Zitto omba radhi watanzania yaishe

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,289
12,582
Kama ilivyo kwa nchi nyingine kama za Ulaya, Marekani, Asia na Afrika zilizoendelea, Tanzania pia tunahitaji chama tawala kama CCM na vyama vya upinzani kama Chadema, CUF, NCCR, TLP,..... vyenye nguvu ili kuchagiza sera mbovu za vyama tawala na kuchochea maisha yenye ahueni kwa wananchi. Hivyo watanzania kwasasa tunaihitaji Chadema na CCM pamoja kama ilivyo kule Marekani wanavyohitaji Democrat na Republican pamoja, Uingereza wanavyohitaji Labour na Conservative kwa wakati mmoja, Ujerumani wanavyohitaji CDU, SDP na SSU na kwingineko kwingi kwenye maendeleo ya kweli.

Wananchi wengi hawana haja na vyama vya siasa ila wanachohitaji ni maisha bora, na maisha bora hayawezi kuletwa na chama kimoja tu kinachotawala, lazima kuwe na vyama shindani ambavyo vina uwezo wa kuingia Ikulu wakati wowote kama chama tawala kitakosea ama kuzembea katika kuwaletea maisha yenye unafuu wananchi wote wa dini, elimu, rangi, umri, afya zote, na ngazi zote toka vijijini hadi mijini. Hii ina maana kuwa watanzania wote tunaihitaji CHADEMA yenye nguvu hata kama haiko Ikulu. Chama tawala kinapokuwa kinajirekebisha kwa kuogopa chama kingine kisije kikawabwaga kwenye chaguzi mbalimbali wanaonufaika ni watanzania wote bila kujali itikadi zao za vyama vya siasa wala za dini. Hata viongozi wa chama tawala mmoja mmoja nao pia huwa wananufaika na uwepo wa vyama vya upinzani vyenye nguvu kwakuwa hata wao pia wanao ndugu, majirani na marafiki waliotawanyika nchi nzima ambao wanahitaji maisha yenye nafuu pia ambayo hawawezi wote kuyapata kutoka kwao hata kama wao ni viongozi wa chama tawala. Hivyo, kuleta mtafaruki kwa vyama vya upinzani ili visiimarike ni kuwakosea wapwa zako, binamu, shangazi, wajomba, dada, kaka, baba mdogo, wajukuu, mashemeji na watanzania wote kwa ujumla ambao wanahangaika kupata maisha nafuu ndani ya nchi yao.

Kambi ya Zitto imekiri kuhusika na waraka ule wa siri wenye lengo la kuuangusha uongozi halali wa chadema, kosa kama hili ni kosa hata kama lingekuwa limetokea kwa vyama vya CCM, Democrat, Republican, Labor, Conservative, Jubilee, CDU, SSU, SDP, n.k. Tusimung'unye maneno hapa, Zitto na wenzake wamekosea, wamewakosea viongozi wenzao wa chadema, wanachama na watanzania wote kwa ujumla wanaonufaika kwa nja moja au nyingine na uwepo wa vyama vingi nchini.

Kinachotakiwa Zitto na wenzake wenye waraka ule wasimame jukwaani na kuomba radhi kwa kilichotokea, na watanzania wawe tayari kuwasamehe, kisha tutawafuatilia nyendo zao kila kona kila dakika. Ninaimani wanaonufaika na vyama vingi wako wengi kuanzia vijijini hadi mijini, mitaani hadi Ikulu, sungusungu hadi JWTZ, na vyombo mawasiliano vyote, watakosa kwa kujifisha tu. Watumie njia za wazi kutaka mabadiliko CHADEMA wataungwa mkono tu na wapenda demokrasia ndani ya chama. Kutenda kosa sio kosa ila kurudia kosa. Ujenzi wa vyama vya upinzani sio jambo rahisi hata nyakati zile za utawala wa Warumi na wakoloni, wapo watu wamepoteza maisha, mali, muda, wake, waume, watoto, damu, kupigwa, na kubezwa, kushitakiwa na kutiwa gerezani. Kuvihujumu vyama vya upinzani kwa aina na sababu yoyote ile ni kujihusisha na dhambi kubwa ambayo itagharimu historia ya maisha yako, familia na uko wako mzima.

