Zitto’s letter to Cameron over dirty Swiss billions

well alisema kuwa atawataja walioficha pesa huko nje sasa kikowapi?

aliyejidhalilisha ni yeye,

Perhaps angefocus on tax avasion inayoendelea TRA na sio kutufanya sote wajinga na watoto kwa kutoa empty statements ndani ya bunge huku akijua wazi kuwa he cant back them up
 
well alisema kuwa atawataja walioficha pesa huko nje sasa kikowapi?

aliyejidhalilisha ni yeye,

Perhaps angefocus on tax avasion inayoendelea TRA na sio kutufanya sote wajinga na watoto kwa kutoa empty statements ndani ya bunge huku akijua wazi kuwa he cant back them up
So you thought, kwamba by putting him down, utasaidia tupate hizo pesa au???
Au bora zibaki huko?
Au una fununu kuwa hazipo?(au unajua ziko wapi)

Tunadanganyawa kuwa ni wawekezaji wa nje wenye mitaji, mitaji ni yetu wenyewe, ila inatokea huko na faida unarudi huko,
Jamani basi muache sasa kuiba muwe kidogo na huruma.
Fuatilia kawa undani wawekezaji wetu utawaona tu, wachache ndio genuine KABISA, wengi wao kuna mkono wa ndugu yetu alieasi.
 
There is this sickening fact that the Tanzanian government is completely dumb on this matter, leaving Zitto to spearhead such a huge and heart-touching issue on his personal endevours!

Even that so called Parliamentary committee will end up with no tangible conclusion, just as it has been the norm of such many past committees, which are teethless.
Zitto, go ahead, do anything under yr abilities, this whole matter is branded under your name as a leading fighter, so dont let yr name be tarnished, while simultaneously nudging millions of Tanzanians out of agony!
Its better Mr Zito should forward this letter to the President of the EU, to add more weight and stimulation!!
 
You can't kill a practice without cracking down on those who engage in it. That is why I think it is important to name names, forward them to the authorities, and if they don't do anything about it then that is on them. And you can't crack down on nameless people either.

Also, by doing that (naming names) you can build a stronger case against the culture of impunity by citing specific examples of your own efforts.
Mkuu Nyani Ngabu nadhani wewe unaishi ulimwengu wa kwako sio TZ, kwani mkubwa alipopewa majina ya EPA unakumbuka alisema je??
Warudishe fedha ili wasamehewe!! Where is that money, what transpired in those transactions, cant we conclude that was the source of offshore ACCT???
Don't you know the owners of those ACCTS, nani atamfunga paka kengele kipindi hiki, kama walishindwa wakati ule????
 
I do appriciate what Mr. Zitto did but honestly this is typically impossible and some of these issues we dont need to impose politics. That is convenant for Swiss Government. Nothing can be done there.
:)
 
BAK umenisoma. Vyema lakini kwenye bandiko langu uliloliquote?

Umesoma niliposema kuwa wenzetu wamehsafanya hayo tunayoyafanyia ushabiki na ukichwa maji?

Mkuu mimi si mwanasiasa lakini siasa nazifahamu vyema.Na tatizo tulilonalo sisi watanzania ni umbumbumbu na ukichwa maji pamoja ufuata mkumbo bila hata kujitambua kwamba na sisi tuna uwezo wa kufikiri na si kushikiwa akili tu tu kama ambavyo nimekuwa nikiona toka nijiunge humu. Pamoja na maoni niliyoyaona kwenye thread hii.
Sasa wewe unaweza kuniambia serikali ya Nigeria ilichukuwa hatua kama za Zitto ndo wakapata pesa zao?

Mbona wanaijeria walizungumzia issue ya fedha zao na balozi wa uswisi aliyeko nigeria akishirikiana na serikali ya nigeria?

Sisi hizi porojo za ushabiki hazitatufikisha mahali.

Hakuna individual atakayeikomboa tanzania kama messiah!watanzania watajikomboa wenyewe.Na ukombozi huo lazima uanzie kwenye fikra.

Lakini kama akili zetu ndo hizi,basi hata tukulalamika tunastahili yote yanayotupata.

Tafadhali sana fuatilia walivyozipata hizo pesa halafu uweke hizo data hapa na tulinganishe na haya ya Zitto.

Siyo tu kusema pesa zilirudi.Tusipoenda zaidi ya hapo basi ndo ufuata mkumbo na kichwa maji.
 
Last edited by a moderator:
Alalamikia fedha za Tanzania zinavyoishia Ughaibuni kifisadi

KWA miaka mingi Tanzania imekuwa na mahusiano ya kimaendeleo na Uingereza ambayo yamekuwa na manufaa makubwa. Tanzania ni miongoni mwa nchi za Afrika zinazopata misaada mikubwa kutoka Uingereza kupitia shirika lake la kimataifa la misaada ya maendeleo (DFID).


Kwa hakika, katika miaka ya karibuni Serikali ya Uingereza imeisaidia Tanzania kuweka misingi imara ya uwajibikaji wa serikali na uwazi. Katika kufikia mafanikio hayo, nchi yako pia imelisaidia bunge letu, taasisi za umma na asasi za kiraia.
Hata hivyo, msaada huo umekuwa ukififishwa na hali ya sasa ambapo Serikali ya Tanzania imekuwa, kila mwaka, ikipoteza fedha nyingi kwa njia za udanganyifu katika ulipaji kodi na ukwepaji kodi. Kwa kiasi kikubwa udanganyifu huu katika kulipa kodi na ukwepaji kodi hufanywa na mashirika makubwa ya kibiashara duniani (Multinational Corporations); huku mengi yakiwa yamesajiliwa nchini mwako Uingereza.


Hii ni changamoto kubwa na ya muda mrefu kwa taifa letu – changamoto ambayo, kwa hakika, hufifisha juhudi zote ambazo nchi yetu imekuwa ikifanya kujenga, kuimarisha na kudumisha misingi hiyo hiyo ya uwajibikaji.


Utafiti wa hivi karibuni uliofanywa na Global Financial Integrity (GFI) unaonyesha kwamba Nchi Zinazoendelea duniani hukosa mapato kwa njia hizo ya kati ya dola za Kimarekani bilioni 858 na dola za Kimarekani trilioni 1.06 kwa mwaka.


Utafiti huo unaonyesha kwamba kwa kila dola moja ya Kimarekani inayoingizwa katika Afrika kama msaada wa kimaendeleo, dola 10 hutolewa nje ya bara hilo kwa njia hizo haramu! Na ndiyo msingi wa hoja ya wataalamu kwamba ‘bara la Afrika ni mkopeshaji mkubwa wa dunia’ kwa sababu kuna fedha nyingi za bara hilo ambazo zimefichwa katika mabenki ya Ughaibuni (offshore) zinazozidi deni lote la nje ambalo bara hilo linadaiwa. Dunia haipaswi kuvumilia uchafu huu kuendelea. Ni lazima kuukomesha mwenendo huu kwa kuvunjilia mbali michakato hii ya kisiri.


Kila mwaka nchi yangu Tanzania hupoteza dola za Kimarekani milioni 560 kupitia udanganyifu katika ulipaji kodi na ukwepaji kodi. Hicho ni kiwango kikubwa cha fedha ambazo vinginevyo zingeweza kutumika kuboresha miundombinu ya Tanzania na kuboresha sekta za elimu na afya kote nchini – mambo ambayo yangewahakikishia Watanzania wengi maisha bora zaidi.

Kiwango hiki cha pesa za mapato ya kodi ambacho Tanzania inakipoteza kingeweza kusaidia kukuza uchumi wa nchi, na hivyo baadaye kusaidia pia kupanua wigo wa kodi wa nchi yetu. Kati ya mwaka 2002 na 2008 Tanzania ilipoteza kiasi cha dola za Kimarekani bilioni 2 kupitia utoroshaji huu mchafu wa fedha nje ya nchi kupitia ukwepaji kodi, udanganyifu katika ulipaji kodi na ufisadi. Upotevu huo mkubwa wa fedha ni takriban asilimia 5 ya Pato la Taifa (GDP).


Sehemu kubwa ya fedha hizo zimo mikononi mwa asasi na mashirika ya Uingereza yaliyo chini ya British Overseas Territories and Crown Dependencies. Tanzania na nchi nyingine zinazoendelea barani Afrika zimekuwa zikipata vikwazo kukomesha ufisadi huu, kwa sababu ya kuwepo sheria za usiri za fedha (financial secrecy laws).


Lakini Serikali yako inaweza kukomesha ufisadi huu kama itachukua hatua madhubuti kufutilia mbali sheria hizo za usiri za fedha, kwa sababu kuendelea kushikiliwa fedha hizo ni kukwaza juhudi za nchi zetu za Afrika kujiletea maendeleo. Hakika, kufutiliwa mbali kwa usiri katika sheria hizo za fedha kutakuwa na matokeo chanya katika suala zima la Tanzania, na Afrika kwa ujumla, kupambana na umasikini wa watu wao.


Katika mkoa wangu wa Kigoma, Magharibi mwa Tanzania, takwimu zinaonyesha kwamba watoto 933 kati kila 100,000 hufariki kabla ya kufikisha umri wa miaka mitano. Kiwango hicho kikubwa cha vifo ni kwa sababu ya kuwepo huduma duni za afya Tanzania.


Serikali ya Tanzania haina uwezo mkubwa kifedha kuboresha huduma za afya kwa sababu ya mapato madogo ya kodi inayopata. Ukwepaji kodi na udanganyifu katika ulipaji kodi wa mashirika ya kimataifa unaoshamirishwa na mfumo huo wa usiri wa sheria za fedha, ni moja ya sababu za Serikali ya Tanzania kuwa na mapato hayo madogo ya kodi.


Ni imani yangu kwamba kama serikali za nchi tajiri za kundi la G8 zitachukua hatua ya kuweka kanuni na sheria za fedha zinazosisitiza uwazi, ufisadi huu wa kimataifa wa ukwepaji kodi na udanganyifu katika ulipaji kodi utakomeshwa, na hilo pia litaichochea nchi yangu Tanzania kuzidi kupigania uwepo wa uwajibikaji na uwazi katika masuala hayo.


Kwa upotevu huu wa kila mwaka wa asilimia 5 ya Pato la Taifa (GDP) kupitia ufisadi huo wa ukwepaji kodi na udanganyifu katika ulipaji kodi, Tanzania haiwezi tena kuendelea kupuuzia kikwazo hicho katika mapambano yake ya kukuza uchumi. Vivyo hivyo washirika wetu wa nje wa maendeleo hawawezi kuendelea kupuuzia kikwazo hicho.


Na ndiyo maana nachukua fursa hii kuupongeza uongozi wako kwa kuamua kulifanya tatizo hili la ukwepaji kodi na udanganyifu wa ulipaji kodi katika biashara za kimataifa kuwa dondoo muhimu kwa Serikali yako katika mkutano ujao wa 38 wa nchi tajiri za G8 utakaofanyika Lough Erne, Ireland Kaskazini mwezi ujao (Juni).


Ni matumainji yangu kuwa utaonyesha uwezo wako wa uongozi katika kikao hicho cha G8 kwa kuyawekea vikwazo makampuni yote ya British Overseas Territories and Crown Dependencies kwa kushiriki katika ufisadi huu wa kutuchotea mabilioni yetu ya fedha za kodi na kuyapeleka nje kwa njia hizo za ukwepaji kodi na udanganyifu katika ulipaji kodi.


Nahimiza ziwekwe sheria za kuondoa usiri kuhusu taarifa mbalimbali za akaunti zote za siri za fedha katika nchi ambazo zimekubuhu kwa kuwa kimbilio la mafisadi, wadanganyifu na wakwepakodi wakubwa duniani.


Nahimiza kuwekwe sheria za kulazimisha utoaji taarifa za akaunti hizo katika nchi zinazolinda wakwepa kodi na wadanganyifu katika ulipaji kodi - nchi zinazotambulika duniani kuwa ni tax havens.



Kama serikali ya nchi fulani ina hoja nzito ya kuamini kuwa kiasi kikubwa cha fedha kilichomo kwenye akaunti fulani katika moja ya nchi hizo kimepatikana kwa njia za ufisadi, ukwepaji kodi na udanganyifu katika ulipaji kodi, sheria lazima ilazimishe taarifa za akaunti hizo za kigeni kuwekwa wazi ili nchi husika zifanikiwe, hatimaye, kukirejesha nyumbani kiasi hicho cha fedha kilichoibwa kwa njia hizo.

Barua hii ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA), Zitto Kabwe kwa Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameroon, ilitumwa kwake wiki hii na ilitarajiwa kuchapishwa kwenye magazeti kadhaa ya nchi hiyo Jumatano. Kopi asilia ya barua hii ni katika lugha ya Kiingereza
 
Kwahiyo anatuchongea?

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom