Zitto njia panda | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zitto njia panda

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by JoJiPoJi, Mar 22, 2010.

 1. JoJiPoJi

  JoJiPoJi JF-Expert Member

  #1
  Mar 22, 2010
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 2,460
  Likes Received: 1,334
  Trophy Points: 280
  • Akabiliana na shinikizo kutoka Kigoma, Geita

  UAMUZI wa Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, kutangaza azma yake ya kufanya kile alichokiita utafiti wa kujua ni jimbo gani agombee kati ya matano aliyoyaainisha unaonekana kumuweka katika mazingira magumu kisiasa; Tanzania Daima limebaini.

  Majimbo hayo matano ambayo tayari yanaonekana kuanza kumgonganisha kichwa Zitto kwa upande mmoja na viongozi na wanachama wa kawaida wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa upande mwingine ni Geita, Kahama, Kigoma Kaskazini, Kigoma Mjini na Kinondoni.

  Matukio ya hivi karibuni yanayoweza kumuweka njia panda Zitto ni lile la kuwapo kwa taarifa za vyombo vya habari zinazoonyesha kuwapo kwa shinikizo kutoka kwa wazee wa Kigoma anakotoka mwanasiasa huyo kijana la kumtaka aachane na mipango yake ya kutaka kugombea jimbo lolote nje ya mkoa huo.

  Habari iliyoandikwa na gazeti moja la kila siku (siyo Tanzania Daima) ambalo kwa muda mrefu sasa limekuwa na mwelekeo wa kumjenga kisiasa Zitto zinaeleza kuwa wazee wa Kigoma wameshtushwa na hatua ya kijana wao huyo kuanza kusaka jimbo la kugombea.

  Wakati wazee wa Kigoma wakitoa tamko hilo, habari kutoka Geita zinaeleza kuwa wakazi wa eneo hilo wameanza kuchangishana fedha zinazofikia sh 50,000 zitakazomwezesha Zitto kuchukulia fomu za kugombea huko.

  Katibu wa CHADEMA wilayani Geita, Rogers Luhega, aliliambia Tanzania Daima kwa njia ya simu jana kuwa uamuzi wa kumtaka mwanasiasa huyo kugombea ubunge kwao ulijadiliwa katika kikao cha Kamati ya Utendaji cha jimbo hilo kilichoketi hivi karibuni.

  Luhega alisema uamuzi wa kumpendekeza Zitto kuwa mgombea pekee wa ubunge katika jimbo hilo uliwasilishwa ofisini kwake kwa njia ya barua iliyokusanya maoni ya wana CHADEMA kutoka kata 11 zilizomo jimboni humo.

  “Haya ni maombi ya kata zote zilizopo Geita ambazo zilifikia uamuzi huo Machi 14 mwaka huu na kutoa mapendekezo haya ambayo pamoja na mambo mengine yanataka Zitto ateuliwe kuwa mgombea pekee,” alisema.

  Alibainisha kuwa kutokana na maombi hayo, CHADEMA wilaya imeshamuandikia barua Zitto, yenye kumbukumbu namba CDM/GT/2010 ikimjulisha kile kilichopendekezwa na wanachama.

  Akizungumza kwa simu na Tanzania Daima jana, Zitto alikiti kupokea barua hiyo na mara moja akawataka wana CHADEMA hao wa Geita kuwa na subira.

  “Tayari nimeipokea barua ya kuombwa kuwa mgombea pekee nafasi ya ubunge jimbo la Geita mjini kupitia CHADEMA, nafurahi kwa heshima hii, siwezi kukataa lakini ninachowaomba wakazi wa Geita ni kuwa na subira ili nikamilishe taratibu zote ndani ya chama,” alisema Zitto.

  Zitto alisema jambo hilo ni kubwa na si busara kulitolea kauli au uamuzi katika kipindi hiki ambacho bado hajaamua ni jimbo gani anapaswa kuwania ubunge.

  Alibainisha kuwa alikuwa akikusudia kutoa uamuzi wake Jumamosi hii ya Machi 27 wakati wa mkutano wa Kamati ya Utendaji ya CHADEMA uliopangwa kufanyika mkoani Dodoma.

  Jimbo la Geita ambalo linaongozwa na Ernest Mabina kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwa kipindi cha miaka 10 katika siku za hivi karibu limeonekana kuwa na ushindani mkubwa kati ya CCM na CHADEMA.

  Umaarufu wa Zitto katika majimbo ya Geita na Kahama yenye utajiri wa dhahabu, kwa kiwango kikubwa yalijengwa tangu mwanasiasa huyo alipoibua kashfa ya mkataba wa madini wa Buzwagi miaka mitatu iliyopita.

  Hata hivyo, nafasi ya Zitto kutoa uamuzi huo Jumamosi hii ni finyu kutokana na chama hicho kufikwa na msiba wa kiongozi wake wa juu, Mzee Christopher Ngaiza, aliyefariki Nairobi, Kenya mwishoni mwa wiki.

