni kichekesho. Hivi tunajua vitalu vingapi vimegawiwa na vingapi vimebaki? Hivi sasa kuna mikataba 29 na leseni 26. Vitalu vilivyobaki hivi sasa ni tisa tu.

Wizara inatuambia tunaangalia hii mikataba 29 ili kuboresha 9. Haya si mapitio bali ni kuangalia tu kama nilivyosema katika sentensi iliyotangulia. Mapitio bora zaidi ni uwazi wa mikataba yote tuliyoingia mpaka sasa na kuzuia kabisa mikataba mipya wala kugawa vitalu vipya vya kutafuta mafuta na gesi.

Uporaji wa rasilimali ni wa namna mbili, moja ni watu wachache na kampuni zao kupora kwa kupitia mikataba mibovu na pili ni kizazi kimoja kunyonya rasilimali zote bila kujali kizazi kijacho. Katika maandiko yangu nimeshauri kuwa tusigawe vitalu vipya mpaka tuone mafanikio ya mikataba hii 29 na leseni 26 tulizonazo hivi sasa. Wito wangu ni mmoja tu, uwazi wa mikataba. Kutaka uwazi si dhihaka. Uwazi ni uwajibikaji.

Suala la mapitio ya mikataba kwa jicho la juu juu ni suala la kuunga mkono. Lakini ukitazama historia ya nchi yetu katika masuala haya utabaini kwamba tunapaswa kufanya zaidi ya mapitio ya mikataba.

Tunapaswa kufanya jambo ambalo hatujawahi kulifanya nalo ni kuiweka wazi mikataba hii kwa umma. Hii ndiyo hoja yangu.

Inawezekana kabisa kwamba maneno niliyotumia yameudhi watu fulani lakini ikumbukwe mimi ni Mbunge wa Upinzani na ni wajibu wangu kukosoa serikali kila inapowezekana. Bahati nzuri miaka yangu saba bungeni hivi sasa imetumika kwa kiasi kikubwa sana katika kufuatilia kwa karibu sekta ya madini, mafuta na gesi. Ni rahisi sana mimi kuweza kuona suala linalosemwa na serikali linasemwa tu au serikali inamaanisha? Katika suala la mapitio ya mikataba kwenye sekta ya madini na mafuta kwa kweli serikali haipo makini. Watu wajuvi wa mambo kama kina Mbwambo wanapaswa kwenda zaidi ya mapitio na kutaka mikataba iwekwe wazi na kuchambuliwa kwa uwazi kabisa.

Waziri Muhongo anayo nafasi ya kufanya kazi yake, afanye kazi yake bila bugudha. Mbwambo ajue kuwa Mbunge Zitto pia anayo kazi yake kwa mujibu wa Katiba ibara ya 63 nayo ni "kuisimamia" serikali. Niacheni nami nifanye kazi yangu.


Makala hii iliyoandikwa na Kabwe Zitto, Mbunge wa Kigoma Kaskazini ni majibu kwa makala iliyoandikwa na Mwanasafu wetu, Johnson Mbwambo, katika toleo lililopita la gazeti hili la Raia Mwema, kupitia safu yake ya Tafakuri Jadidi.

Makala iliyopelekea Zitto kueleza kuwa hanijui ni hii hapa chini. Si ajabu kwa mwanasiasa maarufu kama Zitto kutomfahamu mwananchi wa kawaida kama mie.Pia natumaini Mheshimiwa Zitto anatambua kuwa kuna tofauti kati ya "NINAMFAHAMU" na "TUNAFAHAMIANA." Ninatarajia huko mbeleni atapata wasaa wa kujibu hoja nyinginezo katika makala hii zaidi ya hiyo ya kutonifahamu

