Zitto: Serikali iko tayari kulipia ndege Sh1 trilioni kuliko kuokoa wakulima 1.4M wa tumbaku kwa Sh150 bilioni tu

Kuna utaratibu upo kwa mataifa makubwa yote serikali inanunua mazao yote ya ziada kwa bei ya soko au kubwa kidogo kuwa subsidize wakulima then inatafuta soko kwa mfumo wa bulk supply G to G , Ufaransa , UK , Canada ndo kabisa hadi nyanya wakizalisha sana kuliko hitaji serikali inanunua then inauzia mashirika WFP , redcross etc
China ndo walifanyakufuru wakati wana himiza mapinduzi ya kilimo, serekali likuwa inanua mazao yote yatakayo baki hivyo wakulima walikuwa na soko la huhakika, miaka na miaka watu wengi wakarudi kwenye kilimo tena huku wakitabasamu kuwa wakulima....Serikali ilikuwa iko radhi inunue mazao yote ya ziada hata kama itakosa soko zuri la hayo mazao ila siyo wakulima ndo wapate hasara nakushuka morali ya kulima.....

Angalia tz wakulima wanazidi kuwa masikini, nani tena leo anataka kulima Pamba kule usukumani???? tumbaku??? kahawa??? mipira kule uchagani??? wanyanya ndo kila siku wanalia...
Uzalishaji wetu umepungua sana kwenye kilimo hasa kwenye mazao yasiyo chakula moja kwa moja, hapa najua watoto wa 1985+ hamtanielewa, maaana kabla ya hapo uzalishaji kwenye kilimo tz ulikuwa juu mno, simnakumbuka somo la jografi darasa la 5 au 6,mikoa iliyokuwa inaongoza kwa kilimo cha mazao ya biashara eg chai IRINGA, Pamba ...... Kahawa ......
Sahavi hamna kitu...... hamna mtu utampeleka tena kulima hayo mazao
 
Umesema kweli na kwa uchungu mkubwa sana
 
Serikali inunue tumbaku yote hiyo alafu iifanyie nini??
Zito bwana!
Hujaona hapo juu....wa Tanzania wavivu sanaa kufikiri na wanaona kam ni jambo jipya!! Serikali itafute masoko kwa jumla G2G sio suala geni....duniani kote soko fulani lik serikali inawakomboa wakulima wake inanunua mazao hayo na kuhifadhi.....kuanza kutafuta masoko.....hata kwa bei sawa alimradi kumkomboa mkulima!!.....hatupendi kujiongeza kufikiri nje box na kusoma.......tunachojua kuandika mstari mmoja tu kama............!! Eti ndio sisi tutafika uchumi wa kati....sio kwa attitude hizi
 
Kama kuna demand kwenye soko la kimataifa wanunuzi wangetokea. Aache porojo
makampuni yanayo nunua huwa yanavuta, amekwambia ifanyike mpango wa G-G serikali inunue na kuuza kwa serikali nyingine (nje ya nchi kwa wenye mahitaji)

ajakwambia inunue ikavute acha umkunduchi
 
Huenda ndege itabeba watalii wengi na kuongeza pato la pesa za kigeni, kuna walichoona kama serikali, wanauchumi wanasemaje kwa tamko la pamoja? Weka siasa pembeni, weka mbele uzalendo
 
Urambo. Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe ametaka Serikali kununua tumbaku yote ya wakulima iliyoshindikana kununuliwa.

Akihutubia wananchi leo Ijumaa katika mkutano wa kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani katika Kijiji cha Kalemela A, Kata ya Muungano wilayani Urambo Zitto ameishangaa Serikali kutumia fedha nyingi kununua ndege aina ya bombardier zinazopakia watu wachache badala ya kuwekeza kwenye kilimo kinachoajiri wananchi wengi.

Zitto amesema katika ziara yake amezunguka vijijini na kushuhudia nyuso za huzuni, huku wananchi wakimwambia tumbaku ya mwaka jana haijauzwa na msimu mpya umeanza.

“Serikali makini ingefanya nini kwenye kadhia hii ya tumbaku? Sisi ACT- Wazalendo tungekuwa madarakani tungenunua tumbaku yote ya ziada ya wakulima kwa kutumia kasma ya fedha za dharura kwenye Fungu la 50 Wizara ya Fedha,” amesema.

Amesema Serikali iliwahimiza wananchi kufanya kazi kwa bidii, lakini baada ya kuzalisha kwa wingi wanaadhibiwa kwa kukosa masoko.

Zitto ameshauri Serikali kutafuta soko kwa mfumo uliosema ni wa G to G (Government to Government) na kuuza tumbaku hiyo na kurejesha fedha hizo kwenye mfuko wa dharura.

Amesema wakati asilimia 65 ya Watanzania wanategemea kilimo kama ajira, kilimo kimekuwa kikishuka na kusababisha wakulima kuendelea kuwa masikini na kukosa chakula.

“Tunazalisha watu zaidi kuliko chakula, ni dhahiri tunaelekea kubaya,” amesema Zitto.

Amesema katika hali hiyo ya kudumaa kwa kilimo bado wakulima wa Tabora hawajafutwa machozi na zao lao la tumbaku wakati ndilo linaloingiza fedha za kigeni kuliko korosho.

