Zitto: Wabunge watetezi wa Escrow walihongwa m10 na IPTL

amakyasya

JF-Expert Member
Jun 26, 2013
3,463
0
Mwenyekiti wa kamati ya bunge hesabu za serikali (PAC) Zitto Kabwe amemlipua mbunge wa Kishapu mkoani Shinyanga Suleimani Nchambi {CCM} kuwa ni kati ya waliohusika kugawa rushwa ya sh milioni kumi kwa baadhi ya wabunge waliosimama kutetea kashfa ya uchotaji fedha sh Bilioni 360 katika Akaunti ya Escrow.

Kulipuliwa kwa Nchambi nje ya Bunge ,kumekuja siku chache baada ya mbunge huyo kuzomewa Bungeni na wabunge wenzake wakati akipingana na ripoti ya kamati ya Bunge ya hesabu za Serikali (PAC), inayoongozwa na mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe akizungumza na Tanzania Daima katika mahojiano maalum Jijini Dar es Salaam jana, Zitto alidai kuwa Nchambi anahusika kuwahonga wabunge kati ya sh milion 3 hadi 10. Alisema Nchambi alikuwa akigawa rushwa hiyo kwa awamu kwani kabla ya mbunge kuingia na kuchangia hoja ya kuwatetea.

CHANZO: Tanzania Daima
 
Communist

JF-Expert Member
Jun 1, 2012
5,392
2,000
Mwenyekiti wa PAC Zitto Zuberi Kabwe amesema kuwa wabunge waliokuwa mstari wa mbele kutetea na kuwalinda mafisadi wa ESCROW walihongwa kila mmoja milioni 10.

Source: TANZANIA DAIMA, leo.
Mpelekee Dr Slaa akusaidie kwenga mwembe yanga.
 
Simba mnyama

JF-Expert Member
Jul 14, 2012
348
170
Mbona hilo tunalijua! Yale mapovu waliyokuwa wanayatoa bungeni pasipo hoja tulijua wamelamba mapesa. Watu kama Assumpta Mshama (Mbunge wa Nkenge), Suleiman Nchambi (Mbunge wa Kishapu), Mbunge wa Viti maalum na Mwenyekiti wa( UWT) Temeke, Mariam Kisangi na wengine wengi hawafai kuwa viongozi. Wamedhihirisha kuwa sio watetezi wa wananchi bali mafisadi. Hawa ni wasaka tonge ambao hatuhitaji kuwa nao tena katika bunge lijalo la 2015. Ni shidaaaa!
 
East African Eagle

JF-Expert Member
Jul 26, 2013
3,761
1,195
Mwenyekiti wa PAC Zitto Zuberi Kabwe amesema kuwa wabunge waliokuwa mstari wa mbele kutetea na kuwalinda mafisadi wa ESCROW walihongwa kila mmoja milioni 10.

Source: TANZANIA DAIMA, leo.
Kama ni mzalendo kweli Zitto apeleke majina ya hao wabunge na vielelezo vya ushahidi TAKUKURU na awe tayari kuwa shahidi namba moja mahakamani
 
MUSSA ALLAN

JF-Expert Member
Oct 13, 2013
18,939
2,000
Zitto siku hizi kamekuwa kaongo kaongo, Jana Nilimsikia akihojiwa CLOUDS FM , akasema walihongwa Milioni tatu, Leo kupitia TANZANIA DAIMA anasema walihongwa milioni kumi.
Hii inaonyesha hakuna mtu aliyehongwa ila ni uzushi tu kama kawaida yake!
 
Last edited by a moderator:

ndenga

JF-Expert Member
Dec 20, 2010
1,761
2,000
Mbona hilo tunalijua! Yale mapovu waliyokuwa wanayatoa bungeni pasipo hoja tulijua wamelamba mapesa. Watu kama Assumpta Mshama (Mbunge wa Nkenge), Suleiman Nchambi (Mbunge wa Kishapu), Mbunge wa Viti maalum na Mwenyekiti wa( UWT) Temeke, Mariam Kisangi na wengine wengi hawafai kuwa viongozi. Wamedhihirisha kuwa sio watetezi wa wananchi bali mafisadi. Hawa ni wasaka tonge ambao hatuhitaji kuwa nao tena katika bunge lijalo la 2015. Ni shidaaaa!
Umemsahau Kibajaji Joseph Lusinde aka mzee wa matusi na mipasho..
 