Rais Kikwete anapofikiri kama Kabwe Zitto

Evarist Chahali

Uskochi
Toleo la 261
3 Oct 2012

NIMEKUWA nikiulizwa swali hili takriban kila wiki baada ya makala zangu kuchapishwa katika jarida hili maridhawa: Hivi kuna wakati unaishiwa na cha kuandika? Na siku zote jibu langu linakuwa lile lile; Tanzania yetu haiishiwi mambo yanayopaswa kujadiliwa-iwe gazetini, mtandaoni, kijiweni au popote pale. Kuweka rekodi sawia, kila ninapoingia mtandaoni huwa ninakumbana na wastani wa angalau habari tano zinazoweza kutengeneza mada za makala zangu.
Wiki hii nitazungumzia matukio mawili makubwa yanayoihusu CCM na CHADEMA. Kwa namna moja au nyingine, matukio yote mawili yanahusiana, na nitajitahidi kuonyesha uhusiano wao mwishoni mwa makala haya.

Tukio la kwanza ni kauli ya Mwenyekiti wa Taifa wa CCM, Rais Jakaya Kikwete kwamba CCM haitokufa, na pengine wanaodhani hivyo wanaweza kufa wao kabla ya chama hicho tawala kufa.

Kwa baadhi yetu tunaosoma siasa kama eneo la taaluma, tunatambua ukweli mmoja, kwamba chama cha siasa kinazaliwa, kinakua, na kama ilivyo kwa binadamu, kinaweza kufa. Na tofauti na binadamu ambao hatuna udhibiti mkubwa wa kurefusha au kufupisha maisha yetu (kuna watenda dhambi na wanaotumia kila aina ya ‘sumu’-pombe, dawa za kulevya na kadhalika ama kumkera Muumba au kuharibu afya zao-lakini si tu wapo hai bali pia wana afya za kuridhisha, huku wengine mambo yao yakizidi kuwanyookea, huku upande mwingine kukiwa na wacha Mungu, wanaojali afya zao lakini wanataabika muda huu); Vyama vya siasa vinaweza kurefusha maisha yao kwa kuitumikia jamii kulingana na matarajio ya jamii husika au ikaipuuza jamii hiyo na kujichimbia kaburi.

Pamoja na heshima yangu kubwa kwa Rais Kikwete, ninaomba kutofautiana naye katika kauli hiyo kuwa CCM haitokufa. Si tu kuwa vyama vya siasa hufa, bali pia ninaamini kuwa kila Mtanzania anayefuatilia kwa karibu historia na mwenendo wa chama hicho anaweza kabisa kubashiri kuwa ama mwanzo wa mwisho wake unakaribia au kinaharakisha kifo chake.

Simlaumu Rais Kikwete kwa kauli hiyo kwa sababu kama Mwenyekiti wa Taifa wa Chama anachoongoza ana jukumu kubwa la kuwahakikishia viongozi na wanachama wenzake kuwa ‘mambo si mabaya’ kama inavyoelezwa na wapinzani wao.

Binafsi, nasema kinachoweza kuiua CCM kabla ya wakati wake, ni pamoja na mtizamo huo wa Rais Kikwete wa kwamba ‘chama hicho kipo imara na kinaendelea kupendwa na Watanzania wengi-uthibitisho (kwa mujibu wao) ni idadi ya wana-CCM waliojitokeza kugombea nafasi mbalimbali kwenye chaguzi zinazoendelea ndani ya chama hicho.

Ni kweli kwamba idadi ya waliojitokeza kugombea inaweza kujenga picha kuwa CCM bado kinapendwa na wengi. Lakini haihitaji ufahamu mkubwa wa siasa zetu kumaizi kuwa baadhi ya wanaokimbilia uongozi ndani ya chama hicho wana ajenda zao binafsi. Ikumbukwe kuwa huko nyuma chama hiki kilishaonyesha dhamira ya kutenganisha biashara na siasa, hatua iliyotafsiriwa na wengi kuwa ni kutambua kuwa kuna kundi la wafanyabiashara wanaokimbilia kwenye siasa si kwa minajili ya kuutumikia umma, bali kusaka ‘kinga’ ya kuwalinda katika biashara zao.

