Zitto: Serikali yalikoroga ujenzi standard gauge, wachina wanyimwa zabuni, wagoma kutoa pesa

Mturuki hana hela kwasasa,ana commitment nyingi mno kugharamia vita kule syria,na uchumi wake siyo mkubwa kivile,

sidhani kama watatoa mkopo wa kandarasi kubwa kama ile,
miradi mikubwa kama hiyo hata wamarekani huwa wanaikimbia kukwepa gharama,
Ni kweli, MAREKAni aliukimbia mradi wa TAZARA akisema hauwezekani,akakimbilia barabara ya Mbeya-Moro,then Mchina akasema its possible akaanza project ile
 
Du kweli Zitto nae kichwa maji, kwahiyo watu wakiuke taratibu za zabuni kumpendelea mtoa pesa?
kutakuwa na utawala wa sheria hapo sasa?
 
Kama mkopo watatupa wachina sio lazima na mkandarasi atoke kwao ni jukumu la chi husika kuangali mkandarasi ambae atakizi vigezo vyao .kama unapewa mkopo kwa sharti kuwa wao ndio wakujengee hilo sasa ni suala jingine na ni lazima tuangalie kwa makini sana
Ubepar haupo hivyo,Hela anakupa mchina na mkandaras anatoka HUKO.Fatilia kwa makini
 
Yan akina Zitto wamgenyamaza.. Ili 2020 tuone jinsi miti itakavyogeuka maua
 
Lakini wachina nao ni vimeo tu. Sijaona la maana waliofanya miaka hii ya karibu zaidi ya TAZARA kwa miaka ya zamani. Naona wanatoaga ahadi nyingi lakini hazitekelezeki.
Tunataka kuiuza nchi kwa China? Sioni tatizo kujaribu wengine kama itakuwa na manufaa kwa nchi. Tukumbuke hii mikopo lazima ilipwe
 
What if serikali ya Uturuki nayo imeamua kutoa mkopo wa mradi huo pengine kwa riba nafuu kuliko China?

Tukumbatie wachina tu hata kama kampuni yao haina vigezo kisa marafiki?

Nadhani Zitto angetafuta taarifa sahihi kwanza akajiridhisha badala ya"tumesikia".

Huyu jamaa amekuwa na tabia ya kuokota okota udaku halafu akiombwa evidences anakimbilia tena kwenye issue nyingine.
Itakuwaje sasa jamaa akigoma kutoa pesa???I mean mchina
 
Sisi wenyewe nasikia mkubwa alishasema mwaka huu tunaaza kukopesha nchi zingine. Tuna madini tuna gesi tuna mbuga za wanyama Kwani kuna wasi wasi gani Jamani?

Tumeanza kwa kuikopesha Zanzibar pesa ya uchaguzi wa marejeo.

Hahaha! Kumbe tulipoambiwa mwaka huu tutaanza kuzikopesha nchi nyingine fedha walikuwa wanamaanisha Zanzibar baada ya Wazanzibar kusema wao ni nchi? Hii kali kweli kweli!!!
 
Du kweli Zitto nae kichwa maji, kwahiyo watu wakiuke taratibu za zabuni kumpendelea mtoa pesa?
kutakuwa na utawala wa sheria hapo sasa?

I say, Zitto akiona comments kama hizi nadhani anaelewa kwa nini nchi hii chama cha upinzani sio rahisi washinde uraisi. Tatizo sio ubaya wa CCM, bali upeo wa uelewevu wa wapiga kura.

Na hilo ndilo wanalokesea vyama vya upinzani nchini, wanakazana kuongea juu ya ubaya wa CCM na viongozi wake badala ya kuongeza upeo wa kuelewa wa wapiga kura, au hata kulenga wale wanaowaelewa ambao mara nyingi hawaendi kukaa kwenye foleni ili wapige kura.
 
