Zitto: Serikali ya JK katika hali mbaya kifedha; Mkulo Akanusha!

Watanzania tulisubiri kufikishwa hapa,mwezi wa kwanza nilipata kusoma gazeti moja likinukuu chanzo k1 kikieleza kwamba kuna wizara moja ilikuwa imebakiwa na 800m ikiwa ni pesa ya kuhudumia wizara toka chini-juu ktk shughuri zote mpaka juni,nilshangaa kama hyo ni wizara ama ni idara1

tusisahau ripoti ya TRA iliyoonyesha kupungua kwa makadirio ya mapato mwezi wa3,lakini pia Mkullo alisema machi kwamba kuanzia April uchumi utashuka sana hadi mwisho wa mwaka,sasa hapa hujaweka 96b tunazotakiwa kuwapa wahuni wa Rchmonduli,

hii imechagizwa na mgao wa umeme,lakn bado jana umetangazwa mgao mwingne funga kazi wa masaa16 kwa siku,hapa ndugu zangu mbali ya kutokuongezwa mishahara,tusitarajie kutimizwa kwa ahadi hata 0.5 yake.

nadhani hapa tulipo siyo tena serikali na chama chake wenye kuweza kuretreat hali hii,labda nguvu ya umma ikiongozwa na CDM walitoe hapa taifa hili kwa maana JK amekwama kwenye matope mazito ni lazma apigwe push ama ajiuzulu,

na kwa hali hii mishahara itaongezwa kweli? je serikali inao uwezo tena wa kuajiri wafanyakazi wapya na kutoa ajira kama mwajiri mkuu??na vipi vijana wapya wanaotegemea kuanza vyuo sept wataweza kupewa mikopo wote...tukubali tukatae huu mwaka JK atatubu kuiba haki za wapiga kura wa Dr.Slaa..hapo bado ishu ya katiba na muungano,tusubili tuone
 
  • Thanks
Reactions: Obe
Kweli serikali ya kisanii niya kisanii tu.. majibu ya Mkulo "Serikali haiwezi kujibu tuhuma za mitaani za Chadema ambao wana ajenda yao ya mitaani ambayo wataendelea nayo. Serikali inashughulika na masuala ya wananchi na itajibu maswali yao kuhusu matatizo yao na serikali kupitia bajeti ya mwaka huu."

Swali ni kwamba hayo masuala ya wananchi ni yapi kama uhakika wao na familia zao kuishi?

Kwani CHADEMA sio wananchi jamani? Naomba definition ya neno "wananchi!"
 
business times walishaandika kitambo. Labda kwa kuwa yalikuwa mambo ya english. Tatizo watanzania hatusomi
Swala sio kuandika lini swali ni Serikali ya JK inafanya nini kukabiliana na hali halisi ya sasa. Mkulo alitakiwa aseme Serikali inasolution kukabiliana na hali hiyo na sio kudai budget ya serikali juni ndio itasema. Sitashangaa June atakachosema ni kwamba ataendelea kuwakandamiza wafanyakazi kwa kodi zaidi maana serikali haina tena chanzo cha pesa. Kuongeza kodi katika pombe kitu kitakachochangia kufukuza wawekezaji. Na kudai kuimarisha ukusanyaji wa kodi madai ya kila siku lakini utekelezaji hakuna.

But wait what do you expect from the government whose leader's son anasema publicly kwamba tunaishi kimjini mjini!!!!!! Subirini tu tuumizane hapo kwasababu ya kukua kwa tabaka la maskini na tajiri and the rest is history. Egypt, Tunisia, Sierra Leone, Thailand, hawakuanza mbali time will tell.
 
Maswali kwa JK:
1. LJ: Hivi Mh Rais, unafikiri Tanzania ni nchi maskini?
JK: Ndiyo.
2. LJ: Kwa nini Mheshimiwa unafikiri kuwa Tanzania ni nchi maskini?
JK: Sijui!
3. LJ: Kwani Mheshimiwa Rais hukusomea mambo ya uchumi UDSM?
JK: Ni kweli nimesomea mambo ya uchumi lakini ni vizuri nikaunda Tume ili kukusanya maoni ya wananchi kuhusu kisababisho cha umaskini wa Tanzania!
LJ: Kwa nini Mheshimiwa Rais usitumie wataalamu wa Wizara ya Fedha ili wakupatie taarifa sahihi za kiuchumi?
JK: Mara nyingi wataalamu wangu wamekuwa wakinipatia taarifa potofu, kwa hiyo sasa hivi nataka kubadili mikakati! Umesahau mbona hata kwenye uchaguzi nilibadili mbinu za kuingia Ikulu baada ya kubaini kwamba kikulacho ki nguoni mwako?
Mahojiano yamesitishwa kwa muda, mchana mwema!
 