  Hatua ya Zitto kulazimika kusaka jimbo la kugombea na hususan ule wa kuonekana akibadili uamuzi wa kuendelea kugombea Kigoma Kaskazini umekuwa ukichochewa na mabadiliko ya hali ya hewa kisiasa kwa upande wake.

  Kiongozi mmoja wa CHADEMA aliyezungumza na gazeti hili alisema, suala la Zitto kubadili mwelekeo wa kutaka kuendelea kuwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini kulianza kujengwa miaka takriban mitatu iliyopita alipokaririwa na gazeti hili akisema alikuwa hana mpango wa kugombea ubunge mwaka 2010.

  Tamko hilo la Zitto ambalo liliibua mshtuko mkubwa ndani na nje ya CHADEMA, lilifuatiwa na lile lililotolewa bungeni na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, akimtaka mbunge huyo kijana kuwa makini asije akashtukia amepoteza jimbo hilo.

  Kumbukumbu zinaonyesha kuwa Pinda alitoa tamko hilo siku chache tu baada ya kufanya ziara mkoani Kigoma ambako pamoja na mambo mengine alizindua barabara muhimu inayopita katika Jimbo la Kigoma Kaskazini.

  Mbali ya hayo, kuwapo kwa taarifa kwamba moja ya kata muhimu yenye wapiga kura 15,000 ya Mwandiga iliyoko katika Jimbo la Kigoma Kaskazini itahamishiwa katika jimbo la Kigoma Mjini, kumekuwa kukitajwa hata na Zitto mwenyewe kuwa sababu iliyomfanya afikirie mara mbili mbili kurejea huko.

  Kuhamishwa kwa kata ya Mwandiga yenye wanachama wengi wa CHADEMA kwenda Kigoma Mjini kumewafanya wengi kuanza kuona nafasi ya kijana wao kuendelea kuwa mbunge ikihamia pia katika jimbo hilo.

  Hata hivyo, habari zinaeleza kuwa, Zitto mwenyewe amekuwa akisita kugombea Jimbo la Kigoma Mjini kutokana na kukwepa kujiingiza katika mzozo wa kisiasa na Mbunge wa sasa wa CCM, Peter Serukamba, ambaye wana uhusiano wa kihistoria wa kifamilia.

  Mkanganyiko huo, habari zinaeleza, ulimfanya mwanasiasa huyo aamue kimsingi kulipa jimbo la Kinondoni chaguo lake la kwanza na kuyaacha mengine manne yakifuatiwa kutegemea na upepo wa kisiasa utakavyovuma.

  Source: Tanzania Daima
   
 2. Felixonfellix

  Felixonfellix JF-Expert Member

  #2
  Mar 22, 2010
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 1,680
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Tunasubiri tamko lake wakati muafaka ukifika
   
 3. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #3
  Mar 22, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,579
  Likes Received: 3,882
  Trophy Points: 280
  Kweli hapa pagumu, but I still think angegombea kule kule kwa awali, bado anaweza kutumikia kwingineko
   
 4. M

  Msharika JF-Expert Member

  #4
  Mar 23, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 936
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Zitto, make a wise decision, forget not where you came from. Unless otherwise you will loose
   
 5. Bonnie1974

  Bonnie1974 JF-Expert Member

  #5
  Mar 23, 2010
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 407
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Bwana Mdogo is too ambitious.
   
 6. M

  Mzee Kibiongo JF-Expert Member

  #6
  Mar 23, 2010
  Joined: Jun 18, 2008
  Messages: 241
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Bado hajakomaa huyu!!!!!!!! Naona utoto bado unamsumbua. Period.
   
 7. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #7
  Mar 23, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  jamani labda kuna kitu ameona huko anakotaka kukimbilia ...
  lakini viongozi wengi wanapenda sana kukaa Jijini na kutusahau sisi wananchi wao
   
 8. T

  TANURU Senior Member

  #8
  Mar 23, 2010
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 162
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Popote pale atakapogombea HAWEZI KURUDI BUNGENI. Labda ajifariji kwa kumsindikiza JK kwenye Urais.
   
 9. Felixonfellix

  Felixonfellix JF-Expert Member

  #9
  Mar 23, 2010
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 1,680
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  bungeni atarudi tu hata kama sisiemu hawataki
   
 10. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #10
  Mar 23, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Mtaka mawili hukosa yote kama anakubalika nyumbani kwa nn asigombee huko huko nyumbani unaweza kuja huku mafisadi wakakufanyizia ukashangaa unadondokea pua maana anaposema anapima upepo siku hizi kuna wapiga kura wanafiki watakudanganya wanakupenda kumbe zuga tu mara chaliiiiii CCM wamechukua unaanza kulalamika nenda nyumbani tu.
   
