Zitto: Tunaomba radhi kwa mapungufu yaliojitokeza | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zitto: Tunaomba radhi kwa mapungufu yaliojitokeza

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kibanga Ampiga Mkoloni, Jun 19, 2012.

 1. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #1
  Jun 19, 2012
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,565
  Likes Received: 1,652
  Trophy Points: 280
  [h=6]Maelezo ya Bajeti Kivuli

  Katika mjadala unaoendelea Bungeni kuhusu Bajeti, baadhi ya wabunge wameeleza kwamba Bajeti Kivuli haikuonyesha vyanzo vya mapato na hivyo kuita ni vyanzo sifuri. Ukweli ni kwamba tumeweka vyanzo vya mapato ya ndani kwa ujumla bila kuainisha mapato ya kikodi ni ngapi, mapato yasiyo ya kikodi ni ngapi na mapato ya Halmashauri ni kiasi gani. Hivyo tunakiri kosa hili na tumechukua hatua ya kuainisha mapato hayo Kama inavyoonekana kwenye jedwali hili hapa chini.

  Mapato haya yamo ndani ya Hotuba ya Bajeti Mbadala lakini kwa makosa ya kihariri hayakuonyeshwa kwenye jedwali na hivyo kuleta usumbufu kwa Wabunge na Watanzania wengine waliopata fursa ya kusoma Hotuba yetu. Tunaomba radhi kwa usumbufu. Nawashukuru walioona tatizo hili na hii inaonyesha kuwa wabunge wanasoma kwa makini Bajeti ya Upinzani.

  Ninawatakia mjadala mwema wa Bajeti.

  JUMLA YA MAPATO YA NDANI
  Tshs. Millioni 11,889,078/-

  MAPATO YA KODI
  Tshs. Millioni 10,232,539/-

  MAPATO YASIYO YA KODI
  Tshs. Milion 1,163,533/-

  MAPATO YA HALMASHAURI
  Tshs. Milioni. 493,006/-

  Kabwe Zuberi Zitto,Mb
  Waziri Kivuli wa Fedha[/h]
   
 2. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #2
  Jun 19, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,506
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  Still amekosea kama sio ku-copu jedwali sawasawa. Nadhani ni katika maelfu?I mean figure ni za mabilioni na sio mamilioni...
   
 3. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #3
  Jun 19, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  Next time kuwa makini Mheshimiwa, mmempa yule mzinzi wa kitaifa Mwigulu Nchemba jukwaa la kusemea maana kwa kuwa yeye ni chongo kati ya vipofu CCM anaikashifu sana hiyo bajeti. Anadai figure imechomekwa dakika za mwisho. Kosa lisirudiwe tena hilo
   
 4. shegaboy

  shegaboy JF-Expert Member

  #4
  Jun 19, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 214
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tunashukuru kwa kukiri na kuonyesha mko makini pia. Ila najua kwa vyovyote mlikuwa nalengo si bure nalengo limetimia Mh. Zito kwani imeonyesha wenzetu wamesoma kifungu hadi kifungu hii ni changamoto kwao big -up
   
 5. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #5
  Jun 19, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Zitto unapopambana na adui jitahidi kadri uwezavyo kutofanya kosa kwani adui atatumia udhaifu huo, kama walivyofanya baadhi ya wabunge wa ccm. Pamoja na kosa hilo, nakupongeza kwa kukiri kosa. Endeleeni vijana wetu kulikomboa taifa letu. Watanzania tunaona tena mpaka vijijini jinsi mapambano yenu yanavyoleta mabadiliko makubwa kimtazamo. Hali hii ikiendelea, hakika nasema tena hakika ccm haina chake ifikapo 2015.
   
 6. Jiwe Linaloishi

  Jiwe Linaloishi JF-Expert Member

  #6
  Jun 19, 2012
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 3,734
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 145
  noted sir
   
 7. m

  mwongozo Member

  #7
  Jun 19, 2012
  Joined: Oct 26, 2011
  Messages: 45
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ni uungwana mtu kukiri kosa lkn nadhani ktk takwimu hapo juu bado kuna kosa. neno sahihi ni bilioni siyo milioni. nadhani hivyo. kosa hilo limewagharimu sn wabunge wa chdm bungeni. walio wengi wanatukana hata kuchangia bajeti hawachangii. chdm changieni bajeti kwa kuonesha mapungufu yake. kutukana hakusaidii chochote. mtaonekana wakorofiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
   
 8. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #8
  Jun 19, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,528
  Likes Received: 882
  Trophy Points: 280
  Yes lazima iwe a sifuri tatu
   
 9. m

  majebere JF-Expert Member

  #9
  Jun 19, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 4,520
  Likes Received: 567
  Trophy Points: 280
  Hili ndio tatizo la kutokujipanga,wanasiasa vijana wana papara sana.
   
 10. KOMBESANA

  KOMBESANA JF-Expert Member

  #10
  Jun 19, 2012
  Joined: Jun 18, 2009
  Messages: 862
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  wewe hesabu hiyo iko fresh
   
 11. KOMBESANA

  KOMBESANA JF-Expert Member

  #11
  Jun 19, 2012
  Joined: Jun 18, 2009
  Messages: 862
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Majebere,pole kwa uzee,wapiga kura wazee nao wamepungua,tuache na matatizo yetu,ng'atuka kama Nyerere!
   
 12. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #12
  Jun 19, 2012
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,677
  Likes Received: 633
  Trophy Points: 280
  10bn$ zitatufikisha wapi?
  Ni upuuzi ule ule
   
 13. Pinokyo Jujuman

  Pinokyo Jujuman JF-Expert Member

  #13
  Jun 19, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 553
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mmmh ni uungwana sana kuomba radhi; lakini hivi Zigo hili walikuachia peke ako kaka?
  Imekuaje hata wenzako nao waloipitia hawakuyagundua makosa haya hata kabla hujaileta mjengoni au ndio mpango nyemelezi wa kukupunguza nguvu kwa kusaka makosa madogo madogo ktk safari ya 2015?
  Be strong jombaa usitetereke makosa ya kibinadamu ingawa naona umeikosea tena hapo juu, tulia Usipanic.
  Wewe ni Kiongozi Makini.
   
 14. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #14
  Jun 19, 2012
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,068
  Trophy Points: 280
  Kwani trillion moja ina sifuri ngapi? Najua million ni sifuri sita, billion ni sifuri tisa.
   
 15. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #15
  Jun 19, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,736
  Likes Received: 1,447
  Trophy Points: 280
  Asante kwa sahihisho, tafadhali endelea na maandalizi mazuri ya hitimisho la bajeti yako ili tuweze kupata action-plan
   
 16. K

  Kiula Senior Member

  #16
  Jun 19, 2012
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 114
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Matatizo Kama hayo hutokea naomba tu yarekebishwe ili next time msiwape nguvu adui zenu
   
 17. Endeleaaa

  Endeleaaa JF-Expert Member

  #17
  Jun 19, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,223
  Likes Received: 314
  Trophy Points: 180
  Saa ngapi wataweza kuandaa bajeti makini wakati mda wote wameuweka kwenye M4U, hawajali majukumu yao. hivi kweli wanaweza kuwa chama m-badala hawa? Mtanzania ni mtanzania tu regardless CCM or CDM
   
 18. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #18
  Jun 19, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,692
  Likes Received: 12,738
  Trophy Points: 280
  Hivi makalio ya viongozi wa serikali kwenye almashauri zetu yana misumeno?
   
 19. h

  hans79 JF-Expert Member

  #19
  Jun 19, 2012
  Joined: May 4, 2011
  Messages: 3,802
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 145
  waliomchomeka jakaya akasaini lakini dr kamili, akasema hicho sicho nao walikuwa vijana? acha unjaa njaa.
   
 20. h

  hans79 JF-Expert Member

  #20
  Jun 19, 2012
  Joined: May 4, 2011
  Messages: 3,802
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 145
  waliomchomeka jakaya akasaini lakini dr kamili, akasema hicho sicho nao walikuwa vijana? acha unjaa njaa.
   
Loading...