Zitto: Sijahongwa, ni siasa za urais na hasira za posho!

Status
Not open for further replies.
Mwananchi na Zitto ni sawa na Gobal publishers na Wema/Diamond. Bila habari zao kuandikwa, mauzo yanakuwa madogo
 
Ni vipi asimame kumtetea Mhando na uozo wote huo? mbona anataka kutuharibia chama huyu mwenzetu,ndugu yetu?zito ur my brother lakini kwa hili hapana kaka acha uchunguzi ufanyike ili kama huhusiki bunge likusafishe.
 
SMH!! Hivi vyote ni visasi tu,we unafikiri oparesheni uwajibikaji ilifurahiwa na wote..Zitto can be many thing but "kuhongwa" this is totally ridiculous!!

Eyes on hands off..hiki ndicho Zitto anacho kipigania lakini itajafahamika tu!!Af mi nashangaa sana kwanini Zitto akisema ana uwezo wa kuwa rais watu wanachachawa...ye ka mtanzania mwingine yeyote ana haki hiyo!!

outrageous kind of thinking...think outside the box
 
Kiongozi wangu,jembe langu Zitto zubery kabwe nani kakuambia hawa wanaosemwa ni wewe?maana watu walishinikiza majina yatajwe lakin hayakutajwa,
je ndo kutimiza falsafa ya kurusha jiwe jizza!
 

"Hakuna hata mbunge mmoja aliyesimama kusema nani amehongwa nini....

"Kwangu mimi naona hizi ni siasa za urais na hasira za posho. Wenye kutaka urais wa vyama vyote na wapambe wao, wameungana kunichafulia heshima yangu. Wabunge wenye njaa ya posho, wameungana kunikomoa. Ukweli una tabia ya kutopenda kupuuzwa. Mwalimu Nyerere (Julius) alisema katika andiko lake la 'Tujisahihishe'."
.

Kwenye red: Naona kama kuna kujichanganya.

Hata hivyo binafsi siamini kama hizi tuhuma zina uhusiano wowote na mbio za urais wala posho. Nakataa kabisa hayo madai. Zitto wa 2007 ni tofauti sana na Zitto wa 2012. Kadri umaarufu wake wa siasa ulivyokuwa unaongezeka ndivyo hivyo hivyo wajanja walikuwa wanatumia mbinu kuwa karibu naye. Ama kwa kutojua au kwa kujiamini ni mjanja kwenye mahesabu ya siasa, Zitto anajikuta anakuwa karibu na makundi yenye kuzua maswali mengi. Amekuwa very devisive figure na kila anapokanyaga anaacha mtafaruku.

Na kwa sababu amekuwa na siasa za kimwenyewe-mwenyewe, sasa hivi anajikuta hana msingi imara wa kusimamia. Ukitizama comments nyingi hapa JF, anaongelewa yeye kama yeye bila kuhusishwa na chama. Kwangu mimi mtaji wake wa kisiasa (political capital) umelika sana. Sijui kama anaweza kukopa mahali. Na hapo tukumbuke pia madhara ya ule mpango wake wa kukusanya sign 70. Unaweza ukawa another problem. He totally humiliated PM.
 
Watanzani tusiwe wajinga wa kupelekwa kama kuku,wenzetu kipindi chadema inaanza tulikuwa tumekalia ccm tu,kaskazini wakaamua kujiunga na chadema cc bado na ccm,automatically ni lazima chama kionekane sana kule,mfano kanda ya ziwa b4 2010 hakukuwa hata na mbunge wa chadema mlitegemea nn?sasa moto umewaka kaskazini na sie kanda ya ziwa joto limetupata na sie tumeamua kuuwasha wanapita kuongea,haya ni mabadiliko kwa upuuzi uliofanywa na ccm watanzania hatudanganyiki tena.
 
Ucjal mH Zito kaza buti endelea kusema ukweli hawa vijana wanaoshambulia humu mtandaoni wanatumika kisiasa ili kukukatisha tamaa wanatumwa na wale wasiopenda mafanikio yako ndani ya chadema,Posho at work!
 
Hii habari ni kipande tu....

Wenya akili walisema hivi...

Mbunge Silinde
Naye Katibu wa Wabunge wa Chadema, David Silinde alisema: "Kwa kuwa tumesikia, kama kambi tutafanya uchunguzi juu ya tuhuma hizo. Tutakaa kikao cha kuamua nini cha kufanya. Pia tutatoa tamko juu ya mwenendo mzima wa hizi tuhuma na Bunge kwa ujumla."

 
Mdogo wangu acha waseme kumbuka matajiri zako ni cc tuliokutuma huko na watanzania wanaona na kuckia kaza buti
 
Ktika hali isiyokuwa ya kawaida wachaga waliop chadema wameungana na wabunge wapenda posho wa ccm ili kumuadabisha Mh zuberi zitto, yote hayao yametokana na mambo makuu mawili
1.Zitto kukataa posho na kuendelea kutozichukua mpka leo, wahafdhina ndani ya chadema wameona wanaaibika hasa baada ya mbungewa iramba mwigulu kuwachana ukweli, kma hiyo hitoshi wabunge wengi wa chadema ambao ni wa kaskazini waliingia kwenye chama na lengo lake likiwa ni kupata pesa , walitumia mbinu nyingi sana kumharibia zitto reputation yake ndani ya jamii na nje ya siasa ili aonekane yeye amehongwa au alikuwa na ubia na mhando wa tanesco
2.Kitendo cha zitto kutangaza kugombea urais 2015 kiliwastua sana wachaga kiasi cha kutengengeneza mkakati wa kummaliza kwenye medani za siasa kwa kushirikiana na ccm, ikumbukwe kwenye maswala ya ukabila wachaga huweka nje itikadi zao, na hiyo kazi alipewa selasin amabaye uhusiano wake na wachaga wenzio haupo na alizungumza vitu vingi sana
Kama CHADEMA wataendelea na huu ujinga 2015 chma hakifiki na hata kikifika ccm wameshajuwa mahali pa kuwamamlizia ni juu ya urais na posho pekee yake
Mnyika amabye yeye daiama ni mnafiki huwa anazungumzia hilo chini ya meza na maelezo yake niliyoyapata kwa njia ya kiintelejensia nitayaweka very soon baada ya secretary wangu kumalaiza kuyatype
Kafulila alisema CHADEMA ni ya wachaga na wewe ukijifanya ni yako wako tayari kukuharibia kwa gharama yoyote ile

Mkuu, umekuwa na haraka sana ya kupost utumbo huu, mpaka maneno mengine yameshindwa kueleweka.
Wabunge wengi waliochangia hotuba ya wizara ya Nishati na Madini hawakutaja majina ya waliopokea rushwa, jina la Mhe. zito limekujaje hapa?

Kuhusu uchagga kama ambavyo umetaka kutuaminisha kutokana na maelezo yako, ni mchagga yupi kati ya waliopo CDM ametangaza kugombea URAIS?
Umezungumzia intelijensia yako!!!???, kama na wewe unayo ya kwako basi nchi ya TZ imekwisha, maana kama na utumbo huu usio mpangilio umeutoa huko basi hapo kazi ipo.

Naomba nikupe ushauri wa bure, kama uko karibu sana na Mhe. Zitto, mwambie asiwe na papara katika kujibu kwa majibu rahisi yanayomvunjia hadhi hot issues kama hizi. Anaposema eti wamesema vile kwa sababu ya hasira za posho na urais wa 2015, havilingani kabisa na hadhi yake.
Ni majibu au hoja nyepesi mno kumlinganisha na hadhi aliyopata kuwa nayo hapo awali.
Amelewa umaarufu kiasi cha kufikiri kwamba watu wazima hawawezi kuhoji matamshi yake?
 
Zito zuberi kabwe,kaka hebu nyamaza unaposema ni maadui wa ndani na nje kwani walikutuma hao maadui umtetee mhando kwa aliyofanya?ulienda ulikuwa unategemea nn?kama ulijua basi una maslahi ndani yake na kama hukujua basi kamati ya maadili itasema,suala la urais una haki ya kufanya vile kama chama kitakupitisha lakini kwa sasa hilo la urais c ajenda ya chama tupo na operation za kuimarisha chama kwa sasa.
 
