Zitto: Tunaomba radhi kwa mapungufu yaliojitokeza

Zitto alimaanisha kila figure times 1,000,000 au times 1000? hapo sijamsoma vizuri
 
Huu ndio uungwana sio kung'ang'ania kitu hata kama naona kabisa kuwa hakuna maslahi ya umma. Sisis wote tu binadamu hivyo kufanya makosa ni kilimwengu. CCM wajifunze kuwa kukosea na kukosolewa ni kawaida.
 
Zitto alimaanisha kila figure times 1,000,000 au times 1000? hapo sijamsoma vizuri

ukipitia michango ya wajumbe hapo juu utaelewa vizuri wameisha dadafua; ila ki-ukweli inabidi aandike figure iliyokamilika kama ni Trilion basi iandikwe kama ilivyo ili watu waelewe siyo tena kuwaweka kwenye utata, huyu Mwigulu Nchemba yeye anaangalia makosa madogo tu ndo anayavalia njunga as if kwamba ni makosa makuuubwa.
,
 
ni uungwana mtu kukiri kosa lkn nadhani ktk takwimu hapo juu bado kuna kosa. neno sahihi ni bilioni siyo milioni. nadhani hivyo. kosa hilo limewagharimu sn wabunge wa chdm bungeni. walio wengi wanatukana hata kuchangia bajeti hawachangii. chdm changieni bajeti kwa kuonesha mapungufu yake. kutukana hakusaidii chochote. mtaonekana wakorofiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii

Figa zipo sahihi, kusingekuwa na neno milioni ndio ingekuwa imekosewa.
Muungwana yeyote huomba randhi haijalishi kosa ni kubwa kiasi gani au dogo kiasi gani. Na mapungufu katika shuhuri za kinadam hutokea, la msingi ni kuona na kukubali kuwa umekosea na kurekebisha makosa yaliotokea.
Kila kitu katika maisha kinakuwa bora zaidi siku hadi siku kutokana na kurekebisha au kuboresha zaidi yaliofanyika kabla ya sasa.

Otherwise ni hekima uungwana na uajsiri kuomba radhi.
 
Still amekosea kama sio ku-copu jedwali sawasawa. Nadhani ni katika maelfu?I mean figure ni za mabilioni na sio mamilioni...

Kwa hiyo unataka aseme billion 408,318? Itamaanisha trilion ni sawa alivyoweka.
 
Maelezo ya Bajeti Kivuli

Katika mjadala unaoendelea Bungeni kuhusu Bajeti, baadhi ya wabunge wameeleza kwamba Bajeti Kivuli haikuonyesha vyanzo vya mapato na hivyo kuita ni vyanzo sifuri. Ukweli ni kwamba tumeweka vyanzo vya mapato ya ndani kwa ujumla bila kuainisha mapato ya kikodi ni ngapi, mapato yasiyo ya kikodi ni ngapi na mapato ya Halmashauri ni kiasi gani. Hivyo tunakiri kosa hili na tumechukua hatua ya kuainisha mapato hayo Kama inavyoonekana kwenye jedwali hili hapa chini.

Mapato haya yamo ndani ya Hotuba ya Bajeti Mbadala lakini kwa makosa ya kihariri hayakuonyeshwa kwenye jedwali na hivyo kuleta usumbufu kwa Wabunge na Watanzania wengine waliopata fursa ya kusoma Hotuba yetu. Tunaomba radhi kwa usumbufu. Nawashukuru walioona tatizo hili na hii inaonyesha kuwa wabunge wanasoma kwa makini Bajeti ya Upinzani.

Ninawatakia mjadala mwema wa Bajeti.

JUMLA YA MAPATO YA NDANI
Tshs. Millioni 11,889,078/-

MAPATO YA KODI
Tshs. Millioni 10,232,539/-

MAPATO YASIYO YA KODI
Tshs. Milion 1,163,533/-

MAPATO YA HALMASHAURI
Tshs. Milioni. 493,006/-

Kabwe Zuberi Zitto,Mb
Waziri Kivuli wa Fedha

Waziri kivuli wa Fedha = Waziri Giza wa Fedha
 
kila mtu anaweza kukosea ila MAGAMBA yakikosea hayataki kukiri. wamenunua ndege mbovu ya rais hawajatokeza hadharani kuomba radhi!
 
Kwa wachumi na tunaofanya kazi za Bajeti. Hilo ni kosa kubwa sana.

Shukran kwa kuliona na kuwa makini sana kwani hicho ndio moyo wa bajeti yako.
 
Cdm wako makini wamekosea na wamekiri hao ccm hadi waandamane watu ndio wakiri.
Big up Zitto muungwana ni vitendo!
 
kumbe na chadema wanakoseaga!!!!!!!!!!,tehe tehe

Kweli wabongo ni wavivu wa kufikiri, be great thinker, hiyo figure haijakosewa, kwani hamjui kuwa kuna million 1000 katika billion moja, na kuna billion 1000 katika trilion moja, sasa kakosea nini?
 
Kikubwa ni kurekebisha mapungufu kule kwa Dr Mgimwa ili buget isimame kama ruler!
Tatizo wachangiaji wasomi wanakuacha upotee. Ngoja mimi mpumbavu mwenzako nikusaidie. Bajeti ya Mgimwa/mafisadi imetenga pesa nyingi kwa matumizi ya kawaida ya serikali i.e 70% wamefanya hivyo kwa kusudi ili ziweze kurudi kwenye mifuko ya mafisadi. Asilimia chache ndo imeelekezwa kwenye maendeleo ujenzi wa barabara, shule, hospitali, maji, kuboresha kilimo n.k. TETEA BAJETI YA MGIMWA UNUNUE DUMU LA MAJI SH'NGI 1500
 
Unajua ni rahisi kumis izi figures bse Zitto hutumia IPAD kupresent so wale wazee wa kufungua kurasa ndo ilikuwa inamiss ila kwake kitu soft copy kilikuwa intact!
Chamsingi ni content izo tarakimu haitakiwi kuwa issue!
 
10bn$ zitatufikisha wapi?
Ni upuuzi ule ule


Huo ndiyo uwezo wa Taifa lako kwa sasa............. sasa sijui ulitaka waseme wataenda kuomba kama Matonya au??? Off course unatakiwa kuquestion given that hizo pesa zina uwezo wa kujenga nyumba tatu tu za Prof. Ndullu wa BOT!!! Otherwise, kuna kosa kwenye hizo figure!!
 
Back
Top Bottom