Zitto: Watanidharau, watanicheka, watapambana lakini nitashinda! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zitto: Watanidharau, watanicheka, watapambana lakini nitashinda!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzalendo JR, Oct 12, 2012.

 1. Mzalendo JR

  Mzalendo JR JF-Expert Member

  #1
  Oct 12, 2012
  Joined: Jun 6, 2012
  Messages: 1,188
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  JOHNSON Mbwambo ameandika katika Gazeti la Raia Mwema la Oktoba 3, mwaka huu, kuhusu dhihaka za Zitto kwa Prof. Muhongo (Waziri wa Nishati na Madini).

  Nimesoma na nimemuelewa.

  Kwanza naomba radhi iwapo tafsiri ya taarifa yangu niliyoitoa kwa vyombo vya habari na kuwekwa kwenye blogu yangu (zittokabwe.com) ilikuwa ina dhihaka.

  Nimefundishwa kutodhihaki watu na hasa watu wanaonizidi umri na siasa zangu sio za dhihaka bali za masuala (issues). Kupitia kwa ndugu Mbwambo naomba radhi kwa wote walioona kuna dhihaka katika andiko langu. Sikuwa na nia ya kumdhihaki Waziri Muhongo. Nia yangu ni kuonyesha kuwa Waziri Muhongo alichokifanya ni kuwacheza shere Watanzania, kwa kuwaambia maneno ambayo yeye mwenyewe alikuwa anaamini kuwa hayawezekani.

  Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Wizara yake, Eliakim Maswi, ilithibitisha kauli yangu siku chache tu baada ya kuitoa. Mbwambo kaandika makala yake kana kwamba hapakuwa na kauli ya kufuta maneno ya Waziri. Ninaamini Mbwambo aliiona kauli ile lakini aliamua kupuuza ili kujifurahisha na imani yake kwa Prof. Muhongo na mawaziri aliowataja kwenye makala yake kwamba ni mawakala wa mabadiliko. Mbwambo anaamini kabisa kwamba ndani ya utawala wa CCM, kuna mawaziri wenye nia ya dhati ya kuleta mabadiliko.

  Nieleze wazi kwamba nilishtuka sana kuona toleo moja la Gazeti la Raia Mwema likiwa na makala tatu, zote dhidi ya Zitto Kabwe. Wakati makala ya ndugu Mbwambo ilikuwa inahusu suala nyeti sana la rasilimali za taifa na ni makala nzuri yenye mafundisho, makala mbili nyingine zilikuwa ni za siasa dhidi ya Zitto. Mwandishi Mayage Mayage aliandika makala yenye kichwa cha habari "Zitto, Urais 2015 kwa chama gani?" na Mwanasafu wa gazeti hili la Raia Mwema, Evarist Chahali aliandika makala yenye kichwa cha habari "Rais Kikwete anapofikiri kama Kabwe Zitto."

  Namwambia Mayage akasome vizuri historia ya ujenzi wa CHADEMA. Yeye anadhani CHADEMA imeanza mwaka 2010. CHADEMA kimejengwa na watu, si mtu mmoja. Wanaoamua mgombea wa chama si watu wachache anaowadhani yeye Mayage bali ni wanachama wa CHADEMA kutoka sehemu mbalimbali za Tanzania, ikiwamo Munanila, mkoani Kigoma anapotoka Mayage.

  Huyu Chahali anasema ananijua sana. Inawezekana ananijua kuliko mimi ninavyojijua. Lakini mimi simjui na wala sijawahi kumwona ana kwa ana, nimekuwa nikimwona tu kwenye mitandao ya kijamii akinizushia, kunitukana na kunisema. Sikushangaa kusoma makala yake ya wiki iliyopita. Wote wawili nawakumbusha msemo wa Mahatma Gandhi aliposema; "Kwanza wanakudharau, kisha wanakucheka, kisha wanapambana na wewe, kisha unashinda".

  Sasa nirejee kwenye makala ya ndugu Mbwambo. Prof. Muhongo simjui, licha ya kwamba nimekuwa mmoja wa wabunge walioko mstari wa mbele kuhakikisha utajiri wa nchi unatumika kwa manufaa ya nchi, sikuwahi kumsikia Prof. Muhongo mpaka alipoteuliwa kuwa Waziri wa Nishati na Madini.