Ana maana na heri ya mtu yule aliyepanda mti mmoja tu wa kivuli utakaoishi zaidi ya miaka 100 kuliko mtu mwenye mabilioni ya hela haramu asiyeweza kuishi nayo hata kwa miaka 30 mingine.

Inshallah chadema itaendelea kusimama na kuendelea kufanya kazi ya checks and balance kati ya watawala na watawaliwa
 
mkuu, acha mahaba na mbowe na kushindwa kuona mapungufu yake - lengo la waraka lilikuwa ni kwa ajili ya maandalizi ya uchaguzi HALALI ndani ya chama, sasa wewe unatuaminisha habari za mapinduzi wapi na wapi......nakushauri uusome vizuri ukiwa umetulia, tena soma na waraka mwingine uliokuwa wa chacha wangwe (r.i.p) kisha tumia akili huru kuchanganua kama hutaona tatizo kwa mbowe! zinatumika mbinu zilezile kukabiliana na anayempinga - simply kuwaaminisha wanachadema kwamba wanaompinga ni wasaliti, wahaini nk........jitaidi uusome tafadhali.
 
Mkuu Zitto alishaomba radhi tangu mwaka jana kwenye ishu ya masalia, lakini si unajua tena kawaida ya wanafiki! Let him go
 
Ni kweli kabisa kama kweli Zito ni mwanasiasa mkomavu na ana mapenzi mema na CDM inabidi aombe radhi hadharan, ili kukijenga chama na kushusha hiki kijoto kisicho cha lazima!

sometimes kujifanya mjinga hakumaanishi umekuwa mjinga.....
 
Mnyika akiwa anahojiwa pale Mlimani radio alisema hivi,ukiona CDM leo imefikia kuchukua uamuzi wa hivi kwa mwanachama ama kiongozi wake ni kwamba tayari huko nyuma yameshatokea makosa na tayari kwa nyakati tofauti watu wanakuwa washaitwa,kuonywa na kukanywa bila mafanikio ..kwahiyo ieleweke,kila jambo lazima lifike liwe na mwisho kwa hari yoyote ile,thus,such people must face whichever is set.
 
Zito hawezi kuiomba radhi mara mbili. Dr. Kitila alimsafisha kuwa hausiki na huo waraka, leo mnataka aombe radhi. Kwa kosa gani alilofanya? Issue hapa ni kwenda kwenye uchaguzi mkuu. Mnatuweka tusio na makundi mahali pabaya. Fahamu Zito akiondoka, chadema hakitakufa, lakini kitapukuchika sana. Vile vile Mbowe akiondoka Chadema hakitakufa bali kitapukuchika sana. Kama lengo ni kutetea Chadema isonge mbele, kwa nini viongozi wasikae wayamalize haya? Itisheni basi Mkutano mkuu wajieleze, hamtaki! Mimi nadhani viongozi wa Chadema na hasa mwanasheria wao Tundu Lisu hawana nia njema na Chadema. Yatosha.
 
Kambi ya Zitto imekiri kuhusika na waraka ule wa siri wenye lengo la kuuangusha uongozi halali wa chadema, kosa kama hili ni kosa hata kama lingekuwa limetokea kwa vyama vya CCM, Democrat, Republican, Labor, Conservative, Jubilee, CDU, SSU, SDP, n.k. Tusimung'unye maneno hapa, Zitto na wenzake wamekosea, wamewakosea viongozi wenzao wa chadema, wanachama na watanzania wote kwa ujumla wanaonufaika kwa nja moja au nyingine na uwepo wa vyama vingi nchini.

