Zitto: Sheria ya utawala wa Bunge kifungu cha 19 imevunjwa na spika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zitto: Sheria ya utawala wa Bunge kifungu cha 19 imevunjwa na spika

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kibanga Ampiga Mkoloni, Dec 7, 2011.

 1. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #1
  Dec 7, 2011
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,565
  Likes Received: 1,653
  Trophy Points: 280
  Zitto anasema from facebook

  " Spika wa Bunge anajua kwamba posho zote hulipwa Baada ya Rais kuidhinisha. Posho anazotangaza hazijaidhinishwa kwani uthibitsho wa kuidhinisha ni Masharti Mapya ya Kazi kwa Wabunge ambayo hayajatolewa na Ofisi ya Rais. Hivyo kitendo cha kuanza kulipa posho mpya bila Masharti Mapya ya kazi za Wabunge ni kukiuka sheria ya utawala wa Bunge kifungu cha 19.

  Tume ya Bunge inapaswa kuwajibika kwa kutumia vibaya mamlaka yake, posho mpya zifutwe na zilizolipwa zirejeshwe mara moja kwani zimelipwa kinyume na sheria.

  Spika anapaswa kuheshimu sheria ambazo Bunge limepitisha na kwenda kinyume na sheria kwa makusudi ni kosa la kuvuliwa Uspika.

  Wabunge wasifanye mchezo na suala la posho. Wananchi wamekasirishwa sana na kwa kweli hatuwaelewi. Wakati Bunge la Tisa lilisifika kwa kupambana na ufisadi, Bunge la kumi litabatizwa Bunge la Posho. Ni lazima tukatae kuonekana tunajijali badala ya kujali wananchi.

  Namsihi Spika aachane kabisa na suala hili la posho. Tukazane kukuza uchumi wa nchi ili wananchi wapate ajira, kodi iwe nyingi na tuongeze mishahara kwa wafanyakazi wote. Hoja ya ugumu wa maisha ni kwa wananchi wote sio wabunge peke yao.

  Jambo la kuzingatia kwa sasa ni kwamba, iwapo posho hizi zitalipwa kwa wabunge, nini kitazuia posho Kama hizo kulipwa kwa wabunge wa Bunge Maalumu la katiba? Huo mzigo serikali itaubeba namna gani na Hali hii ya uchumi?

  Wabunge tujielekeze katika kukuza uchumi, kuongeza uzalishaji viwandani, mashambani na kwenye shughuli nyingine za huduma za kiuchumi. Tuachane na fikra za posho
  ."
   
 2. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #2
  Dec 7, 2011
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  ndio maana tunasema kuwa hawa wote wako kwenye list ya kuondolewa madarakani. Cdm tumewapa jukumu hili
   
 3. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #3
  Dec 7, 2011
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Bibi Kiroboto hamna kitu mle, mtu anajenga hoja eti vyumba vimepanda hadi 100,000.00 kwa hiyo wabunge waongezewe posho, swali la kujiuliza hivi ni lazima wabunge walale vyumba vya 100,000.00?
  Ni kama mtu umefiwa halafu mtu anakuletea uchuru tena, wananchi hali mbaya halafu watu wanaleta matani bungeni!!!
   
 4. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #4
  Dec 7, 2011
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Sehemu niliyobold siyo CDM bali wananchi, CDM ni kuonyesha njia na sisi kufanya maamuzi bila unafiki!!!!!
   
 5. Chatumkali

  Chatumkali JF-Expert Member

  #5
  Dec 7, 2011
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,045
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Zitto aongeze haya mapambano dhidi ya huu wizi.Watanzania tuko nyuma yake na kwa umoja wetu tutashinda tu!
   
 6. All TRUTH

  All TRUTH JF-Expert Member

  #6
  Dec 7, 2011
  Joined: Nov 20, 2011
  Messages: 3,276
  Likes Received: 984
  Trophy Points: 280
  Tatizo speed ya CDM ndo inawachanganya. Wacha wawape crd CDM
   
 7. M

  Middle JF-Expert Member

  #7
  Dec 7, 2011
  Joined: Feb 7, 2007
  Messages: 243
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  mdogo wangu Zitto,uyo spika wako kawekwa na mafisadi,hatufai,kwa kweli watatujua 2015 ikifika
   
 8. Mbugi

  Mbugi JF-Expert Member

  #8
  Dec 7, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,488
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 160
  kwa kweli kama haya ndiyo maisha bora kwa mtanzania tumekwisha, nilidhani hayo yanawezekana tu kwa kutumia raslimali vizuri, ktk maana kumlipa mtu kwa kazi aliyofanya na si posho za kukaa ambazo kimsingi zinapelekea hata kushuka kwa thamani ya fedha yetu, hoja ya eti wabunge wanapata mshahara mdogo wanajilinganisha na nani? ktk nchi hii? na mabaya zaidi posho hizo hazitozwi kodi yoyote, na zaidi ya yote wanalipwa perdiem shs 80,000, fedha ya mafuta 50,000, inayofanya jumla ya shs 330,000 kwa siku kiasi ambacho ni zaidi ya mara mbili ya mshahara wa kima cha chini, na ni sawa kabisa na mshahara wa mtu mwenye degrii moja.