  Sikuwahi kusikia akipaza sauti yake dhidi ya mikataba mibovu ya madini licha ya kwamba yeye ni msomi aliyebobea katika masuala ya miamba. Wakati Bunge la tisa, chini ya Spika Samuel Sitta, likiwa limecharuka kutaka mikataba mibovu ipitiwe na kubadilishwa tulitarajia sana kupata ushauri wa wataalamu wetu lakini hawakuonekana, "walikwina"?

  Walikuwa waoga kusema maana wangeharibu uhusiano kati yao na watawala. Tulihangaika wenyewe bila maarifa yoyote kuhusu sekta ya madini. Wengine ilibidi kuacha kazi za ubunge na kwenda masomoni ili kuongeza ujuzi wa masuala ya kisheria na kiuchumi kuhusu sekta ya rasilimali (madini na mafuta).

  Wasomi wetu hawakuwa nasi. Walichague kuendelea kufanya kazi za ushauri kwa kampuni za utafutaji madini nchini. Leo Mbwambo anawaona hawa ndiyo mawakala wa mabadiliko. Labda anasema kweli. Ila mimi nimekata tamaa na mabadiliko kuletwa na watu waliomo serikalini, kwa sababu kadhaa.

  Moja, kama alivyosema ndugu Mbwambo, nilipigia kelele sana mkataba wa Buzwagi na mikataba mingine ya madini. Niliendelea kupiga kelele mpaka sheria mpya ya madini ilipopitishwa na Bunge. Nimuulize Mbwambo kwamba, licha ya sheria mpya kuandikwa imechukua miaka mingapi kampuni za madini kufanya kazi zao kwa kutumia sheria hiyo mpya? Je, mikataba mingapi iliyopitiwa imerekebishwa au hata kuvunjwa? Pengine niwasaidie kuwakumbusha taarifa kwamba, hakuna kilichofanyika kwa mujibu wa sheria mpya, licha ya kufuatilia kwa kina bungeni kupitia michango na hata maswali bungeni sambamba na makala mbalimbali.

  Tangu Waziri Prof. Muhongo na timu yake waingie ofisini ni maneno tu tunayosikia bila matendo. Hata suala la mgawo wa umeme ambalo ndugu Mbwambo analisema kama mfano, yeye anajua namna ambavyo wananchi wanalalamikia umeme kukatika hovyo, tena bila taarifa wala maelezo. Muhongo alifanikiwa sana kuaminisha watu wenye mawazo huru kama Mbwambo wakamwona yupo sahihi kiasi hata cha kufumbia macho mgawo wa umeme usio na maelezo, unaoendelea nchini.

  Siwaamini mawaziri kwa sababu wanasema lolote linalowajia midomoni mwao hata kama wanaamini kuwa wanalosema haliwezekani kutekelezwa. Waziri wa Nishati na Madini alisema kuhusu mikataba ya mafuta na gesi ili kufurahisha watu. Huo ni msingi wa kwanza wa kauli yangu ambayo ndugu yangu Mbwambo ameitafsiri kuwa ni dhihaka. Nilikuwa nasema ukweli mchungu kwamba, serikali haiwezi kufanya lolote kuhusu mikataba. Nilitoa changamoto kuwa kama serikali kweli imedhamiria, iweke mikataba hii wazi. Je, wameiweka wazi?

  Pili, Waziri wa Nishati na Madini anataka umma umwone kwamba anajua sana masuala ya sekta kuliko Mtanzania mwingine yeyote. Nitatoa mfano mmoja unaonihusu moja kwa moja. Katika mkutano wa Bunge uliopita, Tanzania ilitembelewa na Waziri Mkuu mstaafu wa Urusi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Kirusi iliyonunua leseni ya kutafuta uranium kule Selous. Kampuni ya UraniumOne iliyonunua leseni hii ya Mkuju River Project kutoka Kampuni ya Mantra ya Australia, kwa dola za Marekani milioni 980.

  Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ilitaka ilipwe kodi ya ongezeko la mtaji (capital gains tax) kampuni hii ilikataa. TRA wakaenda mahakamani kudai malipo ya kodi yenye thamani ya dola za Marekani milioni 116 ambazo ni sawa na asilimia 20 ya thamani ya mauzo na kesi inaendelea. Kwa mujibu wa sheria zetu kampuni zinapouziana leseni, lazima Waziri wa Nishati na Madini atoe idhini ya mauzo hayo. Mgeni huyo kutoka Urusi alikuja nchini kupigia debe idhini hii, ili itolewe leseni maalumu ya uchimbaji (special mining licence).