Binafsi, nilikuwa miongoni mwa wapinzani wakubwa wa wazo hilo, si tu kwa sababu siafikiani na aina yoyote ya ubaguzi, bali pia sikuona kuwa tatizo ni wafanyabiashara kujihusisha na siasa bali wafanyabiashara ‘wachafu’ kuruhusiwa kujihusisha na siasa. Kwa kuharamisha biashara kwenye siasa kungeweza kuwa na hatari ya kuwakwaza wazalendo wazuri tu ambao walichagua kujihusisha na biashara kabla ya kuingia kwenye siasa.

Na ingekuwa ubaguzi wa wazi kuwazuia wafanyabiashara kujihusisha na siasa, lakini kuwaruhusu askari wastaafu, wasomi na wanajamii wengineo kufanya hivyo. Sawa, wanasema samaki mmoja akioza basi wote wameoza, lakini usemi huu hauzingatii ukweli kwamba binadamu hutofautiana.

Kwa mfano, kwa vile Mndamba wa kwanza kumfahamu ni mie ambaye pengine ninakukera na kwa mtizamo wangu haimaanishi kuwa kila Mndamba utakayekutana nae maishani atakukera. Waingereza wana msemo kuwa “people vary because we differ” yaani watu huwa na tofauti kwa sababu wanatofautiana, na kwa mantiki hiyo hiyo, mfanyabiashara anayeingia kwenye siasa kwa minajili ya kujitengenezea kinga katika ufisadi wake kwa taifa, haimaanishi kuwa kila mfanyabiashara anayeingia kwenye siasa ana malengo hayo.

Ninaamini kilichopelekea CCM kudhamiria kumtenganisha biashara na siasa ni historia na uzoefu iliopata kutoka kwa baadhi ya wafanyabiashara walioingia kwenye siasa. Na wazo lilikuwa zuri, kwamba mfanyabiashara atakayeamua kuingia kwenye siasa achague moja: biashara au siasa.

Tukirejea kwenye tamko la Kikwete kuwa CCM haitokufa, yayumkinika kuamini kuwa kauli hiyo ni ya kujipa matumaini tu na kukwepa ukweli kwamba kwa kiasi kikubwa chama hicho kinaonekana machoni mwa baadhi ya Watanzania kuwa ni chanzo cha matatizo mengi yanayoikabili nchi yetu. Kwa kifupi, kitakachoiua CCM si kauli za hao wanaoikitabiria kifo bali matendo ya chama hicho ambayo kimsingi ndio ‘pumzi’ inayokifanya kiwe hai.

Tukio jingine ambalo kwa namna moja au nyingine linahusiana na uhai wa chama cha siasa (kwa maana ya kuwa hakitokufa au la) ni tamko la Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe (CHADEMA), ya kwamba hatogombea ubunge katika uchaguzi mkuu ujao wa 2015, bali atagombea urais.

Kwanini ninalinganisha tamko la Zitto na kauli ya Mwenyekiti wa CCM, Kikwete? Jibu fupi ni kwamba matamko yote mawili yanaelekea kupuuza hali halisi ya mwenendo wa siasa za huko nyumbani.

Wakati Mwenyekiti Kikwete anajigamba kuwa CCM haitokufa japo kuna mamia kwa maelfu ya wana-CCM wanaokihama chama hicho kutokana na kutoridhishwa na mwenendo wake, huku pia baadhi ya viongozi wa chama hicho kama kina Samuel Sitta wakionyesha hadharani ‘maovu’ ya chama hicho, Zitto hataki kujihangaisha kutambua wengi wa Watanzania wanamtaka mwanasiasa gani kutoka chama chake ili kubeba dhamana ya kugombea urais kwenye uchaguzi mkuu ujao.

Kabla sijaendelea kuijadili kauli ya Zitto, ningependa kuweka bayana masuala matatu ya msingi. Kwanza, Zitto ana kila haki si tu ya kutaka kuwa Rais wa Tanzania, bali pia kutangaza kuwa ana nia hiyo. Ni haki yake ya kidemokrasia, hasa ikizingatiwa kuwa anatoka katika chama cha Demokrasia na Maendeleo.

Pili, ni suala la kukubalika kwa wapiga kura watarajiwa (potential voters). Kila mara ninapomsikia Zitto akielezea dhamira yake ya kutaka kuwa Rais, huwa ninajiuliza swali moja la msingi; ni lini amefanya ‘utafiti’ wa kutambua Watanzania wanamhitaji awe rais wao?

Wenzetu huku Magharibi, kabla mwanasiasa hajakurupuka kutangaza kuwa anataka kuwa rais huwa inamlazimu kujihangaisha ‘kusoma upepo,’ yaani kufahamu iwapo wapigakura wanamhitaji.

Sawa, Tanzania si nchi ya Magharibi, na pengine hakuna umuhimu wa kusaka mtizamo wa wapigakura. Lakini kwa mwanasiasa anayejali maslahi ya chama chake na wananchi kwa ujumla, yayumkinika kuamini kuwa atajihangaisha kufahamu iwapo dhamira yake ya kugombea ni kwa maslahi ya chama chake na umma kwa ujumla au ni kwa ajili ya kutimiza ndoto zake binafsi tu.

Suala la tatu, na ambalo kwangu si tu ni la msingi zaidi bali pia linanishawishi kuamini kuwa dhamira ya Zitto kugombea urais ni sawa na kubariki ushindi wa CCM hapo 2015, ni uadilifu wa mwanasiasa huyo.

Ninamfahamu Zitto vizuri, na si kupitia social media. Ni mmoja wa wanasiasa wachache wenye kipaji cha hali ya juu katika ujenzi wa hoja. Lakini, kama mwanadamu mwingine, mwanasiasa huyo ana mapungufu fulani. Kwa wanaomfahamu kupitia social media (hususan Twitter) wanaweza kuafikiana nami kuwa si mwepesi sana wa kuafikiana na watu wenye mtizamo tofauti na wake.

Ni rahisi kumhukumu kuwa ana jazba (japo sitaki kuamini hivyo) pindi mtu anapotofautiana naye katika anachoamini yeye kuwa ni sahihi. Nafasi haitoshi kutoa mifano halisi, lakini waliotofautiana nae kimtizamo ndani ya Twitter wanaweza kuwa mashahidi wazuri.

Tatizo la msingi kuhusu Zitto ni ‘tuhuma’ zilizowahi kuandikwa na jarida moja la kila wiki kwamba katika kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu uliopita, jarida hilo lilinasa mawasiliano kati ya mwanasiasa huyo na mmoja wa viongozi wa juu wa Idara ya Usalama wa Taifa.

Katika mazingira ya kawaida, mwanasiasa wa chama cha upinzani kuwa na mawasiliano na mtumishi wa taasisi hiyo nyeti (ambayo ilishutumiwa na CHADEMA-ambayo Zitto ni mbunge wake-kuwa ilikihujumu chama hicho kwenye uchaguzi huo) inazua maswali kadhaa.

Ndio, watumishi wa Idara ya Usalama wa Taifa ni Watanzania wenzetu kama ilivyo kwa wanasiasa wa vyama vya upinzani. Lakini mawasiliano kati ya mwanasiasa wa chama cha upinzani kama Zitto na kiongozi wa idara hiyo, yanaweza kuibua maswali mengi. Kibaya zaidi, Zitto hajawahi kutoa ‘maelezo ya kueleweka’ kuhusu mawasiliano hayo.
Kimsingi, Zitto anatambua bayana hisia zilizojengeka baada ya habari hiyo kuchapishwa. Kuna waliotafsiri kuwa mawasiliano hayo yalilenga kukihujumu chama hicho, na kwa kuzingatia mantiki ya kawaida tu hatuwezi kuwalaumu kwa hisia hizo.

