Zitto, sikubaliani nawe kuhusu hela za fidia kutoka BAE | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zitto, sikubaliani nawe kuhusu hela za fidia kutoka BAE

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zak Malang, May 22, 2011.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  May 22, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  WanaJF;
  Hii ni sehemu ya stori kuu ya gazeti la T. Daima la leo. Kwa maoni yangu anayosema Zitto ni sahihi isipokuwa tu pale anaposema kuzipitisha hela kwenye mashirika hapana kwa vile nayo yamekumbwa na ufisadi. Jee, na serikali nayo si hivyo hivyo – imejaa ufisadi? Popote pale hela hizo hazitakuwa salama.

  Nashauri ni bora BAE ingeiomba serikali ya TZ orodha ya vitu ambavyo inataka kununua – yaani vitabu, madawati nk kwa ajili ya mashuile kama inavyodai na BAE watafute zabuni ya kuleta vitu hivyo ikishirikiana na Wizara yetu ya Elimu.

  Vivyo hivyo iwe kwa ujenzi wa nyumba za walimu etc.

  Wasiwasi wa wananchi wengi ni kwamba serikali ikizipata zile hela hazitazitumia kamwe kama inavyosema, zitafisidiwa au kulipia mambo mengine yasiyokuwa na maana kwa ajili ya ten percent kuingia mifukoni mwa wakubwa.

  __________

  CHADEMA yaikaanga serikali


  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimehitimisha ngwe nyingine ya maandamano ya amani kuishinikiza serikali iboreshe maisha ya wananchi, kikielekeza mashambulizi kwa viongozi na watendaji wa serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwamba wanasababisha vifo na maisha magumu kwa wananchi.

  Katika kusisitiza umuhimu wa serikali kuwajibika kwa wananchi na kutetea falsafa ya chama ya ”nguvu ya umma,” Katibu Mkuu, Dk. Willibrod Slaa, na Naibu wake, Zitto Kabwe, jana na juzi waliwasha moto katika maeneo tofauti nchini…………………………………

  …………………Wakati huo huo, Zitto aliunga mkono msimamo wa Tanzania wa kuitaka serikali ya Uingereza kurejesha fedha za rada serikalini moja kwa moja badala ya kuzipitishia kwenye mashirika yasiyo ya kiserikali.

  Alisema fedha hizo si msaada kwa Tanzania bali ni zake, hivyo hakuna sababu ya kuzipitisha kwenye mashirika hayo ambayo amesema nayo yamekumbwa na ufisadi.

  Chanzo: T. Daima Jumapili
   
 2. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #2
  May 22, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Kwanza iwapo kweli serikali ilikuwa inatambua matatizo makubwa katika sekta ya elimu, kwa nini isitumie zile hela il 40 kununua vitabu, madawati, kujenga nyumba za walimu etc badala yake ikaona ni vyema kununua rada chakavu? Yes -- tatizo ni 10 percent tu, na siyo kutoa elimu bora kwa wananchi wake.

  Shame upon you, Membe.
   
 3. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #3
  May 22, 2011
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Hoja hapa ni kwamba hela hizo serikali haina uchungu nazo.Serikali haina imani tena kutoka kwa wananchi.Hoja kwamba hizi si hela za msaada oh mara Heshima ya Taifa inashuka,ni kweli nakubaliana nazo.Lakini sisi ndiyo tuliojidhalilisha wenyewe zaidi.Tuweke vipaumbele,halafu hela hizo ziingie huko moja kwa moja.
   
 4. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #4
  May 22, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  I concur with u kafirimaji.
  These moron dont plan anything gud for this country.
   
 5. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #5
  May 22, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  These are matters of principle. It is not in order for Britain to channel these funds through NGOs. These are our tax payers funds and they ought to be channelled back to the source. I also agree with Zito's view on the dubious integrity of most NGOs. If the basis for the Britain's decision is the Government's credibility, Zito's views should make them think twice.
   