“Serikali ipo tayari kutumia Sh1 trilioni kulipia ndege ambazo ni Watanzania asilimia tano wanapanda kuliko kuokoa wakulima 1.4 milioni wa tumbaku nchi nzima kwa Sh150 bilioni tu, tena ikiwa fedha hizo zinarudi ndani ya muda mfupi,” amesema Zitto.

Amewataka wananchi wa kijiji hicho kuchagua mgombea udiwani wa chama hicho ili apambane kuhakikisha tumbaku ya mwaka jana inanunuliwa.

Amesema Ilani ya Uchaguzi ya ACT -Wazalendo ilitangazwa na Taasisi ya Mviwata (Muungano wa vikundi vya wakulima) kuwa ilani bora zaidi kuhusu masuala ya kilimo kuliko ilani za vyama vyote katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 kwa kuwa ilipendekeza kuwapo kwa Hifadhi ya Jamii kwa Wakulima.

Tanganyika chini ya CCM imo katika laana Kwa kuivamia Zanzibar ,kuuwa watu wasio na hatia kuwafunga masheikh na kuwatesa na udhalimu mwingi. Mabalaa zaidi yatakuja mpaka mtapoiachia Zanzibar kuwa huru na kuomba radhi
 
Haya madege si ndiyo business ambayo haitengenezi profit, hata Kenya wameuza mbili.
 
Kama kuna demand kwenye soko la kimataifa wanunuzi wangetokea. Aache porojo
tumbaku sio mahindi wewe ndo maana kuna makambuni ya kununua na vyama vya wakulima kuuzia huko.

ingekuwa inauzwa kama mahindi hao wanunuzi ungewaona wao hununua toka kwenye makampuni
 
Jana kwenye taarifa ya habari kuna wakulima walikuwa wanalia sana sana na tumbaku imeanza kuharibika Tabora huko. Bado mwezi tu tuanze.kudaiwa school fee na pesa yote ipo ghalani,mayo weeeeew
Waendelee kuitumaini ccm ni chama cha walala hoi ili uendelee kuwepo madarakani itabidi uzalishe walala hoi wengi wakuwatawala
 
Urambo. Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe ametaka Serikali kununua tumbaku yote ya wakulima iliyoshindikana kununuliwa.

Akihutubia wananchi leo Ijumaa katika mkutano wa kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani katika Kijiji cha Kalemela A, Kata ya Muungano wilayani Urambo Zitto ameishangaa Serikali kutumia fedha nyingi kununua ndege aina ya bombardier zinazopakia watu wachache badala ya kuwekeza kwenye kilimo kinachoajiri wananchi wengi.

Zitto amesema katika ziara yake amezunguka vijijini na kushuhudia nyuso za huzuni, huku wananchi wakimwambia tumbaku ya mwaka jana haijauzwa na msimu mpya umeanza.

“Serikali makini ingefanya nini kwenye kadhia hii ya tumbaku? Sisi ACT- Wazalendo tungekuwa madarakani tungenunua tumbaku yote ya ziada ya wakulima kwa kutumia kasma ya fedha za dharura kwenye Fungu la 50 Wizara ya Fedha,” amesema.

Amesema Serikali iliwahimiza wananchi kufanya kazi kwa bidii, lakini baada ya kuzalisha kwa wingi wanaadhibiwa kwa kukosa masoko.

Zitto ameshauri Serikali kutafuta soko kwa mfumo uliosema ni wa G to G (Government to Government) na kuuza tumbaku hiyo na kurejesha fedha hizo kwenye mfuko wa dharura.

Amesema wakati asilimia 65 ya Watanzania wanategemea kilimo kama ajira, kilimo kimekuwa kikishuka na kusababisha wakulima kuendelea kuwa masikini na kukosa chakula.

“Tunazalisha watu zaidi kuliko chakula, ni dhahiri tunaelekea kubaya,” amesema Zitto.

Amesema katika hali hiyo ya kudumaa kwa kilimo bado wakulima wa Tabora hawajafutwa machozi na zao lao la tumbaku wakati ndilo linaloingiza fedha za kigeni kuliko korosho.

“Serikali ipo tayari kutumia Sh1 trilioni kulipia ndege ambazo ni Watanzania asilimia tano wanapanda kuliko kuokoa wakulima 1.4 milioni wa tumbaku nchi nzima kwa Sh150 bilioni tu, tena ikiwa fedha hizo zinarudi ndani ya muda mfupi,” amesema Zitto.

Amewataka wananchi wa kijiji hicho kuchagua mgombea udiwani wa chama hicho ili apambane kuhakikisha tumbaku ya mwaka jana inanunuliwa.

Amesema Ilani ya Uchaguzi ya ACT -Wazalendo ilitangazwa na Taasisi ya Mviwata (Muungano wa vikundi vya wakulima) kuwa ilani bora zaidi kuhusu masuala ya kilimo kuliko ilani za vyama vyote katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 kwa kuwa ilipendekeza kuwapo kwa Hifadhi ya Jamii kwa Wakulima.
Ccm mbele kwa mbele
 
Back
Top Bottom