Ujinga yaani mtu atoe mkopo alaf yeye huyo ndie apewe tenda ili ile hela irudi kwake.
Bila shaka yo yote wewe ndiye mjinga! Mchina ametoa fedha ili kampuni zake zipate kazi na siyo ziendelee kusota wakati serikali yao ina fedha za kujenga reli!

Hata kama ni wewe una kampuni yako huwezi ukatoa fedha kwa kampuni nyingine ijenge mradi ambao kampuni yako ina uwezo wa kuujenga!
 
Zitto ataitwa mchochezi. siku hizi hata maana ya uchochezi nadhani imebadilika kwenye kamusi.. Kuna magazeti tuliambiwa juzi ya kichochezi tukatolewa hadi mifano ya mauaji ya Rwanda! Ukifuatilia sana ni kwamba hayaandiki tu habari za kufurahisha mtu fulani... Wananchi tuachwe tuchambue pumba kwa uelewa wetu sio kuamuliwa na mtu anayejiona anajua kila kitu.

LIKE
''Mipango na Mikakati imekamilika na sasa tuko kwenye mchakato wa mazungumzo na wafadhili"- M Pinda
 
Kumbe wanawaingizaga mjini eehe? Na ule uwanja wa taifa vipi hawakutoa kitu?

Na uturuki wanatupa nini? Na mwenye mchango mkubwa kwa TZ kati ya China na Uturuki ni nani?
Mbona unachanganya mambo, nimeuliza lini China wametoa hela ya ujenzi wa SGR maana kila siku ni ahadi watatoa
 
C ilikuwa ni tender??? Sasa mchina anakasirika nini kukosa? Kama mchina ilikuwa lazima apate kulikuwa na haja gani kualika contractors wengine???
 
Shida ya kumpa madaraka mtu asie na vision wala mission...kwa kifupi jamaa hana future...
 
W
Serikali ilitangaza kuwa ujenzi wa Reli ya Kati ya kisasa utaanza mwezi Disemba mwaka jana kwa msaada kutoka nchi ya China. Leo ni mwezi Januari hata zabuni ya kampuni iliyoshinda kutekeleza mradi huo Serikali haijatangaza. Hata hivyo tumesikia kuwa kampuni kutoka Uturuki imeshinda zabuni hiyo na China (ambao ndio watoa mkopo wa mradi husika) wamekasirika na wamegoma kutoka fedha zao.

Tumesoma kwenye vyombo vya habari kuwa Rais wa Uturuki anakuja nchini wiki ijayo. Hatukatai kuimarisha mahusiano na Uturuki, lakini ni muhimu Serikali ijitazame upya kuhusu mahusiano yake na China. China ni rafiki wa Tanzania wa misimu yote. Tanzania imekuwa na China muda wote na China imekuwa na Tanzania muda wote. Maamuzi ya Serikali ya kutozingatia taratibu za China katika masuala ya mikopo yanaweza kugharimu sana mahusiano yetu ya zaidi ya miaka 50.

Tunamsihi Rais awe makini sana na mwenendo wake wa kutojali misingi imara ya Sera yetu ya mambo ya nje. Serikali ikae chini na China kutazama upya suala la Reli ya Kati vinginevyo hatutajenga Reli hiyo, ama itachukua miaka mingi sana kuijenga Reli hiyo. Madhara ya kuchelewa kujenga Reli ya Kati ni makubwa mno kwani washindani wetu wa kibiashara, Kenya, wanamaliza Reli yao sasa kuunganisha na nchi za Rwanda na Mashariki ya Kongo.

Namkumbusha Rais na Serikali namna ndani ya mwaka mmoja tangu aingie madarakani walivyovunja misingi yetu kadhaa ya Sera ya Mambo ya Nje, hasa kuhusu Sahara Magharibi na Mashariki ya Kati. Tumeikumbatia Moroko kwa ahadi ya viwanja vya mipira na misikiti na kuwaacha wananchi wa Sahara Magharibi ambao Mwalimu Nyerere aliwalinda kwa gharama zote. Juzi juzi kwa mara ya kwanza tumewasaidia Israel kwenye Umoja wa Mataifa bila ya kujali msimamo wetu wa 'Two States Solution' kati ya Palestine na Israel.

Sasa tunakwenda kuweka nyufa kwenye mahusiano yetu na China. Serikali ijitazame upya. Tanzania haikuanza na awamu ya Tano, nchi hii imekuwapo na itaendelea kuwapo. Hatuwezi kukaa kimya tukiendelea kuona misingi ya nchi yetu inavunjwa vunjwa. Lazima tuingie mkopo usio na tija kwa kigezo cha uraf
Serikali ilitangaza kuwa ujenzi wa Reli ya Kati ya kisasa utaanza mwezi Disemba mwaka jana kwa msaada kutoka nchi ya China. Leo ni mwezi Januari hata zabuni ya kampuni iliyoshinda kutekeleza mradi huo Serikali haijatangaza. Hata hivyo tumesikia kuwa kampuni kutoka Uturuki imeshinda zabuni hiyo na China (ambao ndio watoa mkopo wa mradi husika) wamekasirika na wamegoma kutoka fedha zao.

Tumesoma kwenye vyombo vya habari kuwa Rais wa Uturuki anakuja nchini wiki ijayo. Hatukatai kuimarisha mahusiano na Uturuki, lakini ni muhimu Serikali ijitazame upya kuhusu mahusiano yake na China. China ni rafiki wa Tanzania wa misimu yote. Tanzania imekuwa na China muda wote na China imekuwa na Tanzania muda wote. Maamuzi ya Serikali ya kutozingatia taratibu za China katika masuala ya mikopo yanaweza kugharimu sana mahusiano yetu ya zaidi ya miaka 50.

Tunamsihi Rais awe makini sana na mwenendo wake wa kutojali misingi imara ya Sera yetu ya mambo ya nje. Serikali ikae chini na China kutazama upya suala la Reli ya Kati vinginevyo hatutajenga Reli hiyo, ama itachukua miaka mingi sana kuijenga Reli hiyo. Madhara ya kuchelewa kujenga Reli ya Kati ni makubwa mno kwani washindani wetu wa kibiashara, Kenya, wanamaliza Reli yao sasa kuunganisha na nchi za Rwanda na Mashariki ya Kongo.

Namkumbusha Rais na Serikali namna ndani ya mwaka mmoja tangu aingie madarakani walivyovunja misingi yetu kadhaa ya Sera ya Mambo ya Nje, hasa kuhusu Sahara Magharibi na Mashariki ya Kati. Tumeikumbatia Moroko kwa ahadi ya viwanja vya mipira na misikiti na kuwaacha wananchi wa Sahara Magharibi ambao Mwalimu Nyerere aliwalinda kwa gharama zote. Juzi juzi kwa mara ya kwanza tumewasaidia Israel kwenye Umoja wa Mataifa bila ya kujali msimamo wetu wa 'Two States Solution' kati ya Palestine na Israel.

Sasa tunakwenda kuweka nyufa kwenye mahusiano yetu na China. Serikali ijitazame upya. Tanzania haikuanza na awamu ya Tano, nchi hii imekuwapo na itaendelea kuwapo. Hatuwezi kukaa kimya tukiendelea kuona misingi ya nchi yetu inavunjwa vunjwa. Lazima tukemee.
We Zitto acha unaajenda nzuri ila utetezi wako kuhusu China hauangalii maslahi ya nchi.Lama mkopo hauna Tina kwanini tuing

Siasa chacfu hizo.Kama mkopo hauna tija?
 
Utam wa gas ya Ntwala hautamwachia mchina akubali kuikosa. Ametikisa kidogo tu aone ka tutateetemeka. Tukikomaa atazitoa fweza tu. Kama vipi tumpe Mmarekani hiyo gas tuone ka mchina hatatoa fweza kiulainiiii ka kula matoke vile
 
Back
Top Bottom