Zitto: Nilichukua kadi ya CHADEMA mwaka 1993, Wakati wengine wakiwa bado CCM

Status
Not open for further replies.

Mandla Jr.

JF-Expert Member
Dec 15, 2013
3,100
1,195
Wadau wa JF!
Nimefurahishwa na kauli aliyoitoa Mbunge wa Kigoma Kaskazini mh Zitto. Ya kuwa yeye Zitto alichukua kadi ya chadema akiwa na miaka 16 mwaka 1993 wakati "hao wenye midomo mikubwa wanao ongea sasa walikuwa wamewakumbatia watawala"

Zitto wakati anachukua kadi ya chadema mwaka 1993, Katibu Mkuu wa chadema Dr Slaa alikuwa yuko CCM.

Kumbe Zitto ana miaka mingi ndani ya cdm, kuliko hata Viongozi wake!!

SWALI: Lissu, Mnyika na Lema walikuwa wapi mwaka huo??
 
kilele pori

JF-Expert Member
Aug 6, 2013
232
0
Ungemuuliza kwann labda hakuanzisha chama chake kama anajihisi alikua na vision kuliko hao anaowateta?
Kisiasa huyu jamaa alishajimaliza tokea alipounda team na maccm
 
Abdillahjr

JF-Expert Member
Oct 3, 2011
694
0
Kuku mpuuzi na mwendekeza tumbo lake hula mayai yake mwenyewe na dawa ya kuku wa namna hii ni kumkata mdomo au kumchinja kabisa,na hata paka mshenzi hula mtoto wake baada ya kumzaa, kwa hiyo kuchukua kadi zamani kisha matendo yako yakawa ya hovyo dhidi ya umoja wa wenzio hupaswi kuvumiliwa kisa kadi ulichukua mapema!!

Nyerere alileta uhuru kutoka kwa wakoloni baada ya kuacha kufundisha na ajira ya mkoloni kwa hiyo waliokuja baada ya Zitto waweza kuwa bora kuliko uzandiki wake!!
 
Malafyale

JF-Expert Member
Aug 11, 2008
13,068
2,000
Akiwemo slaa ambae alikua mbunge wa ccm

Dr Slaa amewahi kuwa Mbunge wa CCM?Viroba hivi vya asubuhi vinapoteza nguvu kazi nyingi sana za vijana wetu!

Kukufundisha:Dr Slaa alichukua form kugombea kupitia CCM mwaka 1995 kwenye uchaguzi mkuu wa kwanza wa vyama vingi na akamshinda Mbunge aliyekuwa anatetea kiti chake Patrick Qorro kwa kura nyingi kwenye kura za maoni;lkn Kamati Kuu ya CCM chini ya Rais Mwinyi na Ben Mkapa wakalitupa jina la Dr Slaa na kumrudisha Qorro!

Dr Slaa akatangaza kuondoka CCM na ndipo CCM kwa hatari ya kupoteza Jimbo wakamtuma Daniel Ole Njoolay(Balozi wetu Nigeria kwa sasa)kumshawishi Dr Slaa ili asiondoke CCM na wakamuhaidi ubalozi!Dr Slaa akakataa na akaingia CHADEMA na akashinda vipindi 3 mfululizo na kuweka himaya ya Karatu kwa wapinzani!

Historia kama Dr Slaa kawahi kuwa Mbunge kupitia CCM ndiyo mnafundishwa na walimu wa Mulugo?
 
Mandla Jr.

JF-Expert Member
Dec 15, 2013
3,100
1,195
Kuku mpuuzi na mwendekeza tumbo lake hula mayai yake mwenyewe na hata paka mshenzi hula mtoto wake baada ya kumzaa kwa hiyo kuchukua kadi zamani kisha matendo yako yakawa ya hovyo dhidi ya umoja wa wenzio hupaswi kuvumiliwa kisa kadi ulichukua mapema!!

Nyerere alileta uhuru kutoka kwa wakoloni baada ya kuacha kufundisha na ajira ya mkoloni kwa hiyo waliokuja baada ya Zitto waweza kuwa bora kuliko uzandiki wake!!

Una hoja nzito mkuu! Ila umetumia mifano mikali kuifikisha.
 
Babkey

JF-Expert Member
Dec 10, 2010
4,834
2,000
..nadhani waliopita vyama mbali mbali wamejifunza mengi kuliko aliekaa sehemu moja pasi na ''kujua" changamoto za vyama vingine. Inaonyesha hao wengine ni wazoefu wa siasa kuliko yeye.