 6. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #6
  May 22, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,267
  Likes Received: 19,410
  Trophy Points: 280
  usimpinge Zitto, kwa sababu huna taarifa au hujui kitu gani kinandelea kwenye hayo mashirika,
  kiufupi ni kuwa waingereza wanatudharau kwa upumbavu wetu (wa viongozi wetu) kwani toka watupe uhuru tumerudi nyuma badala ya kwenda mbele,tumepiga hatua kwenye kuongeza population tu na wananchi wa mwanza kula vichwa vya samaki huku minofu ikienda nje ya nchi
   
 7. Japhari Shabani (RIP)

  Japhari Shabani (RIP) R I P

  #7
  May 22, 2011
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 721
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Hapa nakubalina na Zitto kwa sababu zifuatazo;Kwanza kuzipitisha pesa hizo kupitia mkondo usio,nikukubaliana na serikali ya kifisadi hapa ni lazima kuibana serikali iliyosababisha ufisadi huo na waliohusika wachukuliwe hatua za kisheri, sheria ichukue mkondo wake.

  Kwani tukiendelea na tabia ya kukwepa mikondo halali ya utekeleza wa majukumu mbalimbali tunaenda kubaya. Daktari anapokea rushwa au hospitali hazifanyi kazi ipasavyo twende kwa Babu Loliondo au hospitali binafsi.

  Kiongozi anakula rushwa au mzembe shughuli za kiongozi huyo ziamishiwe kwa kiongozi mwingine au kuundwe tume kumchunguza. Huku ni kukwepa ufumbuzi wa tatizo lenyewe.

  Kuhamisha shughuli au kazi za taasisi au kiongozi fulani na kuiacha taasisi husika bila kuchukua hatua ni uzembe zaidi. Hapa kwa upande mwingine kauli au pingamizi la serikali kuhusu hatua lingeandamana na maelezo ya hatua gani za kisheria zilizochukuliwa kwa wahusika.

  Vinginevyo ni kichekesho.
   
 8. A

  Anyambilile Member

  #8
  May 22, 2011
  Joined: Jan 18, 2011
  Messages: 28
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni jambo la kuchekesha na kufarahisha hivi waliofanya kazi ya kwamba watanzania tumeibiwa si walikuwa ni waingerza na kama nakimbuka kuna waziri katika serikali ya uingereza alijiuzuru sababu ya hizi pesa tulizoibiwa akiwa anatutetea sisi watz, leo serikali yetu inakuwa na kimbelembele kuwa hiyo pesa warudishiwe wao hii inakaaje sipati picha serikali kupitia takukuru walisha sema hakuna rushwa MAAANA HATUKUIBIWA
  mimi kwa mawazo yangu nadhani serikali ya uingereza iangalie ni namna gani hizo pesa zinaweza kurudi na kuwafaidisha watz. na wale wote walio husika ktika jambo hili wachukuliwe hatua za kisheria NA SERIKALI YETU MAANA HIYO NDIYO AIBU KUBWA KWETU HATUNA WAZALENDO
  NA HAPO GAMBA LITAKUWA LIMEVULIWA.
   
 9. lifeofmshaba

  lifeofmshaba JF-Expert Member

  #9
  May 22, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 868
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  hizo kanuni unazosema zingetumika toka mwanzo leo hii tungekuwa tunajadili huu uhuni wa viongozi wetu?
  wakati wa unununi hakuna aibu tumeshitukiwa na sasa tunapewa change tunaona ni aibu bora zirudi serikalini
  kama ni hivyo serikali ya uingereza itoe pima joto moja tu kwa serikali yetu, ya kwamba ichukuwe hatua kwamba kwa waliohusika harafu wanapewa hiyo pesa!!!!!
  mimi nana amini wakiambi hivyo watakimbia na kusahau hiyo pesa,
  kila siku mimi najiuliza kama ni aibu kwa taifa hiyo pesa ilifikaje huko
  aliyekuwa waziri wa wizara uhusika kafanywa nini?
  Zitto atapa tunu na heshima kama atakwenda bungeni kushinika waliotuingiza katika ili wawajibishwe kwa ujumla wao na serikali ya ccm kuwaomba msamaha wananchi kwa kudhalilisha nchi
   
 10. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #10
  May 22, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Tutake tusitake serikali ya Tanzania haina uhalali wowote na fedha hiyo.Kwani; "in life you dont get what you deserve but what you bargain for," na serikali ilipata kile ilicho "bargain for." Baya zaidi mpaka sasa inaonekana kuridhika na ilichopata, vinginevyo wale walioiingiza kwenye mkenge wangelikwisha chukuliwa hatua. Hivyo sioni ni wapi serikali imepata jeuri ya kutangaza ya kuwa fedha hizo ni zake.
   
