Zitto: Ukweli ndege zinazonunuliwa ni mitumba wanafanya marekebisho na kuuziwa kwa bei ya mpya

Wajinga hufanikiwa kwa kupata wafuasi wenye akili kama wao. Kama angalau unajua mambo ya aeiou, soma relay mojawapo ya gari lako ilitengenezwa mwaka gani, linganisha na mwaka wa gari lako. Utaiona ignorance yako. Dreamliner ilianza kutengenezwa lini? Vioo vya dreamliner ya 2018 vinatofautiana na vile vya 2011? Msikilize Zitto kama unaona kagundua mbinu mpya za kuunda ndege. Muko wote kwenye himaya ya wapumbavu.
na mara nyingi wapumbavu sana huwaona wapumbavu kidogo ndio wapumbavu wa kutupa.wenye subira tunamsubria hakimu wa haki[muda]huwa haongopi
 
Tundu lissu alisema ukweli mwingiii walipoona unakaribia kupasuka wakamshindilia risasi za kiuno kibao,na mshenzi yule kasusa kabisa kufa kweli mungu sio kigwangala.
 
wewe kipi ujaelewa hapo... umeambiwa ndege iliyo tumika kazakstan ndio tuna kuja itumia... wewe una kuwa kama una maruani yakiamka basi hushikiki? una jadili milango na madirisha tu,,, mbona hili la kazakstan una liacha au hulioni?

usi zalau michango ya wengine wakati michango yako pia ina gap... mkuu heshimu na wengine... sasa jiulize tume nunua ndege kazakstan au boingi? na kwanini boingi akarabati hii ndege? je kwanini kuna makubaliano ya kulipa kidogo kidogo? kwa kuwa tume nunua mtumba? ili isije tokea kama ile ilyo kwama mwanza?

watanzania tuna bisha bisha tu bila hata kujiuliza....

ndege kioo kutengenezwa nchi nyingine na injini nchi nyingine ndio kuna uhalali wa kupewa mtumba? hata kama sio mtumba ni nini hasa.....

jana spika ame tamka kama serkali haina pesa iseme... lakini wakisema wengine serkali haina pesa deni lina kuwa tuna bisha haya mpingeni na spika sasa...

nyinyi watu waajabu sana... taifa letu limekuwa la shida shida hamna nafuu kila uchwao... ni bora tuka oji kuliko kutetea usicho kijua au tusicho kijua... kama uongo na zitto ana potosha umma basi hashitakiwe kwa uongo, ila mbona hashitakiwi?
huyu hana akili huyu anapinga kila kitu.
 
Terrible teen .........mzigo mpya ulioko sokoni kwa sasa ni 787-10 nashangaa Tanzania inaenda kununua 787-8 kama sio mtumba ni nini ? bora hata ingekuwa 787-9 maana ni za juzi juzi hii ni used imefanyiwa refurbishment tumepigwa.

Acha uvivu wewe. 787-10 na 787-9 ni line tofauti za production na bei yake ni tofauti sana. Usi comment kitu usichokijua. Nadhani kundi kubwa linalochangia jamiiforums siku hizi ni la vilaza watupu.
 
View attachment 786026 Anatujulisha Zitto Kabwe

Serikali inaficha jambo kuhusu Dreamliner 787-8, Tunaambiwa kwamba Ndege tunayonunua Boeing 787-8 Dreamliner Ndio kwanza inaundwa. Sio Kweli. Ndege hiyo iliundwa mwaka 2009 na kinachofanyika Sasa ni kubadilisha Injini yake Kwa sababu Injini za ndege hizo zilikuwa na matatizo ya kuwaka moto ( imetokea Kwa Ethiopian na Nippon Air ya Japan ). Ndege iliyoundwa mwaka 2009 leo inafanyiwa marekebisho kidogo tunauziwa bei ya ndege mpya.!!