  Nikasimama kutoa taarifa bungeni kwamba mawaziri wanakutana na huyu Waziri Mkuu mstaafu wa Urusi kuhusu leseni ya Mkuju River Project na kuweka wazi kwamba Kampuni ya UraniumOne hawajalipa kodi ya capital gains. Nilisimama kutoa taarifa baada ya majibu ya Waziri Muhongo kwamba, kilichouzwa si kampuni ya Tanzania bali Australia na hivyo hakuna kodi.

  Kwa makusudi kabisa niliacha habari ya kesi ya TRA dhidi ya kampuni hii ili kuona umakini wa mawaziri wetu wapya kabla ya kukutana na lobbyists (washawishi) wa kampuni hizi za madini. Waziri Muhongo aliposimamishwa na Naibu Spika, Job Ndugai, akasema "Sisi tunajua zaidi kuliko Zitto" Kwanza Waziri hakuwa anajua.

  Ni makosa kabisa kujadili suala ambalo mamlaka mojawapo ya nchi wamelipeleka mahakamani na linasubiri uamuzi. Lakini suala la Waziri kutokuwa na taarifa lilidhibitishwa na ujio wa Naibu Waziri George Simbachawene, aliponifuata na kuomba "details" kuhusu taarifa niliyotoa. Kulikuwa na haja gani kwa Waziri kusema bungeni yeye anajua zaidi na baadaye kumtuma Naibu wake kutafuta taarifa?

  Huu ni udhaifu mkubwa sana wa uongozi. Kutojua si makosa, inawezekana kuwa wengine hatukusomea miamba lakini tumesomea masuala ya kodi kwenye madini na mafuta. Waziri makini anayejali nchi yake anawezaje kukutana na mwekezaji anayekataa kukulipa kodi yako bila wewe hata kuulizia utalipwa lini?

  Unaulizwa bungeni unasema "ninajua zaidi" na Mwandishi mahiri kama Mbwambo anasema "mpeni nafasi atende"!

  Nilipomsikia Waziri anasema ameagiza TPDC (Shirika la Maendeleo la Mafuta) kupitia mikataba nikajua na hili nalo hajui. Amesema tu ili watu wafurahi kwamba mikataba inapitiwa. Kupitia mikataba bila kuchukua hatua dhidi ya mikataba mibovu ni nini kama sio kutafuta umaarufu tu? Unapitia mikataba ili iwe nini kama huwezi kuchukua hatua?

  Kuna mikataba ambayo imeingiwa kwa rushwa, sheria zetu zinasema kuwa mikataba iliyoingiwa kwa rushwa ni sawa na haipo. Hata sheria za kimataifa za mikataba zinatambua hivyo. Waziri anaposema kuwa tunapitia mikataba ili kuhakikisha kuwa mikataba ijayo inakuwa mizuri ni kichekesho. Hivi tunajua vitalu vingapi vimegawiwa na vingapi vimebaki? Hivi sasa kuna mikataba 29 na leseni 26. Vitalu vilivyobaki hivi sasa ni tisa tu.

  Wizara inatuambia tunaangalia hii mikataba 29 ili kuboresha 9. Haya si mapitio bali ni kuangalia tu kama nilivyosema katika sentensi iliyotangulia. Mapitio bora zaidi ni uwazi wa mikataba yote tuliyoingia mpaka sasa na kuzuia kabisa mikataba mipya wala kugawa vitalu vipya vya kutafuta mafuta na gesi.

  Uporaji wa rasilimali ni wa namna mbili, moja ni watu wachache na kampuni zao kupora kwa kupitia mikataba mibovu na pili ni kizazi kimoja kunyonya rasilimali zote bila kujali kizazi kijacho. Katika maandiko yangu nimeshauri kuwa tusigawe vitalu vipya mpaka tuone mafanikio ya mikataba hii 29 na leseni 26 tulizonazo hivi sasa. Wito wangu ni mmoja tu, uwazi wa mikataba. Kutaka uwazi si dhihaka. Uwazi ni uwajibikaji.

  Suala la mapitio ya mikataba kwa jicho la juu juu ni suala la kuunga mkono. Lakini ukitazama historia ya nchi yetu katika masuala haya utabaini kwamba tunapaswa kufanya zaidi ya mapitio ya mikataba.

  Tunapaswa kufanya jambo ambalo hatujawahi kulifanya nalo ni kuiweka wazi mikataba hii kwa umma. Hii ndiyo hoja yangu.