 11. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #11
  Mar 23, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 218
  Trophy Points: 160
  Crap...

  Tuambie wewe utu uzima wako unakuwaje? mtu yeyote anaweza kuamua kugombea jimbo lolote analotaka -nakushangaa wewe unayejiita mtu mzima unatema pumba kiasi mtu anaweza kujua mtoto ni yupi.

  Cha msingi atafuata chama chake kitapendekeza nini, wazee wa huko kwao watapendekeza nini, watu wa karibu yake pamoja na familia kwa ujumla watapendeleza nini , atafanya tathimni then atakuja na majibu yake kwetu. sasa utoto wake upo wapi?

  Be serious kama huwezi kuchangia acha, siyo unaleta pumba bila justificaction yoyote ile au kibiongo kinakukosesha busara?
   
 12. M

  Mzee Kibiongo JF-Expert Member

  #12
  Mar 24, 2010
  Joined: Jun 18, 2008
  Messages: 241
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hata ukihamaki kiasi gani kama unavyoonekana, huyu hana maamuzi yanayostahili. Ataangukia pua asipokuwa makini. Bora arudi kwao akagombee kwa kuwa bado anakubalika. Mshika mawili...........jaza mwenyewe. Nakwambia kama wewe unayejibu hapa nawe bado una mawazo kama ya Zito, basi wote watoto tu. Pumba ni zako mwenyewe. Usinihukumu na kuniambia nikae kimya, who are you to me ?

  Nina uhuru wa kuchangia na kama unakereka basi kajitundike. I will never say YES where I am supposed to say NO. That is my principle. By the way, does Zitto even know you ? Kwenda zako.
   
 13. Celebrity

  Celebrity Member

  #13
  Mar 24, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 66
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Acha hasira rafiki yako KIMEO siku hizi
   
 14. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #14
  Mar 24, 2010
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,297
  Likes Received: 601
  Trophy Points: 280
  Hakuna cha njiapanda wala nini, akigombea Kigoma mjini ushindi ni zaidi ya 60%
   
 15. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #15
  Mar 24, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 218
  Trophy Points: 160
  Hakuna hasira hapa, wewe na mwenzako Kibiongo leteni points za maana za kumwita Zitto ni Mtoto - wewe na jamaa yako mna akili za kwenye kikombe cha uji.
  Unless mje na full page ku -justfy utoto wake otherwise i don't have time to waste with crap people.
   
 16. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #16
  Mar 24, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 218
  Trophy Points: 160
  Great Thinkers!....
   
 17. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #17
  Mar 24, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,579
  Likes Received: 3,882
  Trophy Points: 280
  loosers bwana! ulishachemka mkuu kibiongo
   
 18. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #18
  Mar 24, 2010
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,068
  Trophy Points: 280
  Lakini kama ile nia yake ya kutogombea/kuachana na ubunge bado ipo, then hii ya kugombea jimbop jingine inaweza kuwa good exit plan kwake na kwa Chadema. Jimboni kwake tayari Chadema imeshajenga jina (kupitia Zitto), hivyo kuna uwezekano hata wakiweka mtu mwingine wa Chadema atashinda (kwa imani kuwa wapiga kura wa Kigoma watachagua chama na si mtu). Kwa kugombea jimbo jingine ambako Chadema hawana nguvu, bado anaweza kushinda kwa kutegemea 'umaarufu' aliokwisha jijengea (kwa imani kuwa wapiga kura wa jimbo husika watachagua mtu na sio chama). .
   
 19. Drifter

  Drifter JF-Expert Member

  #19
  Mar 24, 2010
  Joined: Jan 4, 2010
  Messages: 1,968
  Likes Received: 669
  Trophy Points: 280
  Somo zuri nililopata ni jinsi tulivyopiga hatua katika nyanja ya demokrasia. Kwamba hata ubunge au uwakilishi kwa ujumla unaweza kunadiwa popote. Kwa mfano, sisi tulioko mahali huko kusini nyanda za juu tukivutiwa na utendaji wa mtu kama Zitto twaweza kumkodi atuwakilishe Bungeni bila taabu hata kama haishi wala hajawahi kuwa na makazi kwetu. Hapo hatuna budi kujipongeza Watanzania. Jirani zetu hawana jeuri hiyo. At least one more thing to be proud of in this blessed country of ours.
   
 20. A

  August JF-Expert Member

  #20
  Dec 9, 2017
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,505
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  Baada ya Anna Mgwirha, Prof Kitila na wengineo kutoka ktk Chama cha ACT, na baada ya Zitto kuikimbia CDM, na kuinanga Serekali ya Awamu ya 5 , kwa kumnyima mahali pa kumi milia kama kamati za Bunge , sasa hivi Zitto yupo ktk njia panda arudi au aende wapi Kwa Tadea ya Shibuda, Kwa Mbowe au Kwa Magufuli?
   
Loading...