Kinachotakiwa Zitto na wenzake wenye waraka ule wasimame jukwaani na kuomba radhi kwa kilichotokea, na watanzania wawe tayari kuwasamehe, kisha tutawafuatilia nyendo zao kila kona kila dakika. Ninaimani wanaonufaika na vyama vingi wako wengi kuanzia vijijini hadi mijini, mitaani hadi Ikulu, sungusungu hadi JWTZ, na vyombo mawasiliano vyote, watakosa kwa kujifisha tu. Watumie njia za wazi kutaka mabadiliko CHADEMA wataungwa mkono tu na wapenda demokrasia ndani ya chama. Kutenda kosa sio kosa ila kurudia kosa. Ujenzi wa vyama vya upinzani sio jambo rahisi hata nyakati zile za utawala wa Warumi na wakoloni, wapo watu wamepoteza maisha, mali, muda, wake, waume, watoto, damu, kupigwa, na kubezwa, kushitakiwa na kutiwa gerezani. Kuvihujumu vyama vya upinzani kwa aina na sababu yoyote ile ni kujihusisha na dhambi kubwa ambayo itagharimu historia ya maisha yako, familia na uko wako mzima.

hamna uchaguzi unaofanyika bila kuwa na strategy za ndani. Kuuondoa uongozi halali wa chama kwa njia ya uchaguzi kuna kosa gani?

CHADEMA is a looser, and you will pay for it. bado sura ya udini hamjaiondoa mmeanza ukanda. mimi ntaendelea kumchagua mbunge wangu Mnyika wherever I will be, I will travel all the way back to Nkurumah to vote for him as much of the UDSM alumns will be doing the year 2015, but I tell you mmepotea njia and gone stray . mnafanya CCM ku-take opportunities hambazo hata hawakutegemea

you are lost and I will never vote for your presidential candidate
 
au aachane na cdm na aanzishe chama au ajiunge na vyama vingine kwani pale cdm hatakuwa huru
 
........Kinachotakiwa Zitto na wenzake wenye waraka ule wasimame jukwaani na kuomba radhi kwa kilichotokea, na watanzania wawe tayari kuwasamehe, kisha tutawafuatilia nyendo zao kila kona kila dakika. ........

Fukuza mbali
Zitto hakuna mtu mwenye mda wa kukaa kufuatilia tena nyendo zake wakati tulishafuatilia toka anaanza mawasiliano na TISS Chadema ikapuuzia na sasa mchawi amebainika, mimi naamini kumuacha Zitto ndani ya chama ni hatari sana, mtu anayewetongozeka na TISS kama katoto kashule masikini kanavyotongozeka kwa Chips
 
Last edited by a moderator:
mkuu, acha mahaba na mbowe na kushindwa kuona mapungufu yake - lengo la waraka lilikuwa ni kwa ajili ya maandalizi ya uchaguzi HALALI ndani ya chama, sasa wewe unatuaminisha habari za mapinduzi wapi na wapi......nakushauri uusome vizuri ukiwa umetulia, tena soma na waraka mwingine uliokuwa wa chacha wangwe (r.i.p) kisha tumia akili huru kuchanganua kama hutaona tatizo kwa mbowe! zinatumika mbinu zilezile kukabiliana na anayempinga - simply kuwaaminisha wanachadema kwamba wanaompinga ni wasaliti, wahaini nk........jitaidi uusome tafadhali.

maamdalizi gani harari ya kuwachafua wengine,maandalizi gani ya kuwatumia ccm kufanikisha mpango wao haramu,kama wangejenga hoja kwa wanachama ili wakubalike hayo ndo maandalizi harari,wewe kusema viongozi waliopo wameshindwa ni kweli? wamekitoa chama nafasi ya 4 mpaka kuwa chama kikuu cha upinzani wakikiandaa kuingia ikulu wanasema hawajafanya lolote ,tatizo ni mapepo na vidonyo mnavyotembea navyo mfukoni
 
hamna uchaguzi unaofanyika bila kuwa na strategy za ndani. Kuuondoa uongozi halali wa chama kwa njia ya uchaguzi kuna kosa gani?

Chadema is a looser, and you will pay for it. Bado sura ya udini hamjaiondoa mmeanza ukanda. Mimi ntaendelea kumchagua mbunge wangu mnyika wherever i will be, i will travel all the way back to nkurumah to vote for him as much of the udsm alumns will be doing the year 2015, but i tell you mmepotea njia and gone stray . Mnafanya ccm ku-take opportunities hambazo hata hawakutegemea

you are lost and i will never vote for your presidential candidate

pm7 + mkakati...2013= let him go,
 
Katika kosa ambalo Chadema watalifanya basi ni kumsamehe Zitto Kabwe...hakika huyu mtu atawasumbueni hadi siku mnaizika rasmi Chadema kaburini.

