Evans-Arsenal
JF-Expert Member
- Jan 10, 2016
- 868
- 1,385
Mbunge wa Kigoma Mh Zitto Zuberi Kabwe ambaye pia ni kiongozi wa ACT wazalendo amesema kwamba wameamua kumuweka pembeni mwenyekiti wao wa zamani Mama Anna Mghirwa ili kutoa dhana kwamba ACT ni CCM B.
"Sasa tunaweka kanuni ambazo mtu akichaguliwa na uongozi wa juu unaoongozwa na Chama kingine tofauti na ACT basi tufanye kwanza mazungumzo kabla ya mtu kukubali tu bila kutoa taarifa" alisema Mh Zitto Kabwe.
Pia akaongeza kwa kusema kwamba kwa sasa wameshachagua kaimu mwenyekiti wao wa Chama na anaendelea na majukumu kama kawaida.