Zitto: Sio kosa kuiandikia barua Benki ya Dunia isiipe mkopo Tanzania

Makanyaga

JF-Expert Member
Sep 28, 2007
4,582
2,000
Zitto kuandika barua Benki ya Dunia siyo kosa ndiyo, ila kosa ni kutumia nembo ya Bunge kuiandikia Benki ya Dunia, na kusaini barua kama Mbunge wa JMT, wakati Bunge halikuwa na taarifa rasmi kuhusiana na barua yake hiyo.

Zitto alitakiwa aandike barua hiyo kama Kiongozi Mkuu wa ACT Wazalendo, na aisaini kama kiongozi wa ACT na si kama Mbunge. Au angeiandika kama mtu asiyekuwa na cheo kama mimi hapa, yaani kama raia tu mkereketwa na angeisaini kwa kutumia hadhi hiyo.
Sasa yeye analiumia Bunge la JMT kuipiga Nchi halafu bado kosa anakuwa halioni?

Ninasikitika kwamba kosa hili liko wazi na kwamba hakutakiwa kuwa angekuwa hajaliona mpaka leo, intelligent as he is!

================================

Dar es Salaam. Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo nchini Tanzania, Zitto Kabwe amesema haoni kama Mwanasheria Mkuu wa Serikali atamkuta na kosa kutokana na kuiandikia barua Benki ya Dunia (WB) akitaka isiidhinishe mkopo wa Sh1.2 trilioni kwa Tanzania kwa ajili ya sekta ya elimu.

Zitto ameeleza hayo leo Jumanne Februari 18, 2020 katika mkutano wake na waandishi wa habari baada ya kuchukua fomu ya kutetea nafasi yake katika uchaguzi wa chama hicho.

Katika mkutano wa 18 wa Bunge uliomalizika hivi karibuni mjini Dodoma, Zitto alishukiwa na wabunge kwa kitendo chake hicho huku Spika Job Ndugai akisema watamsubiri arejee nchini ili wamuulize sababu za kufanya hivyo, hapohapo akamtaka Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuangalia kama kuna uwezekano wa kuwemo jinai katika kitendo hicho.

Katika mkutano wake huo Zitto amesema, “sioni kosa lolote ambalo Mwanasheria Mkuu wa Serikali anaweza akalikuta kwamba nimelifanya kwa kuandika barua WB. Hizi ni siasa tu ambazo zilikuwa hazifanyiki huko nyuma, au watu walikuwa wanafanya kwa kificho sasa mimi nimezifanya kwa uwazi ndio tofauti tu hiyo, haina maana kuwa ni kitu kipya sana”

Amesema kila Mtanzania ana haki ya kuwasiliana na Benki ya Dunia iwapo Serikali yake kuna mambo imekosea katika maombi ya fedha katika benki hiyo.

Chanzo: Mwananchi
 
chabuso

JF-Expert Member
Feb 18, 2013
5,575
2,000
Kwani huyu Zitto hana ofisi pale Bungeni, Je na Yeye hajumuiki na Wabunge wengine kutoka chama tawala na cha upinzani kukubali au kupinga baadhi ya mambo ya Bunge..?

Nafikiri Zitto katuma ile barua kwa WB kama Mbunge sio Mwenyekiti wa ACT..
 
MkamaP

JF-Expert Member
Jan 27, 2007
7,923
2,000
Huyu jamaa amejaribu kila namna ili ashikwe kuwe na headlines kwa vyombo vya kitaifa na kimataifa.

Jamaa huyu wampotezee hivyo hivyo, wala wasimguse ili akisema hakuna uhuru wa kuongea watu wamshangae.
 
Mwananchi

JF-Expert Member
Oct 4, 2012
2,931
2,000
Kwani huyu Zitto hana ofisi pale Bungeni, Je na Yeye hajumuiki na Wabunge wengine kutoka chama tawala na cha upinzani kukubali na kupinga baadhi ya mambo ya Bunge..

Nafikiri Zitto katuma ile barua kwa WB kama Mbunge sio Mwenyekiti wa ACT..
Mara ngapi tunaona masenata au representative wa Marekani wanatumia headed letter za mabunge yao. Waache ushamba
 
Jorojik

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
2,885
2,000
Huyu jamaa amejaribu kila namna ili ashikwe kuwe na headlines kwa vyombo vya kitaifa na kimataifa.

Jamaa huyu wampotezee hivyo hivyo, wala wasimguse ili akisema hakuna uhuru wa kuongea watu wamshangae.
Kwani watu hawajui tayari kuna watu washamiminiwa risasi za kutosha na akina Kabendera sasa wapo mahakamani kutokana na mambo hayo ya uhuru wa kusema?
 
Stuxnet

JF-Expert Member
Feb 12, 2011
3,207
2,000
Zitto kuandika barua Benki ya Dunia siyo kosa ndiyo, ila kosa ni kutumia nembo ya Bunge kuiandikia Benki ya Dunia, na kusaini barua kama Mbunge wa JMT, wakati Bunge halikuwa na taarifa rasmi kuhusiana na barua yake hiyo.

