Mati Mkenda
Senior Member
- Mar 4, 2018
- 171
- 211
Kati ya watu wachache waliotumia nguvu kubwa sana kuzibeza juhudi zilizochukuliwa na serikali ya awamu ya tano, pamoja na wataalam wetu wa ndani katika kupambana na Ugonjwa wa Corona (COVID-19), ni ndugu yetu Zitto Kabwe. Huyu bwana kwake hakukuwa na jema lolote lililofanywa na serikali, kwani kila kilichofanywa alikibeza.
Na mara nyingi alitumia akaunti yake ya Twitter kuandika ujumbe wa kubeza ambao alikuwa akiwa-tag raia wa Mataifa mengine, na taasisi nyingine za kimataifa ambao yeye aliona kwamba wanatakiwa kujua kile alichokuwa akikisema, au wenyewe kwa nyakati tofauti waliibeza serikali yetu, hao tunaweza kuwaita ni “Accomplices” wake kwenye harakati zake hizo
Zitto alianzisha kampeni yake aliyoiita “M3 Campaign” akisema kuwa “M” hizo zinawakilisha Miguu, Mikono, na Mdomo. Kampeni yake hiyo mbali na kuwa na components za yale yaliyokuwa yanasisitizwa na serikali, lakini ilifunikwa na Mwavuli wa kupinga sehemu kubwa za yale ambayo serikali ilikuwa ikiyafanya. Ilijikita sana kuikosoa serikali hasa pale ilipofanya tathmini na kuona kuwa kwa mazingira ya nchi yetu isingekuwa vema ku-impose “LOCKDOWN” kwa wananchi wake
Zitto kila siku alisisitiza kuwa hali ni mbaya sana hapa nchini, na kuwa nchi ingeingia katika hali mbaya zaidi ikiwa ni pamoja na kutengwa na jumuiya za kimataifa
Kinachonishangaza ni kuwa baada ya Rais kutangaza kuwa sasa tunarudi kwenye mfumo mpya wa maisha, Zitto naye kimya kimya amerudi kwenye utaratibu huo. Na mbaya zaidi yale aliyokuwa akiyasisitiza kwenye kampeni yake ya M3 hakuna analolifuata hata moja kwa sasa. Yeye ndiye amekuwa mzungukaji sana, anawakusanya watu kila siku kwa makundi, anashikana nao mikono, havai barakoa n.k
Kwa nafasi yake nilitarajia ndo awe wa kwanza kuitekeleza kampeni yake, na si kuanzisha kampeni ambayo yeye mwenyewe hawezi kuiishi. Nimuombe tu ndugu yangu Zitto Kabwe awe muungwana; atumie nafasi yake hiyo tena, kuiambia dunia kuwa sasa Tanzania ni salama kwa COVID-19, na kisha awa-tag ndugu zake wale wale aliowatag upotoshaji wa awali. Tanzania ni nchi yetu sote