  Inawezekana kabisa kwamba maneno niliyotumia yameudhi watu fulani lakini ikumbukwe mimi ni Mbunge wa Upinzani na ni wajibu wangu kukosoa serikali kila inapowezekana. Bahati nzuri miaka yangu saba bungeni hivi sasa imetumika kwa kiasi kikubwa sana katika kufuatilia kwa karibu sekta ya madini, mafuta na gesi. Ni rahisi sana mimi kuweza kuona suala linalosemwa na serikali linasemwa tu au serikali inamaanisha? Katika suala la mapitio ya mikataba kwenye sekta ya madini na mafuta kwa kweli serikali haipo makini. Watu wajuvi wa mambo kama kina Mbwambo wanapaswa kwenda zaidi ya mapitio na kutaka mikataba iwekwe wazi na kuchambuliwa kwa uwazi kabisa.

  Waziri Muhongo anayo nafasi ya kufanya kazi yake, afanye kazi yake bila bugudha. Mbwambo ajue kuwa Mbunge Zitto pia anayo kazi yake kwa mujibu wa Katiba ibara ya 63 nayo ni "kuisimamia" serikali. Niacheni nami nifanye kazi yangu.


  Makala hii iliyoandikwa na Kabwe Zitto, Mbunge wa Kigoma Kaskazini ni majibu kwa makala iliyoandikwa na Mwanasafu wetu, Johnson Mbwambo, katika toleo lililopita la gazeti hili la Raia Mwema, kupitia safu yake ya Tafakuri Jadidi.
   
 2. mangikule

  mangikule JF-Expert Member

  #2
  Oct 12, 2012
  Joined: Jun 11, 2012
  Messages: 3,171
  Likes Received: 1,256
  Trophy Points: 280
  ZZK ndugu yangu mbona ghafla mabadiliko? Umelipwa bei gani kuja kuvuruga? Lakini leo ninakuapisha mbele ya Mungu kama una mpango wa shetani!! wa kutumwa kuvuruga basi hutofika popote!!

  Kwa sababu mpango wa ukombozi wa TZ ni mpango wa Mungu. Na soma katika vitabu vyote yaliyowapata wale waliojaribu kuingilia mpango wa Mungu!! Tafadhali sana!! tulia uongozi utaupata na hata urais!! Lakini kwa mtindo huu wa kuwafanya hata maadui wa CDM wakachekelea hutosamehewa believe me!!
   
 3. Root

  Root JF-Expert Member

  #3
  Oct 12, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 26,168
  Likes Received: 12,877
  Trophy Points: 280
  Kwa hapa naona ZZK yuko sawa kabisa sisi tunachezewa akili zetu hauwezekani mtu aseme hakuna mgao tena halafu unakuja tena kwa kasi

  Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
   
 4. MPALESTINA MWEUSI

  MPALESTINA MWEUSI Senior Member

  #4
  Oct 12, 2012
  Joined: Jun 6, 2012
  Messages: 125
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 45
  Sijaelewa hapo mpango wa ukombozi ni mpango wa Mungu, yaani hii M4C ndio mpango wa Mungu, Mungu yupi huyo wakati serikali haina dini au CDM ina dini, pananitatiza hapo
   
 5. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #5
  Oct 12, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,157
  Likes Received: 1,246
  Trophy Points: 280
  Nimewahi kusoma na vijana wengi kutoka Kigoma wakati nikiwa sekondari, na pia Chuoni. Nilichokuja kugundua wachache wanatabia ya usaliti wakiweka mbele masilahi binafsi. Wako ladhi kumsaliti yeyote na kuvujisha siri za ndani kabisa ili mradi tu waweze kufikia malengo yao.

  Kulikuwa na katibu mkuu wa Chadema - Dr Walid Amani Kaborou, huyu usaliti wake kwa upinzani kila mmoja anauelewa. Amekuwepo pia Daniel Nsanzugwanko wa NCCR. Huyu pia anajulikana kwa usaliti wake. Kafulila amejaribu Chadema, akashindwa, NCCR pia ameshindwa. Hawa ni wachache, lakini pia kule chuoni alikuwepo rafiki yangu kutoka Kigoma ambaye kwa hakika alikuwa ni msaliti wa aina ile ile kama akina Walid Kaborou, siwezi kusimulia sana juu yake

  Zito Kabwe ni msaliti na anajli zaidi maslahi binafsi. Baada ya kujipatia umaarufu, akiwa kijana kati ya Vijana wachache ndani ya bunge, akaweza kukaa karibu na rais na kukutana na viongozi mbalimbali duniani akaona anaweza kufanya lolote bila kujali amewezaje kufika hapo alipo.

