Zitto: Polisi Nyamongo hupewa kitu kidogo kuruhusu wananchi kuingia kuiba mawe

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
234
WanaJF:
Hii ni sehemu ya habari kuu katika gazeti la T. Daima la leo Jumapili, na nimekiweka kipande hiki kutokana na kauli ya Mh Zitto hasa hapo kulikoonyeshwa kwa rangi nyekundu. Kama ni kweli polisi wa mgodi wanafanya vitendo vya namna hiyo, kwa nini tena baadaye waamue kuwatwanga askari wananch wanaoingia kuiba mawe?

Serikali ya CCM ingefaa kuchukuwa ushauri wa LHRC na kuufunga mgodi huo, angalau kwa muda ili masuala yote haya yachunguzwe kwa ajili ya kupatikana ufumbuzi wa kudumu.

Kwani serikali inachopendelea kufanya yanapotokea haya (kufuatana na kauli ya baadhi ya wafiwa wa walew waliouawa mgodini wiki iliyopita - soma stori nyingine ktk pg 3 ya gazeti hilo hilo) ni kwamba badala ya kuunda tume, wakubwa hupendelea "kufanya ziara za mara kwa mara ndani ya mgodi huo, ziara ambazo hazina tija."

Kwa maoni yangu, wanapotembelea mgodi huo (na ile mingine) hupewa vipande vya dhahabu na kuondoka, na kusahau kabisa kutatua migogoro inayowaletea wananchi wa maeneo hayo adha kubwa.

__________

CHADEMA yaikaanga serikali

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimehitimisha ngwe nyingine ya maandamano ya amani kuishinikiza serikali iboreshe maisha ya wananchi, kikielekeza mashambulizi kwa viongozi na watendaji wa serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwamba wanasababisha vifo na maisha magumu kwa wananchi………………………..


……………………….Naye Zitto alimvaa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Hamis Kagasheki, akimtaka kukiri kuwa serikali inahusika na mauaji ya raia yaliyotokea katika mgodi wa Nyamongo wilayani Tarime, mkoani Mara.

Zitto alitoa kauli hiyo jana mkoani Mwanza ambapo alisema Kagasheki, hawezi kukwepa lawama kwani polisi ndio waliohusika kuwaua kwa risasi raia wasio na hatia na si chama cha siasa alichokituhumu.

Alisema anazo taarifa kwamba askari polisi wanaolinda mgodi huo wa Nyamongo wamekuwa wakipewa kitu kidogo kisha kuruhusu watu kuchukua mawe.

"Namshangaa Naibu Waziri Kagasheki kutuhumu chama cha siasa kwa mauaji haya. Polisi isikwepe lawama kwa hili. Inakuwaje polisi impige risasi mtu anayekimbia?" alihoji.


Alisema mtu anayekimbia ana lengo la kusalimisha maisha yake, kwa hiyo hakukuwa na sababu za kufyatuliwa risasi.

Alibainisha kuwa matukio ya polisi kuua raia yanalipaka matope taifa katika uso wa dunia, jambo ambalo kwa namna moja au nyingine linaweza kuwakimbiza watalii.

Zitto aliitaka Polisi na serikali kuacha kuwapotosha Watanzania kwamba CHADEMA imeingiza mkono kwenye mauaji hayo badala yake serikali itekeleze ushauri wa Kamati ya Madini ya mzee Bomani kutoa asilimia 20 ya fedha………………………….


Chanzo: T. Daima Jumapili
 
nilimsikiliza kagasheki nilifadhaika sana..yaani alikuwa analalamika as if hicho alichokiita chama cha siasa ndo kimeuwa hao watu..kwanza mi siamini eti watu 1200 wamevamia pit kwenda kuiba mawe? najaribu kufikiria sana hii sielewi...
 
nilimsikiliza kagasheki nilifadhaika sana..yaani alikuwa analalamika as if hicho alichokiita chama cha siasa ndo kimeuwa hao watu..kwanza mi siamini eti watu 1200 wamevamia pit kwenda kuiba mawe? najaribu kufikiria sana hii sielewi...


Hata mie siamini hilo. Serikali huongeza idadi ili kuonyesha kwamba polisi walizidiwa na hivyo kuhalalisha matumizi ya risasi. Ni serikali ya ki-mauaji tu.
 
Na ndiyo maana serikali haitaki kabisa kuunda Tume kuchunguza suala hili na mengineyo yaliyotokea. Haitaki, sijui kwa nini.
 
serikali na hizo tume zao ni vijiwe vya kulipiana extra money tu afu report zenyewe wanatupa kapuni ka ni kuchunguza wapewe hiyo kazi wataalamu huru na wala wasiwe wafanyakazi wa serikali sababu wao wanalinda ugali wao serikali
TUME = TUMECHOKA
 
hii serikali iondoke madarakani, hata mubarak alikuwa na roho ngumu hivi hivi sembuse kina kagasheki?
 
inabidi tufanye juu chini tumlete yule mwendesha mashitaka wa umoja wa mataifa bwana O Campo aje kuwafungulia mashitaka viongozi wa jeshi la polisi na askari wao wanao ua raia bila hatia maana huku kwetu mahakama zetu kutokana na kukiogopa chama cha magamba hawawezi kuwahukumu wote wanaotuhumiwa na mauaji ya raia wasio kuwa na hatia maeneo mbali mbali ya nchi yetu.
 
Na ndiyo maana serikali haitaki kabisa kuunda Tume kuchunguza suala hili na mengineyo yaliyotokea. Haitaki, sijui kwa nini.
na afadhali hata wasiunde tume maana huishia kula hela za Watanzania na wala hawana la maana wasemalo! Kwa huu mtindo! tutafika tu!
 
Back
Top Bottom