Lakini pengine kubwa zaidi ni kwanini bado kuna idadi kubwa tu ya wafuasi wa CHADEMA wanaotafsiri uamuzi wa Zitto kutaka urais kama ‘tamaa ya madaraka.’ Hivi akiweka kando imani yake kuwa ana uwezo na uadilifu wa kuongoza taifa la Tanzania, Zitto ameshawahi kufikiria kuwashawishi sceptics hawa hata kama hoja zao hazina mashiko?

Kubwa zaidi ni ukweli kwamba matokeo ya uchaguzi mkuu uliopita yanaonyesha bayana jinsi mgombea urais kupitia CHADEMA, Dk Willibrod Slaa, alivyokubalika kwa idadi ya kuridhisha tu wapiga kura. Kama dhamira ya Zitto ni kuona CHADEMA inaingia Ikulu, kwanini asiwekeze jitihada kumsapoti Dk Slaa katika uchaguzi ujao na kusubiri ‘zamu yake’ hasa kwa vile umri bado unamruhusu hata kwa miaka mingine 15 ijayo?

Kwa mujibu wa Katiba ya sasa ya Jamhuri ya Muungano, mgombea urais sharti awe na miaka 40. Mwaka 2015 Zitto atakuwa na umri pungufu na huo. Hivi kung’ang’ania kuwa anataka kugombea ilhali akijua Katiba haimruhusu si ni dalili ya tamaa ya madaraka?

Nimalizie makala haya kwa kulinganisha matukio mawili haya niliyozungumzia. Kama ambavyo Rais Kikwete hataki kujiuliza kwanini baadhi ya watu wanaitabiria kifo CCM, Zitto hataki kujiuliza kwanini baadhi ya watu wanatafsiri dhamira yake ya kutaka urais mwaka 2015 kama mikakati wa kuirejesha CCM madarakani na kuinyima CHADEMA nafasi hiyo.

Suluhisho katika masuala hayo mawili, linaweza kupatikana katika busara hii ya Waingereza isemayo “never ever put emotions in front of common sense” (kwa tafsiri isiyo rasmi, kamwe usitangulize hisia mbele ya tabasuri/ busara).







 
ZZK ndugu yangu mbona ghafla mabadiliko? Umelipwa bei gani kuja kuvuruga? Lakini leo ninakuapisha mbele ya Mungu kama una mpango wa shetani!! wa kutumwa kuvuruga basi hutofika popote!!

Kwa sababu mpango wa ukombozi wa TZ ni mpango wa Mungu. Na soma katika vitabu vyote yaliyowapata wale waliojaribu kuingilia mpango wa Mungu!! Tafadhali sana!! tulia uongozi utaupata na hata urais!! Lakini kwa mtindo huu wa kuwafanya hata maadui wa CDM wakachekelea hutosamehewa believe me!!

Zitto kavuruga wapi hapa? Hoja zake ziko wazi na nimezielewa. Leta za kwako pia tupembue.
 
ZZK ndugu yangu mbona ghafla mabadiliko? Umelipwa bei gani kuja kuvuruga? Lakini leo ninakuapisha mbele ya Mungu kama una mpango wa shetani!! wa kutumwa kuvuruga basi hutofika popote!!

Kwa sababu mpango wa ukombozi wa TZ ni mpango wa Mungu. Na soma katika vitabu vyote yaliyowapata wale waliojaribu kuingilia mpango wa Mungu!! Tafadhali sana!! tulia uongozi utaupata na hata urais!! Lakini kwa mtindo huu wa kuwafanya hata maadui wa CDM wakachekelea hutosamehewa believe me!!
Napata tabu kuelewa fikra za watu wengi wanapo jihisi kuingiza kila kitu katika harakati za kimungu !ndugu hebu simama halafu rtudi nyuma hatua moja ,tafakari bandiko lako na kile anachokizungumza Zitto,na kwanini anakizungumza halafu ndipo ulete hukumu zako.
 
