Zitto: Watanidharau, watanicheka, watapambana lakini nitashinda!

Well Said Zitto. Hapa nakubaliana na ww kwa kiasi kikubwa kwenye ishu ya mikataba. Mambo mengine "No Comment"

Sasa unaposema unakubaliana na Zitto kuhusu mikataba unakubaliana nae nini? Zitto katika jibu lake kwa hoja ya Mbwambo kuhusu DHIHAKA yake anasema yeye anataka kuwa mikataba iwe wazi [ transparent] lakini mkumbuke kuwa ni Zitto huyu huyo aliyesema hatua ya Porf. Muhongo kutaka kuipitia mikataba ya gesi ingewakatisha tamaa na kuwatisha wawekezaji!! Sasa tujiulize je kuipitia hii mikataba sio kuiweka wazi kwa wananchi?

Tukumbuke kuwa kuipitia hii mikataba kwa bodi kama alivyoagiza waziri kunafaida ya kutuwezesha kujua wapi tulipotoka kwenye mikata iliyopita ili tusirudie makosa hayo kwenye mikataba ijayo!! Sio lazima kuwa unapoipitia upya mikataba na ukagundua mapungufu [ mapungufu ya makusudi ya mafisadi ili watu wapate 10% wanazoficha USWISI] hayo mapungufu yatarekebishwa kama tulivyojifunza kwenye mikataba ya madini kuwa ukisha ingia mikataba hii ni lazima uheshimu sheria za kimataifa!! Tanapozungumzia dhana ya kuwa wazi kwa mikataba sio maana yake kila mmoja wetu atapata nafasi ya kuisoma bali wale wawakilishi wetu wakiwa ni wajumbe wa bodi husika au kamati za bunge zenye wajumbe wazalendo na wenye weledi wao wanaweza kuwakilisha jamii katika kukagua na kuona kama mikataba inakidhi matakwa ya jamii yetu.

Hivyo basi kitendo cha Muhongo kuwapa wajumbe wa bodi adidu za rejea za kuipitia ile mikataba ya gesi haitawakatisha tamaa wawekezaji kwa sisi kunufaika nayo kwani wao wanazihiitaji maliasili zetu kwa manufaa yao kama sisi tunavyowahitaji wao ,hivyo ni lazima tunegotiate nao from a strong position badala ya kuwa wanyonge!!
 
Wanajamii,

ZZK ametoa maelezo yake ya utetezi. Nadhani ni utetezi mzuri. Busara ingetutuma tujadili utetezi huo badala ya kumjadili yeye binafsi. hapa tunatoka nje ya mjadala. Nashauri turejee huko. Vinginevyo tusiendelee kulalama kwamba taifa halipati chochote kutokana na raslimali zake nyingi. Hii ndiyo hoja ya ZZK pamoja na mfano wa kampuni ya kirusi inayotka kuvuna urani yetu bila kulipa kodi inayostahili na hali watoto wa shule za msing wanakaa chini, sekondari hawana maabara, hospitali hazitoshi na zilizopo nyingi hazina vifaa vya kupimia, watabibu nk. Aidha bajeti ya serikali imeendelea kuwa tegemezi wakati taifa halina viwanda vya kulisaidia kuingia katika ushindani wa karne ya 21.

Wakati makampuniya kigeni hayalipi kodi zinazotakiwa, wenyeji wakamuliwa kwa kodi zakila aina pamoja na VAT. Tunalalamika sana kwamba viwango vya kodi ni vikubwa lakini hatutaki kukuna vichwa kupanua wigo kwa kutoza haya makampuni yanayovuna raslimali zetu bure. Changamoto ni nyingi, na madini yetu yangetuwezesha angalao kufanya zaidi na kwa kasi kubwa. Hii ndiyo hoja ya ZZK. Kwa nini tunasita kuijadili?
 
Nimewahi kusoma na vijana wengi kutoka Kigoma wakati nikiwa sekondari, na pia Chuoni. Nilichokuja kugundua wachache wanatabia ya usaliti wakiweka mbele masilahi binafsi. Wako ladhi kumsaliti yeyote na kuvujisha siri za ndani kabisa ili mradi tu waweze kufikia malengo yao.

Kulikuwa na katibu mkuu wa Chadema - Dr Walid Amani Kaborou, huyu usaliti wake kwa upinzani kila mmoja anauelewa. Amekuwepo pia Daniel Nsanzugwanko wa NCCR. Huyu pia anajulikana kwa usaliti wake. Kafulila amejaribu Chadema, akashindwa, NCCR pia ameshindwa. Hawa ni wachache, lakini pia kule chuoni alikuwepo rafiki yangu kutoka Kigoma ambaye kwa hakika alikuwa ni msaliti wa aina ile ile kama akina Walid Kaborou, siwezi kusimulia sana juu yake

Zito Kabwe ni msaliti na anajli zaidi maslahi binafsi. Baada ya kujipatia umaarufu, akiwa kijana kati ya Vijana wachache ndani ya bunge, akaweza kukaa karibu na rais na kukutana na viongozi mbalimbali duniani akaona anaweza kufanya lolote bila kujali amewezaje kufika hapo alipo.

Zito ni msaliti. Mtakaumbuka 2010 wakati wa kampeni, badala ya kumkampenia mgombea urais wa Chadema yeye alikuwa akitangaza kuwa 2015 atagombea urais. Kwa mwenye akili anaelewa huyu kijana namna gani vipi!

Zito huyu huyu, wakati wa vuguvugu la kutangaza matokeo ya urais, yeye yuko bize na Jack Zoka, afisa usalama anayeshughulika na siasa. Na walikuwa wakiwasiliana mara kwa mara. Hapa shaka kuu ipo kwa huyu bwana mdogo.

Zito, wakati wenzake wanaimarisha chama, yeye anajitangazia kugombea urais na hata siku moja hajawahi kushughulika na harakati za M4C. Kuna jambo hapa. Ikiwa anataka urais kupitia chadema ataupataje akiwa chama kitabaki kuwa cha msimu.

Zito Kabwela, anafahamu fika kuwa, enzi hizo alikuwa na nafasi kubwa ya kuweza kushika madaraka ya juu ndani ya chama na hata ya nchi ikiwa chama kingeweza kufanya vizuri katika uchaguzi mkuu siku zijazo. Lakini sasa matumaini hayo yanafutika taratibu baada ya kuona kuna Vijana wengi, wenye maono na uwezo mkubwa pengine kushinda hata yeye wameibuka chadema. Mfano Tundu Lissu, John Mnyika, Godbless Lema, Benson Kigaila na wengine. Sasa kwa kuelewa hili na kwa sababu za ubinafsi na usaliti anajaribu kutafuta namna ya kukivuruga chama, akiondoe kwenye lengo la msingi la kuimarisha uhai wa chama.

Zito Kabwe, atakuwa ndumila kuwili. Anatumwa na kutumiwa na pia ana tabia ya kujipendeza kwa wenye madaraka.

Conclusion: Zito anajiona anaweza, lakini namhakikishia hataweza. Kaborou alikuwa maarufu kumshinda yeye, Mrema (Augustino) alikuwa maarufu kumshinda yeye, lakini leo yupo wapi.

Kama ilivyo kwa wakristo, Yesu Kristo aliwaambia mitume wake "Sikuwachagua mitume 12 na mmoja wenu ni shetani?"

Wito wangu kwa WanaChadema, mjue kuna Viongozi wengi lakini miongoni mwao kuna wasaliti na mmoja wao ni Zito Zuberi Kabwe. Kwa mataendo yake kwa ustawi wa chama anajidhihirisha wazi.

Chadema, nawasihi muishi na huyu mtu kama mlivyoweza kuishi hata na Shibuda, mwisho wa siku ataamua kujinyonga mwenyewe kwani anguko lake litakuwa kubwa na la aibu.
Ni keli mkuu
 
ZZK ndugu yangu mbona ghafla mabadiliko? Umelipwa bei gani kuja kuvuruga? Lakini leo ninakuapisha mbele ya Mungu kama una mpango wa shetani!! wa kutumwa kuvuruga basi hutofika popote!!