Labda atuambie hao wengine walitakiwa kuwa wapi kutokana na mfumo uliokuwepo!?
0†7
 
Ciril

JF-Expert Member
Jan 10, 2011
8,562
2,000
Wadau wa JF!
Nimefurahishwa na kauli aliyoitoa Mbunge wa Kigoma Kaskazini mh Zitto. Ya kuwa yeye Zitto alichukua kadi ya chadema akiwa na miaka 16 mwaka 1993 wakati "hao wenye midomo mikubwa wanao ongea sasa walikuwa wamewakumbatia watawala"

Hata kama angalikuwa yeye ndio muasisi wa Chadema hiyo sio hoja ,hoja iliyopo ni kuwa ameivunja katiba ya chama ambayo ndio msingi wa chama chochote.Ukiikiuka katiba hatutaangalia wewe ni nani ndio maana viongozi wa kiserikali huapa kuilinda katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania..Sioni hoja yenye mashiko hapo kwa Zitto ,sana ni kutapatapa na kutafuta huruma kwa wasiofikiri zaidi.
 
Malafyale

JF-Expert Member
Aug 11, 2008
13,068
2,000
Wadau wa JF!
Nimefurahishwa na kauli aliyoitoa Mbunge wa Kigoma Kaskazini mh Zitto. Ya kuwa yeye Zitto alichukua kadi ya chadema akiwa na miaka 16 mwaka 1993 wakati "hao wenye midomo mikubwa wanao ongea sasa walikuwa wamewakumbatia watawala"

Hii kauli kaitoa wapi?na lini?

Maana juzi kalialia hapa na facebook kuwa kuna watu wanamchomekea maneno ambayo hajayasema!Una hakika kasema kama ulivyoandikia hasa kauli hii "alichukua kadi ya chadema akiwa na miaka 16 mwaka 1993 wakati hao wenye midomo mikubwa wanao ongea sasa walikuwa wamewakumbatia watawala"

Hapo nilipo bold kwa wino mweusi ni kweli Zitto kayasema haya au umeongeza maneno yako jamaa wewe mgeni hapa JF?
 
Abdillahjr

JF-Expert Member
Oct 3, 2011
694
0
Dr Slaa amewahi kuwa Mbunge wa CCM?Viroba hivi vya asubuhi vinapoteza nguvu kazi nyingi sana za vijana wetu!

Kukufundisha:Dr Slaa alichukua form kugombea kupitia CCM mwaka 1995 kwenye uchaguzi mkuu wa kwanza wa vyama vingi na akamshinda Mbunge aliyekuwa anatetea kiti chake Patrick Qorro kwa kura nyingi kwenye kura za maoni;lkn Kamati Kuu ya CCM chini ya Rais Mwinyi na Ben Mkapa wakalitupa jina la Dr Slaa na kumrudisha Qorro!

Dr Slaa akatangaza kuondoka CCM na ndipo CCM kwa hatari ya kupoteza Jimbo wakamtuma Daniel Ole Njoolay(Balozi wetu Nigeria kwa sasa)kumshawishi Dr Slaa ili asiondoke CCM na wakamuhaidi ubalozi!Dr Slaa akakataa na akaingia CHADEMA na akashinda vipindi 3 mfululizo na kuweka himaya ya Karatu kwa wapinzani!

Historia kama Dr Slaa kawahi kuwa Mbunge kupitia CCM ndiyo mnafundishwa na walimu wa Mulugo?

Mkuu safi kwa kuwapa somo hao maroboti wa uzandiki wanaotaka kumfananisha Dr. Slaa na mtu anaehongwa magari na kamati za uwakilishi!!
 
rifwima

JF-Expert Member
Apr 21, 2010
491
250
Tena alikuwa anajiona bora kama huyu huyu Zitto!

Hapo ndo watu wanashindwa kuona jinsi Zitto alivyo k.I.a.z.i mbatata. Anataka kujenga hoja gani hapo? Lakini the fact to his Fallacy ni "Hao anaodhani walichelewa kuja CHADEMA, si ndo wamemvua vyeo"? and if they do what it takes Hao hao Watamvua uanachama.
Alitakiwa kujiuliza yafuatayo kabla ya kutoa ----- full of nonsense!
1. Kabla ya 1992 na 1993 alipokuwa at 16 Tanzania ilikuwa na vyama vyingi vya siasa?
2. Anaowaita walikuwa CCM walikuwa na umri gani 1993 na walijiunga CCM lini? Manake kunawaliojiunga CCM kipindi cha Nyerere, Mwinyi na Hata Mkapa?
3. Kwa hiyo wale wanaotoka vyama vingine vya siasa I.e NCCR Mageuzi to CCM to CHADEMA to CUF etc wawe treated kama second grade members?
NB. Nashangaa sana wanaomsifia Zitto eti kichwa! Kichwa boga tu huyu who can talk anything goes.!
 
Ckattovic

Member
Jun 15, 2013
95
0
Kuwa wa Kwanza kuanzisha Jambo fulani haina maana kwamba kuwa ni halali kwako kuamua au kutokuamua kulifanyia malekebisho pindi linapokuwa katika hali tete.

Maana yangu ni kuwa sio kwamba kisa ye ndo alichukuwa kadi wa kwanza kuliko hao wanaomuajibisha, ndo ana haki ya kutokuwajibishwa pale anapokosea au wakitaka kumuajibisha wamuulize adhabu ipi anaona inamstahili.
 
Status
Not open for further replies.

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom