Zitto: Serikali iko tayari kulipia ndege Sh1 trilioni kuliko kuokoa wakulima 1.4M wa tumbaku kwa Sh150 bilioni tu

Amesikia serikali inavutaga tumbaku mpaka inunue tena yote??
Huyi jamaa anavyozidi kuwa mtu mzima na akili zinapungua.
Kuna utaratibu upo kwa mataifa makubwa yote serikali inanunua mazao yote ya ziada kwa bei ya soko au kubwa kidogo kuwa subsidize wakulima then inatafuta soko kwa mfumo wa bulk supply G to G , Ufaransa , UK , Canada ndo kabisa hadi nyanya wakizalisha sana kuliko hitaji serikali inanunua then inauzia mashirika WFP , redcross etc
 

Urambo. Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe ametaka Serikali kununua tumbaku yote ya wakulima iliyoshindikana kununuliwa.

Akihutubia wananchi leo Ijumaa katika mkutano wa kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani katika Kijiji cha Kalemela A, Kata ya Muungano wilayani Urambo Zitto ameishangaa Serikali kutumia fedha nyingi kununua ndege aina ya bombardier zinazopakia watu wachache badala ya kuwekeza kwenye kilimo kinachoajiri wananchi wengi.

Zitto amesema katika ziara yake amezunguka vijijini na kushuhudia nyuso za huzuni, huku wananchi wakimwambia tumbaku ya mwaka jana haijauzwa na msimu mpya umeanza.

“Serikali makini ingefanya nini kwenye kadhia hii ya tumbaku? Sisi ACT- Wazalendo tungekuwa madarakani tungenunua tumbaku yote ya ziada ya wakulima kwa kutumia kasma ya fedha za dharura kwenye Fungu la 50 Wizara ya Fedha,” amesema.

Amesema Serikali iliwahimiza wananchi kufanya kazi kwa bidii, lakini baada ya kuzalisha kwa wingi wanaadhibiwa kwa kukosa masoko.

Zitto ameshauri Serikali kutafuta soko kwa mfumo uliosema ni wa G to G (Government to Government) na kuuza tumbaku hiyo na kurejesha fedha hizo kwenye mfuko wa dharura.

Amesema wakati asilimia 65 ya Watanzania wanategemea kilimo kama ajira, kilimo kimekuwa kikishuka na kusababisha wakulima kuendelea kuwa masikini na kukosa chakula.

“Tunazalisha watu zaidi kuliko chakula, ni dhahiri tunaelekea kubaya,” amesema Zitto.

Amesema katika hali hiyo ya kudumaa kwa kilimo bado wakulima wa Tabora hawajafutwa machozi na zao lao la tumbaku wakati ndilo linaloingiza fedha za kigeni kuliko korosho.

“Serikali ipo tayari kutumia Sh1 trilioni kulipia ndege ambazo ni Watanzania asilimia tano wanapanda kuliko kuokoa wakulima 1.4 milioni wa tumbaku nchi nzima kwa Sh150 bilioni tu, tena ikiwa fedha hizo zinarudi ndani ya muda mfupi,” amesema Zitto.

Amewataka wananchi wa kijiji hicho kuchagua mgombea udiwani wa chama hicho ili apambane kuhakikisha tumbaku ya mwaka jana inanunuliwa.

Amesema Ilani ya Uchaguzi ya ACT -Wazalendo ilitangazwa na Taasisi ya Mviwata (Muungano wa vikundi vya wakulima) kuwa ilani bora zaidi kuhusu masuala ya kilimo kuliko ilani za vyama vyote katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 kwa kuwa ilipendekeza kuwapo kwa Hifadhi ya Jamii kwa Wakulima.

Zitto Kabwe anaonekana yupo very frustrated na hii serikali kwani alikula good times na serikali ya awamu ya nne. Nakumbuka Zitto ni miongoni mwa wanasiasa walioiingizia taifa hili hasara kwa safari za nje kwani kila msafara wa Rais wa awamu hiyo alikuwa hakosekani. Kuna kosa gani kwa serikali ya awamu ya tano kufufua shirika la ndege ATC.

Tanzania ilianza kugeuka kuwa kama Zaire kwa kuwa na mashirika ya ndege kutoka nje.
Zitto Kabwe hajui kuwa serikali ilikuwa inatumia mabilioni ya fedha kulipia watumishi wa serikali kwa kusafiri na ndege hizo kwa gharama kubwa. Je ACT Wazalendo leo ikipewa madaraka inauwezo wa kuwalipa hao wakulima bilioni 150.
 
Zitto Kabwe anaonekana yupo very frustrated na hii serikali kwani alikula good times na serikali ya awamu ya nne. Nakumbuka Zitto ni miongoni mwa wanasiasa walioiingizia taifa hili hasara kwa safari za nje kwani kila msafara wa Rais wa awamu hiyo alikuwa hakosekani. Kuna kosa gani kwa serikali ya awamu ya tano kufufua shirika la ndege ATC. Tanzania ilianza kugeuka kuwa kama Zaire kwa kuwa na mashirika ya ndege kutoka nje.
Zitto Kabwe hajui kuwa serikali ilikuwa inatumia mabilioni ya fedha kulipia watumishi wa serikali kwa kusafiri na ndege hizo kwa gharama kubwa. Je ACT Wazalendo leo ikipewa madaraka inauwezo wa kuwalipa hao wakulima bilioni 150.
Kwa hili nakukubalia asiimia 100 zito alikula bata sana la JK na jamaa wa system walimbeba mno kuwanyoosha CDM sasa ngosha acheki na masnitch ila kinadharia za uchumi ZZK mzuri sana sema ndumi la kuwili mno
 
tumbaku inayoleta kansa halafu baadae mlalamike mbona serikali hainunui madawa ya kutibu wagonjwa wa kansa, ningemuunga mkono kama angesema serikali inunue mazao ya chakula kwa wakulima
 
Huyu Zitto vipi? Sisi wananchi wa Namtumbo Ndege ndio kipaumbele chetu. ( Katika uandishi wa Team Buku Saba).
 
Kwa hili nakukubalia asiimia 100 zito alikula bata sana la JK na jamaa wa system walimbeba mno kuwanyoosha CDM sasa ngosha acheki na masnitch ila kinadharia za uchumi ZZK mzuri sana sema ndumi la kuwili mno
Lipumba je
 
Serikali inunue tumbaku yote hiyo alafu iifanyie nini??
Zito bwana!
Mashirika yanatoa ajira na Kofi kubwa kabisa ni TCC..
Wakinunua tumbaku hiyo mabilioni yanaingia katika mzunguko kunakuwa na unafuu katika maisha na wengi wanalipwa.. Wanagharamia matibabu, wanasafiri sekta ya usafirishaji inaguswa..wanalipa ada watoaji Wa hidima hiyo wanapata ..wananunua chakula walipa Umeme ..wananunu nguo mafuta ya taa nk. Kwa kifupi wengi hizo pesa zitawafikia...

Mean while serikali inatengeneza sigara..inapata faida ianendelea kuwalipa wafanyakazi Wa TCC na contracted companies zote.. Anaguza watu wengi mjini na wooote wanarusosha tena serikalini kupitia vat ..na mzunguko unaendelea
 
Serikali inunue tumbaku yote hiyo alafu iifanyie nini??
Zito bwana!
Inunue wakati inatafuta wanunuzi, kuliko ambavyo wakulima ndio wasubiri Kwani msimu wa kilimo ushaanza na wanategemea kutumia hizo fedha kufanya kilimo
 
makampuni yanayo nunua huwa yanavuta, amekwambia ifanyike mpango wa G-G serikali inunue na kuuza kwa serikali nyingine (nje ya nchi kwa wenye mahitaji)

ajakwambia inunue ikavute acha umkunduchi
Hongera kwa kumpa za uso huyo nguchiro
 
Back
Top Bottom