Kwa sababu mpango wa ukombozi wa TZ ni mpango wa Mungu. Na soma katika vitabu vyote yaliyowapata wale waliojaribu kuingilia mpango wa Mungu!! Tafadhali sana!! tulia uongozi utaupata na hata urais!! Lakini kwa mtindo huu wa kuwafanya hata maadui wa CDM wakachekelea hutosamehewa believe me!!
mkuu umekurupuka kumkemea zitto bila kuwa na hoja ya msingi,wewe ndo hutasamehewa kwa kurudisha nyuma juhudi za zitto katika kutetea gesi na madini yetu
 
JOHNSON Mbwambo ameandika katika Gazeti la Raia Mwema la Oktoba 3, mwaka huu, kuhusu dhihaka za Zitto kwa Prof. Muhongo (Waziri wa Nishati na Madini).

Nimesoma na nimemuelewa.

Kwanza naomba radhi iwapo tafsiri ya taarifa yangu niliyoitoa kwa vyombo vya habari na kuwekwa kwenye blogu yangu (zittokabwe.com) ilikuwa ina dhihaka.

Nimefundishwa kutodhihaki watu na hasa watu wanaonizidi umri na siasa zangu sio za dhihaka bali za masuala (issues). Kupitia kwa ndugu Mbwambo naomba radhi kwa wote walioona kuna dhihaka katika andiko langu. Sikuwa na nia ya kumdhihaki Waziri Muhongo. Nia yangu ni kuonyesha kuwa Waziri Muhongo alichokifanya ni kuwacheza shere Watanzania, kwa kuwaambia maneno ambayo yeye mwenyewe alikuwa anaamini kuwa hayawezekani.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Wizara yake, Eliakim Maswi, ilithibitisha kauli yangu siku chache tu baada ya kuitoa. Mbwambo kaandika makala yake kana kwamba hapakuwa na kauli ya kufuta maneno ya Waziri. Ninaamini Mbwambo aliiona kauli ile lakini aliamua kupuuza ili kujifurahisha na imani yake kwa Prof. Muhongo na mawaziri aliowataja kwenye makala yake kwamba ni mawakala wa mabadiliko. Mbwambo anaamini kabisa kwamba ndani ya utawala wa CCM, kuna mawaziri wenye nia ya dhati ya kuleta mabadiliko.

Nieleze wazi kwamba nilishtuka sana kuona toleo moja la Gazeti la Raia Mwema likiwa na makala tatu, zote dhidi ya Zitto Kabwe. Wakati makala ya ndugu Mbwambo ilikuwa inahusu suala nyeti sana la rasilimali za taifa na ni makala nzuri yenye mafundisho, makala mbili nyingine zilikuwa ni za siasa dhidi ya Zitto. Mwandishi Mayage Mayage aliandika makala yenye kichwa cha habari “Zitto, Urais 2015 kwa chama gani?” na Mwanasafu wa gazeti hili la Raia Mwema, Evarist Chahali aliandika makala yenye kichwa cha habari “Rais Kikwete anapofikiri kama Kabwe Zitto.”

Namwambia Mayage akasome vizuri historia ya ujenzi wa CHADEMA. Yeye anadhani CHADEMA imeanza mwaka 2010. CHADEMA kimejengwa na watu, si mtu mmoja. Wanaoamua mgombea wa chama si watu wachache anaowadhani yeye Mayage bali ni wanachama wa CHADEMA kutoka sehemu mbalimbali za Tanzania, ikiwamo Munanila, mkoani Kigoma anapotoka Mayage.

Huyu Chahali anasema ananijua sana. Inawezekana ananijua kuliko mimi ninavyojijua. Lakini mimi simjui na wala sijawahi kumwona ana kwa ana, nimekuwa nikimwona tu kwenye mitandao ya kijamii akinizushia, kunitukana na kunisema. Sikushangaa kusoma makala yake ya wiki iliyopita. Wote wawili nawakumbusha msemo wa Mahatma Gandhi aliposema; “Kwanza wanakudharau, kisha wanakucheka, kisha wanapambana na wewe, kisha unashinda".

Sasa nirejee kwenye makala ya ndugu Mbwambo. Prof. Muhongo simjui, licha ya kwamba nimekuwa mmoja wa wabunge walioko mstari wa mbele kuhakikisha utajiri wa nchi unatumika kwa manufaa ya nchi, sikuwahi kumsikia Prof. Muhongo mpaka alipoteuliwa kuwa Waziri wa Nishati na Madini.

Sikuwahi kusikia akipaza sauti yake dhidi ya mikataba mibovu ya madini licha ya kwamba yeye ni msomi aliyebobea katika masuala ya miamba. Wakati Bunge la tisa, chini ya Spika Samuel Sitta, likiwa limecharuka kutaka mikataba mibovu ipitiwe na kubadilishwa tulitarajia sana kupata ushauri wa wataalamu wetu lakini hawakuonekana, "walikwina"?

Walikuwa waoga kusema maana wangeharibu uhusiano kati yao na watawala. Tulihangaika wenyewe bila maarifa yoyote kuhusu sekta ya madini. Wengine ilibidi kuacha kazi za ubunge na kwenda masomoni ili kuongeza ujuzi wa masuala ya kisheria na kiuchumi kuhusu sekta ya rasilimali (madini na mafuta).

Wasomi wetu hawakuwa nasi. Walichague kuendelea kufanya kazi za ushauri kwa kampuni za utafutaji madini nchini. Leo Mbwambo anawaona hawa ndiyo mawakala wa mabadiliko. Labda anasema kweli. Ila mimi nimekata tamaa na mabadiliko kuletwa na watu waliomo serikalini, kwa sababu kadhaa.

Moja, kama alivyosema ndugu Mbwambo, nilipigia kelele sana mkataba wa Buzwagi na mikataba mingine ya madini. Niliendelea kupiga kelele mpaka sheria mpya ya madini ilipopitishwa na Bunge. Nimuulize Mbwambo kwamba, licha ya sheria mpya kuandikwa imechukua miaka mingapi kampuni za madini kufanya kazi zao kwa kutumia sheria hiyo mpya? Je, mikataba mingapi iliyopitiwa imerekebishwa au hata kuvunjwa? Pengine niwasaidie kuwakumbusha taarifa kwamba, hakuna kilichofanyika kwa mujibu wa sheria mpya, licha ya kufuatilia kwa kina bungeni kupitia michango na hata maswali bungeni sambamba na makala mbalimbali.

Tangu Waziri Prof. Muhongo na timu yake waingie ofisini ni maneno tu tunayosikia bila matendo. Hata suala la mgawo wa umeme ambalo ndugu Mbwambo analisema kama mfano, yeye anajua namna ambavyo wananchi wanalalamikia umeme kukatika hovyo, tena bila taarifa wala maelezo. Muhongo alifanikiwa sana kuaminisha watu wenye mawazo huru kama Mbwambo wakamwona yupo sahihi kiasi hata cha kufumbia macho mgawo wa umeme usio na maelezo, unaoendelea nchini.

Siwaamini mawaziri kwa sababu wanasema lolote linalowajia midomoni mwao hata kama wanaamini kuwa wanalosema haliwezekani kutekelezwa. Waziri wa Nishati na Madini alisema kuhusu mikataba ya mafuta na gesi ili kufurahisha watu. Huo ni msingi wa kwanza wa kauli yangu ambayo ndugu yangu Mbwambo ameitafsiri kuwa ni dhihaka. Nilikuwa nasema ukweli mchungu kwamba, serikali haiwezi kufanya lolote kuhusu mikataba. Nilitoa changamoto kuwa kama serikali kweli imedhamiria, iweke mikataba hii wazi. Je, wameiweka wazi?

Pili, Waziri wa Nishati na Madini anataka umma umwone kwamba anajua sana masuala ya sekta kuliko Mtanzania mwingine yeyote. Nitatoa mfano mmoja unaonihusu moja kwa moja. Katika mkutano wa Bunge uliopita, Tanzania ilitembelewa na Waziri Mkuu mstaafu wa Urusi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Kirusi iliyonunua leseni ya kutafuta uranium kule Selous. Kampuni ya UraniumOne iliyonunua leseni hii ya Mkuju River Project kutoka Kampuni ya Mantra ya Australia, kwa dola za Marekani milioni 980.

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ilitaka ilipwe kodi ya ongezeko la mtaji (capital gains tax) kampuni hii ilikataa. TRA wakaenda mahakamani kudai malipo ya kodi yenye thamani ya dola za Marekani milioni 116 ambazo ni sawa na asilimia 20 ya thamani ya mauzo na kesi inaendelea. Kwa mujibu wa sheria zetu kampuni zinapouziana leseni, lazima Waziri wa Nishati na Madini atoe idhini ya mauzo hayo. Mgeni huyo kutoka Urusi alikuja nchini kupigia debe idhini hii, ili itolewe leseni maalumu ya uchimbaji (special mining licence).

Nikasimama kutoa taarifa bungeni kwamba mawaziri wanakutana na huyu Waziri Mkuu mstaafu wa Urusi kuhusu leseni ya Mkuju River Project na kuweka wazi kwamba Kampuni ya UraniumOne hawajalipa kodi ya capital gains. Nilisimama kutoa taarifa baada ya majibu ya Waziri Muhongo kwamba, kilichouzwa si kampuni ya Tanzania bali Australia na hivyo hakuna kodi.

Kwa makusudi kabisa niliacha habari ya kesi ya TRA dhidi ya kampuni hii ili kuona umakini wa mawaziri wetu wapya kabla ya kukutana na lobbyists (washawishi) wa kampuni hizi za madini. Waziri Muhongo aliposimamishwa na Naibu Spika, Job Ndugai, akasema “Sisi tunajua zaidi kuliko Zitto" Kwanza Waziri hakuwa anajua.

Ni makosa kabisa kujadili suala ambalo mamlaka mojawapo ya nchi wamelipeleka mahakamani na linasubiri uamuzi. Lakini suala la Waziri kutokuwa na taarifa lilidhibitishwa na ujio wa Naibu Waziri George Simbachawene, aliponifuata na kuomba "details" kuhusu taarifa niliyotoa. Kulikuwa na haja gani kwa Waziri kusema bungeni yeye anajua zaidi na baadaye kumtuma Naibu wake kutafuta taarifa?

Huu ni udhaifu mkubwa sana wa uongozi. Kutojua si makosa, inawezekana kuwa wengine hatukusomea miamba lakini tumesomea masuala ya kodi kwenye madini na mafuta. Waziri makini anayejali nchi yake anawezaje kukutana na mwekezaji anayekataa kukulipa kodi yako bila wewe hata kuulizia utalipwa lini?

Unaulizwa bungeni unasema "ninajua zaidi" na Mwandishi mahiri kama Mbwambo anasema "mpeni nafasi atende"!

Nilipomsikia Waziri anasema ameagiza TPDC (Shirika la Maendeleo la Mafuta) kupitia mikataba nikajua na hili nalo hajui. Amesema tu ili watu wafurahi kwamba mikataba inapitiwa. Kupitia mikataba bila kuchukua hatua dhidi ya mikataba mibovu ni nini kama sio kutafuta umaarufu tu? Unapitia mikataba ili iwe nini kama huwezi kuchukua hatua?

Kuna mikataba ambayo imeingiwa kwa rushwa, sheria zetu zinasema kuwa mikataba iliyoingiwa kwa rushwa ni sawa na haipo. Hata sheria za kimataifa za mikataba zinatambua hivyo. Waziri anaposema kuwa tunapitia mikataba ili kuhakikisha kuwa mikataba ijayo inakuwa mizuri ni kichekesho. Hivi tunajua vitalu vingapi vimegawiwa na vingapi vimebaki? Hivi sasa kuna mikataba 29 na leseni 26. Vitalu vilivyobaki hivi sasa ni tisa tu.

Wizara inatuambia tunaangalia hii mikataba 29 ili kuboresha 9. Haya si mapitio bali ni kuangalia tu kama nilivyosema katika sentensi iliyotangulia. Mapitio bora zaidi ni uwazi wa mikataba yote tuliyoingia mpaka sasa na kuzuia kabisa mikataba mipya wala kugawa vitalu vipya vya kutafuta mafuta na gesi.

Uporaji wa rasilimali ni wa namna mbili, moja ni watu wachache na kampuni zao kupora kwa kupitia mikataba mibovu na pili ni kizazi kimoja kunyonya rasilimali zote bila kujali kizazi kijacho. Katika maandiko yangu nimeshauri kuwa tusigawe vitalu vipya mpaka tuone mafanikio ya mikataba hii 29 na leseni 26 tulizonazo hivi sasa. Wito wangu ni mmoja tu, uwazi wa mikataba. Kutaka uwazi si dhihaka. Uwazi ni uwajibikaji.

Suala la mapitio ya mikataba kwa jicho la juu juu ni suala la kuunga mkono. Lakini ukitazama historia ya nchi yetu katika masuala haya utabaini kwamba tunapaswa kufanya zaidi ya mapitio ya mikataba.

Tunapaswa kufanya jambo ambalo hatujawahi kulifanya nalo ni kuiweka wazi mikataba hii kwa umma. Hii ndiyo hoja yangu.

Inawezekana kabisa kwamba maneno niliyotumia yameudhi watu fulani lakini ikumbukwe mimi ni Mbunge wa Upinzani na ni wajibu wangu kukosoa serikali kila inapowezekana. Bahati nzuri miaka yangu saba bungeni hivi sasa imetumika kwa kiasi kikubwa sana katika kufuatilia kwa karibu sekta ya madini, mafuta na gesi. Ni rahisi sana mimi kuweza kuona suala linalosemwa na serikali linasemwa tu au serikali inamaanisha? Katika suala la mapitio ya mikataba kwenye sekta ya madini na mafuta kwa kweli serikali haipo makini. Watu wajuvi wa mambo kama kina Mbwambo wanapaswa kwenda zaidi ya mapitio na kutaka mikataba iwekwe wazi na kuchambuliwa kwa uwazi kabisa.

Waziri Muhongo anayo nafasi ya kufanya kazi yake, afanye kazi yake bila bugudha. Mbwambo ajue kuwa Mbunge Zitto pia anayo kazi yake kwa mujibu wa Katiba ibara ya 63 nayo ni "kuisimamia" serikali. Niacheni nami nifanye kazi yangu.

Makala hii iliyoandikwa na Kabwe Zitto, Mbunge wa Kigoma Kaskazini ni majibu kwa makala iliyoandikwa na Mwanasafu wetu, Johnson Mbwambo, katika toleo lililopita la gazeti hili la Raia Mwema, kupitia safu yake ya Tafakuri Jadidi.
Ni makala nzuri na Zitto kanikumbusha mazungumuzo baada ya habir ya zamani sana,kulikuwa na ili suala la ALIKWINA[wakati tunajenga chama ulikuwa wapi]Ukiachilia ilo Zitto aelewe kwamba he is not as pupular as he used to be,muda unavyokwenda anazidi kujipambanua na watu wanamuelewa zaidi,wenzake wakina HECHE hawalali wako busy kujenga chama yeye anawazia uraisi,pia asipende sana kuongea ongea kwenye magazeti,mbona Lowasa haongei ongei hovyo and yet he is strong?sometimes silence is more wiser.
 
Nimewahi kusoma na vijana wengi kutoka Kigoma wakati nikiwa sekondari, na pia Chuoni. Nilichokuja kugundua wachache wanatabia ya usaliti wakiweka mbele masilahi binafsi. Wako ladhi kumsaliti yeyote na kuvujisha siri za ndani kabisa ili mradi tu waweze kufikia malengo yao.

Kulikuwa na katibu mkuu wa Chadema - Dr Walid Amani Kaborou, huyu usaliti wake kwa upinzani kila mmoja anauelewa. Amekuwepo pia Daniel Nsanzugwanko wa NCCR. Huyu pia anajulikana kwa usaliti wake. Kafulila amejaribu Chadema, akashindwa, NCCR pia ameshindwa. Hawa ni wachache, lakini pia kule chuoni alikuwepo rafiki yangu kutoka Kigoma ambaye kwa hakika alikuwa ni msaliti wa aina ile ile kama akina Walid Kaborou, siwezi kusimulia sana juu yake

Zito Kabwe ni msaliti na anajli zaidi maslahi binafsi. Baada ya kujipatia umaarufu, akiwa kijana kati ya Vijana wachache ndani ya bunge, akaweza kukaa karibu na rais na kukutana na viongozi mbalimbali duniani akaona anaweza kufanya lolote bila kujali amewezaje kufika hapo alipo.