Nimewahi kusoma na vijana wengi kutoka Kigoma wakati nikiwa sekondari, na pia Chuoni. Nilichokuja kugundua wachache wanatabia ya usaliti wakiweka mbele masilahi binafsi. Wako ladhi kumsaliti yeyote na kuvujisha siri za ndani kabisa ili mradi tu waweze kufikia malengo yao.

Kulikuwa na katibu mkuu wa Chadema - Dr Walid Amani Kaborou, huyu usaliti wake kwa upinzani kila mmoja anauelewa. Amekuwepo pia Daniel Nsanzugwanko wa NCCR. Huyu pia anajulikana kwa usaliti wake. Kafulila amejaribu Chadema, akashindwa, NCCR pia ameshindwa. Hawa ni wachache, lakini pia kule chuoni alikuwepo rafiki yangu kutoka Kigoma ambaye kwa hakika alikuwa ni msaliti wa aina ile ile kama akina Walid Kaborou, siwezi kusimulia sana juu yake

Zito Kabwe ni msaliti na anajli zaidi maslahi binafsi. Baada ya kujipatia umaarufu, akiwa kijana kati ya Vijana wachache ndani ya bunge, akaweza kukaa karibu na rais na kukutana na viongozi mbalimbali duniani akaona anaweza kufanya lolote bila kujali amewezaje kufika hapo alipo.

Zito ni msaliti. Mtakaumbuka 2010 wakati wa kampeni, badala ya kumkampenia mgombea urais wa Chadema yeye alikuwa akitangaza kuwa 2015 atagombea urais. Kwa mwenye akili anaelewa huyu kijana namna gani vipi!

Zito huyu huyu, wakati wa vuguvugu la kutangaza matokeo ya urais, yeye yuko bize na Jack Zoka, afisa usalama anayeshughulika na siasa. Na walikuwa wakiwasiliana mara kwa mara. Hapa shaka kuu ipo kwa huyu bwana mdogo.

Zito, wakati wenzake wanaimarisha chama, yeye anajitangazia kugombea urais na hata siku moja hajawahi kushughulika na harakati za M4C. Kuna jambo hapa. Ikiwa anataka urais kupitia chadema ataupataje akiwa chama kitabaki kuwa cha msimu.

Zito Kabwela, anafahamu fika kuwa, enzi hizo alikuwa na nafasi kubwa ya kuweza kushika madaraka ya juu ndani ya chama na hata ya nchi ikiwa chama kingeweza kufanya vizuri katika uchaguzi mkuu siku zijazo. Lakini sasa matumaini hayo yanafutika taratibu baada ya kuona kuna Vijana wengi, wenye maono na uwezo mkubwa pengine kushinda hata yeye wameibuka chadema. Mfano Tundu Lissu, John Mnyika, Godbless Lema, Benson Kigaila na wengine. Sasa kwa kuelewa hili na kwa sababu za ubinafsi na usaliti anajaribu kutafuta namna ya kukivuruga chama, akiondoe kwenye lengo la msingi la kuimarisha uhai wa chama.

Zito Kabwe, atakuwa ndumila kuwili. Anatumwa na kutumiwa na pia ana tabia ya kujipendeza kwa wenye madaraka.

Conclusion: Zito anajiona anaweza, lakini namhakikishia hataweza. Kaborou alikuwa maarufu kumshinda yeye, Mrema (Augustino) alikuwa maarufu kumshinda yeye, lakini leo yupo wapi.

Kama ilivyo kwa wakristo, Yesu Kristo aliwaambia mitume wake "Sikuwachagua mitume 12 na mmoja wenu ni shetani?"

Wito wangu kwa WanaChadema, mjue kuna Viongozi wengi lakini miongoni mwao kuna wasaliti na mmoja wao ni Zito Zuberi Kabwe. Kwa mataendo yake kwa ustawi wa chama anajidhihirisha wazi.

Chadema, nawasihi muishi na huyu mtu kama mlivyoweza kuishi hata na Shibuda, mwisho wa siku ataamua kujinyonga mwenyewe kwani anguko lake litakuwa kubwa na la aibu.

Nashindwa kuelewa umejadili hoja gani, ni hii taarifa ya Zitto au umerukia tu. Tafadhali isome tena hii taarifa ili ujibu hoja sahihi.

Ninachokisoma toka kwako ni UNAFIKI, UNAFIKI, USALITI, USALITI, tafadhali nukuu sehemu moja ya taarifa ya Kabwe ukihusianisha na Usaliti. Mimi ninachokiona katika taarifa hii ni kile Kabwe anachokiamini katika suala la rasilimali ya Taifa. Ni nini kibaya katika hayo ya rasilimali aliyoyaandika. Hivi hakuwa Kkikwete katika kampeni zake aliyetuahidi kubadilisha mikataba na niu yeye mwenyewe kutueleza kuwa kulikuwa na makosa katika mikataba hiyo.

Na hata Profesa Lipumba aliyarudia hayo mara kwa mara. Kwa hiyo kuwa Mikataba ina matatizo sio geni limekubaliwa na wote. Ninachokuomba utamke ni kimoja tu kuwa mikataba haina matatizo yeyote, tamka hili tafadhali kabla sijaendelea kukujibu ili watanzania wakujue sura yako. Napenda ifahamike wazi kuwa , usipoweza kutamka hilo basi MSALITI NI WEWE, tena unawasaliti watanzania wanyonge ili uendelee kushiba.

Kua, na usikilize wasomi wanavyolikemea suala la Rasilimali za Taifa. Na janga kubwa wasomi wanalofikiria ni Tanzania kuwa Nigeria ya pili ikiwa hakuna mikakati madhubuti ya Rasilimali kuwekwa itayowasaidia walala hoi. Nawe unatusaliti hapa, baada ya kushirikiana katikakuiepusha Tanzania kugeuka Nigeria (ukanda wa DELTA) wewe umepewa vipesa kidogo na kubwabwaja matapishi. Futa taarifa yako tafadhali, tunakuheshimu.
 
ZZK ndugu yangu mbona ghafla mabadiliko? Umelipwa bei gani kuja kuvuruga? Lakini leo ninakuapisha mbele ya Mungu kama una mpango wa shetani!! wa kutumwa kuvuruga basi hutofika popote!!

Kwa sababu mpango wa ukombozi wa TZ ni mpango wa Mungu. Na soma katika vitabu vyote yaliyowapata wale waliojaribu kuingilia mpango wa Mungu!! Tafadhali sana!! tulia uongozi utaupata na hata urais!! Lakini kwa mtindo huu wa kuwafanya hata maadui wa CDM wakachekelea hutosamehewa believe me!!

Hongera ZZK Hapo ndipo ninapokukubali. Mungu azidi kukuimarisha na kukupa uelewa mkubwa zaidi ktk mambo ya kiuchumi.

Sasa urudi upige kazi ya namna hii ndani ya chama, ucjitenge mbali na chama, stay blessed u r my role model in economy analysis.
 
R.I.P Chama Cha Magamba.... CCM 1977-2015, Bwana alitoa, Bwana atatwaa.
JINA LA BWANA LIHIMIDIWE.
AMEN.
 
nashindwa kuelewa umejadili hoja gani, ni hii taarifa ya zitto au umerukia tu. Tafadhali isome tena hii taarifa ili ujibu hoja sahihi.

Ninachokisoma toka kwako ni unafiki, unafiki, usaliti, usaliti, tafadhali nukuu sehemu moja ya taarifa ya kabwe ukihusianisha na usaliti. Mimi ninachokiona katika taarifa hii ni kile kabwe anachokiamini katika suala la rasilimali ya taifa. Ni nini kibaya katika hayo ya rasilimali aliyoyaandika. Hivi hakuwa kkikwete katika kampeni zake aliyetuahidi kubadilisha mikataba na niu yeye mwenyewe kutueleza kuwa kulikuwa na makosa katika mikataba hiyo.