Kati ya wanasiasa ninao waamini kwa kujenga hoja wewe ni miongo mwao lakini kulingana na habari naanza kupata mashaka makubwa. Ulichotakiwa kufanya ni kuwaonesha watanzania wapi kanuni zilikosewa unlike kanuni ambazo Muhongo alizielezea bungeni kusupport maamuzi ya kuipa tenda kampuni ya PUMA.
Lakini kitendo chako chako cha kusema watu wanakukosoa kwa sababu ya posho na mbio za urais nadhani hazistahali kutoka kwa mwanasiasa wa carible yako.
Give logic answers to strong questions,remember your reputation you built in a hard way is at stake here.
 
Kwenye red: Naona kama kuna kujichanganya.

Hata hivyo binafsi siamini kama hizi tuhuma zina uhusiano wowote na mbio za urais wala posho. Nakataa kabisa hayo madai. Zitto wa 2007 ni tofauti sana na Zitto wa 2012. Kadri umaarufu wake wa siasa ulivyokuwa unaongezeka ndivyo hivyo hivyo wajanja walikuwa wanatumia mbinu kuwa karibu naye. Ama kwa kutojua au kwa kujiamini ni mjanja kwenye mahesabu ya siasa, Zitto anajikuta anakuwa karibu na makundi yenye kuzua maswali mengi. Amekuwa very devisive figure na kila anapokanyaga anaacha mtafaruku.

Na kwa sababu amekuwa na siasa za kimwenyewe-mwenyewe, sasa hivi anajikuta hana msingi imara wa kusimamia. Ukitizama comments nyingi hapa JF, anaongelewa yeye kama yeye bila kuhusishwa na chama. Kwangu mimi mtaji wake wa kisiasa (political capital) umelika sana. Sijui kama anaweza kukopa mahali. Na hapo tukumbuke pia madhara ya ule mpango wake wa kukusanya sign 70. Unaweza ukawa another problem. He totally humiliated PM.

Ningekua mshauri wake ningemshauri asijigeuze yatima wa kisiasa,kwamba anaelea juu juu bila msingi imara. Bado ni mdogo,afanye kazi ya kukijenga chama na taifa lake,urais utakuja tu kama imepangwa!
 
Zitto, Zittooo! Hakika malengo yako hayaji fanikiwa hata siku moja! Mosi huendani na mapigo na midundo ya mziki unaopigwa, wenzako wana hili wewe unatangaza hili. Mbili wewe ni mnafiki sana, na mtu usiye na utaratibu, katika kundi la watu, wenye nia na malengo mamoja hujiwekea utaratibu wa kuufuata unapokuwa na nia ya kufanya jambo fulani kwa niaba au kwa kutegemea kuungwa na wenzako. Utakurupukaje katikati ya maombolezo ya msiba na kutangaza kuwa nina nia ya kugombea URAIS? Wafiwa watakuelewaje na huku nawe msiba unakuhusu?? Umesoma lakini hujaelimika wewe. Utapotea kwenye siasa kama hubadili tabia. Gharaghabaho.
 
No, no, no! Zitto DON'T think of becoming president of this country it is too early for you to hope for that, better think on solving problems of your people in your constituency.
 
eti wabunge wenye njaa ya posho

anazidi kuongeza maadui.....
Nilichogundua huyu bwana anaropoka tu bila kujua madhara ya maneno yanayotoka kwenye kinywa chake.
Kitendo cha kusema wabunge wenye njaa ya posho ina maana kawadharau na kuwatukana wabunge wote wa tanzania. kwa sababu ni yeye tu amabye hachukui posho.
Huyu ndio anasema anataka kuwa rais wa tanzania. labda rais wa kigoma nitamuelewa
 
Nilichogundua huyu bwana anaropoka tu bila kujua madhara ya maneno yanayotoka kwenye kinywa chake.
Kitendo cha kusema wabunge wenye njaa ya posho ina maana kawadharau na kuwatukana wabunge wote wa tanzania. kwa sababu ni yeye tu amabye hachukui posho.
Huyu ndio anasema anataka kuwa rais wa tanzania. labda rais wa kigoma nitamuelewa

halafu iliyovunjwa ni kamati ya nishati

ambayo wamo kina Mnyika na wengineo

lakini anae hangaika kujitetea ni yeye.....
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom