NAMTUMBA
JF-Expert Member
- Feb 20, 2014
- 1,939
- 596
Zitto ni mfano wa masikini aliehangaika sana kutafuta Mali na baadae akafanikiwa kupata Mali na kujenga nyumba mzurii ya kifahari alafu mwishoe anasusa kuishi kwenye nyumba ile kisa maneno maneno ya watu na kujiaminisha atajenga nyingine.
Umeitwa msaliti sawa, umetukanwa sana sawa tu, Sijui oooh Zitto amehongwa mabilioni sawa, hayo ni maneno tu hata kwenye kanga yapo. Ulitakiwa kukaa kimya kama Lowassa hayo maneno yangeisha tu. Nikuulize Zitto, Hivi kuna mwanasiasa gani nchi hii ametukanwa na CHADEMA kama Lowassa, lakini CHADEMA hao hao walimshangilia Lowassa huyohuyo. Hii iliwezekana tu baada ya kupatikana ukweli. Hata wewe unaweza kuwa kama Lowassa ndani ya CHADEMA.
Una nia mzuri kwa taifa hili lakini unapitia njia ndefu sana. Ni kama vile unaenda Kigoma unaamua kupitia Mtwara, Songea, Mbeya, Mpanda ndo ufike Kigoma wakati kuna njia fupi. Sikukatishi tamaa la hasha ila napenda juhudi zako na malengo kwa taifa hili yatimie kabla nguvu zako za ujana wako hazijaisha. Mafanikio yako unayachelewesha wewe mwenyewe either kwa kutokujua au washauri wako wanakushauri vibaya.
Kama CHADEMA wamempokea Lowassa waliemsema nchi mzima kwanini Zitto asipokelewe tena kwa furaha na vifijo. Hivi ni mzazi gani atamkataa mwanae arudipo nyumbani.
Choonde choonde Zitto rudi nyumbani kwenye nyumba yako uliyoijenga kwa nguvu zako, Usisikilize maneno ya kwenye kanga ambayo wanafiki wataongea. Njia sahihi yakufikia mafanikio yako kwa wakati ni kupitia CHADEMA chama ulichokijenga kwa nguvu. Huko ACT unazunguka sana na unachelewa sana.
Rudi nyumbani Zitto, CHADEMA inakuhitaji sana kipindi hiki kuliko wakati mwingine wowote ule katika siasa za upinzani wa Nchi hii. Ndoto zitatimia CHADEMA na si mahali pengine popote.
Asanteni kwa kusoma
Naomba samahani kwa kutaja majina ya watu ila nimetaja kwa lengo la kufikisha ujumbe. Naamini sijamchafua mtu yoyote.