So long as deals kama hizi za ununuzi wa ndege zitabaki mambo ya kufanywa na mtu na mpwa wake bila kufuata taratibu za kisheria za manunuzi, tutarajie tu taarifa kama hizi nyingi tu huko tuendako.Zitto mwenyewe yuko wapi? Ni mwanachama hapa JF. Tunamuomba aje hapa tujadili badala yenu watumwaji.
Kuna mambo yanaleta utoto JF. Au, Zito mwenyewe ignorance iko juu. Taarifa hii yaweza kuwa ni kweli lakini siyo kwa ushahidi huo anaouonyesha Zitto. Boeing siyo duka la mtaa wa Kongo, kariakoo. wanalinda heshima kwa nguvu zote. Sema kwamba serikali imenunua ndege zilizotumika na kudanganya ni mpya, lakini Boeing watatoa wapi ndege zilizotumika? Boeing haina shirika la usafiri! Suala la kusoma ser. # ya kioo cha ndege ni upuuzi mwingine uliozidi. Ndege au hata magari hayatengenezwi kama fanicha za Keko.
Parts za ndege na magari huundwa na makampuni mbali mbali duniani. Ukiangalia gari lako unaweza ukakuta ignition switch imetengenezwa Germany wakati gari limetoka Japan. Au hapo hapo Japan, kuna parts zinatengenezwa na makampuni maalumu nje ya kiwanda cha magari. Ser. # na tarehe inayoandikwa ni ya huko part ilikotengenezwa. Anzeni kuelewa kwamba kutegemea bunge kama kigezo cha ufahamu ni hatari.
Zitto lete ushahidi mwingine na siyo namba za kwenye vioo. That is nonsense!
Mtu hawezi tu kukurupuka kununua ndege utafikiri ananunua kwa fedha zake bila kuhusisha bunge ili yapatikane mawazo ya wawakilishi wa wananchi, hii ni kinyume cha sheria..!!
Kwa mambo kama haya, ni sharti hawa wahusika waelewe kuwa huko mbele lazima watakuja waeleze siku moja wapi walipopata mamlaka ya kufanya hayo waliyofanya.