mcubic

JF-Expert Member
Mar 3, 2011
10,298
2,000
Zitto siku hizi kamekuwa kaongo kaongo, Jana Nilimsikia akihojiwa CLOUDS FM , akasema walihongwa Milioni tatu, Leo kupitia TANZANIA DAIMA anasema walihongwa milioni kumi.
Hii inaonyesha hakuna mtu aliyehongwa ila ni uzushi tu kama kawaida yake!
Unapenda sana rushwa ww
 
Last edited by a moderator:

Chigwiyemisi

JF-Expert Member
Jun 22, 2011
533
225
Ni kweli kabisa walikuwa wamekula mlungula. Hata hivyo kuna baadhi yao ambao walikuwa wanafuata upepo na kujipendekeza tu, mfano Lusinde na yule Waziri asiye na lolote kichwani Hawa Ghasia. Kuna Mama mmoja alisema PAC ni njama za wapinzani na CCM iko imara na itaendelea kushinda, huyu naamini hakupewa hata jero ila ni kufuata mkumbo tu na hana uelewa wowote. Naamini kwa dhati kabisa hakuwa anaelewa lolote kwenye maelezo juu ya kuuziana hisa, maana ya account ya escrow, ukokotoaji wa kodi n.k. Jaji Warioba alikuwa sahihi sana aliposema Mbunge at least awe na elimu ya Form Four (Refer mchango wa Lusinde).
 
OgwaluMapesa

JF-Expert Member
May 24, 2008
10,945
1,225
Mwenyekiti wa PAC Zitto Zuberi Kabwe amesema kuwa wabunge waliokuwa mstari wa mbele kutetea na kuwalinda mafisadi wa ESCROW walihongwa kila mmoja milioni 10.

Source: TANZANIA DAIMA, leo.
Du mpaka yule Mariam Kisanga alikula million 10 wakati kichwani empty......Kweli Pinda hana watetezi makini kabisa
 
BONGE BONGE

JF-Expert Member
Oct 19, 2011
3,712
2,000
Zitto siku hizi kamekuwa kaongo kaongo, Jana Nilimsikia akihojiwa CLOUDS FM , akasema walihongwa Milioni tatu, Leo kupitia TANZANIA DAIMA anasema walihongwa milioni kumi.
Hii inaonyesha hakuna mtu aliyehongwa ila ni uzushi tu kama kawaida yake!
......kuhongwa ni kuhongwa tu, iwe shilingi 10, 20 ama 30; suala ni kwamba walihongwa, na hilo halihitaji kumulikwa tochi ili lionekane
 
mjepo

JF-Expert Member
Aug 8, 2013
4,917
1,225
Ni kweli kabisa walikuwa wamekula mlungula. Hata hivyo kuna baadhi yao ambao walikuwa wanafuata upepo na kujipendekeza tu, mfano Lusinde na yule Waziri asiye na lolote kichwani Hawa Ghasia. Kuna Mama mmoja alisema PAC ni njama za wapinzani na CCM iko imara na itaendelea kushinda, huyu naamini hakupewa hata jero ila ni kufuata mkumbo tu na hana uelewa wowote. Naamini kwa dhati kabisa hakuwa anaelewa lolote kwenye maelezo juu ya kuuziana hisa, maana ya account ya escrow, ukokotoaji wa kodi n.k. Jaji Warioba alikuwa sahihi sana aliposema Mbunge at least awe na elimu ya Form Four (Refer mchango wa Lusinde).
Unajua kuwa zitto naye kahongwa?
 
Mkoroshokigoli

JF-Expert Member
Dec 20, 2012
14,605
2,000
Mbunge Zitto amesema kuwa wabunge waliokuwa wakiitetea IPTL na ESCROW yake walipokea mlungula, ambapo kabla ya kwenda kuongea walipewa mil 3 na baada ya mbunge kuchangia wanamaliziwa mil 7 jumla ni mil 10. Zitto amesema kuwa mkwanja huo ulikua unagaiwa na Suleiman Nchambi Mbunge wa Kishapu CCM,

Maeneo ambako pesa hizo zilikua zikitolewa yalikua ni Rocky Hotel na St,Gasper.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom