Zitto: Unawezaje kuwa na mabombadia, maSRG, madremliner unashindwa kuwa na vifaa vya kuokoa wanyonge?

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
49,086
103,316
IMG-20180921-WA0025.jpg
 
Ili neno wanyonge silipendi basi tu

kwanza kulitumia ni kukiuka haki za binadamu ilo watu hawalijui

Kwanza ni aibu kama nchi kukosa vivuko vidogo vidogo vipya kila baada ya miaka 3 hivi

tena kivuko cha watu 100 miaka karibu 60 ya uhuru bado tumeshindwa kuondoa MARADHI, UJINGA NA UMASKINI

badala yake tunaitumia kama kete kuwatawala watanzania

inauma sana sana kumpoteza mtu ambaye alikuwa ajaugua

R.I.P Wote na poleni sana wafiwa.
 
Kivuko kipya MV Mwanza,8.9 B,Tzs, uwezo Abiria 1000; magari 36;Mizigo tani 200; hivyo kwa visiwa na miji midogo mfano Mafia,nusu yake sema 4B; 80 B ktk chaguzi za tamaa= vivuko 20 vipya!!! Kupanga ni kuchagua ,Kuna MTU anajiita mpenzi wa ....... Mie nasema ni mpenzi wa shetani.Kwani anawekeza katika kuwagawa Watanzania kwa kuharibu mifumo na umoja wa taifa letu.
Screenshot_20180921-180022.jpg
pic+mv+mwanza.jpg
 
Kupanga ni kuchagua, tumechagua Ndege na SGR na sio vifaa vya uokoaji, kwa sababu sisi ni positive thinkers, tunawaza mema tuu na maendeleo na sio kuwaza mabaya na majanga!. Ajali ni ajali tuu, na hutokea kwa bahati mbaya tuu!.

Kuzaliwa na na kufa ni mipango ya Mungu. Mtu yoyote anapokufa, hiyo ndio inakuwa siku yake imefika. Hivyo
wote waliokufa katika ajali hiyo siku hiyo ilikuwa ndio siku yao na vifo hivyo ndivyo walivyoandikiwa na Mungu tangu ile siku wanaumbwa na wanazaliwa.

Tena kwa msio jua, yule malaika mtoa roho, Israel, humpitia kila mtu kwa saba mara sabini kwa siku, ili kuhakikisha saa yako ikifika, hazidishi hata nukta moja ya sekunde!. Kama saa yako haijafika, hufi, ndio maana mtu kama Lissu ameweza ku survive risasi 38!, kwa sababu saa yake ilikuwa haijafika. Saa yako ikifika, unaondoka tuu hata ukiwa usingizini na hauumwi chochote wala huna tatizo lolote!.

Poleni sana.
P
 
Back
Top Bottom