Zito ni msaliti. Mtakaumbuka 2010 wakati wa kampeni, badala ya kumkampenia mgombea urais wa Chadema yeye alikuwa akitangaza kuwa 2015 atagombea urais. Kwa mwenye akili anaelewa huyu kijana namna gani vipi!

Zito huyu huyu, wakati wa vuguvugu la kutangaza matokeo ya urais, yeye yuko bize na Jack Zoka, afisa usalama anayeshughulika na siasa. Na walikuwa wakiwasiliana mara kwa mara. Hapa shaka kuu ipo kwa huyu bwana mdogo.

Zito, wakati wenzake wanaimarisha chama, yeye anajitangazia kugombea urais na hata siku moja hajawahi kushughulika na harakati za M4C. Kuna jambo hapa. Ikiwa anataka urais kupitia chadema ataupataje akiwa chama kitabaki kuwa cha msimu.

Zito Kabwela, anafahamu fika kuwa, enzi hizo alikuwa na nafasi kubwa ya kuweza kushika madaraka ya juu ndani ya chama na hata ya nchi ikiwa chama kingeweza kufanya vizuri katika uchaguzi mkuu siku zijazo. Lakini sasa matumaini hayo yanafutika taratibu baada ya kuona kuna Vijana wengi, wenye maono na uwezo mkubwa pengine kushinda hata yeye wameibuka chadema. Mfano Tundu Lissu, John Mnyika, Godbless Lema, Benson Kigaila na wengine. Sasa kwa kuelewa hili na kwa sababu za ubinafsi na usaliti anajaribu kutafuta namna ya kukivuruga chama, akiondoe kwenye lengo la msingi la kuimarisha uhai wa chama.

Zito Kabwe, atakuwa ndumila kuwili. Anatumwa na kutumiwa na pia ana tabia ya kujipendeza kwa wenye madaraka.

Conclusion: Zito anajiona anaweza, lakini namhakikishia hataweza. Kaborou alikuwa maarufu kumshinda yeye, Mrema (Augustino) alikuwa maarufu kumshinda yeye, lakini leo yupo wapi.

Kama ilivyo kwa wakristo, Yesu Kristo aliwaambia mitume wake "Sikuwachagua mitume 12 na mmoja wenu ni shetani?"

Wito wangu kwa WanaChadema, mjue kuna Viongozi wengi lakini miongoni mwao kuna wasaliti na mmoja wao ni Zito Zuberi Kabwe. Kwa mataendo yake kwa ustawi wa chama anajidhihirisha wazi.

Chadema, nawasihi muishi na huyu mtu kama mlivyoweza kuishi hata na Shibuda, mwisho wa siku ataamua kujinyonga mwenyewe kwani anguko lake litakuwa kubwa na la aibu.

Tumeyasikia vizuri hayo mapungufu makubwa ya zito!Lakini
mimi naona unge focus kwenye mada yake. Hebu zungumzia basi yale yaliyomo kwenye hii thread ambayo amegusia kwa ufasaha hizi rasilimali kuu (madini,mafuta na gass) pamoja na mikataba yake
 
hizi ngonjera za ZZK zimenichosha, huyu jamaa cna hakika km anajua anafanya nini na anatafuta nini, maana haeleweki, nikama kinyonga, watu wa namna hii ni hatari kwa taifa letu na chama chake kwa ujumla.
 
Let's discuss what has been brought before us, na sio kudiscuss mtu. Jamaa kaleta hoja yake nzito kweli kweli, tuisome na kuichambua. Tuache kumdiscuss mleta mada. Tunapoteza maana halisi ya forum yenyewe. Ina maana yeye sasa hivi haruhusiwi kuongea chochote kwa ajili alishatangaza nia?poor thinking...
ZZK umeleta issue ya maana sana, kwa wanaoelewa issues wameshaelewa, kwa wapika majungu wamepata kingine cha kuongea...
 
JOHNSON Mbwambo ameandika katika Gazeti la Raia Mwema la Oktoba 3, mwaka huu, kuhusu dhihaka za Zitto kwa Prof. Muhongo (Waziri wa Nishati na Madini).

Nimesoma na nimemuelewa.

Kwanza naomba radhi iwapo tafsiri ya taarifa yangu niliyoitoa kwa vyombo vya habari na kuwekwa kwenye blogu yangu (zittokabwe.com) ilikuwa ina dhihaka.

Nimefundishwa kutodhihaki watu na hasa watu wanaonizidi umri na siasa zangu sio za dhihaka bali za masuala (issues). Kupitia kwa ndugu Mbwambo naomba radhi kwa wote walioona kuna dhihaka katika andiko langu. Sikuwa na nia ya kumdhihaki Waziri Muhongo. Nia yangu ni kuonyesha kuwa Waziri Muhongo alichokifanya ni kuwacheza shere Watanzania, kwa kuwaambia maneno ambayo yeye mwenyewe alikuwa anaamini kuwa hayawezekani.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Wizara yake, Eliakim Maswi, ilithibitisha kauli yangu siku chache tu baada ya kuitoa. Mbwambo kaandika makala yake kana kwamba hapakuwa na kauli ya kufuta maneno ya Waziri. Ninaamini Mbwambo aliiona kauli ile lakini aliamua kupuuza ili kujifurahisha na imani yake kwa Prof. Muhongo na mawaziri aliowataja kwenye makala yake kwamba ni mawakala wa mabadiliko. Mbwambo anaamini kabisa kwamba ndani ya utawala wa CCM, kuna mawaziri wenye nia ya dhati ya kuleta mabadiliko.

Nieleze wazi kwamba nilishtuka sana kuona toleo moja la Gazeti la Raia Mwema likiwa na makala tatu, zote dhidi ya Zitto Kabwe. Wakati makala ya ndugu Mbwambo ilikuwa inahusu suala nyeti sana la rasilimali za taifa na ni makala nzuri yenye mafundisho, makala mbili nyingine zilikuwa ni za siasa dhidi ya Zitto. Mwandishi Mayage Mayage aliandika makala yenye kichwa cha habari “Zitto, Urais 2015 kwa chama gani?” na Mwanasafu wa gazeti hili la Raia Mwema, Evarist Chahali aliandika makala yenye kichwa cha habari “Rais Kikwete anapofikiri kama Kabwe Zitto.”

Namwambia Mayage akasome vizuri historia ya ujenzi wa CHADEMA. Yeye anadhani CHADEMA imeanza mwaka 2010. CHADEMA kimejengwa na watu, si mtu mmoja. Wanaoamua mgombea wa chama si watu wachache anaowadhani yeye Mayage bali ni wanachama wa CHADEMA kutoka sehemu mbalimbali za Tanzania, ikiwamo Munanila, mkoani Kigoma anapotoka Mayage.

Huyu Chahali anasema ananijua sana. Inawezekana ananijua kuliko mimi ninavyojijua. Lakini mimi simjui na wala sijawahi kumwona ana kwa ana, nimekuwa nikimwona tu kwenye mitandao ya kijamii akinizushia, kunitukana na kunisema. Sikushangaa kusoma makala yake ya wiki iliyopita. Wote wawili nawakumbusha msemo wa Mahatma Gandhi aliposema; “Kwanza wanakudharau, kisha wanakucheka, kisha wanapambana na wewe, kisha unashinda".

Sasa nirejee kwenye makala ya ndugu Mbwambo. Prof. Muhongo simjui, licha ya kwamba nimekuwa mmoja wa wabunge walioko mstari wa mbele kuhakikisha utajiri wa nchi unatumika kwa manufaa ya nchi, sikuwahi kumsikia Prof. Muhongo mpaka alipoteuliwa kuwa Waziri wa Nishati na Madini.

Sikuwahi kusikia akipaza sauti yake dhidi ya mikataba mibovu ya madini licha ya kwamba yeye ni msomi aliyebobea katika masuala ya miamba. Wakati Bunge la tisa, chini ya Spika Samuel Sitta, likiwa limecharuka kutaka mikataba mibovu ipitiwe na kubadilishwa tulitarajia sana kupata ushauri wa wataalamu wetu lakini hawakuonekana, "walikwina"?

