Zitto: Wabunge wa CCM akiwemo Magufuli waliniadhibu kwa kuibua sakata la madini mwaka 2007

Johnny Sack

JF-Expert Member
Jan 21, 2017
8,936
19,129
Zitto Kabwe akihojiwa na Azam Tv amesema ripoti kamati iliyoongozwa na Prof. Osoro iliyowakilishwa kwa Magufuli haina mapendekezo mapya tofauti na kmamati ya Jaji Bomani ya Mwaka 2008 ambayo yeye alikuwa ni mjumbe pia wa kamati hiyo, tofauti ya sasa na kipindi kile ni rais kuthubutu kufanyia kazi mapendekezo hayo

Pia amesema mwaka 2007 aliibua suala hilo bungeni ila aliambiwa anakimbiza wawekezji ni mchochezi na akaadhibiwa kutohudhuria vikao vya bunge Magufuli akiwa ni mmoja wa watu waliomuadhibu
 
Tena nakumbuka kwa jinsi alivyo na haraka ya kukamilisha jambo yeye alikuwa wa kwanza kumaliza kupiga kura ya kumfukuza Zitto bungeni. Mbona wote tunalijua hilo?

Kamati ya wizi wa nyumba za serikali inaundwa lini? Tufukue tu Makaburi.
 
sasa zitto anaongea nini wakati kikwete alishamfikisha bei

Mbabe ni Lissu Peke yake..Tangu mwaka 1994 Jamaa anakomaa na sekta ya madini to date
 
Swali lako limenifanya nicheke kidogo kwani lime nikumbuka ule usemi wa dokta mmoja kuhusu: "Choo, kinyesi na sebule" (LoL)
Mantiki yangu ni kwamba kwenye kufanya maamuzi ya kisiasa wingi ndiyo huamua. Kama hawa aliowataja ndiyo wabaya basi waliobakia CCM ambao ndiyo anadhani ni wema ni wengi kuliko aliowtaja, sasa ni kwa nini hawafanyi maamuzi dhidi ya hawa wachache waliokwenda CHADEMA?

Bunge ni lao na serikali ni yao na mahakama sijui kama iko kinyume chao.Kwa nini wanashindwa kufanya maamuzi dhidi ya mafisadi machache walioko CHADEMA?
 
Ndugu yangu zitto kabwe, huu sio muda wa "kulaumulaumu",kipindi kile watanzania walikuwa hawana uzoefu na makampuni makubwa ya uwekezaji,(kumbe mengine yakitapeli)haswa kwenye sekta ya madini..tumuunge mkono raisi magufuli wewe kama muasisi wa ACT munakubalika ni vichwa.
 
Ukiweka uwiano na wale waliobakia CCM wepi wengi?
Ishu sio wingi, kumbuka PM ndio Mwenyekiti wa Wabunge wa CCM.. Kwahiyo alikua na nguvu sana katika ilo ukizingatia gazeti la MwanaHalisi lilishapisha habari kuwa Lowasa alikuwepo wakiwa mkataba wa buzwagwi unasainiwa
 
Back
Top Bottom