Ushauri wangu kwa Chadema: mufanye mnavyojua lakini hakikisheni mnaachana na Zitto kwa hekima na busara.

Ushauri wangu kwa Zitto: kama wewe ni maarufu na mwanasiasa kijana na unayependwa na watu wote basi siyo mbaya ukianzisha chama chako au nenda jiunge CCM maana wao wanakupenda sana kushinda unavyopendwa na mama yako mzazi
 
Zito hawezi kuiomba radhi mara mbili. Dr. Kitila alimsafisha kuwa hausiki na huo waraka, leo mnataka aombe radhi. Kwa kosa gani alilofanya? Issue hapa ni kwenda kwenye uchaguzi mkuu. Mnatuweka tusio na makundi mahali pabaya. Fahamu Zito akiondoka, chadema hakitakufa, lakini kitapukuchika sana. Vile vile Mbowe akiondoka Chadema hakitakufa bali kitapukuchika sana. Kama lengo ni kutetea Chadema isonge mbele, kwa nini viongozi wasikae wayamalize haya? Itisheni basi Mkutano mkuu wajieleze, hamtaki! Mimi nadhani viongozi wa Chadema na hasa mwanasheria wao Tundu Lisu hawana nia njema na Chadema. Yatosha.

Kwa nini magamba wote wanashabikia zitto asamehewe? nadhani wanataka wapate nafuu katika chaguzi zijazo kutokana na usaliti wake na vibaraka vyake.LAZIMA AFUKUZWE TU!
 
hamna uchaguzi unaofanyika bila kuwa na strategy za ndani. Kuuondoa uongozi halali wa chama kwa njia ya uchaguzi kuna kosa gani?

CHADEMA is a looser, and you will pay for it. bado sura ya udini hamjaiondoa mmeanza ukanda. mimi ntaendelea kumchagua mbunge wangu Mnyika wherever I will be, I will travel all the way back to Nkurumah to vote for him as much of the UDSM alumns will be doing the year 2015, but I tell you mmepotea njia and gone stray . mnafanya CCM ku-take opportunities hambazo hata hawakutegemea

you are lost and I will never vote for your presidential candidate

Hiyo kura yako moja kawape magamba wenzio.sisi tuliopo field tutaendelea kutoa elimu ya uraia huku vijijini kwa mtu mmoja,vikundi vya watu na hata misibani ili tu kuhakikisha ushindi unapatikana 2015.Mamluki saa zao zinahesabika na vijana wa cdm tupo imara.VIVA CDM
 
Mpwa wangu Zitto una asili ya uasi ambao hauna maana .Uasi uko katika damu .Ulianza na akina Shonza ukaomba msamaha watu walikuwa wanaku vumilia .Sasa yamekufika na si ajabu hata Mkumbo alikuwa ana ku fix ili wakuondoe maana Kitila kaweli anaweza kukaa akawa na mawazo ya chini namna hii ? Omba msamaha ila ujue hutaaminika tena kwa tabia zako za majungu
 
Katika kosa ambalo Chadema watalifanya basi ni kumsamehe Zitto Kabwe...hakika huyu mtu atawasumbueni hadi siku mnaizika rasmi Chadema kaburini.

Ushauri wangu kwa Chadema: mufanye mnavyojua lakini hakikisheni mnaachana na Zitto kwa hekima na busara.

Ushauri wangu kwa Zitto: kama wewe ni maarufu na mwanasiasa kijana na unayependwa na watu wote basi siyo mbaya ukianzisha chama chako au nenda jiunge CCM maana wao wanakupenda sana kushinda unavyopendwa na mama yako mzazi

Nakuunga Mkono kwa asilimia zote.Zitto ni wakumtosa kabisa.Kwanza anajifanya Superster na hana ushirikiano na wenzake.
 
Back
Top Bottom