Zitto V/S Pinda & Chenge relashon | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zitto V/S Pinda & Chenge relashon

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwiba, Aug 17, 2009.

 1. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #1
  Aug 17, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Afu uyu si alisema agombei tena na atameguka katika siasa ?

  [​IMG]
  Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (Chadema).  Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (Chadema), ameshtukia mpango unaodaiwa kuandaliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa kutaka kumng'oa katika jimbo hilo kupitia Uchaguzi Mkuu mwakani kwa kutumia ‘siasa za uongo' kuhusu maendeleo yaliyopatikana jimboni humo.
  Maendeleo hayo, ni pamoja na ujenzi wa barabara ya Mwandiga-Manyovu kwa kiwango cha lami, ambapo amesema wakati anashika ubunge wa jimbo hilo, serikali ilitenga Sh. milioni 800, lakini baadaye akaupigania na katika bajeti ya mwaka huu wa 2009/10, ujenzi huo umetengewa Sh. bilioni 7.
  Akijibu hoja mbalimbali za wabunge 206 waliochangia moja kwa moja na kwa maandishi wakati akifanya majumuisho ya mjadala wa hoja ya hotuba ya bajeti ya ofisi yake katika kipindi cha mwaka wa fedha wa 2009/10, bungeni mjini Dodoma, Pinda alisema Zitto alitaka kutumia ujenzi wa barabara za lami alizokwenda kuzizindua hivi karibuni kujipatia umaarufu kuwa kazi hiyo imefanyika kutokana na msukumo wake na wa chama chake cha Chadema.
  Pinda alisema Zitto alitaka kutumia ujenzi wa barabara za lami zilizojengwa mkoani Kigoma kuwa zimetokana na ushawishi wa chama chake wakati si kweli, bali ni mpango wa serikali. "Wakati wa uzinduzi, nilikwenda Kigoma, kwa bahati mbaya Zitto hakuwapo, nilipouliza wapiga kura wake kuwa mbunge wenu yuko wapi, wengine walisema amehama, wengine walisema sijui yuko Busanda, ila mimi nasema, kwa hali niliyoiona kule jimboni mwake, 2010 Zitto itabidi ajipange sawa sawa, vinginevyo..." alisema Pinda bila kumaliza.
  Katika hotuba yake, Zitto alisema: "Nimepigania kuhakikisha hilo, mchakato wa ujenzi wa barabara umeanza, viongozi wa CCM wanaanza kuweweseka na kudai kuwa wanatekeleza Ilani ya CCM. Mimi nawaambia viongozi wenzangu, mnapaswa kuwauliza ni wapi ndani ya Ilani ya CCM wameahidi kujenga barabara ya Mwandiga-Manyovu kwa kiwango cha lami? Hakuna! Mimi najua nimefanya nini kuhakikisha hili linafanyika! Ndio sababu mlinichagua."
  Zitto alisema hayo kupitia hotuba yake aliyoitoa katika ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Chadema Jimbo la Kigoma Kaskazini, uliofanyika eneo la Kalinzi, juzi.
  Alisema viongozi wa Chadema wanapaswa kuwauliza viongozi wa CCM wanaojipitisha jimboni humo kwa aibu na kudai kwamba ni Ilani ya CCM ndiyo inayojenga barabara hiyo.
  Zitto alisema barabara hiyo ni ya kwanza ya kiwango cha lami kujengwa ndani ya jimbo hilo tangu Tanzania ipate uhuru, hivyo akawataka wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chadema jimboni humo kuwauliza CCM walikuwa wapi miaka yote hiyo hadi wakumbuke leo? Hata hivyo, alisema yeye anajua ni kwa nini Kigoma Kaskazini inafuatiliwa na CCM na kuongeza kuwa ndio sababu walimchagua.

  Aliwashukuru aliyekuwa Waziri wa Miundombinu, Andrew Chenge na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Enos Bukuku kwa msaada mkubwa waliompa kuhakikisha wanajenga barabara hiyo kwa lami.
   
 2. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #2
  Aug 17, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Kashukuru kuna ubaya kusema asante kama jamaa ni fisadi lakini aliweza kuelewa hoja ya Zitto na kumpa pesa mi sawa tu .Serikali ni ya wote ni CCM tu wanakuw awajinga kwa mawazo mgando kila mara .
   
 3. Exaud J. Makyao

  Exaud J. Makyao JF-Expert Member

  #3
  Aug 17, 2009
  Joined: Nov 30, 2008
  Messages: 1,523
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Zitto ni mtu wa watu.
  Wanaowaza kumng'oa watakaa sana.
  Nawapa pole anyway.
   
Loading...