 11. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #11
  May 22, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,912
  Likes Received: 213
  Trophy Points: 160
  Serikali ya Tanzania ni kama Mwanamke anayependa kujijali peke yake wala hafikirii kuhusu watoto wake, kila anapoachiwa na mumewe pesa za matumizi anaishia nazo saluni kutengeneza nywele, kucha n.k. Sasa pale mumewe anapomwambia kuwa atakuwa anaacha pesa za matumizi kwa Msichana wa kazi ili watoto wapate kula basi anakasirika kuwa mumewe anamkosea Heshima, na vitisho vya kumfukuza msichana wa kazi juu. Bila kuzingatia kuwa yeye mwenyewe ndiyo chanzo cha mtafaruku wote huo..
   
 12. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #12
  May 22, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Ukweli ni kwamba kwa Tanzania ya sasa hata hizo hela ziende wapi zitaliwa tuu! Hakuna accountability yoyote iwe serikalini au mashirika ya umma. Kwa hiyo mimi naona bora hata hizo hela tusingelipwa kama hizo hela zitaenda kwenye mifuko ya wajanja wale wale waliotuingiza kwenye mtego huo wa rada.

  Hili dili zima la BAE inajulikana wazi lilikua lakifisadi likishirikisha pia viongozi wa serikali. Leo hii serikali hiyo hiyo ndiyo ilipwe fidia? Kwa lipi haswa? Kwa uzembe wao wenyewe?

  Ila mimi kunakitu najiuliza na nashangaa kwa nini Watz hatuhoji hili. Dili la BAE lilikua kati ya kampuni ya kigeni na serikali ya Tanzania. Kutokana na katiba yetu wizara ya mambo ya nje ni lazima kwa wakati mmoja au mwingine ilihusika hata kama mtazamaji tu wakati wa dili hili. Waziri wa mambo ya nje wakati huo ni Mh. raisi wetu. Je mheshimiwa JK alikuwa na maoni gani kuhusu hili dili wakati lina tendeka? Hapa simhukumu raisi ila ningependa tu kujua alihusikaje tujue kama reaction ya serikali yake ni justified au la.
   
 13. babu M

  babu M JF-Expert Member

  #13
  May 22, 2011
  Joined: Mar 4, 2010
  Messages: 3,992
  Likes Received: 990
  Trophy Points: 280
  Na tunaendelea kujidhalilisha.Nguvu ya kudai pesa tunayo lakini nguvu ya kuwapeleka mahakamani walio tufikisha hapo hatuna.
   
 14. Nyangomboli

  Nyangomboli JF-Expert Member

  #14
  May 22, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 2,307
  Likes Received: 649
  Trophy Points: 280
  But guys, let us be honest and we better think deeply on this matter. To me, if the uk people would just keep quiet or not raise this issue then no one would have known anything about this scandal.

  And i am sure that we did not assist them fully during the investigation of this issue. If so, do you think we have the right to raise our voices or demand them to give us this money while we still keeping them mafisadi free and no single action is taken against them, au ndiyo deal kuona?

  To me, that is msaada if they decide to give the money to the government na tusiwapangie. Kama tumeridhika kama hela zile ni zetu na zinatokana na fraud ambayo baadhi ya wahusika wake ni viongozi wetu na wengine ama wapo madarakani ama wamestaafu then tuwachukulie hatua za kisheria na ikiwezekana wafungwe chapchap kwa kuwa ushahidi kumbe upo.

  Ila kama hatuwezi chukua hatua kwa wahusika kama waingereza walivyofanya then hatuna haki ya kuwapangia wazilete vipi.

  Huu ugoli kipa ni wa aina yake, wenzetu wamefanya maamuzi magumu sana nayafananisha na mzazi mwenye mtoto then mtoto aibe hela lundo alete home kwa kushiriana na mtoto wa ile family iloibiwa kisha mzazi akamate mwanaeapeleke mahakamani.

  Mzazi yule aloibiwa mwanae amkalie kimya na akae kwa raha mstarehe. Yule mwingine ahangaike na kesi dhidi ya mtoto wake na ikiisha na mwanae kuhukumiwa yule mzazi wa mwizi akadai na kuweka masharti bila aibu.