Walikuwa waoga kusema maana wangeharibu uhusiano kati yao na watawala. Tulihangaika wenyewe bila maarifa yoyote kuhusu sekta ya madini. Wengine ilibidi kuacha kazi za ubunge na kwenda masomoni ili kuongeza ujuzi wa masuala ya kisheria na kiuchumi kuhusu sekta ya rasilimali (madini na mafuta).

Wasomi wetu hawakuwa nasi. Walichague kuendelea kufanya kazi za ushauri kwa kampuni za utafutaji madini nchini. Leo Mbwambo anawaona hawa ndiyo mawakala wa mabadiliko. Labda anasema kweli. Ila mimi nimekata tamaa na mabadiliko kuletwa na watu waliomo serikalini, kwa sababu kadhaa.

Moja, kama alivyosema ndugu Mbwambo, nilipigia kelele sana mkataba wa Buzwagi na mikataba mingine ya madini. Niliendelea kupiga kelele mpaka sheria mpya ya madini ilipopitishwa na Bunge. Nimuulize Mbwambo kwamba, licha ya sheria mpya kuandikwa imechukua miaka mingapi kampuni za madini kufanya kazi zao kwa kutumia sheria hiyo mpya? Je, mikataba mingapi iliyopitiwa imerekebishwa au hata kuvunjwa? Pengine niwasaidie kuwakumbusha taarifa kwamba, hakuna kilichofanyika kwa mujibu wa sheria mpya, licha ya kufuatilia kwa kina bungeni kupitia michango na hata maswali bungeni sambamba na makala mbalimbali.

Tangu Waziri Prof. Muhongo na timu yake waingie ofisini ni maneno tu tunayosikia bila matendo. Hata suala la mgawo wa umeme ambalo ndugu Mbwambo analisema kama mfano, yeye anajua namna ambavyo wananchi wanalalamikia umeme kukatika hovyo, tena bila taarifa wala maelezo. Muhongo alifanikiwa sana kuaminisha watu wenye mawazo huru kama Mbwambo wakamwona yupo sahihi kiasi hata cha kufumbia macho mgawo wa umeme usio na maelezo, unaoendelea nchini.

Siwaamini mawaziri kwa sababu wanasema lolote linalowajia midomoni mwao hata kama wanaamini kuwa wanalosema haliwezekani kutekelezwa. Waziri wa Nishati na Madini alisema kuhusu mikataba ya mafuta na gesi ili kufurahisha watu. Huo ni msingi wa kwanza wa kauli yangu ambayo ndugu yangu Mbwambo ameitafsiri kuwa ni dhihaka. Nilikuwa nasema ukweli mchungu kwamba, serikali haiwezi kufanya lolote kuhusu mikataba. Nilitoa changamoto kuwa kama serikali kweli imedhamiria, iweke mikataba hii wazi. Je, wameiweka wazi?

Pili, Waziri wa Nishati na Madini anataka umma umwone kwamba anajua sana masuala ya sekta kuliko Mtanzania mwingine yeyote. Nitatoa mfano mmoja unaonihusu moja kwa moja. Katika mkutano wa Bunge uliopita, Tanzania ilitembelewa na Waziri Mkuu mstaafu wa Urusi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Kirusi iliyonunua leseni ya kutafuta uranium kule Selous. Kampuni ya UraniumOne iliyonunua leseni hii ya Mkuju River Project kutoka Kampuni ya Mantra ya Australia, kwa dola za Marekani milioni 980.

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ilitaka ilipwe kodi ya ongezeko la mtaji (capital gains tax) kampuni hii ilikataa. TRA wakaenda mahakamani kudai malipo ya kodi yenye thamani ya dola za Marekani milioni 116 ambazo ni sawa na asilimia 20 ya thamani ya mauzo na kesi inaendelea. Kwa mujibu wa sheria zetu kampuni zinapouziana leseni, lazima Waziri wa Nishati na Madini atoe idhini ya mauzo hayo. Mgeni huyo kutoka Urusi alikuja nchini kupigia debe idhini hii, ili itolewe leseni maalumu ya uchimbaji (special mining licence).

Nikasimama kutoa taarifa bungeni kwamba mawaziri wanakutana na huyu Waziri Mkuu mstaafu wa Urusi kuhusu leseni ya Mkuju River Project na kuweka wazi kwamba Kampuni ya UraniumOne hawajalipa kodi ya capital gains. Nilisimama kutoa taarifa baada ya majibu ya Waziri Muhongo kwamba, kilichouzwa si kampuni ya Tanzania bali Australia na hivyo hakuna kodi.

Kwa makusudi kabisa niliacha habari ya kesi ya TRA dhidi ya kampuni hii ili kuona umakini wa mawaziri wetu wapya kabla ya kukutana na lobbyists (washawishi) wa kampuni hizi za madini. Waziri Muhongo aliposimamishwa na Naibu Spika, Job Ndugai, akasema “Sisi tunajua zaidi kuliko Zitto" Kwanza Waziri hakuwa anajua.

Ni makosa kabisa kujadili suala ambalo mamlaka mojawapo ya nchi wamelipeleka mahakamani na linasubiri uamuzi. Lakini suala la Waziri kutokuwa na taarifa lilidhibitishwa na ujio wa Naibu Waziri George Simbachawene, aliponifuata na kuomba "details" kuhusu taarifa niliyotoa. Kulikuwa na haja gani kwa Waziri kusema bungeni yeye anajua zaidi na baadaye kumtuma Naibu wake kutafuta taarifa?

Huu ni udhaifu mkubwa sana wa uongozi. Kutojua si makosa, inawezekana kuwa wengine hatukusomea miamba lakini tumesomea masuala ya kodi kwenye madini na mafuta. Waziri makini anayejali nchi yake anawezaje kukutana na mwekezaji anayekataa kukulipa kodi yako bila wewe hata kuulizia utalipwa lini?

Unaulizwa bungeni unasema "ninajua zaidi" na Mwandishi mahiri kama Mbwambo anasema "mpeni nafasi atende"!

Nilipomsikia Waziri anasema ameagiza TPDC (Shirika la Maendeleo la Mafuta) kupitia mikataba nikajua na hili nalo hajui. Amesema tu ili watu wafurahi kwamba mikataba inapitiwa. Kupitia mikataba bila kuchukua hatua dhidi ya mikataba mibovu ni nini kama sio kutafuta umaarufu tu? Unapitia mikataba ili iwe nini kama huwezi kuchukua hatua?

Kuna mikataba ambayo imeingiwa kwa rushwa, sheria zetu zinasema kuwa mikataba iliyoingiwa kwa rushwa ni sawa na haipo. Hata sheria za kimataifa za mikataba zinatambua hivyo. Waziri anaposema kuwa tunapitia mikataba ili kuhakikisha kuwa mikataba ijayo inakuwa mizuri ni kichekesho. Hivi tunajua vitalu vingapi vimegawiwa na vingapi vimebaki? Hivi sasa kuna mikataba 29 na leseni 26. Vitalu vilivyobaki hivi sasa ni tisa tu.

Wizara inatuambia tunaangalia hii mikataba 29 ili kuboresha 9. Haya si mapitio bali ni kuangalia tu kama nilivyosema katika sentensi iliyotangulia. Mapitio bora zaidi ni uwazi wa mikataba yote tuliyoingia mpaka sasa na kuzuia kabisa mikataba mipya wala kugawa vitalu vipya vya kutafuta mafuta na gesi.

Uporaji wa rasilimali ni wa namna mbili, moja ni watu wachache na kampuni zao kupora kwa kupitia mikataba mibovu na pili ni kizazi kimoja kunyonya rasilimali zote bila kujali kizazi kijacho. Katika maandiko yangu nimeshauri kuwa tusigawe vitalu vipya mpaka tuone mafanikio ya mikataba hii 29 na leseni 26 tulizonazo hivi sasa. Wito wangu ni mmoja tu, uwazi wa mikataba. Kutaka uwazi si dhihaka. Uwazi ni uwajibikaji.

Suala la mapitio ya mikataba kwa jicho la juu juu ni suala la kuunga mkono. Lakini ukitazama historia ya nchi yetu katika masuala haya utabaini kwamba tunapaswa kufanya zaidi ya mapitio ya mikataba.

Tunapaswa kufanya jambo ambalo hatujawahi kulifanya nalo ni kuiweka wazi mikataba hii kwa umma. Hii ndiyo hoja yangu.

Inawezekana kabisa kwamba maneno niliyotumia yameudhi watu fulani lakini ikumbukwe mimi ni Mbunge wa Upinzani na ni wajibu wangu kukosoa serikali kila inapowezekana. Bahati nzuri miaka yangu saba bungeni hivi sasa imetumika kwa kiasi kikubwa sana katika kufuatilia kwa karibu sekta ya madini, mafuta na gesi. Ni rahisi sana mimi kuweza kuona suala linalosemwa na serikali linasemwa tu au serikali inamaanisha? Katika suala la mapitio ya mikataba kwenye sekta ya madini na mafuta kwa kweli serikali haipo makini. Watu wajuvi wa mambo kama kina Mbwambo wanapaswa kwenda zaidi ya mapitio na kutaka mikataba iwekwe wazi na kuchambuliwa kwa uwazi kabisa.

Waziri Muhongo anayo nafasi ya kufanya kazi yake, afanye kazi yake bila bugudha. Mbwambo ajue kuwa Mbunge Zitto pia anayo kazi yake kwa mujibu wa Katiba ibara ya 63 nayo ni "kuisimamia" serikali. Niacheni nami nifanye kazi yangu.

Makala hii iliyoandikwa na Kabwe Zitto, Mbunge wa Kigoma Kaskazini ni majibu kwa makala iliyoandikwa na Mwanasafu wetu, Johnson Mbwambo, katika toleo lililopita la gazeti hili la Raia Mwema, kupitia safu yake ya Tafakuri Jadidi.

....salute zzk...!!! hoja zako zina mashiko na uzito zaidi...makala ya mzalendo mwenzangu mbwambo imesaidia sana kupata kwa undani kile ambacho zzk akimaananisha ktk hoja zake dhidi ya "purofesa".....ilikuwa ni chachu iliyopelekea zzk aje na somo ambalo wengi hatukulielewa....mbwambo kwa mara ingine ametusaidia ss wa mitaani..jambo moja linabaki...kama kahuli za purofesa, ni moto ambao hauchelewi kugeuka moshi kama tunavyoelewa kutokana na ufafanuzi wa zzk, ni suala la muda...tutakaojaaliwa kuwa hai tutajua...na kama ni dhihaka kama ilivyoweka na mzalendo mwenzetu mbwambo...hali kadhalika...wote watatu wamechangia taifa kupitia michango yao ktk suala hili kwa sasa...wabarikiwe sana...again...salute to zzk.....!
 
ZZK for sure you need a Break. Kwa sasa we know un abifu na Prof. Upo impaired u cany judge well. Hii vita upo peke yako huku wanafiki wanaojua wataibika wakikusupport. Angalia Kaka dunia haina Siri.
 
frankly speaking hoja ya ZITTO ina mashiko naona watu wanamjadili Zitto na sio hoja yake. mimi binafsi naunga mkono hoja.
 
Duh, hiki timbwili si mchezo, ngoja tusubiri hiyo 2015 kama hamjachinjana kwa madaraka!
 
Sasa unaposema unakubaliana na Zitto kuhusu mikataba unakubaliana nae nini? Zitto katika jibu lake kwa hoja ya Mbwambo kuhusu DHIHAKA yake anasema yeye anataka kuwa mikataba iwe wazi [ transparent] lakini mkumbuke kuwa ni Zitto huyu huyo aliyesema hatua ya Porf. Muhongo kutaka kuipitia mikataba ya gesi ingewakatisha tamaa na kuwatisha wawekezaji!! Sasa tujiulize je kuipitia hii mikataba sio kuiweka wazi kwa wananchi?

Tukumbuke kuwa kuipitia hii mikataba kwa bodi kama alivyoagiza waziri kunafaida ya kutuwezesha kujua wapi tulipotoka kwenye mikata iliyopita ili tusirudie makosa hayo kwenye mikataba ijayo!! Sio lazima kuwa unapoipitia upya mikataba na ukagundua mapungufu [ mapungufu ya makusudi ya mafisadi ili watu wapate 10% wanazoficha USWISI] hayo mapungufu yatarekebishwa kama tulivyojifunza kwenye mikataba ya madini kuwa ukisha ingia mikataba hii ni lazima uheshimu sheria za kimataifa!! Tanapozungumzia dhana ya kuwa wazi kwa mikataba sio maana yake kila mmoja wetu atapata nafasi ya kuisoma bali wale wawakilishi wetu wakiwa ni wajumbe wa bodi husika au kamati za bunge zenye wajumbe wazalendo na wenye weledi wao wanaweza kuwakilisha jamii katika kukagua na kuona kama mikataba inakidhi matakwa ya jamii yetu.

Hivyo basi kitendo cha Muhongo kuwapa wajumbe wa bodi adidu za rejea za kuipitia ile mikataba ya gesi haitawakatisha tamaa wawekezaji kwa sisi kunufaika nayo kwani wao wanazihiitaji maliasili zetu kwa manufaa yao kama sisi tunavyowahitaji wao ,hivyo ni lazima tunegotiate nao from a strong position badala ya kuwa wanyonge!!

Nimependa ulivyoweka wazi kile Prof Muhongo alichosema maana wengine tulikuwa gizani. Kama kweli nia ni kuipitia mikataba ya gass na kubaini kilichomo ndani ya mikataba kwa nia ya uwazi, sioni kosa lolote. Tunawakatisha tamaa kivipi. Wao ni watafutaji na hii ni mali yetu tena adimu na wanaihitaji kwa faidi watakayopata. Hakuna cha kuwakatisha tamaa. Kwani umeambiwa gass inaoza ikaa? Wapo wengi wanaotafuta hiyo gass, wale kama wanaona kuweka mikataba yao wazi na kubaini wizi wao tunawakatisha tamaa acha waende na sisi tubaki na maliasili yetu watakuja wengine na tena kwa kutupigia magoti siyo sisi tuwapigie magoti
 
hizo ni hoja za msingi kabisa kutoka kwa zito, zinahitaji majibu ya kina.

kinachonikwaza ni tabia yako ya kujaribu kukivuruga chadema, kutokana na kupata mashaka nawe nashindwa kuelewa kama umeandika haya kama mtanzania au wakala wa mafisadi waliovuruga tanesco na madini yetu, i believe watu kama akina ngeleja wanatamani mawaziri waliochukua nafasi zao washindwe ili tuwakumbuke nakuwaona walikuwa bora.

Kama mwanasiasa unawajibu mkubwa sana kutuaminisha kuwa bado tunaimba wimbo mmoja.

JOHNSON Mbwambo ameandika katika Gazeti la Raia Mwema la Oktoba 3, mwaka huu, kuhusu dhihaka za Zitto kwa Prof. Muhongo (Waziri wa Nishati na Madini).

Nimesoma na nimemuelewa.

Kwanza naomba radhi iwapo tafsiri ya taarifa yangu niliyoitoa kwa vyombo vya habari na kuwekwa kwenye blogu yangu (zittokabwe.com) ilikuwa ina dhihaka.

Nimefundishwa kutodhihaki watu na hasa watu wanaonizidi umri na siasa zangu sio za dhihaka bali za masuala (issues). Kupitia kwa ndugu Mbwambo naomba radhi kwa wote walioona kuna dhihaka katika andiko langu. Sikuwa na nia ya kumdhihaki Waziri Muhongo. Nia yangu ni kuonyesha kuwa Waziri Muhongo alichokifanya ni kuwacheza shere Watanzania, kwa kuwaambia maneno ambayo yeye mwenyewe alikuwa anaamini kuwa hayawezekani.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Wizara yake, Eliakim Maswi, ilithibitisha kauli yangu siku chache tu baada ya kuitoa. Mbwambo kaandika makala yake kana kwamba hapakuwa na kauli ya kufuta maneno ya Waziri. Ninaamini Mbwambo aliiona kauli ile lakini aliamua kupuuza ili kujifurahisha na imani yake kwa Prof. Muhongo na mawaziri aliowataja kwenye makala yake kwamba ni mawakala wa mabadiliko. Mbwambo anaamini kabisa kwamba ndani ya utawala wa CCM, kuna mawaziri wenye nia ya dhati ya kuleta mabadiliko.

