Zitto: Serikali ya Magufuli imekopa zaidi ya tril 3 toka uswisi kufadhiri SGR na Stiglers yenye riba kubwa

Baada ya kuangalia hii video nimegundua kwanini Zitto aliwekwa korokoroni si kwa kumchamba mkuu wa malaika kwa kiasi hicho!
 
Zito naye kapoteza uelekeo.
Ukikopa yes ni fedha zako umetumia na utalipa. Sasa kuna jipya gani hapo?
 
Kipimo kimojawapo cha ufukara ni kushindwa kutumia mikopo ili kujiendeleza. Watanzania tu wachovu kiuchumi kwa sababu mojawapo ni kutokuwa na uwezo wa kukopa so mkopo si dhambi ni ishara mojawapo ya ukombozi .niiombe serikali iwawekee mazingira mazuri na watanzania kukopa katika individual level
 
Acha ujinga ndugu, ukikopa ni pesa zako? Je usipolipa? Ni nani asiyejua kwamba tuna deni kubwa la taifa lililoanza toka enzi za Nyerere? Je kote huko tulikuwa tunatumia hela zetu kisa tulikopa?

Ukikopa pesa ni zako, usipolipa huachiwi hivi hivi tu kwamba umeshindwa kulipa , lazima ulipe ndiyo maana unaweka bonds kabla ya kukopa. Kukopa maana yake nikutumia pesa zako in advance. Mfano unaweza chukua mshahara wako ukatanguliziwa mapema kabla ya mwisho wa mwezi kufika maana utazifanyia kazi. ama ukachukua tenda ukavuta advance mapema hata kabla yakuanza kazi, lakini mwisho wa siku utazifanyia kazi ndo mana ya pesa yako.

Ujinga ni kivumishi ambata ambacho hakina madhara ktk ujengaji hoja na ukweli ulivyo.
 
Athari za huo mkopo ni nini? Mbona haja changa ua?

Kitendo cha kukopa huku ukiongopa ni fedha za ndani hapo tu ni walakini. Athari zake ni jinsi gani utalipa hasa ukizingatia hata masharti hayako wazi, ni dhahiri ni mkopo wenye riba kubwa sana au malipo yake ni ya haraka kabla ya hata mradi kuanza kurejesha. Udhaifu niliogundua kwa rais wetu ni kutokujali matokeo ya maamuzi yake hasa pindi anaposaka mtaji wa kisiasa.
 
Kwani sheria za kukopa zinasemaje, kwamba wapitie bungeni au? Ili tujue kama sheria zimevunjwa tujadili uvunjaji wa sheria
Nimeandika mambo mengi kwenye mistari michache....ndio maana nimeweka alama hizi....hivyo jiongeze
Ila kwa sasa tubaki kwenye hili la mkopo ila usisahau na deni la taifa pia
 
Ukikopa pesa ni zako, usipolipa huachiwi hivi hivi tu kwamba umeshindwa kulipa , lazima ulipe ndiyo maana unaweka bonds kabla ya kukopa. Kukopa maana yake nikutumia pesa zako in advance. Mfano unaweza chukua mshahara wako ukatanguliziwa mapema kabla ya mwisho wa mwezi kufika maana utazifanyia kazi. ama ukachukua tenda ukavuta advance mapema hata kabla yakuanza kazi, lakini mwisho wa siku utazifanyia kazi ndo mana ya pesa yako.

Ujinga ni kivumishi ambata ambacho hakina sababu madhara ktk ujengaji hoja na ukweli ulivyo.

Acha kupiga siasa mfu hapa jukwaani, nimekuambia tuna madeni toka enzi za Nyerere na hatujalipa mpaka tumefikia mahali pa kuomba kusamehewa, je pesa zako utaomba usamehewe? Halafu usichanganye advance payment na mkopo. Kama hujui tofauti ya mkopo na advance payment rudi shule ukajifunze. Na sasa hivi elimu ni bure hivyo hakuna kisingizio.
 
17 Reactions
Reply
Back
Top Bottom