  Sina hakika kama CHAMA CCM Kinayabariki haya, sina hakika kama Anna Makinga anamaanisha kile alichosema kama si kutwambia wameamua kuua chama chao kwa maana wanajua wamekwisha zeeka na hawataki sisi kuirithi hiyo CCM, maana akufukuzae hakuambii toka utaona vitendo vyake tu. HOJA YA "Dodoma maisha yako juu", kwa kuwa ni mji wa wanavyuo wengi, mbona wanafunzi walipoleta hoja ya kuongezewa kiwango cha mkopo hamkuwasikiliza tena ni mkopo wanalipa, je Dodoma hiyo hiyo kuna wananchi ktk maana ya watumishi na consideration hiyo haipo wananchi wawaelewe vipi ccm na serikali yake? labda wabunge na huyo main speaker wenu mniambie "Nchi hii huliwa na wenye meno (watunga na wapitisha miswada) na hujengwa na wasio na meno".


  Tafadhali Rais wetu hili si swala la mchezo kiasi cha kusema ulione ni dogo kama kweli hiyo bill ipo kwako kwa ajili ya endorsement/assent ili iwe sheria na wao wameamua kulipana p/se usiisaini. Tumeona vituko vingi sana vinavyoendelea lakini hii ni zaidi, hawa watu wa mepeana fedha za majimbo lakini majimbo hayana yanachopata zaidi tu ya kujenga vitambi vyao, serikali imetoa mikopo ya pembejeo yote wao ndiyo wameweza kuchukua fedha hizo, mikopo ya JK NAYO UKIENDA KWA UNDANI WAMEFAIDI WAO, WABUNGEEEEE kuweni na jicho la unyenyekevu kwa hawa watenda zambi wenu walioamua kwa kutoa mishipa yao na kwenda kupiga hizo kura wakiamini manakwenda kusimamia maslahi yao kumbe hakuna kitu.

  Nimekuwa nikijiuliza sana kama mwana CCM wa kawaida sana nguvu hii ya umma cdm inatokana na nini? sasa napata jibu kuwa wenye (waasisi wa ccm) wameamua kuigawana kwa hofu ya kutaka kila mtu afe na chake, maana ukienda kwenye miradi ya chama huku kwa akina mzee Mkama nako mambo ni hovyo kabisa miradi iliyopo na mapato yanayopatikana ni tofauti kabisa, mgawanyo hata wa hicho kidogo ndo kwanza haufiki chini (kwa wanachama wenyewe) ukiona wakishirikishwa siku hiyo kuna uchaguzi, ama mwenyekiti wa chama anapita hapo, watawaaandikiwa mabolozi wapeleke wanachama uwanja wa ndege na nk, UTEUZI WENYEWE NDANI YA CHAMA UMEGEUKA DILI / WA RUSHWA NA UJANJA WA MTU KUJIPENDEKEZA KWA WAKUBWA WA CHAMA, HAKUNA CHA SIFA ILIYOWEKWA KAMA KIGEZO halafu tunazungumzia karne ya technolojia na KUDAI tunafanya MORDENISATION YA CHAMA CHETU. leo hii hatuogopi tunajisifu kabisa eti chakula cha msaada kilitusaidia kupata kura igunga, na bado kwa miaka yetu ya kushika dola tunazungumzia swala la tumethubutu (to dare) lini tuanataka kuwambia watu tutafanya.

  wabunge ninyi kweli ni watetezi wetu sisi kama wanyonge au ???? ubunge ni diri kwa sasa? tutaonana 2015 kwa heri
   
 9. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #9
  Dec 7, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Nimechoka sana
  ramsa zimezidi!
   
 10. nice 2

  nice 2 JF-Expert Member

  #10
  Dec 7, 2011
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 746
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kwa bahati mbaya sana mama huyu ana mgongano wa kimaslahi kwenye maswala ya fedha. Alipokuwa anatetea ishu ya posho hakuwa hata anakumbuka kama kuna sheria ya namna hiyo. Pia viongozi wetu wamezoea kwamba hata wakikosea hawachukuliwi hatua yoyote! Lakini uovu kama huu katika hatua ya juu hivyo ni hatari sana kwa nchi,
   
 11. N

  Ngoiva JF-Expert Member

  #11
  Dec 7, 2011
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 236
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wale wale ndio wao,
  Bado wapo palepale,
  Wao wale wenye vyao
  Na vya kwako vilevile,
  Wala kale wala leo,
  Kura huko kula kule,
  Mwendo huu ndio huo
  Bado tupo palepale.
   
 12. M

  Magarinza Senior Member

  #12
  Dec 7, 2011
  Joined: May 9, 2008
  Messages: 122
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Lakini we Zitto si ndo ulimsifia bi kiroboto ktk bunge la bajet na kuwaponda waliokuwa wanamkosoa!?? Leo imekuwaje unaanza kusema hafai eti anavunja sheria?? Zitto siamini kama bado una dhamira njema katika siasa za ukombozi wa taifa letu.
   
 13. Remote

  Remote JF-Expert Member

  #13
  Dec 7, 2011
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 14,875
  Likes Received: 1,561
  Trophy Points: 280
  Kwel ukishangaa ya pinda
  utayaona ya makinda
   
 14. I

  ICHONDI JF-Expert Member

  #14
  Dec 7, 2011
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 588
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Kuna version nyingi kuhusu hili swala la nyongeza ya posho. Katibu wa bunge kasema mapendekezo yapo mezani na viwango vipya havijaamuliwa kulipwa. Spika anasema " tumemuongezea mbunge posho" which means tayari viwango vipya vya posho vilitumika bunge lililomalizika. Zito Kabwe anasema viwango vipya vya posho "vikilipwa " kwa maana havijalipwa! Najiuliza what is the truth. I expected Zito aseme with whole truth kuwa viwango vipya vililipwa na hela ziliingia kwenye account yake. No body is standing up na kueleza ukweli. Nawapenda CDM but kuna unafiki mkubwa sana kwenye issue ya posho. Makes me wonder if there is a difference between CDM na CCM ukiachilia mbali kuwa CDM hawana tu Dola. Zito Kama unasoma hapa please let the public know kama viwango vya posho vipya vimeshaanza kutumika. Kama bado then Makinda ajiuzulu kwa kumuumbua Katibu wake
   
 15. M

  MASIKITIKO JF-Expert Member

  #15
  Dec 7, 2011
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 841
  Likes Received: 203
  Trophy Points: 60
  Bunge limekuwa sehemu ya anasa,vyumba vya laki moja kwa siku,huku kwetu mbagala kodi ya mwaka ya chumba
   
 16. N

  Ngarenaro JF-Expert Member

  #16
  Dec 7, 2011
  Joined: Nov 29, 2011
  Messages: 312
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hilo swala la kupanda kwa gharama za maisha, spika anapataje ujasiri wa kusema dodoma gharama za maisha zimepanda, na kuhalalisha ongezeko la posho toka elf 70 hadi laki 2, ambalo ni ongezeko la zaidi ya 185%. Kama kweli gharama za maisha zimeongezeka, vp kuhusu wafanyakazi wengne wa taasisi za umma waishio dodoma, kuna mpango wowote wa kuwaongezea kima cha mshahara ili pato lao liendane na hilo ongezeka la gharama ya maisha? mama Anne Makinda, wabunge na wengine wote ambao wapo nyuma ya mpango huu, lazima wajitafakari upya na wajipime wenyewe kama wanastahili kuendelea kuwepo ktk nyazifa zao, ukwei ni kwamba viongozi wa namna hii wasioguswa na umasikini wa watanzania hawastahili kuendelea kuwepo ktk nafasi walizonazo.
   
 17. M

  MASIKITIKO JF-Expert Member

  #17
  Dec 7, 2011
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 841
  Likes Received: 203
  Trophy Points: 60
  Zao la nyoka ni nyoka,Zao la mafisadi..........Mtamalizia wataalam wa methali
   
 18. nice 2

  nice 2 JF-Expert Member

  #18
  Dec 7, 2011
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 746
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Ushabiki unaoutaka wewe ni wa kinafiki, mtu anapofanya vizuri anapaswa kupongezwa, akikosea lazima akosolewe. So unataka Zitto amsifu tu spika kisa anakubaliana nae katika maswala mengine? Watanzania mjifunze kubadilika

   
 19. i

  ibange JF-Expert Member

  #19
  Dec 7, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 1,545
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  This amounts to abuse of office
   
 20. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #20
  Dec 7, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Kama mshauri mkuu na msaidizi wa karibu wa spika ndiye huyu katibu bunge ndugu kashilila anayeongea nonsense mbele ya umma, siwezi kushangaa kama spika atakuwa amekwenda kinyume cha sheria.
   
Loading...