Return Of Undertaker
JF-Expert Member
- Jun 12, 2012
- 4,572
- 26,868
“ Juhudi za ujenzi wa Reli ya Kati ni juhudi za kimaendeleo na hazina budi kupongezwa na kila mpenda maendeleo. Reli ina faida kubwa kwa nchi na Kiongozi yeyote anayefanya maamuzi muhimu kama haya hana budi kupongezwa kwa dhati. Hata hivyo, Serikali ni lazima ifungue masikio kusikiliza maoni mbadala katika utekelaji wa miradi mikubwa kama hii ambayo inatumia fedha nyingi, na tumeamua kutumia fedha za ndani.
Uamuzi wa kutumia fedha za ndani ni uamuzi mchungu kwani maana yake badala ya kuwekeza kwenye miradi ya Kilimo ili kuongeza uzalishaji wa chakula na bidhaa za kuuza nje, tumeamua kujenga reli. Badala ya kuongeza vyuo vikuu na vyuo vya ufundi ili kuongeza maarifa na wataalamu katika nchi yetu, tumeamua kujenga reli. Badala ya kuwekeza kwenye kumaliza kabisa tatizo la mtindio wa ubongo (stuntedness) ambalo ni tatizo kubwa sana kwa nchi yetu kwa sasa kwani Watanzania 34 katika 100 wametindiwa ubongo, tumeamua kujenga reli.
Kupanga ni kuchagua. (Serikali) mmeamua kwa niaba yetu kutumia rasilimali fedha zetu kidogo kujenga Reli (na kununua ndege) na haya mengine yasubiri kwanza. Uongozi ni uamuzi. Mmeamua, hatuna namna. Lakini tusikilizeni sisi wawakilishi wa wananchi, mawazo yetu ni kusaidia kupunguza maumivu ya maamuzi yenu bila kuathiri utekelezaji wa miradi husika. Mimi binafsi ninaunga mkono uwekezaji kwenye Reli, lakini siungi mkono namna uwekezaji huu unafanywa.”
Sehemu ya Hotuba yangu Bungeni April, 2017