Zitto alitakiwa aandike barua hiyo kama Kiongozi Mkuu wa ACT Wazalendo, na aisaini kama kiongozi wa ACT na si kama Mbunge. Au angeiandika kama mtu asiyekuwa na cheo kama mimi hapa, yaani kama raia tu mkereketwa na angeisaini kwa kutumia hadhi hiyo.
Sasa yeye analiumia Bunge la JMT kuipiga Nchi halafu bado kosa anakuwa halioni?

Ninasikitika kwamba kosa hili liko wazi na kwamba hakutakiwa kuwa angekuwa hajaliona mpaka leo, intelligent as he is!

================================

Dar es Salaam. Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo nchini Tanzania, Zitto Kabwe amesema haoni kama Mwanasheria Mkuu wa Serikali atamkuta na kosa kutokana na kuiandikia barua Benki ya Dunia (WB) akitaka isiidhinishe mkopo wa Sh1.2 trilioni kwa Tanzania kwa ajili ya sekta ya elimu.

Zitto ameeleza hayo leo Jumanne Februari 18, 2020 katika mkutano wake na waandishi wa habari baada ya kuchukua fomu ya kutetea nafasi yake katika uchaguzi wa chama hicho.

Katika mkutano wa 18 wa Bunge uliomalizika hivi karibuni mjini Dodoma, Zitto alishukiwa na wabunge kwa kitendo chake hicho huku Spika Job Ndugai akisema watamsubiri arejee nchini ili wamuulize sababu za kufanya hivyo, hapohapo akamtaka Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuangalia kama kuna uwezekano wa kuwemo jinai katika kitendo hicho.

Katika mkutano wake huo Zitto amesema, “sioni kosa lolote ambalo Mwanasheria Mkuu wa Serikali anaweza akalikuta kwamba nimelifanya kwa kuandika barua WB. Hizi ni siasa tu ambazo zilikuwa hazifanyiki huko nyuma, au watu walikuwa wanafanya kwa kificho sasa mimi nimezifanya kwa uwazi ndio tofauti tu hiyo, haina maana kuwa ni kitu kipya sana”

Amesema kila Mtanzania ana haki ya kuwasiliana na Benki ya Dunia iwapo Serikali yake kuna mambo imekosea katika maombi ya fedha katika benki hiyo.

Chanzo: Mwananchi
Hakuna hoja ya kujadili kuhusu Zitto Kabwe kutumia nembo ya Bunge la JMT kwa kuwa naye ni Mbunge na kasaini kwa ofisi yake. Kumbukeni kila Halmashauri kuna Ofisi ya Mbunge na anagharamikiwa na Serikali.

Ingekuwa kosa kama Zitto Kabwe angetumia Letterhead ya Bunge la JMT halafu akasaini kwa anuani ya Ofisi ya Bunge Dodoma.
 
MkamaP

JF-Expert Member
Jan 27, 2007
7,923
2,000
Kwani watu hawajui tayari kuna watu washamiminiwa risasi za kutosha na akina Kabendera sasa wapo mahakamani kutokana na mambo hayo ya uhuru wa kusema?
Wamuache tu hivyo hivyo zito bila kumjibu chochote wawe kimya.
 
Ngalikihinja

JF-Expert Member
Sep 1, 2009
21,040
2,000
Zitto kuandika barua Benki ya Dunia siyo kosa ndiyo, ila kosa ni kutumia nembo ya Bunge kuiandikia Benki ya Dunia, na kusaini barua kama Mbunge wa JMT, wakati Bunge halikuwa na taarifa rasmi kuhusiana na barua yake hiyo.

Zitto alitakiwa aandike barua hiyo kama Kiongozi Mkuu wa ACT Wazalendo, na aisaini kama kiongozi wa ACT na si kama Mbunge. Au angeiandika kama mtu asiyekuwa na cheo kama mimi hapa, yaani kama raia tu mkereketwa na angeisaini kwa kutumia hadhi hiyo.
Sasa yeye analiumia Bunge la JMT kuipiga Nchi halafu bado kosa anakuwa halioni?

Ninasikitika kwamba kosa hili liko wazi na kwamba hakutakiwa kuwa angekuwa hajaliona mpaka leo, intelligent as he is!

================================

Dar es Salaam. Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo nchini Tanzania, Zitto Kabwe amesema haoni kama Mwanasheria Mkuu wa Serikali atamkuta na kosa kutokana na kuiandikia barua Benki ya Dunia (WB) akitaka isiidhinishe mkopo wa Sh1.2 trilioni kwa Tanzania kwa ajili ya sekta ya elimu.

Zitto ameeleza hayo leo Jumanne Februari 18, 2020 katika mkutano wake na waandishi wa habari baada ya kuchukua fomu ya kutetea nafasi yake katika uchaguzi wa chama hicho.