hali halisi inaonyesha kwamba uchumi wa tanzania unaangukia mikononi mwa mchumi. Mishahara hailipiki, kodi inadorora, waalimu hawana future, askari rushwa mtindo mmoja
 
Sunday, 08 May 2011 09:17

f%20mbowe%20mbeya.jpg


Mwenyekiti wa chadema Freeman Mboye,akihutubia umati wa watu waliohudhuria mkutano wa hadhara wa chama hicho jijini Mbeya juzi.

ZITTO ADAI INAKOPA HATA MISHAHARA YA KUWALIPA WAFANYAKAZI

Boniface Meena, Mbeya na Exuper Kachenje

VIONGOZI wakuu na wabunge wa Chadema jana waliushambulia mkoa wa Mbeya kona zote kwa mikutano ya hadhara iliyofanyika katika majimbo kadhaa ya uchaguzi ya mkoa huo.Akiwahutubia wanachama wa Chadema na wananchi wa mjini Vwawa, Mbozi jana, Naibu Katibu Mkuu chama hicho, Zitto Kabwe, aliifyatuli kombora zito Serikali ya Rais Jakaya Kikwete akidai kuwa ina hali mbaya kifedha kwa sasa, hata mishahara ya kulipa wafanyakazi inakopa.

Katika mikutano hiyo Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Grace Kiwelu walikuwa katika Jimbo la Rungwe Magharibi, Katibu Mkuu, Dk Willibrod Slaa alikuwa Chunya, Zitto alikuwa jimboni Mbozi Mashariki, Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa na Mbunge wa Mbeya Mjini, Jospeh Mbilinyi walikuwa Jimbo la Kyela na Chiku Abwao alikuwa Mbeya Vijijini.

Zitto ambaye ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, alidai kuwa hali hiyo mbaya fedha kwa Serikali imesababisha watumishi wake pamoja na wabunge kutolipwa mishahara hadi jana Mei 7, 2011.

Akizungumza na wananchi Vwawa katika Jimboni Mbozi Mashariki katika viwanja ya ofisi ya Afisa Mtendaji, Zitto alisema Serikali sasa inatafuta fedha za kuwalipa watumishi wake mishahara ya mwezi Aprili.

"Hata sehemu ya posho za wabunge mkutano uliopita, zikiwemo za kugharamia mafuta ya safari za wabunge majimboni bado hazijalipwa kutokana na Serikali kukosa fedha," alidai Zitto.

Alisema kutokana na hali hiyo Serikali imekwenda kukopa Sh540 bilioni kutoka benki za ndani ili watu wasijue kuwa inakabiliwa na ukata.

"Serikali haikopi fedha ili ijenge bandari, viwanda au kugharamia miradi ya maendeleo, bali inakopa ili ilipe mishahara ya wafanyakazi," alisema Zitto.

Hata hivyo, Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkullo, alipoulizwa na gazeti hili kuhusu suala hilo jana alisema hizo ni habari za barabarani tu.

Alisema kuwa Serikali haiwezi kujibu tuhuma za mitaani za Chadema ambao wana ajenda yao ya mitaani ambayo wataendelea nayo.

Waziri huyo alisema Serikali inashughulika na masula ya wananchi na itajibu maswali yao kuhusu matatizo yao na serikali kupitia bajeti ya mwaka huu.

"Kwa sasa ninapozungumza nipo Kampala, Uganda katika Mkutano wa Mawaziri wa Fedha wa nchi za Afrika Mashariki ambapo tumekubalina bajeti zitasomwa kwa pamoja Juni 8, mwaka huu," alisema Mkullo.

Mikutano ya jana ya Chadema imefuatia maandamano makubwa yaliyofanywa chama hicho yakiongozwa na viongozi na baadhi ya wabunge wake katika Jiji la Mbeya juzi.

Akihutubia katika maeneo tofauti katika Jimbo la Rungwe Magharibi, Mbowe alidai kuwa Mbunge wa jimbo hilo, Profesa David Mwakyusa, ameshindwa kuwatatulia matatizo yao kwa kuwa si mpambanaji.