Na hata profesa lipumba aliyarudia hayo mara kwa mara. Kwa hiyo kuwa mikataba ina matatizo sio geni limekubaliwa na wote. ninachokuomba utamke ni kimoja tu kuwa mikataba haina matatizo yeyote, tamka hili tafadhali kabla sijaendelea kukujibu ili watanzania wakujue sura yako. Napenda ifahamike wazi kuwa , usipoweza kutamka hilo basi msaliti ni wewe, tena unawasaliti watanzania wanyonge ili uendelee kushiba.

Kua, na usikilize wasomi wanavyolikemea suala la rasilimali za taifa. Na janga kubwa wasomi wanalofikiria ni tanzania kuwa nigeria ya pili ikiwa hakuna mikakati madhubuti ya rasilimali kuwekwa itayowasaidia walala hoi. Nawe unatusaliti hapa, baada ya kushirikiana katikakuiepusha tanzania kugeuka nigeria (ukanda wa delta) wewe umepewa vipesa kidogo na kubwabwaja matapishi. futa taarifa yako tafadhali, tunakuheshimu.
Tafadhali naomba mamluki muache kutumika kukiua chadema....... Na siku zote ukweli unauma ndio maana mtu ukisema zzk anatumika watu roho zinawauma sana kama vile anamgawia posho yake ya vikao vya bunge. Siasa maana yake kuna ukweli na uongo wewe mtu wa pembeni unaumizwa na nini????? Sisi raia tunaona kabisa zzzk anavyotumiwa na chama cha magamba kukuiua chadema then anatokea mtu huko from no were sijui ni mjomba ake zzk sijui ni aunt yake anaanza kumtetea zzk kwa kusema anatetea maslahi ya nchi. Nasema sio kweli.... Zzk ni jambazi tena hatari sana hafai tena hata kuwa mwenyekiti wa kijiji. Ni mbaya sana na alivyoingizwa kwenye kamati ya madini ndio walimpa meno na akawa mbaya zaidi huyu kijana. Aende zake kushika mashamba kuko moro alime. Asituone watanzania ni wapumbavu kiivyooo. Anajifanya nae amesoma kumbe ni wizi mtupu alikuwa anapiga kelele kwa vile alikuwa ajapewa chaneli za kuiba.
 
Kundi hili hapa chini CHADEMA muwe nao makini sana kwani ni makamanda wa kichina.

Juliana shonza, Zitoo kabwe, John shibuda, Mtela mwampamba, Benard Saanane, Dr.kitila mkumbo, adam chagulani, Henry matata, Nyakurungu, Rose kamili,erasto tumbo, mbunge wa viti maalum kigoma yule binamu wa Zitto, Habib Mchange etc........

Muwe makini na hawa watu.
Hutaki unaacha.

ww kama bado unashabikia chadema umekwisha.ccm ndio jiwe la msingi.vitakufa vyama vyote ccm itabaki,.
 
Hongera sana Zitto Kabwe. Kwani umeonyesha umahiri mkubwa na misimamo thabiti kwa kile ulichoamini kuwa ni sahihi.

keep it up, utatimiza ndoto zako tu insh'Allah

Kuna kuonyesha umahiri mkubwa wa kufanya mambo ya hovyo kwa staili ya kuwa twisted views za vitu ya kweli, pia kuw ana msimamo thabiti ktk mambo ya hatari na maovu sana.Mfano wale watu waliochoma makanisa Dar week hii, wan aumahiri wa kufanya fujo na wana misimamo thabiti kwa wanachoamini kuwa wakristu ndio wanaohusika kukukojolea Quran, na imani yao pia inawatuma kuwa ni shahihi kuchoma makanisa kama adhabu.
 
ZZK=zana za kilimo i.e anatumika na mafisadi kwa malengo ya kudhoofisha CDM..hawa watu mwisho wa siku wanaumbuka vibaya au wanakufa kifo kibaya.Ni Traitor! Ana uchu wa madaraka kama edward Lowassa!

huyu nae hajasoma makala CHUKI BINAFSI:
 
Back
Top Bottom