Hata hizi Bombardier tulizonunua hazikuundwa baada ya sisi kuweka order. Ndege hizi ziliundwa mwaka 2014 na zilikuwa tayari zimenunuliwa na Kampuni ya ndege ya Kazakhstan kabla ya baadaye kuuziwa sisi. Ushahidi wa hili ni rahisi Sana, ukipanda ATCL Bombardier tafadhali soma maandishi madogo dirishani utaona S/N 0001519017-040 DATE 10/2014. Hiyo 10/2014 ni Oktoba, 2014.

Serikali inaficha jambo katika suala la ununuzi wa Ndege hii ya Dreamliner. Serikali inajua kuwa imenunua Terrible Teen Kwa bei kubwa kuliko ilivyostahili. Shirika la ndege la Boeing linajua kuwa wametupiga bei ya kuruka na kutudanganyia Kwa kubadili injini. Serikali inajua kuwa haikusimamia maslahi ya Taifa katika mazungumzo kuhusu bei.

Hapakuwa na Government Negotiation Team Kama ilivyo kawaida ya manunuzi makubwa ya namna haya. (Bunge halikuhusishwa, baraza la mawaziri halikuhusishwa, wadau wa maendeleo hawakuhusishwa). Bahati mbaya sana mazungumzo ya ununuzi wa ndege yalimhusisha Rais Magufuli na Katibu Mkuu Fedha James Doto peke yao (ambaye Lissu aliwahi kusema ni mtoto wa dada yake. Yani mtu na mjomba wake walijadiliana wakanunua ndege).

Shirika la Boeing wametumia uzoefu wetu mdogo kutupiga na Ni wajibu wa Watanzania wote Kwa kutumia mahusiano yetu yote duniani kuwataka Boeing wawajibike kwa udanganyifu wao kwetu. Boeing wanapaswa kurudisha sehemu ya Fedha yetu. Ni aibu Kwa Kampuni kubwa Kama Boeing kuiibia Nchi masikini Kama Tanzania. Watanzania mnakumbuka sakata la Radar? Hii ni kurushwa zaidi ya radar. Hela zetu zirudi tujenge Reli au kuongeza Ndege.

My uchunguzi:

Tukiangalia mashirika makubwa ya ndege yameweka order tangu 2011 inakuwaje sie tupate faster faster???

In September 2011, the 787 was first officially delivered to launch customer All Nippon Airways.[313] As of September 2017, the top three identified customers for the 787 are: All Nippon Airways with 83 orders (36 -8s, 44 -9s and three -10s), ILFC (an aircraft leasing company), with orders totaling 74 Boeing 787s (24 -8s and 50 -9s), and Etihad Airways with 71 orders (41 -9s and 30 -10s).[1]

Boeing 787 orders and deliveries by type
  • b0092fe38c71e761b2180758030e866a.png
 Orders


 Deliveries


Orders and deliveries through April 2018[1][314]

Habari zaidi, soma=>Diallo amjibu Zitto kuhusu ndege mtumba Dreamliner 787-8
 
Guys wazungu sio waafrica, yaan kama tumepigwa , dunia ya wazungu ingepiga kelele sana kama ilivyokuwa kwenye rada. so kwa vile jamaa wapo kimya naamini ndege yetu ni mpya na kila kitu kipo sawa
Zitto anadhani kampuni kubwa kama Boeing inaweza fanya ujinga kama wauza mawese wa mwandiga!!! Wako serious na biashara na ndo maana wanaexcel kila siku.
 
Kuna ile ndege ya rais ilinunuliwa na serikali ya awamu ya tatu na inasemekana tuliuziwa bei ghali sana hivi watanzania hatujifunzi?
 
Tanzania haiwezi kuwa kisiwa ndani ya East African Community; ni lazima tujipange kushindana. Akina Zito na Nape wanaopinga seroikali kunua Ndege, oneni pia majirani zetu nao wanavyokwenda kwa sipid kubwa kuhusu umiliki wa ndege. Kenya inajulikana iko mbele sana kwa hilo, na Rwanda nayo ilishajisogeza kidogo. Tanzania ndiyo imeanza kujisogeza, na Uganda nayo pia sasa inatia tambo. Twendeni na wakati; siyo kuwaambia wanachi kuwa Bombadia hazhatiztaki; wafundisheni wanachi wenu uzuri wa kusafri kwa ndege hizo kiuchumi

Uganda Airlines signs deal to buy 4 Bombardier jets, two
 
Tanzania haiwezi kuwa kisiwa ndani ya East African Community; ni lazima tujipange kushindana. Akina Zito na Nape wanaopinga seroikali kunua Ndege, oneni pia majirani zetu nao wanavyokwenda kwa sipid kubwa kuhusu umiliki wa ndege. Kenya inajulikana iko mbele sana kwa hilo, na Rwanda nayo ilishajisogeza kidogo. Tanzania ndiyo imeanza kujisogeza, na Uganda nayo pia sasa inatia tambo. Twendeni na wakati; siyo kuwaambia wanachi kuwa Bombadia hazhatiztaki; wafundisheni wanachi wenu uzuri wa kusafri kwa ndege hizo kiuchumi

Uganda Airlines signs deal to buy 4 Bombardier jets, two
hakuna anayekataa tusinunue ndege lakini kwanini tununue secondhand kwa bei ya new brand? huoni hayo ni matumizi mabaya ya hela ya umma? tukimpata rais mwingine kuna watu watapata tabu sana.
 
hakuna anayekataa tusinunue ndege lakini kwanini tununue secondhand kwa bei ya new brand? huoni hayo ni matumizi mabaya ya hela ya umma? tukimpata rais mwingine kuna watu watapata tabu sana.
Siyo kweli; hiyo ndege siyo second hand baba. Mwezi wa Aprili nilikuwa Seattle kikazi na wanafunzi wangu kwa vile ni jimbo la jirani na ninapoishi; mojawapo ya sehemu tuliyopitia ilikuwa ni production line ya dreamliner. Watafiti wa chuoni kwetu (siyo mimi) walihusika katika ufatiti wa composite materials zilizotumika kuunda ndege hiyo miaka ya 2000, hivyo Boeing imekuwa inakaribisha wanafunzi wetu kutembelea kiwanda kile kila mwaka. Niliona kwa macho yangu ndege hiyo ikiwa katika hatua za mwisho mwisho wa matengezo. Ndege huundwa kwa mikono, siyo kwa robot kama ilivyo magari, na ni project kama kujenga nyumba ya ghorofa. Ujenzi wake huenda pole pole sana kwa sababu ya quality control katika kila stage Ni kwa vile tulikuwa haturuhusiwi kupiga picha za production line, ningeweza kuwa na picha za kukuonyesha.

Dreamliner-8 za kwanza zilitoka mwaka 2011; hazikuwa nyingi kwa vile zilikuwa na matatizo kadhaa ya wiring na betri; hizo ndizo zilizopewa jina la Terrible Kid. Zote zilirudishwa kiwandani kurekebisha makosa hayo na zikauzwa tena kwa makampuni mbalimbali kwa bei nafuu. Ethiopian ilinunua terrible kids kama sita au nane hivi; nyingine ziliuzwa ama kama private jest au kwa mashirika mengine madogo madogo kwa matumizi kama regional jets. Mauzo ya terrible kids yalimalizika karibu miezi sita kabla ATCL haiwaweka order yake, hivyo ilibidi kiwanda kiunde ndege ile from scratch!.

Kweli kuna watu watapata tabu sana mwaka huu. Nimesoma kuwa booking ya Dreamliner kwa safari za Mwanza na Kilimanjaro imejaa mpaka katikati ya mwezi wa nane! Wahi ticket yako.
 
mimi huwa nawashangaa sana baadhi ya watanzania wapenda sifa za muda mfupi kupinga manunuzi ya ndege za kibiashara ambazo kila mtu akitaka anaitumia; je sasa ndio Serikali ingenunua ndege vita kwa gharama kubwa kama Uganda kwa mfano walio nunua Su-35 kwa mamilioni ya dola; ndege ambayo matumizi yake ni Mpaka vita itokee?? tuwe objective kidogo na kuunga mkono pale inapostahili.
 
Back
Top Bottom