Zitto: Wabunge watetezi wa Escrow walihongwa m10 na IPTL

Yeye zitto alihongwa ngapi jamaa mnafiki sana huyu,

Mbona aliyelipwa haja-sign kuchukua huo mshiko? Tutajuaje kama hii kitu sio magumashi! Nashangaa li-kampuni kama PAP kulipa 10m vila viambatisho. Btw, who initiated the transaction/payment?
 
Mwenyekiti wa PAC Zitto Zuberi Kabwe amesema kuwa wabunge waliokuwa mstari wa mbele kutetea na kuwalinda mafisadi wa ESCROW walihongwa kila mmoja milioni 10. Pesa hizo zilikuwa zinapitia kwa mbunge wa Kishapu Suleiman Nchambi.

Source: TANZANIA DAIMA, leo.

Taarifa zilizopo ni kuwa hata wabunge wote walioingia katika kamati ya maridhiano na wabunge wa upinzania pia walihgongwa ndio maana wakakubali kuingiza katika mapendekezo ya kamati maneno aliyotoa "fisadi chenge" kuwa watuhumiwa wapelekwe kwenye mamalaka husika.

Jana yake kabla ya wabunge wa upinzani kuhongwa tuliona namna gani walivyokomaa kinoma hadi kutishia kutoka nje ya bunge. Kama si kuhongwa ilikuwaje wabunge wa upinzani ambao jana yake walikomaa kesho walainike na kukubali mapendekezo yenye maneno ya fisadi chenge?
 
hata yule asumpta mshama mwenye sauti kama mpiga debe anayejinasibu na ulokole, nae kalambishwa?
 
Mwenyekiti wa PAC Zitto Zuberi Kabwe amesema kuwa wabunge waliokuwa mstari wa mbele kutetea na kuwalinda mafisadi wa ESCROW walihongwa kila mmoja milioni 10. Pesa hizo zilikuwa zinapitia kwa mbunge wa Kishapu Suleiman Nchambi.

Source: TANZANIA DAIMA, leo.

Asumpta, Ghasia Mzee wa Ashki na wabunge wengine wa CCM waliokuwa wakitetea wizi huu wakamatwe na kufikishwa mahakamani mara moja kwa kuhusika kwenye ufisadi huu.
 
Mbona hilo tunalijua! Yale mapovu waliyokuwa wanayatoa bungeni pasipo hoja tulijua wamelamba mapesa. Watu kama Assumpta Mshama (Mbunge wa Nkenge), Suleiman Nchambi (Mbunge wa Kishapu), Mbunge wa Viti maalum na Mwenyekiti wa( UWT) Temeke, Mariam Kisangi na wengine wengi hawafai kuwa viongozi. Wamedhihirisha kuwa sio watetezi wa wananchi bali mafisadi. Hawa ni wasaka tonge ambao hatuhitaji kuwa nao tena katika bunge lijalo la 2015. Ni shidaaaa!

Huyo Assumpta Mshama alikuwa akiwakilisha wananchi wa Jimbo la Mkenge na sio Nkenge. Wananchi wa jimbo la Nkenge hatuwezi kuwa na mwakilishi Kenge kama Assumpta Mshama!
 
Ni aibu kuwa mtanzania, lakini ni aibu kubwa kuwa rais wa Tanzania.
 
Yeye zitto alihongwa ngapi jamaa mnafiki sana huyu,

acha ujinga wewe, Zitto ni mpumbavu kiasi gani ahongwe mil 10 wakati kuna watu wamekula mpaka bilioni na milioni mia sita(chenge, tibaijuka) na wengine michango ya harusi tu wamekula milioni mia nne?

Akili za kuambiwa, changanya na zako, usiwe gong'ota, kuwa kama mbayuwayu!

Jiongeze dogo...hata kama ndiyo umetumwa ulete utumbo wako JF, jiulize mara mbili kama huo utumbo unalika au umeoza?
 
kama kweli ZITTO kasema basi amekosea,naheshimu maoni yake,kutaja taja majina tu,ata yeye ametajwa,mbowe ametajwa jk ametajwa,tunataka wakitaja majina waje na ushahidi usioshaka
 
Leo nimesikia yule tajiri wa Pap anataka bosi wa TRA akamatwe,jamani kweli hii nchi imewekwa mfukoni mwa mafisadi.
 
Mwenyekiti wa kamati ya bunge hesabu za serikali (PAC) Zitto Kabwe amemlipua mbunge wa Kishapu mkoani Shinyanga Suleimani Nchambi {CCM} kuwa ni kati ya waliohusika kugawa rushwa ya sh milioni kumi kwa baadhi ya wabunge waliosimama kutetea kashfa ya uchotaji fedha sh Bilioni 360 katika Akaunti ya Escrow.

Kulipuliwa kwa Nchambi nje ya Bunge ,kumekuja siku chache baada ya mbunge huyo kuzomewa Bungeni na wabunge wenzake wakati akipingana na ripoti ya kamati ya Bunge ya hesabu za Serikali (PAC), inayoongozwa na mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe akizungumza na Tanzania Daima katika mahojiano maalum Jijini Dar es Salaam jana, Zitto alidai kuwa Nchambi anahusika kuwahonga wabunge kati ya sh milion 3 hadi 10. Alisema Nchambi alikuwa akigawa rushwa hiyo kwa awamu kwani kabla ya mbunge kuingia na kuchangia hoja ya kuwatetea.

CHANZO: Tanzania Daima

Zitto kama "Mtunga sheria" anajua fika kuwa kutoa/kupokea rushwa ni kosa la jinai! Kama ana vithibitisho vya vitendo hivyo vya rushwa kwa nini jambo hilo lisiripotiwe kwenye vyombo husika ili wahusika wafanyiwe uchunguzi stahiki? Hata kama hana imani na vyombo hivyo kwa nini asiripoti kwao kwanza na wasipochukua hatua ndipo amwage vielelezo vyake hadharani ili jamii ione yenyewe uozo uliko? Kwa mtindo huu bado tuna safari ndefu sana kwenye vita dhidi ya rushwa!
 
Mbona hilo tunalijua! Yale mapovu waliyokuwa wanayatoa bungeni pasipo hoja tulijua wamelamba mapesa. Watu kama Assumpta Mshama (Mbunge wa Nkenge), Suleiman Nchambi (Mbunge wa Kishapu), Mbunge wa Viti maalum na Mwenyekiti wa( UWT) Temeke, Mariam Kisangi na wengine wengi hawafai kuwa viongozi. Wamedhihirisha kuwa sio watetezi wa wananchi bali mafisadi. Hawa ni wasaka tonge ambao hatuhitaji kuwa nao tena katika bunge lijalo la 2015. Ni shidaaaa!

ni kweli kabisa kwamba kulikuwa na nguvu ya fedha inatembea mle bungeni. haiwezekani mijitu mizima akina Hawa Ghasia itutumue macho mle bungeni kuwatetea mafisadi bila soni. it's shame!
 
Back
Top Bottom