Katika mkutano wa 18 wa Bunge uliomalizika hivi karibuni mjini Dodoma, Zitto alishukiwa na wabunge kwa kitendo chake hicho huku Spika Job Ndugai akisema watamsubiri arejee nchini ili wamuulize sababu za kufanya hivyo, hapohapo akamtaka Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuangalia kama kuna uwezekano wa kuwemo jinai katika kitendo hicho.

Katika mkutano wake huo Zitto amesema, “sioni kosa lolote ambalo Mwanasheria Mkuu wa Serikali anaweza akalikuta kwamba nimelifanya kwa kuandika barua WB. Hizi ni siasa tu ambazo zilikuwa hazifanyiki huko nyuma, au watu walikuwa wanafanya kwa kificho sasa mimi nimezifanya kwa uwazi ndio tofauti tu hiyo, haina maana kuwa ni kitu kipya sana”

Amesema kila Mtanzania ana haki ya kuwasiliana na Benki ya Dunia iwapo Serikali yake kuna mambo imekosea katika maombi ya fedha katika benki hiyo.

Chanzo: Mwananchi
Kuna mbunge mmoja alitoa msaada kwa Lisu wakati aliposhambuliwa kwa risasi... MNAKUMBUKA BUNGE LILISEMA NINI JUU YA MSAADA ULE..??
 
Pohamba

JF-Expert Member
Jun 2, 2015
22,310
2,000
Bunge la Jamhuri yetu sio Photocopy ya Mabunge ya Mashoga

Zitto anastahili kufungiwa Bunge lijalo 2020~2025 kuonesha Msimamo thabiti dhidi ya Jaribio la Uhain

Kuzuia Fedha kusaidia Taifa lako ni Uhaini dhidi ya Taifa na Serikali

Viva JPM viva Baba lao, Aluta continua

Acha kudhalilisha Muhimili kwa kufananisha na Mabunge ya Kikamerun kameruni
Mara ngapi tunaona masenata au representative wa Marekani wanatumia headed letter za mabunge yao. Waache ushamba
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndebile

JF-Expert Member
Sep 14, 2011
4,949
2,000
Zitto kajikaanga mwemyewe is finished.Kajimaliza kisiasa,atafute kazi nyingine.
Mimi naipongeza serikali kwa kukaa kimya dhidi ya Zitto, huyu siyo wa kumjibu! Aina hii ya wanasiasa pumzi zao huwa ni fupi kumaliza hata mita 100 ya "mbio za kisiasa"
 
Makanyaga

JF-Expert Member
Sep 28, 2007
4,582
2,000
Swali je zitto ni mbunge au si mbunge? Kama ni mbunge kosa lipi kuandika barua kama mbunge?
Hivi wewe, kwa mfano tuseme ni VC wa IFM, halafu una cheo kingine huko nje, ni Mkurugenzi wa Kampuni yako tuseme iko Kawe. Tuseme pia Benki WM walikukopesha mkopo wanataka uji-commit kwa maandishi kuwa deni lako utamaliza lini kulilipa. Je, hawa Benki utawaandikia barua kwa kutumia headed paper ya IFM na kuisaini kama VC wa IFM au utawaandikia barua kwa headed paper ya Kampuni yako na kuisaini kama Mkurugenzi wa Kampuni hiyo?
 
Makanyaga

JF-Expert Member
Sep 28, 2007
4,582
2,000
Hakuna hoja ya kujadili kuhusu Zitto Kabwe kutumia nembo ya Bunge la JMT kwa kuwa naye ni Mbunge na kasaini kwa ofisi yake. Kumbukeni kila Halmashauri kuna Ofisi ya Mbunge na anagharamikiwa na Serikali.

Ingekuwa kosa kama Zitto Kabwe angetumia Letterhead ya Bunge la JMT halafu akasaini kwa anuani ya Ofisi ya Bunge Dodoma.
Issue iko kwenye idea aliyopeleka WB, ilikuwa ni ya kwake binafsi na si ya Bunge. Issue za namna hii huwa zina liabilities zake na credits pia, kwamba ukiandika kitu kikaja kuwa positive, unapewa credits bila kuulizwa maswali lakini kikiwa negative, lazima uulizwe maswali kwamba wewe nani alikuruhusu kuandika barua kwa kutumia letterhead yetu, waktai wazo lilikuwa ni la kwako binafsi?
 
Stuxnet

JF-Expert Member
Feb 12, 2011
3,207
2,000
Bunge la Jamhuri yetu sio Photocopy ya Mabunge ya Mashoga

Zitto anastahili kufungiwa Bunge lijalo 2020~2025 kuonesha Msimamo thabiti dhidi ya Jaribio la Uhain

Kuzuia Fedha kusaidia Taifa lako ni Uhaini dhidi ya Taifa na Serikali

Viva JPM viva Baba lao, Aluta continua

Acha kudhalilisha Muhimili kwa kufananisha na Mabunge ya Kikamerun kameruni

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama Zitto Kabwe ana uwezo wa kusimamisha masada usije wakati siyo Waziri wala Rais kwenye Srikali basi ana akılı kuliko Serikali.
 
Top Bottom