  Zito ni msaliti. Mtakaumbuka 2010 wakati wa kampeni, badala ya kumkampenia mgombea urais wa Chadema yeye alikuwa akitangaza kuwa 2015 atagombea urais. Kwa mwenye akili anaelewa huyu kijana namna gani vipi!

  Zito huyu huyu, wakati wa vuguvugu la kutangaza matokeo ya urais, yeye yuko bize na Jack Zoka, afisa usalama anayeshughulika na siasa. Na walikuwa wakiwasiliana mara kwa mara. Hapa shaka kuu ipo kwa huyu bwana mdogo.

  Zito, wakati wenzake wanaimarisha chama, yeye anajitangazia kugombea urais na hata siku moja hajawahi kushughulika na harakati za M4C. Kuna jambo hapa. Ikiwa anataka urais kupitia chadema ataupataje akiwa chama kitabaki kuwa cha msimu.

  Zito Kabwela, anafahamu fika kuwa, enzi hizo alikuwa na nafasi kubwa ya kuweza kushika madaraka ya juu ndani ya chama na hata ya nchi ikiwa chama kingeweza kufanya vizuri katika uchaguzi mkuu siku zijazo. Lakini sasa matumaini hayo yanafutika taratibu baada ya kuona kuna Vijana wengi, wenye maono na uwezo mkubwa pengine kushinda hata yeye wameibuka chadema. Mfano Tundu Lissu, John Mnyika, Godbless Lema, Benson Kigaila na wengine. Sasa kwa kuelewa hili na kwa sababu za ubinafsi na usaliti anajaribu kutafuta namna ya kukivuruga chama, akiondoe kwenye lengo la msingi la kuimarisha uhai wa chama.

  Zito Kabwe, atakuwa ndumila kuwili. Anatumwa na kutumiwa na pia ana tabia ya kujipendeza kwa wenye madaraka.

  Conclusion: Zito anajiona anaweza, lakini namhakikishia hataweza. Kaborou alikuwa maarufu kumshinda yeye, Mrema (Augustino) alikuwa maarufu kumshinda yeye, lakini leo yupo wapi.

  Kama ilivyo kwa wakristo, Yesu Kristo aliwaambia mitume wake "Sikuwachagua mitume 12 na mmoja wenu ni shetani?"

  Wito wangu kwa WanaChadema, mjue kuna Viongozi wengi lakini miongoni mwao kuna wasaliti na mmoja wao ni Zito Zuberi Kabwe. Kwa mataendo yake kwa ustawi wa chama anajidhihirisha wazi.

  Chadema, nawasihi muishi na huyu mtu kama mlivyoweza kuishi hata na Shibuda, mwisho wa siku ataamua kujinyonga mwenyewe kwani anguko lake litakuwa kubwa na la aibu.
   
 6. Mkaguzi

  Mkaguzi JF-Expert Member

  #6
  Oct 12, 2012
  Joined: Sep 26, 2007
  Messages: 249
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Well Said Zitto. Hapa nakubaliana na ww kwa kiasi kikubwa kwenye ishu ya mikataba. Mambo mengine "No Comment"
   
 7. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #7
  Oct 12, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,196
  Likes Received: 1,977
  Trophy Points: 280
  Ngoja nimcheke huyo mnafiki ZZK kwi! Kwi! Kwi kwi! Kwi! Teh! Teh! Teh! Ha! Ha! Ha! Teh!
   
 8. m

  mamajack JF-Expert Member

  #8
  Oct 12, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 1,162
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Pesa za mafisadi zinamtes a kijana.pole sana bwana kabwe.ki kawaida mwanzo huwa mgumu lakini kwako iko tofauti,maana naona mwisho wako ni mgumu sana.
   
 9. Nivea

  Nivea JF-Expert Member

  #9
  Oct 12, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 7,449
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Kwiwkiwkwiwkiwkwiwkwiwkwiwiwiwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiikwiwkwiwkwiwwiwkwiwkwiwkwiwkwiwikwiwiwiwkwiwkwiwkiwkwiwwkwiwkwiwkwiwkwiwiwiwiwiwkwiiwiwwiwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiikwiwkwiwkwiwiwwiiwiwwiwiwiwiwiwiwiwiwi kele wwoooooooooooooooooooooomiiiiiiiiiiiikwkwiwkiwkwikwiwwkiwwkwiwkwiwi Zitto
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 10. Transkei

  Transkei Member

  #10
  Oct 12, 2012
  Joined: Sep 19, 2011
  Messages: 86
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Bravo zitto!! coz unasimamia unachokiamini,ni vijana wachache sana ktk tz hii!! keep it up!!!
   
 11. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #11
  Oct 12, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,351
  Trophy Points: 280
  Mh ZZK bado yupo detremined kufanya mambo mazuri kwa njia mbaya, na mwisho wake huishia kutenda mabaya kabisa.Zitto ajue ktk response ya aliyoyafanya ni vigumu watu kujibu bila kumhusisha.Kwanza kabisa ni jinsi anavyopresent issue zake.Zitto kawa mahiri sana wa ku play solo.Na primary rewards ya kazi zake za kifikra kazi lock ina such away zije kama personal rewards .Sasa asitegemee kuwa itakuwa rahisi kwa wenzie wanaoona mapungufu kutenganisha blames n yeye personally.Kwanza sababu ya msingi ya kumpa sifa Zitto ktk article zake halafu articles zake zikiwa hovo utafute namna na kutoa blames bila msika Zitto.

  Kwa ujumla jinsi Zitto anavyopanga move zake kwa ubinafsi na kutaka kila kitu kikubwa kiwe linked naye ndio tatizo.Hata mimi personally kitu chohcote kinanchoonesha wendawazimu halafu kikawa kimejengwa na theory kama za Zitto ni rahisi kuongeza sarcasm kwa kuweka kapu moja.Why not?Mbona Kihiyo sasa hivi ni msamiati kwa watanzania wa kawaida?Kwanini zitto asitegemee mengi tuu kutoakana na balnder zake?
   
 12. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #12
  Oct 12, 2012
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Umesoma makala yote ya Zitto au umesoma kichwa cha habari tu na kujibu?
   
 13. m

  mgomba101 JF-Expert Member

  #13
  Oct 12, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,788
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  ZZK=zana za kilimo i.e anatumika na mafisadi kwa malengo ya kudhoofisha CDM..hawa watu mwisho wa siku wanaumbuka vibaya au wanakufa kifo kibaya.Ni Traitor! Ana uchu wa madaraka kama edward Lowassa!
   
 14. M

  Mundu JF-Expert Member

  #14
  Oct 12, 2012
  Joined: Sep 26, 2008
  Messages: 2,719
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Yaani Zitto anajadiliwa humu kama ilivyo kwa Ephraim Kibonde wa Clouds...

  Tuna mambo mengi muhimu ya kuyajadili...kama ajali za pikipiki zinavyoondoa maisha ya vijana wetu kila kukicha (nini kifanyike) n.k

  Hebu tumsahau kwanza huyu ZZK, Ephraim na Baba yao mdogo Lowassa....
   
 15. p

  pembe JF-Expert Member

  #15
  Oct 12, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 2,058
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Umejieleza vizuri kijana.
   
 16. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #16
  Oct 12, 2012
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Hongera sana Zitto Kabwe. Kwani umeonyesha umahiri mkubwa na misimamo thabiti kwa kile ulichoamini kuwa ni sahihi.

  keep it up, utatimiza ndoto zako tu insh'Allah
   
 17. Wingu

  Wingu JF-Expert Member

  #17
  Oct 12, 2012
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,326
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Zitto ni kichwa Rais wa kwanza msomi kijana aliyewahi kutokea Africa Aluta continua
   
 18. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #18
  Oct 12, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,144
  Likes Received: 2,104
  Trophy Points: 280
  Zitto Z. K.
  Wewe ni ndumila kuwili, huna tofauti na AMOEBA. Makala yako uliyoiandika ni nzuri sana, kwani umefanikiwa kuonesha madhaifu ya Waziri Mhungo. Hapo nakupa like. Na hiyo ndo manifest function ya makala yako. Lakini Latent manifest ya makala yako ni kubomoa na sio kujenga.

  Bill kajaribu kueleza sehem ya LATENT function ya harakati zako, hata mimi naunga mkono hoja.
   
 19. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #19
  Oct 12, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,144
  Likes Received: 2,104
  Trophy Points: 280
  perhaps Zitto atakuja kukomesha. Lakini kwa mlango upi? Huu huu anaojaribu kuubomoa kila siku?
   
 20. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #20
  Oct 12, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  Kama kwa kutupia haya maandishi ambayo ni sawa na MKONO MTUPU then unadhani ndio tosha kuwa RAIS wa JMT, basi kila mtu anayo sifa ya kuwa rais...

  Kweli nchi hii itaendelea kuwa maskini tu kwa viongozi wa style yako Zitto.
   
Loading...