"Mwakyusa hawezi kupambana na Mbowe kwa kuwa ni mwoga na hana cha kusema. Tutawasaidia wananchi kupambana mpaka kieleweke na tuondokane na umasikini uliokithiri," alisema Mbowe.

Mbowe alimlinganisha Mbunge wa Chadema mmoja kuwa ni sawa na wabunge 20 wa CCM, hivyo Profesa Mwakyusa hana uwezo wa kupigania wananchi wake.

Aliwaambia wananchi hao kuwa matatizo wanayoyapata ni kutokana na viongozi walioko madarakani kuendekeza tabia ya ufisadi.

"Mnadanganywa kwa kupewa mawaziri na sasa mbunge wenu si waziri tena. Hivyo ni kama ameshindwa na hawasaidii kitu. Sisi tutaandamana nje na ndani ya Bunge kuwatetea wananchi kwa ujumla," alisema Mbowe.

Alisema Tanzania bila CCM inawezekana kwa kuwa kitu chochote kikikaa muda mrefu kinakuwa hakina mvuto, hivyo ni wakati wa wananchi kujipanga kuhakikisha chama hicho kinaondoka madarakani uchaguzi ujao.

Mbowe alisema kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Idara ya Kimataifa ya Maendeleo Uingereza, katika matumizi ya fedha za maendeleo kwenye bajeti ya Tanzania, asilimia 35 hadi 40 zinatumika kuwanufaisha viongozi badala ya kuwaletea wananchi maendeleo.

Naye Grace Kiwelu alisema licha ya matatizo ya wananchi kuwa mengi, wabunge wa Chadema kwa uchache wao watapambana bungeni hadi kieleweke.

"CCM sasa ni ya matajiri si kama zamani. Lazima mbadilike na muachane na chama cha mafisadi ili kulikomboa Taifa,"alisema Kiwelu.

Kiwelu alimshambulia Mwakyusa kwa kushindwa kupambana kwa ajili ya maendeleo ya wananchi wake na kuwaacha wakinyanyasikika na kodi mbalimbali ambazo madiwani wa chama chake wanaoongoza halmashauri kushindwa kuwapunguzia wananchi mzigo huo.

Akiwa Chunya, Katibu mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa alisema anaishangaa Serikali kuendelea kumkumbatia mmoja wa makamishna wa TRA, aliyedai kuwa amelitia taifa hasara kubwa katika kumfilisi mmliki wa kampuni moja ya jijini Arusha.

""Hoja ni kwamba, kwa nini mtu anayesababisha Serikali hasara ya mabilioni mpaka sasa yuko ofisini bila kuchukuliwi hatua za kinidhamu," alisema Dk Slaa.

Alihoji kuwa haelewi ni kwa nini mpaka sasa Serikali haimlipi mmiliki wa kampuni hiyo fedha zake baada ya kumfilisi kiaina ambapo kutokana na hilo ameitaka Serikali kuhakikisha kuw kamishna huyo anaachia ngazi kwa makosa aliyoyafanya.
 
Kwani JK kakosa mshahara? Yeye anakula kuku kama kwa.
Nchi ilimshinda siku nyiiiiingi zilizopita
 
TANZANIA TUNAUMIA KWA WOGA WETU.

Hakika kama tusipobadilika tukapunguza uoga,wenye meno wataendelea kuitafuna Tanzania na familia zao kunehemeka.kilichopo walioko madarakan wanawatumia watoto zao kujilimbikizia mali, baba ridh watanzania siku wakipunguza woga kwa asilimia moja wengi mtaishi uhamishoni.

""" HAKUNA MAENDELEO BILA KUJITOA MHANGA""

:peace:
 
