Zitto: Simjadili Dr. Tulia ni kibaraka, Mdee: Serikali ya Magufuli ni ya kisanii tu!

mpk

JF-Expert Member
Sep 26, 2012
3,115
3,863
Wakihojiwa na redio moja mkoani Kagera inakosemekana wataanzia ziara hivi karibuni Zitto amesema hawezi kumjadili naibu spika maana anajua anatumwa. "Huyu simjadili maana najua anatumwa na akiambiwa geuka anageuka, akiambiwa kimbia anakimbia". Alisema yeye anamwambia aliyemtuma apambane na ufisadi na si demokrasia kwani dunia nzima waliogombana na demokrasia wameangukia pua. Amesisitiza ziara inayotarajia kuanza itawazindua watanzania

Mdee: Amesema kiini cha kuzuia matangazo ya moja kwa moja ni kutaka kuwaaminisha kwamba serikali hii ni tukufu kumbe ya kisanii tu. Amewataka watanzania wajitokeze kwa maelfu kwenye mikutano yao ili wadadavuliwe serikali ilivyo ya kidikiteta. "Ndani ya bunge tumeaacha wabunge makini wa kuweza kuibana serikali, nje tuko mashine za kutosha kuiamsha jamii ya watanzania".

Wote wamesema serikali ya Magufuli ina dalili zote za kidikteta na inaliteka bunge makusudi ili kunyamazisha wakosaoji maana huko ndiko Magufuli anaweza kuanikwa. Wamesema madikteta wote hupenda kusifiwa na kuimbiwa nyimbo za kuabudiwa. Walisema
 
Hata mimi nimeanza kushituka, mzee wa majipu anapambana na demokrasia badala ya kupambana na ufisadi, kama Serikali yake inapenda ukweli na uwazi kwa nini anazuia bunge live
 
Kuna haja ya kutoa na elimu ya uraia kwa wanainchi wenzetu .Hii itawasaidia kujitambua na kujua nini yatupasa kukifanya ikija election nyingine. Tukizijua haki zetu kama raia tutawajibika kuweka madarakani viongozi bora na sio bora viongozi.
You can kill the revolutionaries but you can't kill the revolutions....Mola wabariki wapinzani waendelee kuwafungua macho raia.
 
Wakihojiwa na redio moja mkoani Kagera inakosemekana wataanzia ziara hivi karibuni Zitto amesema hawezi kumjadili naibu spika maana anajua anatumwa. "Huyu simjadili maana najua anatumwa na akiambiwa geuka anageuka, akiambiwa kimbia anakimbia". Alisema yeye anamwambia aliyemtuma apambane na ufisadi na si demokrasia kwani dunia nzima waliogombana na demokrasia wameangukia pua. Amesisitiza ziara inayotarajia kuanza itawazindua watanzania

Mdee: Amesema kiini cha kuzuia matangazo ya moja kwa moja ni kutaka kuwaaminisha kwamba serikali hii ni tukufu kumbe ya kisanii tu. Amewataka watanzania wajitokeze kwa maelfu kwenye mikutano yao ili wadadavuliwe serikali ilivyo ya kidikiteta. "Ndani ya bunge tumeaacha wabunge makini wa kuweza kuibana serikali, nje tuko mashine za kutosha kuiamsha jamii ya watanzania".

Wote wamesema serikali ya Magufuli ina dalili zote za kidikteta na inaliteka bunge makusudi ili kunyamazisha wakosaoji maana huko ndiko Magufuli anaweza kuanikwa. Wamesema madikteta wote hupenda kusifiwa na kuimbiwa nyimbo za kuabudiwa. Walisema
Mdee anasema bungeni wameacha wabunge makini ina maana hajui kuwa Dr Tulia akitoka nao wanatoka?
 
Zitto naye ziro tu siasa zake mpaka apewe maelekezo na waganga wa jadi ndiyo achukue maamuzi.

kwenye bunge la katiba kuna watu humu walikuwa wanasema eti ww ndye yule kiongoz flan wa dar!kunakaukwel!?hahahaaa.... kautani tu bana
 
Back
Top Bottom