Nieleze wazi kwamba nilishtuka sana kuona toleo moja la Gazeti la Raia Mwema likiwa na makala tatu, zote dhidi ya Zitto Kabwe. Wakati makala ya ndugu Mbwambo ilikuwa inahusu suala nyeti sana la rasilimali za taifa na ni makala nzuri yenye mafundisho, makala mbili nyingine zilikuwa ni za siasa dhidi ya Zitto. Mwandishi Mayage Mayage aliandika makala yenye kichwa cha habari "Zitto, Urais 2015 kwa chama gani?" na Mwanasafu wa gazeti hili la Raia Mwema, Evarist Chahali aliandika makala yenye kichwa cha habari "Rais Kikwete anapofikiri kama Kabwe Zitto."

Namwambia Mayage akasome vizuri historia ya ujenzi wa CHADEMA. Yeye anadhani CHADEMA imeanza mwaka 2010. CHADEMA kimejengwa na watu, si mtu mmoja. Wanaoamua mgombea wa chama si watu wachache anaowadhani yeye Mayage bali ni wanachama wa CHADEMA kutoka sehemu mbalimbali za Tanzania, ikiwamo Munanila, mkoani Kigoma anapotoka Mayage.

Huyu Chahali anasema ananijua sana. Inawezekana ananijua kuliko mimi ninavyojijua. Lakini mimi simjui na wala sijawahi kumwona ana kwa ana, nimekuwa nikimwona tu kwenye mitandao ya kijamii akinizushia, kunitukana na kunisema. Sikushangaa kusoma makala yake ya wiki iliyopita. Wote wawili nawakumbusha msemo wa Mahatma Gandhi aliposema; "Kwanza wanakudharau, kisha wanakucheka, kisha wanapambana na wewe, kisha unashinda".

Sasa nirejee kwenye makala ya ndugu Mbwambo. Prof. Muhongo simjui, licha ya kwamba nimekuwa mmoja wa wabunge walioko mstari wa mbele kuhakikisha utajiri wa nchi unatumika kwa manufaa ya nchi, sikuwahi kumsikia Prof. Muhongo mpaka alipoteuliwa kuwa Waziri wa Nishati na Madini.

Sikuwahi kusikia akipaza sauti yake dhidi ya mikataba mibovu ya madini licha ya kwamba yeye ni msomi aliyebobea katika masuala ya miamba. Wakati Bunge la tisa, chini ya Spika Samuel Sitta, likiwa limecharuka kutaka mikataba mibovu ipitiwe na kubadilishwa tulitarajia sana kupata ushauri wa wataalamu wetu lakini hawakuonekana, "walikwina"?

Walikuwa waoga kusema maana wangeharibu uhusiano kati yao na watawala. Tulihangaika wenyewe bila maarifa yoyote kuhusu sekta ya madini. Wengine ilibidi kuacha kazi za ubunge na kwenda masomoni ili kuongeza ujuzi wa masuala ya kisheria na kiuchumi kuhusu sekta ya rasilimali (madini na mafuta).

Wasomi wetu hawakuwa nasi. Walichague kuendelea kufanya kazi za ushauri kwa kampuni za utafutaji madini nchini. Leo Mbwambo anawaona hawa ndiyo mawakala wa mabadiliko. Labda anasema kweli. Ila mimi nimekata tamaa na mabadiliko kuletwa na watu waliomo serikalini, kwa sababu kadhaa.

Moja, kama alivyosema ndugu Mbwambo, nilipigia kelele sana mkataba wa Buzwagi na mikataba mingine ya madini. Niliendelea kupiga kelele mpaka sheria mpya ya madini ilipopitishwa na Bunge. Nimuulize Mbwambo kwamba, licha ya sheria mpya kuandikwa imechukua miaka mingapi kampuni za madini kufanya kazi zao kwa kutumia sheria hiyo mpya? Je, mikataba mingapi iliyopitiwa imerekebishwa au hata kuvunjwa? Pengine niwasaidie kuwakumbusha taarifa kwamba, hakuna kilichofanyika kwa mujibu wa sheria mpya, licha ya kufuatilia kwa kina bungeni kupitia michango na hata maswali bungeni sambamba na makala mbalimbali.

Tangu Waziri Prof. Muhongo na timu yake waingie ofisini ni maneno tu tunayosikia bila matendo. Hata suala la mgawo wa umeme ambalo ndugu Mbwambo analisema kama mfano, yeye anajua namna ambavyo wananchi wanalalamikia umeme kukatika hovyo, tena bila taarifa wala maelezo. Muhongo alifanikiwa sana kuaminisha watu wenye mawazo huru kama Mbwambo wakamwona yupo sahihi kiasi hata cha kufumbia macho mgawo wa umeme usio na maelezo, unaoendelea nchini.

Siwaamini mawaziri kwa sababu wanasema lolote linalowajia midomoni mwao hata kama wanaamini kuwa wanalosema haliwezekani kutekelezwa. Waziri wa Nishati na Madini alisema kuhusu mikataba ya mafuta na gesi ili kufurahisha watu. Huo ni msingi wa kwanza wa kauli yangu ambayo ndugu yangu Mbwambo ameitafsiri kuwa ni dhihaka. Nilikuwa nasema ukweli mchungu kwamba, serikali haiwezi kufanya lolote kuhusu mikataba. Nilitoa changamoto kuwa kama serikali kweli imedhamiria, iweke mikataba hii wazi. Je, wameiweka wazi?

Pili, Waziri wa Nishati na Madini anataka umma umwone kwamba anajua sana masuala ya sekta kuliko Mtanzania mwingine yeyote. Nitatoa mfano mmoja unaonihusu moja kwa moja. Katika mkutano wa Bunge uliopita, Tanzania ilitembelewa na Waziri Mkuu mstaafu wa Urusi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Kirusi iliyonunua leseni ya kutafuta uranium kule Selous. Kampuni ya UraniumOne iliyonunua leseni hii ya Mkuju River Project kutoka Kampuni ya Mantra ya Australia, kwa dola za Marekani milioni 980.

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ilitaka ilipwe kodi ya ongezeko la mtaji (capital gains tax) kampuni hii ilikataa. TRA wakaenda mahakamani kudai malipo ya kodi yenye thamani ya dola za Marekani milioni 116 ambazo ni sawa na asilimia 20 ya thamani ya mauzo na kesi inaendelea. Kwa mujibu wa sheria zetu kampuni zinapouziana leseni, lazima Waziri wa Nishati na Madini atoe idhini ya mauzo hayo. Mgeni huyo kutoka Urusi alikuja nchini kupigia debe idhini hii, ili itolewe leseni maalumu ya uchimbaji (special mining licence).

Nikasimama kutoa taarifa bungeni kwamba mawaziri wanakutana na huyu Waziri Mkuu mstaafu wa Urusi kuhusu leseni ya Mkuju River Project na kuweka wazi kwamba Kampuni ya UraniumOne hawajalipa kodi ya capital gains. Nilisimama kutoa taarifa baada ya majibu ya Waziri Muhongo kwamba, kilichouzwa si kampuni ya Tanzania bali Australia na hivyo hakuna kodi.

Kwa makusudi kabisa niliacha habari ya kesi ya TRA dhidi ya kampuni hii ili kuona umakini wa mawaziri wetu wapya kabla ya kukutana na lobbyists (washawishi) wa kampuni hizi za madini. Waziri Muhongo aliposimamishwa na Naibu Spika, Job Ndugai, akasema "Sisi tunajua zaidi kuliko Zitto" Kwanza Waziri hakuwa anajua.

Ni makosa kabisa kujadili suala ambalo mamlaka mojawapo ya nchi wamelipeleka mahakamani na linasubiri uamuzi. Lakini suala la Waziri kutokuwa na taarifa lilidhibitishwa na ujio wa Naibu Waziri George Simbachawene, aliponifuata na kuomba "details" kuhusu taarifa niliyotoa. Kulikuwa na haja gani kwa Waziri kusema bungeni yeye anajua zaidi na baadaye kumtuma Naibu wake kutafuta taarifa?

Huu ni udhaifu mkubwa sana wa uongozi. Kutojua si makosa, inawezekana kuwa wengine hatukusomea miamba lakini tumesomea masuala ya kodi kwenye madini na mafuta. Waziri makini anayejali nchi yake anawezaje kukutana na mwekezaji anayekataa kukulipa kodi yako bila wewe hata kuulizia utalipwa lini?

Unaulizwa bungeni unasema "ninajua zaidi" na Mwandishi mahiri kama Mbwambo anasema "mpeni nafasi atende"!

Nilipomsikia Waziri anasema ameagiza TPDC (Shirika la Maendeleo la Mafuta) kupitia mikataba nikajua na hili nalo hajui. Amesema tu ili watu wafurahi kwamba mikataba inapitiwa. Kupitia mikataba bila kuchukua hatua dhidi ya mikataba mibovu ni nini kama sio kutafuta umaarufu tu? Unapitia mikataba ili iwe nini kama huwezi kuchukua hatua?

Kuna mikataba ambayo imeingiwa kwa rushwa, sheria zetu zinasema kuwa mikataba iliyoingiwa kwa rushwa ni sawa na haipo. Hata sheria za kimataifa za mikataba zinatambua hivyo. Waziri anaposema kuwa tunapitia mikataba ili kuhakikisha kuwa mikataba ijayo inakuwa mizuri ni kichekesho. Hivi tunajua vitalu vingapi vimegawiwa na vingapi vimebaki? Hivi sasa kuna mikataba 29 na leseni 26. Vitalu vilivyobaki hivi sasa ni tisa tu.

Wizara inatuambia tunaangalia hii mikataba 29 ili kuboresha 9. Haya si mapitio bali ni kuangalia tu kama nilivyosema katika sentensi iliyotangulia. Mapitio bora zaidi ni uwazi wa mikataba yote tuliyoingia mpaka sasa na kuzuia kabisa mikataba mipya wala kugawa vitalu vipya vya kutafuta mafuta na gesi.

Uporaji wa rasilimali ni wa namna mbili, moja ni watu wachache na kampuni zao kupora kwa kupitia mikataba mibovu na pili ni kizazi kimoja kunyonya rasilimali zote bila kujali kizazi kijacho. Katika maandiko yangu nimeshauri kuwa tusigawe vitalu vipya mpaka tuone mafanikio ya mikataba hii 29 na leseni 26 tulizonazo hivi sasa. Wito wangu ni mmoja tu, uwazi wa mikataba. Kutaka uwazi si dhihaka. Uwazi ni uwajibikaji.

Suala la mapitio ya mikataba kwa jicho la juu juu ni suala la kuunga mkono. Lakini ukitazama historia ya nchi yetu katika masuala haya utabaini kwamba tunapaswa kufanya zaidi ya mapitio ya mikataba.

Tunapaswa kufanya jambo ambalo hatujawahi kulifanya nalo ni kuiweka wazi mikataba hii kwa umma. Hii ndiyo hoja yangu.

Inawezekana kabisa kwamba maneno niliyotumia yameudhi watu fulani lakini ikumbukwe mimi ni Mbunge wa Upinzani na ni wajibu wangu kukosoa serikali kila inapowezekana. Bahati nzuri miaka yangu saba bungeni hivi sasa imetumika kwa kiasi kikubwa sana katika kufuatilia kwa karibu sekta ya madini, mafuta na gesi. Ni rahisi sana mimi kuweza kuona suala linalosemwa na serikali linasemwa tu au serikali inamaanisha? Katika suala la mapitio ya mikataba kwenye sekta ya madini na mafuta kwa kweli serikali haipo makini. Watu wajuvi wa mambo kama kina Mbwambo wanapaswa kwenda zaidi ya mapitio na kutaka mikataba iwekwe wazi na kuchambuliwa kwa uwazi kabisa.

Waziri Muhongo anayo nafasi ya kufanya kazi yake, afanye kazi yake bila bugudha. Mbwambo ajue kuwa Mbunge Zitto pia anayo kazi yake kwa mujibu wa Katiba ibara ya 63 nayo ni "kuisimamia" serikali. Niacheni nami nifanye kazi yangu.

Makala hii iliyoandikwa na Kabwe Zitto, Mbunge wa Kigoma Kaskazini ni majibu kwa makala iliyoandikwa na Mwanasafu wetu, Johnson Mbwambo, katika toleo lililopita la gazeti hili la Raia Mwema, kupitia safu yake ya Tafakuri Jadidi.

Ni MANTIKI GANI Ilimfanya huyo ZITTO KABWE kukingia kifua na kumtetea MWIZI yuke MKURUGENZI wa TANESCO bila Hata ya kumfanyia UCHUNGUZI kama MMOJA wa COMMITTEE ya NISHATI BUNGENI ?
ALIKUWA anataka kuficha nini ? HIVI ANAPASWA KUWAOMBA RADHI Wananchi wa Tanganyika na Zanzibar au
Atainyamazia kimya kama Viongozi wa Chama tawala cha CCM Wanavyofanya --- KUNYAMAZA KIMYA ILI YAPITE ? Hajui Hatua yake iliwadhuru Wananchi ? Ambao angependa KURA ZAO ? Sasa kama kawaida yake AKATUTANGAZIA kuwa Wataizima GENERATOR iliyoko NYUMBANI kwa Mr. MHANDO ili ajue Uchungu wa kutokuwa na Umeme, lakini hiyo ilikua vunga wananchi... alimbakiza pale pale kuendelea KULA pesa za NCHI... ZITTO KABWE atatueleza ya kuwa huo sio U-MIMI MIMI MENTALITY ? NI KIJANA NDIO; NI MSOMI NDIO; Lakini faida yake ni kwa nani ? MAFISADI Wachache ? au Wananchi ? Kama ni Wananchi, aende kwenye VYOMBO vya HABARI na kulizungumzia SUALA la kumpigia kifua Mr. MHANDO...

R1.jpg
 
Sasa unaposema unakubaliana na Zitto kuhusu mikataba unakubaliana nae nini? Zitto katika jibu lake kwa hoja ya Mbwambo kuhusu DHIHAKA yake anasema yeye anataka kuwa mikataba iwe wazi [ transparent] lakini mkumbuke kuwa ni Zitto huyu huyo aliyesema hatua ya Porf. Muhongo kutaka kuipitia mikataba ya gesi ingewakatisha tamaa na kuwatisha wawekezaji!! Sasa tujiulize je kuipitia hii mikataba sio kuiweka wazi kwa wananchi?

Tukumbuke kuwa kuipitia hii mikataba kwa bodi kama alivyoagiza waziri kunafaida ya kutuwezesha kujua wapi tulipotoka kwenye mikata iliyopita ili tusirudie makosa hayo kwenye mikataba ijayo!! Sio lazima kuwa unapoipitia upya mikataba na ukagundua mapungufu [ mapungufu ya makusudi ya mafisadi ili watu wapate 10% wanazoficha USWISI] hayo mapungufu yatarekebishwa kama tulivyojifunza kwenye mikataba ya madini kuwa ukisha ingia mikataba hii ni lazima uheshimu sheria za kimataifa!! Tanapozungumzia dhana ya kuwa wazi kwa mikataba sio maana yake kila mmoja wetu atapata nafasi ya kuisoma bali wale wawakilishi wetu wakiwa ni wajumbe wa bodi husika au kamati za bunge zenye wajumbe wazalendo na wenye weledi wao wanaweza kuwakilisha jamii katika kukagua na kuona kama mikataba inakidhi matakwa ya jamii yetu.

Hivyo basi kitendo cha Muhongo kuwapa wajumbe wa bodi adidu za rejea za kuipitia ile mikataba ya gesi haitawakatisha tamaa wawekezaji kwa sisi kunufaika nayo kwani wao wanazihiitaji maliasili zetu kwa manufaa yao kama sisi tunavyowahitaji wao ,hivyo ni lazima tunegotiate nao from a strong position badala ya kuwa wanyonge!!

mkuu huu mjadala ulikuepo hapa nadhani mwezi mmoja uliopita,unachosema siyo kweli. unajua wakati mwingine baadhi yetu tunaishiwa busara,tunaongozwa na chuki na hasira matokeo ni kuandika hoja dhaifu kama ulivyofanya.
 
Anaza uswahili unatakaka kwenda kupiga wali na tende ikulu!! ha ha ha! wi shali siii!!
 
Back
Top Bottom