Mkapa aibuka shujaa
• Atamba kwa uchumi imara, kodi, kudhibiti bei

na Bakari Kimwanga



BAADA ya kimya cha muda mrefu, huku akizongwa na kutuhumiwa kwa mambo kadhaa, Rais mstaafu Benjamin Mkapa ameibuka shujaa katika siku za karibuni. Hata mwenyewe amelitambua na kulithibitisha hilo.
Kuzingatia vipaumbele, kuinua uchumi na kukusanya kodi, ni baadhi ya mambo anayojivunia, na ambayo jamii inayatumia kumpima na kulinganisha utawala wake na wa Rais Jakaya Kikwete.
Mkapa ambaye mara baada ya kumaliza ngwe ya uongozi wake aliandamwa na kashfa za ufisadi, hivi sasa anatajwa kuwa kiongozi mahiri aliyemudu kudhibiti mfumuko wa bei pamoja na kukuza uchumi, tofauti na utawala wa sasa wa Rais Kikwete.
Utawala wa sasa umekuwa ukilalamikiwa kwa kufifisha uchumi, kushindwa kudhibiti mfumuko wa bei pamoja na maisha ya wananchi kuzidi kuwa magumu kadiri siku zinavyosonga mbele.
Serikali ya Awamu ya Nne ilipoingia madarakani mwaka 2005, zilifanyika jitihada za chinichini kubeza kazi za Rais Mkapa na kuibua kashfa mbalimbali zilizowahusu watendaji wake na yeye mwenyewe.
Kuna wakati wananchi walifikia mahali pa kuaminishwa kwamba Rais Mkapa aliharibu nchi, hata baadhi ya vijana wakadiriki kumzomea.
Hata hivyo, ugumu wa maisha, kinyume cha ahadi ya maisha bora ya Rais Jakaya Kikwete, umewafanya wananchi wamwone Rais Mkapa kama shujaa aliyeinua uchumi, ambao sasa hivi unadidimia na maisha yanakuwa magumu zaidi.
Kiongozi huyo ambaye mara nyingi amekuwa kimya kuzungumzia masuala mbalimbali ya utawala wake, alionyesha wazi hisia zake juzi usiku jijini Dar es Salaam baada ya kukabidhiwa tuzo ya heshima kwa mchango wake wa kuthamini michezo nchini, iliyoandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA).
Serikali ya Mkapa ndiyo iliyosimamia ujenzi wa Uwanja wa Taifa kwa ushirikiano na China. Ni uwanja wa kisasa wenye uwezo wa kuingiza watu 60,000 waliokaa.
Mkapa alisema wakati akiingia madarakani aliikuta nchi katika hali ngumu ya kiuchumi, jambo lililomfanya kuweka kando mambo mengi na kutoa kipaumbele katika uchumi ili wananchi waweze kupata unafuu wa maisha.
Alibainisha kuwa alijikita katika uboreshaji wa ukusanyaji wa kodi na kulipa madeni ili kuliokoa taifa na wananchi wake kwenye hatari ya kudidimia kiuchumi.
Alisema kazi ya kuimarisha uchumi haikuwa nyepesi, hivyo alilazimika mara kadhaa kuumiza kichwa na kukubaliana na washauri wake wakiwemo mawaziri katika kipaumbele cha kuimarisha uchumi wa nchi.
Mkapa alisema kutokana na mazingira aliyoyakuta wakati anaingia madarakani alilazimika kutumia kanuni za hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere za kuwa kupanga ni kuchagua na kutenda ni kuamua.
"Mwalimu Nyerere alikuwa akisisitiza umuhimu wa kufanya jambo husika kulingana na wakati uliopo, nami nilipanga, nikachagua na matokeo yake yakaonekana," alisema.
Alisema kuwa aliona ni muhimu kujenga misingi imara ya uchumi kwa kuimarisha ukusanyaji wa kodi ili kuiondoa nchi katika wimbi kubwa la madeni iliyokuwa ikidaiwa.
"Katika kipindi changu cha awamu ya kwanza nilipoingia madarakani, nilionekana kutopenda michezo kwa sababu nililazimika kuongoza kiukapa kutokana na mazingira niliyoyakuta. Hivyo, niliamua kuanza na kuimarisha uchumi kwa kujenga misingi ya kukusanya kodi.
"Pamoja na mambo mengine, kazi hiyo ilifanyika kwa umakini mkubwa na ilinifanya nishindwe kuhudhuria hata masuala ya michezo… na hiyo ikawa sifa yangu ya kuonekana sipendi michezo," alisema.
Aliongeza kuwa mazingira ya wakati ule yalimfanya afikirie zaidi uchumi na aliiwezesha serikali yake kupata msamaha wa madeni iliyokuwa ikidaiwa na nchi wahisani na wafadhili.
Mkapa alisema baada ya awamu ya kwanza kuimarisha uchumi ilipofika awamu ya pili ya utawala wake ndipo sasa akaamua kugeukia mambo mengine, yakiwemo hayo ya michezo ambapo aliona kitu pekee ambacho anaweza kuwaachia Watanzania na kuwa kumbukumbu nzuri kwake ni kujenga uwanja wa soka wa kimataifa katika Jiji la Dar es Salaam.
Hafla hiyo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali wakiongozwa na Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Emmanuel Nchimbi na watu mashuhuri ambao baadhi yao wamelilitumikia taifa katika nyanja mbalimbali.
Mkapa pamoja na kupewa heshima hiyo bado alitoa wito kwa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo nchini (TASWA) kuhakikisha wanautambua mchango wa Rais Kikwete katika medani ya michezo.
Alisema kujengwa kwa uwanja huo wa kimataifa Rais Kikwete amefanya kazi kubwa ya kujenga hoja wakati walipokwenda China kuomba msaada wao ili kufanikisha ujenzi huo.
Alisema kuwa baada ya serikali yake kuamua kujenga uwanja wa mpira wa miguu wa kimataifa, kazi ya kujenga hoja na kufanya mazungumzo ya namna gani uwanja utakuwa alimuachia Rais Kikwete wakati huo akiwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na hatimaye hoja zake kufanikiwa na China kukubali kuujenga.
"Hivyo Rais Kikwete anastahili heshima ya kutambulika kwa mchango wake katika michezo kwa kitendo chake cha kuwezesha kujengwa uwanja huo pamoja na aliyekuwa Waziri wa Kazi, Ajira na Vijana, Profesa Juma Kapuya, kutokana na kuhimiza mara kwa mara kuhusu mchakato wa kuanza kwa ujenzi wetu," alisema Mkapa.
"Kapuya amefanya kazi kubwa katika kufanikisha serikali kujenga uwanja huo wa kimataifa, alikuwa akinihimiza mara kwa mara na hatimaye tukafanikisha. Hivyo TASWA mnapaswa kutambua mchango wake na ikiwezekana naye apewe tuzo ya heshima," alisema.
Aliwaomba Watanzania kutambua haki na wajibu wa kuutunza uwanja huo ili uweze kudumu kwa muda mrefu na hatimaye kuwa kumbukumbu hata kwa kizazi kinachokuja.
Wakati akizungumza hayo, alikuwa akiwaeleza waliofika kushuhudia tukio hilo la utoaji wa tuzo kwa mwanamichezo bora wa mwaka 2010.
Katika hafla hiyo, Mkapa alionekana kukonga nyoyo za waliohudhuria ambapo mara kwa mara alilazimika kusitisha kwa muda kusoma hotuba yake kutokana na kushangiliwa, ikiwa ni ishara ya kuukubali utawala wake na mambo aliyolifanyia taifa.
Akizungumza katika sherehe hizo, kabla ya kutoa tuzo ya mwanamichezo bora, mgeni rasmi Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal, alisema amefanya kazi na Rais Mkapa wakati huo yeye akiwa Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, ambapo alisifu ujasiri aliokuwa nao Mkapa katika mambo mbalimbali.
"Rais wetu mstaafu tunakupa heshima kubwa ya kutambua kuwa nchi yetu inahitaji kufungua njia katika sekta ya michezo na kwa kufanya hivyo ulikubali kubana bajeti ya serikali ambayo ingejenga zahanati na shule lakini ukatambua afya njema na elimu bora hupatikana kama wananchi wanashiriki michezo.
"Uwanja uliotuachia ni kielelezo tosha na wala usikatishwe tamaa na vijana hawa wanaposhindwa kutupa matokeo mazuri katika mechi zao na hakika kazi yako uliyofanya itabaki katika ramani ya michezo nchini na kamwe haitasahulika," alisema Dk. Bilal huku akisifu ujasiri wa rais ambao alithubutu na hata kuweza kujenga uwanja huo wa kimataifa.






Source: Tanzania Daima Mkapa aibuka shujaa
 
Wewe sijui nikuweke katika kundi gani.Huo ndio utaahira kweli kweli,kwa hiyo kama Nyerere alikosea ni ruksa Kikwete naye kukosea,ovyooo.
Mbona hayo matatizo hata nyerere aliyapitia.
 
sasa kama nji ilishamshinda ,anafanya nini ikulu??ananipa hasira sana hii mutu!!
 
Hapa ndipo utaona tofauti kati ya JMK na BWM, hotuba ya Mkapa tuzo za TASWA ilikuwa ni kuwakumbusha watz umuhimu wa kukusanya kwa ajili ya kufanya vitu vya maendeleo kwa umma.

Mkapa aliamua kutokopa katika mabenki ya ndani ili taasisi hizi ziwakopeshe watz, leo kikwete ameanza kukopa katika mabenki ya ndani na hivyo kubana mikopo kwa watanzania (benki zinapenda kufanya kazi na serikali kwa kuwa kuna uhakika wa kulipwa kwa faida kubwa).

Unaposhindwa kubuni mikakati ya kukuza uchumi
 
Ninawasikitikia wafanyakazi ambao hawajalipwa mishahara yao mpaka sasa.Ila siwasikitii wabunge hata kidogo.Infact they don't diserve to be paid at all.Pesa wanazolipwa ni wastage.The money would be better spent kwa kujengea zahanati nk.Jamaa hawa hawana output yeyote, wameshindwa kabisa kuiwajibisa serikali.Kinachoendelea bungeni ni ujinga mtupu, na ukata wa serikali ni moja ya matokeo matokeo ya ujinga wao.
Zitto ambaye ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, alidai kuwa hali hiyo mbaya fedha kwa Serikali imesababisha watumishi wake pamoja na wabunge kutolipwa mishahara hadi jana Mei 7, 2011.

Akizungumza na wananchi Vwawa katika Jimboni Mbozi Mashariki katika viwanja ya ofisi ya Afisa Mtendaji, Zitto alisema Serikali sasa inatafuta fedha za kuwalipa watumishi wake mishahara ya mwezi Aprili.


"Hata sehemu ya posho za wabunge mkutano uliopita, zikiwemo za kugharamia mafuta ya safari za wabunge majimboni bado hazijalipwa kutokana na Serikali kukosa fedha," alidai Zitto.


Alisema kutokana na hali hiyo Serikali imekwenda kukopa
Sh540 bilioni kutoka benki za ndani ili watu wasijue kuwa inakabiliwa na ukata.

"Serikali haikopi fedha ili ijenge bandari, viwanda au kugharamia miradi ya maendeleo,
bali inakopa ili ilipe mishahara ya wafanyakazi," alisema Zitto.

Angalizo:
Kama ndio mwaka wa kwanza tu mambo yamekuwa hivi, ikifika 2014 itakuwaje? Na kama haina hata hela za kulipa mishahara tu je hiyo miradi itawezekana kweli?
 
Tatizo la Tanzania ni tatizo kubwa mno, kwa muono wangu. Tatizo linakuja kwamba nchi yetu ni tegemezi mno na wanaotegemewa sahizi wako ktk crisis moja balaa sasa hapo balaa ndipo lilipo.

Tatizo tumekuwa wategemezi hata kwa vitu ambavyo viko ndani ya uwezo wetu kabisa. Wananchi asilimia 60 ya watanzania hawahitaji
1.Pentrol ili kufurahia maisha
2.Hawahitaji Magari ili kufurahia maisha
3.Hawahitaji umeme ili kufurahia maisha
.........

Wanacho hitaji ni mlo tu wa uhakika asubuhi , mchana na usiku. Kinachoshangaza haya mambo ya msingi bado hayawezekani kwa mtanzania japokuwa
1.tuna ardhi ya kutosha
2.Tanzania imezungukwa na maji

Hivi angalia ramani ya tanzania ni lazima kuwepo na mvua?

Maoni
Serikali badala ya kuimba kilimo kwanza, ingetenga hekta kadhaa ambazo ziko karibu na maji serikali yenyewe ikajipa malengo na kuzalisha mazao mahindi, mpunga , maharage nk kwa umwagiliaji na mavuno yatakuwa mara 3-4 kwa mwaka. Serikali kuna haja ya kuwekeza miundo mbinu ya umwagiliaji.

Na tena serikali inaweza tajirika kwa kuuzia chakula nchi zinazokubwa na njaa zilizotuzunguka. Ktk viwanda na utandawazi mwingine ama biashara ya kawaida huko hatuwezi kushindana na badala yake serikali itumie ardhi na maji tuliyonayo na soko lilotuzunguka nchi nying zina njaa.

Kwa kweli siwaelewi hawa jamaa mipango yao, soko la chakula lipo wazi kabisa na uwezo tunao wa kufanya hivyo tena kwa mtaji ambao umo ndani ya uwezo, utashangaa wanakurupuka sijui flyover barabara for what?
 
Back
Top Bottom