Zitto: Upinzani adui yetu ni CCM, tuweke kando tofauti zetu tushirikiane tuhakikishe kata 3 za Dar CCM haipati hata moja

AKASINOZO

JF-Expert Member
Aug 22, 2016
1,367
2,217
Zikiwa zimesalia siku chache kabla ya kufanyika uchaguzi mdogo wa madiwani, Chama cha ACT Wazalendo kimeviomba vyama vingine vya upinzani kukiachia kipambane na CCM katika kata mbili kati ya tatu za Mkoa wa Dar es Salaam ambazo uchaguzi utafanyika.

Uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika Novemba 26,2017 utahusisha kata 43 nchini, Dar es Salaam ukihusisha za Saranga, Kijichi na Mbweni.

ACT Wazalendo imesema utafiti iliyoufanya unaonyesha chama hicho kinaweza kuchukua kata za Kijichi na Saranga endapo vyama vingine vya upinzani vitakiachia kisimamishe wagombea watakaochuana na wa CCM.

Kiongozi wa chama hicho, Zitto Kabwe akizungumza na waandishi wa habari leo Jumamosi Oktoba 28,2017 jijini Dar es Salaam amesema ACT Wazalendo imeamua kuwasimamisha wagombea wawili na kuiachia kata moja kwa vyama vingine vya upinzani kwa kuwa wamejipima na kuona wanaweza kushinda bila kupingwa Kijichi na Saranga.

“Tumefanya utafiti mdogo kule Mbweni tukaona vyama vikuu vitatu ni ACT, Chadema na CCM tukaona upo uwezekano wa sisi na Chadema kugawana kura, tumeona tuwaachie kata ile,” amesema.

Zitto amesema, “Tumejipima na kuona ACT ikisimama peke yake Kijichi na Saranga tuna uwezo wa kuishinda CCM asubuhi kweupe. Tunachoomba vyama vingine vya upinzani vituachie tusimamishe wagombea halafu tushirikiane nao kuhakikisha tunaiangusha CCM.”

Amesema, “Tunawaambia wenzetu upinzani adui yetu ni mmoja CCM, hivyo tuweke kando tofauti zetu tushirikiane lengo ni kuhakikisha katika kata tatu za Dar es Salaam, CCM haipati hata moja.”
 
Saranga naskia hao act na chadema wameshatolewa automatically kwa kukosea/kutoainisha mambo kadhaa wakat wa kujiandikisha.
 
TANZANIA KUNA VYAMA VYA UPINZANI TAKRIBANI 25 NA KATIKA VYAMA HIVYO KUNA VYAMA HAVINA MBUNGE WALA DIWANI

ACT NI CHAMA CHENYE MBUNGE NA MADIWANI LAKINI KINASHIRIKI UCHAGUZI WA MARUDIO KATA YA SARANGA NA KIJICHI.........

JE VYAMA KAMA VISIVYIKUWA NA DIWANI WALA MBUNGE HAVIRUHUSIWI KUSHIRIKI KAMA WAPINZANIIIII KWA SABABU VYAMA VYENYE NGUVU KISIASA VINESIMAMISHA WAGOMBEA WAO
 
Zitto lini umekua mpinzani? Wapinzani wa ccm wanajulikana kila siku wanakamatwa kwa kesi hewa, kufa ama kupotea na wengine kujeruhiwa. Pambana na hali yako jomba.


Siyo kweli, chadema wanakamatwa kwa sababu they are stupid, Zito Kabwe anafanya Siasa na hatukani, hadhihaki wala hakebehi mtu sasa kwa nini akamatwe? Chadema ni wajinga na hamna mwenye akili na ndiyo maana matatizo yanawaandama!
 
Zitto nilikukubali sana na hata wanachi walikuamini sana, hakika ungebaki vile ungekuwa mbali sana kisiasa, lakini kutokana na undumila kuwili, umepoteza sana trust. In short watu watasikia hoja zako lakini swala la kukuamini tena ni gumu mno.
 
Siyo kweli, chadema wanakamatwa kwa sababu they are stupid, Zito Kabwe anafanya Siasa na hatukani, hadhihaki wala hakebehi mtu sasa kwa nini akamatwe? Chadema ni wajinga na hamna mwenye akili na ndiyo maana matatizo yanawaandama!
Kwa iyo matatizo yanawaandama watu wenye akili kama za chadema?
Miaka 50+ toka tupate uhuru saivi ujue
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom