Zitto: Serikali isipowataja walioficha mabilioni nje, CHADEMA itawataja hadharani!

Sijaelewa bado,its a bit confusing.Ili serikali iwataje waliopokea rushwa wakazipeleka hizo pesa kwenye akaunti ya uswisi,ni lazima serikali ikubali kwanza kuwa walipokea rushwa.

Nadhani hapa issue si kusema serikali iwataje,hapa cha muhimu ni kuwataja na kuweka ushahidi halafu serikali ndo iulizwe kama ni kweli ama si kweli na ishinikizwe kuchukuwa hatua.Kusema serikali iwataje isn't neccessarily a right step...
 
Akiwasilisha kambi ya upinzani katika bajeti ya wizara ya fedha Zito Zuberi Kabwe amesema, katika taarifa za kiuchunguzi zinaonyesha kuna kiongozi wa juu wa serikali iliyopita akishirikiana na baadhi ya watendaji wa serikali walihongwa. Inasemekana waliohongwa na baadhi ya makampuni ya uchimbaji wa mafuta na kwenda kuzificha fedha hizo Uswiss.

Hivyo kambi ya upinzani inaitaka serikali iwataje viongozi hao kabla CHADEMA haijawataja hadharani.

ZZK alipaswa kuiga mfano wa Tundu Lissu, Mch. Msigwa na wenzake wengine waliowataja wezi wa rasilimali zetu bila woga. Ameniudhi kwa kutowataja hadharani, kwani anawaogopea nini? Kuogopana na mbinu ya ccm.

Aaaaaaaaaggggggrrrrrrrrrrrrrrrrr!!!!!
 
Hapa ndiyo huwa nawapenda CDM, hakuna longolongo kama CCM! Go go gooo Zitto.

Ngoja ni refresh my memory, hivi waziri wa nishati na madini wa serikali iliyopita alikuwa nani vile?

Jamani ninaomba mnikumbushe huyu anaweza akawa suspect No. 1.

WILLIAM MGANGA NGELEJA; funguka!?
 
Safi sana Mafisadi wote nchini lazima waumbuliwe. Akimaliza kuwataja hao na yeye Zitto ajibu yanayomuhusu. Mod rudisha ule uzi unaomuhusu Zitto na J.Makamba hii ndio JF kumkoma nyani bila kumwangalia wadhifa wake!!
Hata kama walifanya mambo gizani wakiwa watatu with time watu wanayapata. Tunashukuru atutajie anaowajua kisha na yeye aseme juu ya yanayomuhusu. Tuko katika kusafisha nchi hii.
 
Kambi ya wachaga ndio CHADEMA? Akili yako imeoza

Je aliiba pesa za kagoda ni mchaga, aliyeiba pesa za deep green naye ni mchaga, acha propagada chafu, kuwa mazalendo, watu wanapotetea rasilimali za fedha , ni vyema tukaweka mbele masilahi ya kitaifa.Visenti vya kuhongwa na nape visikufanye uwe mwndawazim wa kutukana watanzania wote ni wachaga, uchanga na utanzania wapi na wapi.acha sera dhaifu za ukabila, taifa la kitanzania ni umoja, mshikamano na upendo na si ukabila,
 
Msome Nape hapa chini

Sasa Subiri uone kama Zitto nae atataja, itaishiaa hiv hivi kama kwa Nape

Zanta, hivi umesikiliza leo mahojiano ya Ch 10 kati ya Komu wa CDM na Nape wa CCM? Ninasikitika sana kama bado unahadaika na longo longo za CCM.

Nape umeliuzwa live awataje hao wafadhiri wa nje wa CDM akabaki kujiumauma. Akaulizwa basi hata awataje wafadhili wa nje wa CCM napo Napelepa akashindwa.

Mwenzake Komu wa CDM akataja taasisi ya nje ambayo CDM inapata pesa, na pia akataja taasisi ya nje ambayo CCM inapokea pesa.

Napelepa masikini ya Mungu akabaki DOMO wazi. CDM they walk the talks, CCM wanacheza comedy hiyo ndiyo TOFAUTI KUBWA ya CCM na CDM.
 
Je aliiba pesa za kagoda ni mchaga, aliyeiba pesa za deep green naye ni mchaga, acha propagada chafu, kuwa mazalendo, watu wanapotetea rasilimali za fedha , ni vyema tukaweka mbele masilahi ya kitaifa.Visenti vya kuhongwa na nape visikufanye uwe mwndawazim wa kutukana watanzania wote ni wachaga, uchanga na utanzania wapi na wapi.acha sera dhaifu za ukabila, taifa la kitanzania ni umoja, mshikamano na upendo na si ukabila,

Wewe Kupelwa, kabla ya kunijibu, umeona nilimjibu nani?? Nilimjibu mtu aliyesema CHADEMA ni kambi ya wachaga!!!

Nilimjibu kwa kumuuliza, "CHADEMA NI KAMBI YA WACHAGA?? AKILI YAKO IMEOZA".

So kama haujakurupuka kunisema, fahamu mimi nilikuwa nimekasirishwa na mtu aliyesema CHADEMA ni kambi ya wachaga! Kiswahili rahisi sana!
 
Yaani tukishawajua tu na kuwaona mtaani ni kuwarushia mawe kwenda mbele. Hawawezi kuangalia familia zao tu na huku robo tatu ya watanzania wanateseka kwa umasikini wakutupwa.
Mbona Chenge katajwa kwenye rada na akasema vile ni vijisenti na bado anapeta? Sisi Watanzania bado sana.
 
Mbona hili suala limebinafsishwa kwa Zitto wakati yeye kalileta kama hoja ya kambi ya upinzani ikiongozwa na CHADEMA? Analinganishwaje hapa na kauli binafsi ya Nape? Si suala la Zitto kama Zitto kuwataja bali ni la CHADEMA kama kiongozi wa kambi ya upinzani Bungeni.
 
Si awataje tu anasubiri nini kama sio unafiki.
Jamani ataje mara ngapi mbona keshasema kuwa ni kiongozi wa juu wa serikali hii ya CCM, mfano ukiambiwa waziri mkuu, waziri wa kawaida, mwanasheria mkuu na Rais, je kati ya hao nani ni kiongozi wa juu?, jamani mbona jibu lipo wazi!
 
James Mbatia anaFloor kwakusema kua majengo yooote makubwa yalioko jijini Dar es salaam hayalipi kodi na anauhakika na kama serikali inataka msaada wakujua ni jengo lipi yuko tayari kuisaidia!
Mh! JK naona anajilaumu kimoyomoyo kwani ameingiza nyoka ndani ya nyumba
 
Ulimboka amerudi sasa movie yake inasubiri continuation baada ya yeye kutoa tamko ya kilicho moyoyni mwake.
Bora hii movie mpya ianze ya hela za uswizi ili kama movie ya Ulimboka ikiisha ghafla kama ya Mwakyembe basi tuwe na movie mpya ya kuangalia.
 
Back
Top Bottom