Zitto: Tunaomba radhi kwa mapungufu yaliojitokeza

[h=6]Maelezo ya Bajeti Kivuli Katika mjadala unaoendelea Bungeni kuhusu Bajeti, baadhi ya wabunge wameeleza kwamba Bajeti Kivuli haikuonyesha vyanzo vya mapato na hivyo kuita ni vyanzo sifuri. Ukweli ni kwamba tumeweka vyanzo vya mapato ya ndani kwa ujumla bila kuainisha mapato ya kikodi ni ngapi, mapato yasiyo ya kikodi ni ngapi na mapato ya Halmashauri ni kiasi gani. Hivyo tunakiri kosa hili na tumechukua hatua ya kuainisha mapato hayo Kama inavyoonekana kwenye jedwali hili hapa chini. Mapato haya yamo ndani ya Hotuba ya Bajeti Mbadala lakini kwa makosa ya kihariri hayakuonyeshwa kwenye jedwali na hivyo kuleta usumbufu kwa Wabunge na Watanzania wengine waliopata fursa ya kusoma Hotuba yetu. Tunaomba radhi kwa usumbufu. Nawashukuru walioona tatizo hili na hii inaonyesha kuwa wabunge wanasoma kwa makini Bajeti ya Upinzani. Ninawatakia mjadala mwema wa Bajeti. JUMLA YA MAPATO YA NDANI Tshs. Millioni 11,889,078/- MAPATO YA KODI Tshs. Millioni 10,232,539/- MAPATO YASIYO YA KODI Tshs. Milion 1,163,533/- MAPATO YA HALMASHAURI Tshs. Milioni. 493,006/- Kabwe Zuberi Zitto,Mb Waziri Kivuli wa Fedha[/h]
Budget ya Zitto haina Jipya!Kelele nyingii mpaka wanasahau vitu muhimu vya Kiufundi!Sehemu kubwa Budget Mh.Zito Kadesa kwa Dr.Mgimwa,Budget ya zito Wala haina mashiko ya kuwa budget mbadala!Kikubwa ni kurekebisha mapungufu kule kwa Dr Mgimwa ili buget isimame kama ruler!Hii ya Upinzani ni MKWECHE kama mimi!Ndo mana mchemba anaitupa!
 
Badala ya kuaandaa bajeti mnaandaa maandamano. Mwishoni mnakuja na madudu bungeni.
 
Are they millions, bilions or milions? Kama mapato ni hizo milioni kadhaa then hata mkoa mmoja hatuwezi kuendesha.
 
Wako busy kuandamana jamani budget mbadala itatengenezwa sangapi
 
hii ilikuwa ni janja ya CDM kujifanya wamesahau na kukubali kurekebisha makosa ili iwe the same kwa CCM. ila sijui kama watarekebisha kama Cdm
 
Duh budget ya Serikali inalaumiwa na serikali kivuli. Serikali kivuli imeleta budget kivuli ambayo ni sifuri kabisaa! Tunaenda wapi kama hata serikali mbadala inaonekana kuvulunda zaidi afadahali ya serikali iliyopo? Tuna kazi kubwa katika nchi hii.
 
Still amekosea kama sio ku-copu jedwali sawasawa. Nadhani ni katika maelfu?I mean figure ni za mabilioni na sio mamilioni...

Ma wee! Kweli number ni aleji(mzio) ya Taifa. Mtu amesha anza na neno milioni, lakini bado watu wanataka masifuri yote yaonekane!
 
Zitto, amechafua zaidi. Lakini imetusaidia sana sisi wapiga kura kugundua na kutambua mapema kuwa hata chadema ikishika hatamu bado uzembe utaendelea kujitokeza.
 
Still amekosea kama sio ku-copu jedwali sawasawa. Nadhani ni katika maelfu?I mean figure ni za mabilioni na sio mamilioni...
TARAKIMU ZA BAJETI TUZIJUE;
100- MIA MOJA
1000-ELFU MOJA
100,000/=-MIA MOJA ELFU(LAKI MOJA)
1,000,000/=-MILIONI MOJA
1,000,000,000/=-BILIONI MOJA
1,000,000,000,000,/=TRILIONI MOJA
Na kuna
-Qadilion
-Octalioni
-Saxilioni
Na n.k:thinking:
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Kila siku nawaeleza hawa jamaa hawana capacity ya kuongoza nchi yetu. Hebu angalia makosa kama hayo. Inaoneka Mh. Zito aliiandika mwenyewe kwa kukesha na hakuna mwingine aliye na uwezo wakusahihisha alicho kosea. AIBU
 
umeeleweka Zitto; ila kwakweli uzembe kama huu usirudiwe tena; watu wanaitolea sana macho CDM kwahiyo viongozi wetu muwe Makini.
 
Still amekosea kama sio ku-copu jedwali sawasawa. Nadhani ni katika maelfu?I mean figure ni za mabilioni na sio mamilioni...

Nadhani wewe ndiyo umekosea. 1000 million hutengenza billion; na 1,000,000 million hutengeneza trilioni; na ndicho alichoandika Zitto.
 
Jamani zito. Nakuamini sana lakini kwa budget hii unaniangusha kaka, haina hats misaada ya kutoka nje, isitoshe Tanzania sio kichaka ktk dunks hii, ulikurupuka kaka, yulle mch feki wa iringa alikuwa wapi au alikuwa anajiandaa kuqoute falsafa. Tanzania haitaweza kuendeshwa kwa falsafa jamani watt wafanye kazi.
 
Back
Top Bottom