  Duh! Hiyo iko sawa jamani?
   
 15. Sophist

  Sophist JF-Expert Member

  #15
  May 22, 2011
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 3,081
  Likes Received: 1,728
  Trophy Points: 280
  Ndugu Zitto na wenzako,
  Tatizo lenu na watanzania wengine ni tabia ya kuacha masuala ya msingi, na badala yake kuanza kujadili pesa, na kwa bahati mbaya, mnaishia hapo.

  Niwakumbushe tena maneno ya busara ya Nyerere, "pesa siyo msingi wa maendeleao". Mnafahamu kuwa Tanzania ilikopa pesa hiyo ya kununulia rada kutoka benki ya Barclays; mkopo wa kibiashara wenye riba kubwa. Hii ilikuwa baada ya Benki ya Dunia kukataa kutoa mkopo kwa serikali ya Tanzania kwa madai kuwa hakukuwa na economic efficiency justification kununua rada kwa kiasi hicho, na ya aina hiyo.

  Binafsi nadhani mjadala wa sasa ungekuwa kufahamu iwapo serikali ya Tanzania imekwishalipa deni la mkopo husika kwa benki ya Barclays au la. Kama deni hilo pamoja na riba vimekamilishwa, au iwapo deni hilo bado lipo tungetaka kufahamu ni kiasi gani. Kama bado benki ya Barclays inaidai Tanzania, basi suluhisho la namna ya kutumia marejesho ya 'prey' lingekuwa kulipa deni husika, siyo mapendekezo ya miradi ya akina Abunuasi ya kupanga bajeti za miradi kwa kuzingatia pesa inayoonekana kuwa ipo mahali.

  Miradi na mipango ya maendeleo sharti itokane na fikra, vichwani siyo midomoni; kwamba zimeletwa shilingi au dola kiasi gani, hivyo tuzitumieje. Huu ni ufinyu kifikra na ndio kikwazo chetu kikuu cha maendeleao. Matatizo ya madaftari, vitabu, madawati, nyumba za walimu, na kadhalika hayawezi kutatuliwa kwa kiasi chochote cha pesa au kununua vifaa kadha wa kadha, bali fikra sahihi za namna ya kuondokana na madhira hayo! Tunahitaji kufikiri juu ya (siyo kununua) namna yakuondokana na matatizo yanayoikabilii nchi yetu.

  Jambo la pili ni kwamba tunapashwa kufahamu kuwa pesa wanazorudisha na ndugu zetu wa BAe ni tambiko (ritual), siyo malipo wala fidia. Wao wanataka 'kutambikia' ikiwa ni makakti wa 'kujiosha' na 'uchafu' wa rushwa ulioghubika kampuni hiyo. Hapa ndipo wakosa busara wa serikali yetu wanapoleta kichefuchefu. Wanataka serikali ikabidhiwe tambiko, wale. Kwa kawaida, hasa sisi tuliozaliwa na kukulia vijijini, kunajua kuwa tambiko hutupwa baharini, ziwani, porini, vichakanai au msituni. Ikiwa mtu amebahatika kupita lilikowekwa tambiko akiwa wa kwanza, na kuona tambiko hilo (nyama, chakula, nguo, fedha, kuku, simbi, pombe au kitu chochote chenye thamani kijamii), basi angeweza kuchukua kiasi chochote anachohitaji/taka. Tambiko haliombwi! Huu ni unyan'gau!

  Kwan nini alipo ya BAe ni tambiko: BAe haidaiwi na serikali ya Tanzania hivyo haina cha kulipa au kuirudishia. Pesa inayorudishwa ndiyo wataalamu wa manunuzi wa serikali ya Tanzania wamekuwawakisema kuwa ni malipo halali ambayo serikali kwa kufuata utaratibu wote wa kisheria (sheria ya manunuzi wa wakati huo) ililipa kampuni ya BAe. Baada ya kupokea malipo hayo na kukata halali yake kwa kuzingatia bei ya rada husika, BAe ilitenga kiasi cha asilimia 45 ambacho kiliongezwa makusudi na maofisa wa Mkapa (naye akiwemo) kwa ajili ya kujilipa (kuiba/kuibia umma wa Tanzania) na kuwarudishia maofisa hao wa serikali ya Mkapa. Wakala wao Vithlani Sailesh na mwenzake (mmiliki wa Shivacom) walipokea kiasi hicho na kisha kuja kugawa kwa kuwasambazia wote; Dr. Idrisa, Mkapa, Balali, Chenge na wenzao. Baada ya habari hizi kufumuka wahusika wote wakaonekana mbele ya macho ya umma kuwa wananuka rushwa na ufisadi. Kampuni ya BAe ikaunganishwa na uchafu huu. Na sasa BAe inataka kutoa tambiko kujisafisha dhidi ya uchafu huu.

  Ni bahati mbaya sana Serikali na akina Zitto wanaomba na hata kulazimisha kwa hoja za kutaka tambiko (uchafu) litolewe mikononi mwao badala ya kutupwa kichakani. Kwamba BAe inapeleka pesa za tambiko kwenye NGOs, maana yake ni kuwa inapeleka tambiko vichakani.

  Binafsi, nadhani NGO inayoheshimika (yenye integrity) inatakataa kupokea pesa hiyo, hasa ingetangazwa hadharani, sembuse serikali kuomba ipewe mikononi! Waache BAe walete NGO yao (kichaka chao), wakamilishe kazi ya kujisafisa/tambiko. Watoe tambiko kichakani.

  BAe imewathamini na kuwaheshimu Watanzania kwa kuamua kuanzisha NGO/kichaka wapitishe tambiko lao. Ila serikali na akina Zitto, wanataka kujidhalilisha wao wenyewe na Watanzania kwa ujumla, kwa kutaka kupewa uchafu (tambiko) mikononi mwao.
   
 16. Nyangomboli

  Nyangomboli JF-Expert Member

  #16
  May 22, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 2,307
  Likes Received: 649
  Trophy Points: 280
  Tz ma shalobalo wa nguvu. wanasubiri wakamatiwe. "kamata mwiz man.
   
 17. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #17
  May 22, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  membe anaingiaje hapa? yaelekea hujui ukiandikacho. we mdada ongelea mramba, mkapa na chenge. usimhukumu mtu ambaye hahusiki. hawa ndo walionunua hiyo rada na 10% unayoongelea inawahusu hao.
   
 18. G

  GJ Mwanakatwe JF-Expert Member

  #18
  May 22, 2011
  Joined: Mar 26, 2011
  Messages: 241
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mwenye fedha ndiye anayepanga matumizi ya fedha zake . Zile fedha ni mali ya serikali ya Tanzania, hivyo hakuna mtu, nchi, kampuni, shirika au taasisi yoyote itakayoipangia serikali yetu jinsi ya kutumia fedha zake. Kwa maana hiyo BAE System hawana haki yoyote ya kisheria kuipangia Serikali ya Tanzania jinsi ya kutumia fedha zetu, waikabidhi serikali yetu fedha zake, kama serikali yetu ikizifanyia ufisadi fedha hizo hayo hayaihusu BAE System, fedha sio zao. Kama wanataka watoe fedha zao kwa Serikali ya Tanzania ndiyo sasa waipangie serikali jinsi ya kuzitumia fedha hizo, sio kwa hizi fedha ambazo ni mali ya Serikali ya Tanzania. Kwanza BAE System wao ni akina nani mpaka waipangie serikali yetu jinsi ya kutumia fedha zake? isitoshe wao ni wasafi kiasi gani mpaka wainyoshee kidole serikali yetu? hizo fedha zetu zilifikaje kwenye mikono yao kama sio wizi na rushwa uliofanywa na BAE dhidi ya serikali ya Tanzania? Watz, tusiwe wepesi wa kuishambulia serikali kwa kila kitu hata ambacho imefanya vyema, hapa waziri Membe kafanya sawa kabisa na anastahili kupongezwa kwa hili, kwa nini tudharirishwe na kupuuzwa na kampuni hii? zile fedha ni zetu, na zirudishwe serikalini kama zilivyo. Suala kwamba kwanini serikali haijawachukulia hatua za kisheria wale watz waliohusika na mchezo huu mchafu, hilo tunaweza kulijadili na kuishutumu serikali, lakini la fedha hapana, serikali ipo sahihi, zile ni fedha zake na inapaswa kukabidhiwa moja kwa moja sio kupitia kwa kijitaasisi chochote.
   
Loading...