Return Of Undertaker
JF-Expert Member
- Jun 12, 2012
- 4,572
- 26,868
Serikali inaficha jambo kuhusu Dreamliner 787-8, Tunaambiwa kwamba Ndege tunayonunua Boeing 787-8 Dreamliner Ndio kwanza inaundwa. Sio Kweli. Ndege hiyo iliundwa mwaka 2009 na kinachofanyika Sasa ni kubadilisha Injini yake Kwa sababu Injini za ndege hizo zilikuwa na matatizo ya kuwaka moto ( imetokea Kwa Ethiopian na Nippon Air ya Japan ). Ndege iliyoundwa mwaka 2009 leo inafanyiwa marekebisho kidogo tunauziwa bei ya ndege mpya.!!
Hata hizi Bombardier tulizonunua hazikuundwa baada ya sisi kuweka order. Ndege hizi ziliundwa mwaka 2014 na zilikuwa tayari zimenunuliwa na Kampuni ya ndege ya Kazakhstan kabla ya baadaye kuuziwa sisi. Ushahidi wa hili ni rahisi Sana, ukipanda ATCL Bombardier tafadhali soma maandishi madogo dirishani utaona S/N 0001519017-040 DATE 10/2014. Hiyo 10/2014 ni Oktoba, 2014.
Serikali inaficha jambo katika suala la ununuzi wa Ndege hii ya Dreamliner. Serikali inajua kuwa imenunua Terrible Teen Kwa bei kubwa kuliko ilivyostahili. Shirika la ndege la Boeing linajua kuwa wametupiga bei ya kuruka na kutudanganyia Kwa kubadili injini. Serikali inajua kuwa haikusimamia maslahi ya Taifa katika mazungumzo kuhusu bei.
Hapakuwa na Government Negotiation Team Kama ilivyo kawaida ya manunuzi makubwa ya namna haya. (Bunge halikuhusishwa, baraza la mawaziri halikuhusishwa, wadau wa maendeleo hawakuhusishwa). Bahati mbaya sana mazungumzo ya ununuzi wa ndege yalimhusisha Rais Magufuli na Katibu Mkuu Fedha James Doto peke yao (ambaye Lissu aliwahi kusema ni mtoto wa dada yake. Yani mtu na mjomba wake walijadiliana wakanunua ndege).
Shirika la Boeing wametumia uzoefu wetu mdogo kutupiga na Ni wajibu wa Watanzania wote Kwa kutumia mahusiano yetu yote duniani kuwataka Boeing wawajibike kwa udanganyifu wao kwetu. Boeing wanapaswa kurudisha sehemu ya Fedha yetu. Ni aibu Kwa Kampuni kubwa Kama Boeing kuiibia Nchi masikini Kama Tanzania. Watanzania mnakumbuka sakata la Radar? Hii ni kurushwa zaidi ya radar. Hela zetu zirudi tujenge Reli au kuongeza Ndege.
My uchunguzi:
Tukiangalia mashirika makubwa ya ndege yameweka order tangu 2011 inakuwaje sie tupate faster faster???
In September 2011, the 787 was first officially delivered to launch customer All Nippon Airways.[313] As of September 2017, the top three identified customers for the 787 are: All Nippon Airways with 83 orders (36 -8s, 44 -9s and three -10s), ILFC (an aircraft leasing company), with orders totaling 74 Boeing 787s (24 -8s and 50 -9s), and Etihad Airways with 71 orders (41 -9s and 30 -10s).[1]
Boeing 787 orders and deliveries by type
Deliveries
Orders and deliveries through April 2018[1][314]
Habari zaidi, soma=>Diallo amjibu Zitto kuhusu ndege mtumba Dreamliner 787-8